Saturday, May 27, 2017

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA DUKA KUBWA LA VIFAA VYA UJENZI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na uwekezaji Charles Mwijage(katikati) akiongoza jopo la Viongozi kuzindua duka kubwa la kisasa litakalokuwa linauza vifaa vyote vya  vya ujenzi kwa bei nafuu  lililopo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam
 aibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na uwekezaji Charles Mwijage akikagua sehemu ya bidhaa zilizopo ndani ya duka hilo ambazo zinazalishwa hapa nchini
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akiwasili katika sherehe za uzinduzi wa duka hilo ilikujionea bidhaa zinazopatikana hapo
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akizungumza Rais wa umoja wa wafanyabiashara wa china wanaotengeza vifaa vya ujenzi,Thomas Cao, kabla ya kuingia ndani ya duka hilo kukagua vilivyomo
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiwa anaangalia moja yakigae ambacho kimo ndani ya duka hilo na kuzalishwa na viwanda vya ndani
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paula Makonda akipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa duka hilo
 Rais wa umoja wa wafanyabiashara wa china wanaotengeza vifaa vya ujenzi,Thomas Cao akitoa maelezo  kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam jinsi duka hilo lilivyosheheni bidhaa kutoka makampuni mbalimbali hapa nchini
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni , Ben Sitta akiwa na viongozi wa duka hilo katika picha ya pamoja

Friday, May 26, 2017

DK Palangyo ; awataka tanesco na Tanroads kufanya kazi kwa pamoja kukamilisha mradi wa umeme Dar es Salaam kwa wakati

Na  Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini , Dk. Juliana Palangyo amewaagiza wahandisi wa Shirika la umeme nchini Tanesco na Wakala wa barabara nchini Tanroads  kufanya nguvu kwa pamoja hili kuweza kuweka alama za miundombinu ya  mradi wa kuboresha umeme wa Dar es Salaam itapita katika barabara ya Mandela mpaka kurasini.

Dk .Palangyo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akikagua sehemu ya miundombinu hiyo itapita  kwa kushirikiana na Tanroads .
“Tanesco wamekubaliana na  Wakala wa Barabara nchini kupitisha sehemu ya miundombinu ya umeme kando kando mwa barabra ya Mandela hili kuweza kuongeza nguvu katika kituo cha kurasini na mkoa mzima wa Dar es Salaam.Makabuliano haya yamefikiwa leo mara baada ya  mimi kutembelea  katika ofsi za Tanroads na sehemu ambapo miundombinu hiyo itatakiwa kupita”.

Dk Palangyo amesema kuwa wameamua kufanya mazungumzo na Tanroads hili kufikia muafaka kwakuwa wao nao walitaka kutumia eneo hilo katika moja ya miradi yao hivyo kufikia muafaka wa hili kumewezesha mradi wa tanesco kwenda kwa kasi zaidi ya awali.
Amesema sote tunajenga nyumba moja na wote tuna miradi miwili tofauti ambayo inamanufaa makubwa kwa Taifa, mradi huu wa Tanesco utasaidia kuongeza nguvu ya umeme katika maeneo ya kurasini na kisha kupeleka katika Substation ya Mbagala na kufanya eneo hilo kuwa na umeme wa uhakika mbali na mbagala pia nguvu hiyo itaweza kutokea kurasini na kuja mpaka katika Subastation ya katikati ya jiji ambapo nako mahitaji ya umeme yameongezeka
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya makubaliano na Wakala Barabara nchini Tanroads kuafiki miundombinu ya Tanesco ipite katika barabara ya mandela
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo, akiwaonyesha watendaji wa Tanesco na Tanroads nini cha kufanya hili miradi yote miwili ifanikiwe
 Mhandishi Mshauri ,Mathias Albers akimueleza  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo jinsi mradi huo utakavyo pita kando kando mwa barabara
 Meneja mradi huo kutoka Tanesco Mhandisi .Gregory Chgere akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari.
 Afisa uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji akisalimiana na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo kabla ya kuanza safari ya kutembelea sehemu y Miundombinu itapita
 Mhandishi wa mradi wa usafirishaji ,Frank Mashalo akitoa maelezo kwa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo akikagua barabara  ya Mandela
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo akivuka Darja kwenda upande wa pili wa barabara
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo akiwa ameshika Mark mahala ambapo miundombinu ya Tanesco itawekwa kandokando mwa barabara ya Mandela

