Tuesday, May 30, 2017

MAONYESHO YA MICHORO YA 14 ARTIST YAFUNGWA RASMI ALLIANCE FRANCA'IAS

 Mchoraji Malulu akitoa maelezo ya picha yake kubwa  kwa Mume wa Balozi wa Uswiz nchini , Balozi Arthur Mattli wakati wa kufunga maonyesho ya picha yaliyokwenda kwa jina la uhuru wa kujieleza yaliyofanyika katika ukumbi wa Aliance Franca'is Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Jamii Forum, Maxence Melo  akiwa katika moja ya picha inayoeleza nmana uhuru wa kujieleza mchoro uliochorwa na Lutengano Mwakisopile
 Baadhi ya wadau waliofika katika kutazama maonyesho hayo wakiangalia moja ya picha iliyokuwa ikivuta hisia za wengi
 Mmoja wa Wachoraji kutoka 14 Artist akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau walifika katika maonyesho hayo ya picha
 Mkurugenzi wa Jamii Forum Maxence Melo akiwa katika picha kubwa iliyochorwa na Malulu juu ya wakimbizi wanvyozuiwa katika nchio wanazokimbilia wakati wa Vita


 Mume wa Balozi wa Uswiz nchini , Balozi Arthur Mattli akizungumza na wasanii wa kundi la 14 Artist amabo waliandaa maonyesho hayo
Wasanii wa kundi la 14 Artist wakiwa katika picha ya pamoja na  Mume wa Balozi wa Uswiz nchini , Balozi Arthur Mattli mara baada ya kufunga maonyesho hayo yaliyodumu kwa zaidi ya siku saba 

TWIGA CEMENT WASEMA WATENDELEAKUWA VINARA WA UZALISHAJI SARUJI LICHA YA KUIBUKA KWA MAKAMPUNI MENGINE NCHINI



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kampuni ya Saruji nchini ya Tanzania Portland Cement  inayozalisha Twiga Cement, imesema kuwa itaendelea kuwa kinara  kwa mauzo ya Saruji hapa nchini licha ya kuwepo wa viwanda vingi katika miaka ya hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na  Mkurugenzi wa kampuni hiyo Alfonso Velez, alipokuwa akitoa ripoti ya mauzo ya kampuni hiyo na changamoto inazokabiliana nazo katika mkutano wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
“licha ya makampuni mengine kuja na mpango wa ujanja wa kushusha gharama za saruji bado Twiga Cement imeendelea kuwa ndio saruji bora kwenye soko  licha ya changamoto ya kupambana na bei ya soko”

Amesema wao wameshuhudia wakiona washindani wao wakiangaika juu ya upataji wa mali ghafi ambazo zitaweza kuwasaidia kuendelea kufanya baishara kwa bei ya chini lakini TPCC bado aijatetereka.

Amesema kuwa mshindani wake bado anawakati mgumu kwani yuko mbali na soko na inamchukua muda mrefu kusafirisha mzigo mpaka sokoni hivyo wakati wowote atapandisha bei ya saruji na Twiga itabaki pale pale kwani ameweza kufanya hivyo katika nchi zingine alizowekeza ambapo amepandisha bei kuwa juu hili kufidia gharama za uzalishaji.
 Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya TPCC , Osward Urasa akizungumza katika mkutano huo juu ya wanahisa kutoa taharifa zitakazosidia kujenga kampuni kuzidi kuwa imara
 Mwenyekiti wa kampuni ya Tanzania Portland Cement, Alfonso Rodriguez akizungumza katika mkutano huo wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika leo katika hotel ya Ramada
 Mkaguzi wa Mahesabu wa kampuni hiyo kutoka kampuni ya Ernist nd Young , Elibariki Fanuel akieleza juuya mehesabu ya mwaka ya kampuni hiyo
 Mkurugenzi wa Twiga Cement Alfonso Velez  akizungumza juuya mafanikio ya kampuni hiyo mara baada ya kuwepo wa ushindani wa makampuni mengine nchini
 Sehemu ya Wanahisa katika mkutano huo wakiwa wanasikiliza kwa makini
 Profesa  akijadili jambo na wakurugenzina uongozi wa juu wa Twiga Cement
 Katibu wa kampuni TPCC,Brain Kangeta akizungumza wakati wa mkutano huo wa wanahisa na wateja wa Twiga Cement
 Mwanahisa Christopher  Mvemo akichangia jambo juu ya kuboresha kampuni hiyo ili izidi kuwa kinara wa mauzo ya Saruji
 Mwana hisa , Godfrey Marik akiuliza swali juu ya mipango ya kampuni katika kuhimili ushindani na makampuni mengine
sehemu ya wajumbe wa mkutano huo waliohudhuria

