Friday, June 9, 2017

SEKTA YA UTALII YATAJWA KUONGEZEKA KATIKA KUCHANGIA UCHUMI WA TANZANIA

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Dk. Aloyce Nzuki  akizungumza juu ya ripoti ya sekta ya utalii kusaidia katika uchumi wa Taifa katika mkutano wake naWaandishi wa habari katika ukumbi wa benki kuu jijini Dar es Salaam.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Sekta ya Utalii imetajwa kuwa moja ya vitu vinavyochangia kukua kwa uchumi wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2016 mpaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Dk. Aloyce Nzuki  amesema pato hilo limekuwa kuanzia miezi ya August na September.
“sekta ya utalii imekuwa ikiingeza asilimia 12.1 ambayo ni sawa na dola za kimarekani 2131.57 Milioni kwa mwaka 2016 kulinganisha na mwaka 2015 ambapo sekta hii ilikuwa kwa dora 1901.95 Milioni” amesema Dk Nzuki.

Amesema ripoti hiyo ambayo imetoa majawabu hayo ilifanywa katika maeneo yote ya viwanja vya ndege na mipakani ambako kulitumika kupokea wageni.


Sehemu ya wajumbe walioshiriki katika mkutano huo juu ya sekta ya utalii kusaidia katika kuongeza mapato nchini    

CTI Bajeti imekidhi mahitaji muhimu yapongeza bajeti ya 2017/2018

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini(CTI),Dk Samuel Nyantahe akizungumza na waandishi wa haabri juu ya Mtazamo wa Bajeti  kutoka tasis
  Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini(CTI),Dk Samuel Nyantahe akiwa na mjumbe wa tasisi hiyo Leodgar Tenga wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari(Picha zote Humphrey Shao)
Sehemu ya Wjumbe wa Shirikisho la Viwanda nchini CTI wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ,(Picha zote  na Humphrey Shao)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Shirikisho la wenye Viwanda Nchini (CTI) limesema bajeti ya mwaka huu ni nzuri na imekidhi mahitaji yote muhimu ikiwa ni pamoja  changamoto za wafanyabiashara kupata majibu.
Akizungumza leo  na waandishi e wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CTI, Dk. Samuel Nyantahe amesema bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango ni bajeti ambayo imegusa changamoto za wafanyabiashara walizokuwa wanazilalamikia.
Amesema  awali wafanyabiashara walikuwa wanalalamika kuwapo kwa kodi zisizokuwa na maana hivyo kwa sasa kumekuwapo na unafuu.
“Lakini Serikali kuongeza kodi katika bidhaa zinazozalishwa hapa nchini sambamba na zile zitokazo nje kidogo haijakaa sawa, walipaswa kuweka kipaumbele bidhaa za ndani kama vile ambavyo hawajaongeza kodi katika maji ya hapa nchini,” alisema Dk. Nyantahe.
Dk. Nyantahe amesema changamoto iliyopo sasa ni Serikali kuongeza uwigo wa ukusanyaji wa kodi katika kufanya bajeti hiyo iweze kutekelezeka kwa kuongezeka kwa kodi ya majengo.

Aidha amesema hatua ya serikali kuondoa kodi ya leseni katika magari na kuongeza katika mafuta ni jambo jema lakini kuna badhi ya watanzania watakuwa wanakatwa pindi watakapokuwa wanakwenda kununua mafuta wakati hawana magari.

HOSPITALI YA AGA KHAN YAZINDUA HUDUMA MPYA YA GHARAMA NAFUU

Mtoto wa Aga Khan Princes Zahra Aga Khan azindua huduma mpya ya huduma za gharama na fuu kwa wagonjwa na Maabara ya kisasa  katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja mawasiliano wa Hospitali hiyo Olayce Lotha amesema kuwa maabara hiyo itasaidia kutoa majibu ya vipimo ambavyo vililazimika kupelekwa nje na kurudi hili waendelee na matibabu.

“tumetengeneza mfano wa vitanda 20 ambavyo vitaonekana katika mradi huu, pia kwa sasa maabara hii mpya itaweza kutoa majibu yote ya vipimo vya kansa na magonjwa mengine sugu ambayo yalikuwa lazima yakapimwe nje ya nchi” amesema Lotha.

Amesema wodi hizo kwa sasa zitaweza kuchukua watu wanne kwa pamoja kwa gharama nafuu tofauti na zile wodi zingine ambazo zilikuwa zinachukua mtu mmoja mmoja kwa gharama ya hali ya juu.

