Saturday, May 20, 2017

TAFITI ;SERIKALI INAPOTEZA MABILIONI KUTOKANA RUSHWA NA UFISADI KWENYE BAJETI

 Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji  wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakizindua Ripoti hiyo, wakiwa na Wabunge
 Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji  wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakiwa na wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakionyesha Vitabu juu mara baada ya uzinduzi
 Profesa ,Honest Ngowi akifafanua juu ya Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani?
 Askofu Stephene Munga akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani?
 Mbunge    wa Msalala , Ezekiel Maige akizungumza wakati wa kuchangia  mapitio ya ripoti hiyo  
 Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrad Kigola akichangia mada
 Sehemu ya washiriki wa mkutano huo

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma

Tafiti mpya iliyozinduliwa leo inasema serikali inapoteza fedha zaidi ya Sh trillion 4 kwa mwaka kutokana na misamaha na ukwepaji wa kodi.
 Pia repoti inasema serikali inasema serikali inapoteza  Dola za kimarekani 1.3 biloni (2.9 trilion) kutokana na rushwa na ufisadi katika bajeti ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Profesa  Honest Ngowi alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utafiti na mapitio ya ripoti ya swali la dola bilioni moja na kuja na swali Tanzania inapoteza kiasi gani cha fedha?.

Profesa Ngowi katika mapitio hayo amepata kutaja kuwa , Mfumo wa ulipaji kodi , Mlipa kodi,Misamaha ya kodi ,Utroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato,Ukwepaji kodi, Madhara na Gharama za upotevu na kutokusanywa kodi ipasavyo ni moja ya mambo yanayochangia kupotea kwa fedha hii.

“Tatizo la utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato limeangaliwa upya katika utafiti huu na kubaini kuwa Tanzania bado inapoteza mapato kwa njia ya utoroshaji fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali ,Zinaondoshwa nchini visivyo na kutumiwa isivyo halali” amesema Prof Ngowi.

Ametaja kuwa fedha hizo zinaweza kuwa ni fedha zitokanazo na biashara haramu kama biashara ya kulevya , biashara haramu mipakani ,uharamia ,usafirishaji binadamu ,mapato kutokana na ukwepaji kodi na mapato yatokanayo na rushwa.
Amesema kuwa sambamba na utoroshwaji wa fedha ,tatizo la kutoa taharifa za uongo wa bei 

DOGO JANJA ; MUZIKI WANGU NI LEVEL ZA KINA JAYZ

Msanii kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amejitamba na kusema ingawa yeye ni mdogo lakini muziki anaofanya ni mkubwa kiasi kwamba watu wanaoweza kuufanya ni level za Jay Z.
Dogo Janja
Msanii huyo akipiga stori na Magic Fm amesema kwanza yeye si mtu wa kushirikishwa au kushirisha wasanii hovyo hovyo katika nyimbo zake, bali yeye anadeal na zile serious project tu.
“Mtoto anafanya muziki wa mtu mzima, muziki ninaofanya mimi angetakiwa afanye mtu kama Jay Z lakini ndio nafanya mimi, ni hatari sana,” amesema na kuongeza.
“Mimi kwanza sifanyi kolabo, kama nitafanya ni zile zipo serious, sio zile kuna kaverse kapo hapa njo ufanye, kama unafiti ibuka. Mimi nafanya project kama ya Chindo ametoka Marekani straight L. A (Los Angeles), mimi nikatoka straight froma Dar es Salaam tukakutana Arusha tukashoot video Kijenge, madirector wanne kutoka nje, tumemaliza mimi nikasepa kuendelea na mitikasi mwana akala flight to L.A,” amemaliza kwa kusema.