Monday, May 29, 2017

FEMINA HIP YAJA NAKAMPENI MPYA YA NGUVU YA BINTI

 Mratibuwa programu ya Nguvu ya Binti , Lydia Charles akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mpango wao wa kuwawezesha  wanawake wanapokuwa katika siku zao.
 Mwakilishi wa Kays Hygien , Sauda Simba akizungumza juu ya kampuni hiyo kudhamini programu hiyo
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wa Waandishi wa habari uliofanyika kuhusu kusaidia kutoea elimu ya afya ya uzazi.


Na  Ashraf Said, Globu ya jamii

Tasisi ya Femina Hip imeanzisha kampeni yake mpya inayokwenda kwa jina Nguvu ya Binti hili kuweza kumsaidia msichana anapokuw katika siku zake .

Akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo  Lydia Charles amesema kuwa Femina Hip imezindua kampeni hii ambayo itawakilishwa na wasichana wenye historia ,Tabia, na uzoefu tofauti .

“ timu mpya ya nguvu ya binti itakuw asauti ya wasichana wote nchini Tanzania , wakichimbua , Kujadili na kujaribu kutatua changamoto na vikwazo mbalimbali kwa pamoja” amesema.

Amesema kuwa wasichna hao watakuwa mawakili kwa mambo ya kijamii ,Kiuchumi na kisiasa.

Ameliza kwa kusema kuwa Femina Hip pamoja na wasichana wa kundi hilo wanamini kwamba ni lazima kufanya kazi pamoja , kufunguka na kuzungumza kuhusiana na hedhi ,maumivu wakati wa hedhi , Usafi wa miiko inayousishwa na hedhi kwa kushirikisha walimu , wazazi, walezi na Wanaume pia .

WABUNGE WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUWASAIDIA WASICHANA WANAOPATA MIMBA SHULENI



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mtandao wa Mashirika yanayopinga ndoa za utotoni wameitaka serikali kuweka mfumo madhubuti utakaowawezesha wanafuzni wa kike kuendelea kufurahia haki yao ya kupata elimu bora mara baada ya kujifungua.

Akitoa tamko hilo Mwenyekiti wa mtandao huo, Valerian  Msoka  amesema Serikali ,wabunge na wadau wengine kujikita katika kupambana na changamoto zinazopelekea mimba za utotoni ikiwemo ubovu wa miundombinu ya elimu kukosekana kwa elimu bora ya afya ya uzazi.

“Mtandao wa kupinga ndoa za utotoni unaamini kuwa Tanzania ina uongozi na wawakilishi wanaojali maslahi ya wananchi ambapo watoto wa kike ni miongoni mwa hao . Na ni kwa sababu hiyo mtandao una imani kuwa sauti yao itsikilizwa kwani wasichana hawa wanaopoteza masomo kutokana na mimba ni sehemu ya nguvu kazi muhimu ya msingi na yenye tija kufikia Tanzania ya Viwanda” amesema  Msoka.

Msoka amemaliza kwa kusema kuwa utafiti wa kitaifa kuhusu Vichocheo na madhara ya ndoa za utotoni  nchini Tanzania  uliofanywa mwaka 2016  umebaini kuwa wasichana wana uelewa mdogo juu ya afya ya uzazi.

 Mwenyekiti wa Mtandao wa kutetea wadada wadogo, Valerian  Msoka  
 Mwenyekiti wa Tamwa , Eda Sanga akizungumza juu ya kuwaomba wabunge kutunga sheria kuwasaidia watoto wanaopata mimba mashuleni  
Mkurugenzi wa Tawla nchini ,Tike Mwambipile akizungumza wakati wa kutoa tamko hilo 
 Mkurugenzi wa Shirika la Watoto, Koshuma Mtengeti akizungumza juu ya tamko hilo

 Waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Baadhi ya wanachama wa tasisi mbalimbali zisizo za kiserikali wakiwa katika mkutano huo
 Waandishi na wana harakati  wakisikiliza tamko hilo kwa makini

REHEMA FOUNDATION YAGAWA FUUTARI KIJIJI CHA KILOMO BAGAMOYO

 Mwakilishi wa tasisi ya Rehema foundation ,Zuber akigawa chakula kwa ajili ya futari  kwa wakazi wa Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya msaada ul;iotolewa na tasisi yao kutoka kwa wananch mbali mbali wa nchi ya Uturuki kwa kipindi hiki cha Ramadhani
 Mwenyekiti wa Tasisi ya Rehema ,Mustafa Diriel akigawa mifuko ya futari kwa wasiojiweza na wazee wa kijiji cha Kilomo Bagamoyo Pwani.Chakula hili kimechangishwa na watu mbali mbali katika inchi ya Uturuki
 Mohamedd akimpatia mzee Miraji fuko lake la futari katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani

 Wafanyakazi wa tasisi ya Rehema Fondutioni wakigawa mifuko ya chakula
Mbunge wa Bagamoyo akiwa na timu mzima ya Taasisi ya Rehema na wakazi wa kilomo baada ya kupewa msaada huo.