Kundi la Waandisi kutoka Tanesco na Tanroads wakijadiliana jambo la kiufundi mara baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Palangyo

Thursday, May 25, 2017

UVCCM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA HATUA ALIZOCHUKUA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Kaimu Katibu mkuu wa Umoja waa  Vijana wa Chama caMapinduzi(UVCMM), Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unampongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  na uzalendo wa hali ya juu alionao kwa Taifa mara baada ya kuchukua maamuzi yenye masalhi ya nchi katika swala zima la Makinikia.

 Shaka amesema hayo leo mapema jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa tamko la UVCCM kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kupambana ma utoroshwaji wa rasilimali za nchi kwa uzembe wa watanzania wachache.

Amesema Umoja wa Vijana wa CCM unaunga mkono maamuzi yote yaliyopitishwa au kutolewa na Rais Dk John Magufuli mara baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi 

“Umoja wa Vijana wa CCM hatuko tayari na hatutakubali kushuhudia tena Tanzania  ikirejea katika zama ya kiza kinene cha ukwapuaji mali,  ulaji, kufilisi mashirika ya umma au wizi wa mali za umma.tunaishauri serikali yetu iendelee na mikakati yake ya kuhakikisha ukwapuaji, ubabaishaji, wizi na ufisadi wa mali za serikali vinavikomeshwa mara moja 

      Amesema kuwa Umoja wa Vijana wa CCM unaiomba kwa dhati Serikali yetu ianze kuipitia upya mikataba yote ya madini ili kubaini kama ni yenye manufaa na maslahi mapana  kwa umma na kumuomba Rais Dk John Magufuli kuwaweka pembeni wasaidizi wake wote ambao bado wanaonekana kuwa na kigugumizi katika kuwatumikia wananchi huku baadhi yao wakiona muhali kupambana na ufisadi. 

       Ameweka wazi kuwa UVCCM Inasisitiza kuwa Watendaji wote waliokuwa na dhamana na ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine kupoteza mapato na kulitia hasara Taifa, hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao haraka . 

Amesema wao wanaishauri Serikali kuendelea kuwabaini na kuwachukulia hatua Viongozi na watendaji wa serikali ambao watabainika kumiliki mali, utajiri na vitega uchumi ambavyo havitokani na mapato yasiolingana na vipato vyao wataifishwe kama ilivyofanyika mwaka 1967 baada ya kutangazwa Azimio la Arusha .


“Vijana wote tunaishauri serikali yetu isikubali na isiafiki  mali za umma zitumike kwa maslahi binafsi badala yake kila miliki ya serikali na mali ya umma ifahamike  kuwa kila mwananchi ana haki kufaidika nayo ambayo ni sehemu ya matunda ya Uhuru na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar”.

Alimaliza kwa kusema kuwa  Umoja wa Vijana wa CCM unawataka wana CCM na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Serikali yake katika mapambano dhidi ya vikundi vya rushwa, ufisadi na uzembe kwa baadhi ya watendaji  ili kuleta maendeleo endelevu katika taifa letu.  
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa maamuzi aliyochukua.
 Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwa na Viongozi wa ngazi za juu wa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akicheza muziki na baadhi ya wanachama wa UVCCM
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Akiwa amebebwa juu  na Vijana wa CCM
Sehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili  katika ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika Ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
 smsehemu ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  wakiwa na furaha kubwa sana
 ehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
 Mabango ya kumpongeza Rais Magufuli


Wednesday, May 24, 2017

TIB WAANZA KAZI SAA 24 BANDARINI KWA MUDA WA SAA 24

 Mkurugenzi wa  Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya benki hiyo kufanya kazi saa 24 Bandari ya Dar es Salaam 
 Mkurugenzi  mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege  , Theresia Soka  akizungumzia ubora wa huduma hizo
  watendaji wa   Benki ya Biashara ya TIB  