WOLPER AKILI KUWA ALIBWAGANA NA HARMONIZE

Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai aliachana na aliyekuwa mpenzi wake Harmonize miezi 3 iliyopita lakini waliamua kuficha kwaajili ya shughuli zao za kibiashara.
Jacqueline Wolper
Muigizaji huyo ambaye alicheza vitendo kwenye video ya wimbo ‘Niambie’ wa Harmonize, amedai wakati kazi hiyo inatoka walikuwa tayari  wameachana lakini waliamua kushirikiana katika promo ya wimbo huo ambao unafanya vizuri.
“Nyie mnajua sisi tumeachana juzi? Tumeacha miezi mitatu iliyopita kabla hata ya wimbo wake Niambie haujatoka,” Wolper alikiambia kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV.
Aliongeza ,“Sisi wenyewe tuliamua kukaa kimya kwa sababu kuachana sio kugombana kuna kesho mnaweza kushirikiana katika mambo mengine ya kibiashara,”
Hata hivyo muigizaji huyo aligoma kueleza sababu ya kuachana na muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Happy Birthday’.

MKUTANO MKUU WA VIJANA KUFANYIKA ARUSHA KWA SIKU SABA


Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.
Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.


AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari Mratibu wa Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa, Tajiel Urioh alisema mkutano huo ni maigizo ya vitendo ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambapo vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 30 kutoka sehemu mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza Diplomasia, Uongozi na namna Umoja Wa Mataifa unavyofanya kazi.Bw. Tajiel Urioh alisema kuwa, Mkutano huo unaojulikana kama kongamano kubwa kabisa la vijana nchini linalowaleta pamoja vijana wadogo kutoka nchi mbalimbali tangu mwaka 1997. Aidha aliongeza kuwa Mkutano huo Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa utafanyika mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi wa Mei mwaka 2017, ambapo vijana takribani 200 kutoka katika nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria kujadili masuala yanayohusiana na Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango, Demokrasia na Amani katika nchi zinazoendelea, Kuhama kuelekea kwenye Nishati safi na ya teknolojia mbadala na Elimu kwa Maendeleo Endelevu.

Aliongeza kuwa majadiliano ya mwaka huu yatajikita katika mada kuu: “Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi”. Mada hii inalenga kuwezesha ushiriki wa vijana na kuwajengea uwezo kwenye masuala ya Diplomasia na Uongozi kwa kuwapa mafunzo ya vitendo katika mada ngumu ambazo zitawaongezea ujuzi wa majadiliano na kufikia muafaka wa masuala mtambuka yanayogusa maslahi ya mataifa.

"Tunaishi katika ulimwengu ambao diplomasia yenye ujasiri na uongozi vinahitajika sana hivyo basi kuwakuza vijana katika uwanja huu itachangia kukua kwa mataifa yenye watu wenye uwezo wa kuamua mambo yao. Katika mkutano wa mwaka huu wajumbe watakuja na maazimio mbalimbali ambayo kwa namna moja hama nyingine yatakuwa na manufaa katika maisha yao ya kila siku na watu wanaowazunguka katika jamii zao," alisema Bw. Urioh.
Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwa katika mkutano huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.

“Ni matarajio yangu makubwa kwamba mtakuwa tayari kujifunza kuendana na mada kuu ya ‛ Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi′ lakini pia kubadilishana mawazo na wajumbe wengine na kutengeneza mtandao wa vijana wenye fikra mnazoendana nazo,” aliongeza Tajiel Urioh, Mratibu wa Kitaifa wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2017.Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo alisema kongamano kama hilo la vijana lina umuhimu mkubwa kwa vijana kwani huwajenga vijana kupitia Club za UN. Aliwataja miongoni mwa vijana ambao ni matunda ya Club za UN ni pamoja na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Benedict Kikove, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John John Mnyika na wengine wengi.
 

MATUKIO KATIKA PICHA: BENKI YA CRDB YAWAPA SEMINA WANAHISA WAKE, JIJINI ARUSHA LEO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha. Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
Mwenyekiti wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Mwasajuni akiongoza semina hiyo
Meja kuu ikifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwa wanahisa.
Muwasilisha Mada ya iliyohusu Mambo yananoathiri Thamani na Bei za Hisa katika Soko, Laurian Malauri kutoka Orbit Securities akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada yake hiyo.
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akipitia moja ya vitabu vya mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Naibu Wakurugenzi  Watendaji wa Benki ya CRDB PLC,  Saugata Bandyopadhyay (kulia) na Esther Kitoka wakiteta jambo, wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...