Sunday, May 28, 2017

HII NI HATARI KWA MTU HUYU ALIYE JUU YA MIZIGO

Mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam akiwa amekaa juuu ya mzigo uliobebwa na Baiskeli ya magurudumu matatu (Guta) akitokea katika soko la Mabibo  kuelekea mtaani kama alivyokutwa katika barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam jambo ambalo ni hatari kwa uasalama wake kutokana na barabra hiyo kupitisha magari makubwa ya mizigo na kutembea kwa kasi kuwa katika bandari ya Dar es Salaam(Picha na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii)

TRA Watoa Somo la Ulipaji Kodi kwa Wafanyabiashara wa Kichina





Meneja wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu semina juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria kwa wafanyabiashara kutoka China iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
2
Mrakibu wa uhamiaji na Afisa Vibali vya Ukazi, Eliud Ikomba akitoa semina kwa wafanyabiashara kutoka China (hawapo pichani) juu ya sheria za uhamiaji katika semina iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
3
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka China wanaofanya biashara zao nchini wakisikiliza mafunzo mbalimbali juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria katika semina iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.    
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa somo la masuala ya kodi kwa wafanyabiashara kutoka China wanaoishi nchini kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya sheria na taratibu za ulipaji kodi katika semina kuhusu mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi amesema kuwa Tanzania ya sasa ina fursa nyingi za uwekezaji hivyo wafanyabiashara hao watakapokuja kuwekeza lazima wafahamu kanuni na taratibu za ulipaji kodi nchini ili waweze kuendana na sheria zilizopangwa na nchini.

“Semina hii mahususi imeandaliwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa kichina wanaoishi nchini kupata mafunzo ya kodi zikiwemo za zuio, majengo pamoja na ushuru na forodha ambazo ni lazima wazifahamu kwa manufaa ya Taifa letu na wao pia,”alisema Mwangosi.

Mwangosi ameongeza kuwa hii ni mara ya 6 kufanyika kwa semina hizo kwa wafanyabiashara hao ambapo tangu zianze kufanyika zimewasaidia kutokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa nchini.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dotto Stanley amesema kuelimisha umma hasa kwa wageni kutoka nje ya nchi ni jambo la msingi litakalowarahisishia kufahamu sheria za nchi ambapo kwa namna nyingine itachochea uwekezaji.

“Kwa kawaida wafanyabiashara wakubwa huwa wanahitaji kufahamu sheria na taratibu za nchi husika kabla hawajaamua kuwekeza mahali hivyo mafunzo hayo yatachochea uwekezaji nchini kwa sababu watakuwa na uelewa wa mchakato mzima juu ya sheria za uwekezaji na kodi.”alisema Stanley.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd, Anne Werema Maneno amesema kuwa changamoto kubwa inayowapata wafanyabiashara wa kichina ni kukosa uelewa juu ya jinsi ya kuwekeza nchini hasa katika suala la ulipaji kodi.

“Changamoto hiyo inawapelekea wafanyabiashara kukosa muelekeo wa biashara waliyopanga kufanya kwani wengi wao wakifika Tanzania hubadilisha biashara baada ya kufahamishwa sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu biashara hivyo semina hiyo itawapa uelewa utakaowawezesha kuchagua biashara watakayoweza kuifanya kulingana na mtaji wa mfanyabiashara husika,”alisema Bi. Anne.

Aidha, katika semina hiyo ya siku moja imeambatana na fursa ya kupata mafunzo kutoka kwa taasisi zingine zinazofanya kazi moja kwa moja katika shughuli ya uwekezaji ambazo ni pamoja na TRA, TIC, Idara ya Uhamiaji, Idara ya Kazi pamoja na Taasisi za Kibenki.

Mafunzo hayo juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria kwa wafanyabiashara hao yameandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ikiwa ni utaratibu wa kawaida wakukutana na wadau mbalimbali wa Kodi.