Sehemu ya Waandishi wa Habari walifika katika  mkutano huo

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
Katika kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli benki ya biashara ya TIB imeanzisha huduma za kibenki kwa masaa 24 katika tawi dogo la benki hiyo lililopo katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa  Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege amesema huduma hiyo inawawezesha wananchi wote kulipia kodi za aina mbali mbali pamoja na tozo zote za bandari.
 Amesema hivi karibuni TIB benki na TRA ziliingia mkataba kwa kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ambapo mtu akilipa kodi kupitia mfumo huo katika tawi lolote la benki hiyo, taarifa zake zitaonekana moja kwa moja kwenye mtandao wa TRA.
Amesema kuwa, benki hiyo ya biashara (TIB), ndiyo benki pekee yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya akaunti za TPA hivyo mwananchi atakapolipia tozo yoyote bandarini taarifa zake huonekana mara moja katika mtandao wake hivyo kurahisisha na kuwezesha kuendelea na taratibu zingine za utoaji mizigo kwa haraka zaidi.
“TIB bank inatoa huduma mbali mbali kutokana na mahitaji ya mteja, zikiwemo za akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya muda mfupi na muda wa kati dhamana za kibenki uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni na shughuli zote za kibenki”, amesema Nyabundege.


Aidha amesema, benki hiyo ya kibiashara yenye matawi 6 nchini,  Dar esSalaam matatu, Mwanza, Arusha na Mbeya inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na pia inatoa huduma kwa watu binafsi taasisi binafsi na serikali.

EFM KUKIPIGA NA MADEREVA BODABODA TANGANYIKA PORKERS LEOKituo cha utangazaji cha EFM redio kitacheza mechi ya kirafiki baina yao na madereva daladala leo tarehe 24/05/2017 katika Kiwanja cha Tanganyika Packers kuanzia saa kumi Jioni, ambapo watangazaji  wa Redio hiyo watachuana vilivyo na wadau wao wakubwa.

Redio hii ya vijana na jamii kwa ujumla imezidi kutoa kipaumbele kwenye michezo hususani mpira wa miguu kwani imekua ikicheza mechi nyingi za kirafiki kila inapobidi ili kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri na jamii inayoizunguka kama wadau wa taasisi mbalimbali ili kukuza vipaji vyao.

Mechi hizi za kirafiki ni kati ya michezo ambayo husaidia jamii kukutana kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri na vile vile husaidia kuhamasisha vijana kufanya mazoezi katika kuunga mkono kampeni ya serikali ya kufanya mazoezi  katika jamii ili kujiepusha na hatari ya kupata magonjwa yasioambukizwa.

Tuesday, May 23, 2017

UMISSETA ARUSHA YAPAMBA MOTO BAADA YA UZINDUZI


 Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akihutubia maelfu ya wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Arusha zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid iliyofanyika mwishoni mwa wiki.   Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akiambatana na Meneja wa Mauzo wa Coca-Cola kwa Jiji la Arusha Boniface Mwasi, wakisalimia wachezaji wa moja ya timu za sekondari zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (Kushoto) akisalimia moja ya timu ya shule za sekondari kutoka mkoa wa Arusha, katika ufunguzi wa mashindano ya Copa Umisseta mkoani hapa yaliyofanyika mwisho wa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola iligawa vifaa mbali mbali vya michezo kwa shule za serikali na binafsi kwa ajili ya ushiriki wa michuano yam waka huu.
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola hapa nchini, kwa ushirikiano na TAMISEMI, imefanya uzinduzi wa mashindano ya umoja wa shule za sekondari (Umisseta) kwa kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha kwa kugawa vifaa vya michezo kwa shule mbalimbali za sekondari za serikali na binafsi. Katika uzinduzi wa mashindano hayo jijini Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwishoni mwa wiki, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha - Mrisho Gambo, ambapo aliishukuru kampuni ya Coca cola kwa udhamini kufanikisha michuano yam waka huu. Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa Coca-Cola mkoa wa Arusha, Boniface Mwasi alisema kuwa kampuni hiyo imeona umuhimu wa kuibua vipaji vya michezo ndio maana wamejikita kufadhili michezo kama hiyo kwa vijana.
“Tumeamua kushirikiana na serikali katika michezo hii ya Umisseta lengo letu kubwa likiwa ni kuibua vipaji vingi vya michezo kwa kuwa tunaamini mtandao wa shule za sekondari ni mkubwa na ni rahisi kuibua vipaji vingi kutoka sehemu zote za nchi”, Alisema Mwasi. Aidha, aliongeza ya kwamba kampuni ya Coca-Cola itaendelea kuunga mkono jitihaa za serikali za kukuza sekta ya michezo nchini hususani katika ngazi za chini ambako imekuwa ni vigumu kupata ufadhili kwa kuwa tunaamini kuwa vipaji vinapaswa kuibuliwa na kukuzwa. “Tunayo dhamira kuona vijana wa kitanzania walioibukia kwenye mashindano haya wanafika mbali kimichezo”, Alisisitiza Mwasi.

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUWA NA MASHAMBA YA MFANO


 Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo.

 Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
 Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akizungumza katika mafunzo hayo.
 Ofisa Ugani kutoka Kata ya Luharanyogu, Aminiel John, akichangia mada.
 Ofisa Ushirika wa Wilaya ya Buchosa, Nyabange Theopista akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Buchosa.
 Maofisa Ugani wakiwa katika mafunzo hayo.
 Ofisa Ushauri wa Kilimo wa Wilaya ya Buchosa, Sospeter Obwago (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Paul Misana. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon na Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus.
 Mkutano ukiendelea.
 Usikivu katika semina hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Buchosa, Kelvin Rweitaka akifungua semina hiyo kwani niaba ya mkurugenzi.
 Taswira ya chumba cha mkutano.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.

Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru, Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB). 

"Ni vema kila ofisa ugani akawa na shamba la mfano ambalo litasaidia wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo bora badala ya kuwaacha bila ya kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya mfano.

Katika hatua nyingine Chirimi alisema uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na maofisa kilimo kushindwa kuwafikia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu ya kilimo bora na cha kisasa.

Alisema kuna kila sababu ya kutolewa elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya pamba ambayo ikitumika itaongeza tija katika uzalishaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.

Alisema hadi leo hii kuna mbegu bora moja tu inayotumika kwa wakulima ambayo aliitaja kuwa ni UKM 08 ambayo ikitunzwa na kuhifadhiwa vizuri itakuwa na  uwezo wa kutoa kilo 700 hadi 800 kwa ekari moja.

Alisema kuwa pamoja na kuwa na mbegu hiyo changamoto kubwa iliyopo bado haijawafikia wakulima wote wa zao hilo la biashara.

Chirimi aliwata wakulima wa zao hilo kuacha kufanya kilimo cha mazoea badala yake wafanya kilimo chenye tija kwa kufuata maelekezo ya watafiti na maofisa ugani.

Akitoa mada katika mafunzo hayo Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange alisema matumizi ya bioteknojia katika kilimo ni muhimu katika uzalishaji wa mazao yenye tija.

Alisema nchi zinatotumia teknojia hiyo katika kilimo zimefanikiwa katika kilimo na kuwakomboa wakulima.

Alisema changamoto kubwa iliyopo kwa wakulima hapa nchini ni mazao yao kukumbwa na magonjwa kama mnyauko wa migomba, funza wa vitumba katika pamba, batobato na michirizi ya kikahawia katika mihogo na ukame ambao unasababisha mahindi kunyauka na kuwa tatizo hilo la ukame si kwa Tanzania pekee bali lipo na nchi za jirani za Afrika Mashariki.

Ofisa Ugani wa Kata ya Nyakalilo, Mariam Alex alisema katika kata yake changamoto kubwa ni wadudu waharibifu wa mazao ambapo licha ya kutumia dawa mbalimbali za kuwaua lakini bado hawajafanikiwa.

Alisema anaamini kupitia mafunzo waliopata kuhusu kilimo yanaweza kuonesha njia ya kukabiliana na changamoto hiyo kubwa waliyonayo.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...