CHAMA CHA WAONGOZA WATALII TANZANIA (TTGA) WALIA NA MIUNDO MBINU MIBAYA YA BARABARA NDANI YA HIFADHI ,WASEMA HADI SASA MIKATABA IMEKUWA DONDA NDUGU KWAO!



Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa chama cha waongoza Watalii Halifa Msangi,Wakwanza kushoto ni Katibu wa umoja huo Emanuel Mollel,Haji Mbuguni Mjumbe wa (TTGA)Omari Rajabu mjumbe,Apolinary Kiwhili M/Msaidizi wakiwa katika maonyesho ya utalii ya 18 ya Karibu Fair 2017Picha na Vero Ignatus Blog.

Wa pili kulia ni mwenyekiti wa Chama cha waongoza Utalii Nchinni Tanzania Halifa Msangi,Wa kwanza kushoto Katibu wa chma hicho Emanuel Mollel,wakiwa na wajumbe wa chama hicho ,pamoja na Hosiana F. Siao.Picha na Vero Ignatus Blog. 
Wakizungumza na wageni mbalimbali Ambao walitembelea banda lao katika maonyesho ya Utalii yaliyo shirikisha zaidi ya makampuni 300 ya utalii,amabapo washiriki wa ndani yanchi ni 60% na yale ya nje ni 40% ambapo huwa wanafanyika lila mwishoni mwa mwezi mei .Picha na Vero Ignatus Blog.Chama cha waongoza Watalii wakiwa kwenye banda lao ndani ya viwanja vya magereza katika maonyesho ya Karibu Fair yaliyo beba kauli mbiu isemayao Utalii endelevu kwa Maendeleo.Picha na Vero Iganatus Blog. 
Maongezi yakiendelea na wageni waliotembelea banda lao.Picha na Vero Ignatus Blog.




Na.Vero Ignatus ,Arusha

Chama cha waongoza Watalii nchini Tanzania (TTGA) wameiomba Serikali iwapatie eneo huru kati ya Hifadhi ya Ngorongoro na ile ya Serengeti ,kwani katika eneo hilo la Ndutu katika upande wa Serengeti hakuna barabara za kufanyia mizunguko za kwenda kuangalia wanyama .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho ndugu Halifa Msangi kwamba changamoto kubwa wanayoipata kama waongoza watalii ,ni kipindi ambacho wanyama pundamilia na Nyumbu wanapohama kuelekea upande mwingine hawawezi kuwapeleka wageni kwenda kuwaona wanyama hao upande wa pili

"Katika eneo la Ndutu wananyama pundamilia na nyumbu huwa wanatabia ya kuhama na kuelemea upande mwingine,sasa unakuta wewe muongozaji ukiwa na kibali cha upande mmoja tu huwezi kuwapeleke wageni mahali wanyama walipo kwani hakuna barabara ya kufanyia mizunguko kwenda kuwaona wanyama jambo ambalo tumekuwa tukipata changamoto kubwa na maswali mengi kutoka kwa wageni tumeizungumzia changamoto hii kwa muda mrefu sasa."alisema Halifa.

Kwa upande wake Katibu wa chama hicho cha waongoza watalii Emanuel Alfayo Mollel amesema kuwa changamoto nyingine kubwa ni barabara zilizopo ndani ya Hifadhi haswa kutoka Ngorongoro kuelekea Serengeti ,barabara hizo zimejazwa vifusi kwa ya km 10 ambavyo havijasambazwa jambo ambalo wakati mwingine vinaweza vikapelekea hata kusababisha ajali pale ambapo dereva anahangaika kuvikwepa.

''jamani miundo mbinu ndani ya hifadhi haswa Tarangire na Manyara ni changamoto kubwa wakati wa mvua hakupitiki, "alisema Emanuel.

Amesema kuwa asilimia 90 ya waongoza Watalii ni waajiriwa kwenye makampuni ya Utalii ,hadi sasa mikataba yao imekuwa ni donda ndugu kwani mikataba hiyi ipo tayari lakini hakuna wakuisimamia ili ifanye kazi kama inavyohitajika.

Amesema Waongoza watalii nchini Tanzania kilianzishwa mwaka 1999,kina jumla ya wanachama zaidi ya 3000 ,Wanachama ni 1130 ,wanachama hai waliolipa ada zao kwa mwaka 2017 ni 567 tu,amewataka waongozaji watalii hao ambao sio wanachama waamue kuiunga kwani hakuna njia nyingine ya kutatua changamoto waliyonayo zaidi ya kuwa wamoja.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimtakia heri mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Mama yake Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa nj...