Amesema mradi huo umetokana fedha kutoka Msaada kutoka kwa Tasisi ya Maendeleo ya ufaransa (FDA) ambayo imetoa Bilioni 120 na bilioni  60 kutoka Aga Khan Development Network.


   

SPESHOZ TANZANIA YAINGIA MKATABA NA TIMU YA LIPULI

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mkataba wake na timu ya soka ya Lipuli ya Mkoani Iringa
 Mwenyekiti wa Lipuli ,Abu Changawa akisaini mkataba wa vifa na kampuni ya Speshoz Tanzania ambayo itatoa vifaa vya michezo kwa timu hiyo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey  na  Mwenyekiti wa Lipuli ,Abu Changawa  wakisaini Mkataba wa Vifaa vya Michezo

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Kampuni ya uuzaji wa vifaa vya Michezo ya ,Speshoz Tanzania imeingia mkataba wa kutoa vifaa vya Michezo  kwa timu ya Soka ya Lipuli ambayo imepanda kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa timu hiyo mkurugenzi wa Speshoz Tanzania,Jeffrey Jessey amesema mkataba huo ambao ni wa zaidi ya Milioni 30 utawawezesha kuuza jezi za Lipuli na kuwagawia vifaa vyote vya mazoezi.

“mkataba huu utaweza kuisadia timu hii kuwa na vifaa vya uhakika na vya kisasa ambavyo vitasaidia timu hiyo kuwa na morali na kuhimili ushindani na timu mkubwa” Amesema Jessey.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya Lipuli, Abu Changawa amesema kuwa mkataba huo ni moja ya vitu ambavyo vitasaidia timu hiyo kuwa na vifaa vya uhakika.

Amesema kuwa kampuni hiyo imewapa masharti kuwa timu hiyo ikifanikiwa kubaki sita bora basi wataongeza udhamini katika msimu ujao.


Changawa amesema  ni vyema makampuni mengine yakajitokeza kusaidia timu hiyo kwa upande wa udhamini hili iweze kufanya vizuri.

Wednesday, June 7, 2017

SAFARI YA MWISHO YA BALOZI ABDUL CISCO MTIRO

 Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wanapokea mwili wa Maraehemu Abdul Cisco Mtiro nyumbani kwake Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma , Adma Kimbisa akisaini Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Abdul Cisco Mtiro
 Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu,Bernard Membe  akisaini Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Abdul Cisco Mtiro Mikocheni B Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi akisaini Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Abdul Cisco Mtiro nyumbani kwake Mikocheni
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi akisalimiana Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu,Bernard Membe
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na watu waliofika katika msiba wa Marehemu Abdul Cisco Mtiro
 Jaji Mkuu Mstaafu , Othman Chande akisaini kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa Abdul Cisco Mtiro Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
 Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Bin Zubery  akisaini kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa Abdul Cisco Mtiro Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiwa ameketi na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya MrishO Kikwete  nyumbani kwa Marehemu Abdul Cisco MtiroMikocheni B jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya watu waliofika kwenye msiba wa marehemu Abdul Cisco MtiroMikocheni B jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakihifadhi mwili wa Marehemu Abdul Cisco Mtiro  katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim akiwa katika mazishi ya Marehemu ,Abdul Cisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Dar es Salaam
 Umati uliofika kuzika  Mwili wa Marehemu Balozi Abdul Cisco Mtiro
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya MrishO Kikwete  akiwa na waombolezaji wengine wakiomba Dua katika Mazishi ya Balozi Abdul Cisco Mtiro  Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete  akiteta na Ankal  mara baada ya Mazishi ya Balozi Abdul Cisco Mtiro
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya MrishO Kikwete  akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda


 Mtoto wa Marehemu Abdul Cisco Mtiro akiweka mchanga  kwenye kaburi la Baba yake
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
  Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Wazirio Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Jaji Mkuu Mstaafu ,Othman Chande,akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 CDF Mstaafu ,Davis Mwamunyange ,akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Balozi ,Ben Mashiba ,akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
Balozi ,Abdulhaman Shimbo, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Ciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam

MAALIM SEIF APATA AJUMUIKA NA WAKAZI WA BUGURUNI KUPATA FUTARI NA SWALA

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif akiwasili katika Mtaa wa Buguruni akipokewa na Naibu Meya wa Jiji Omary Kumbilamoto
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na wakazi wa Buguruni aliojumuika nao pamoja katika futari na swala
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad  akiwa katika ibada iliyofanyika katika Baraza la Mtendeni 2 Buguruni
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Wananchi wa Buguruni ambao alijumika nao katika futari ya pamoja
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na viongozi wa juu wa Chama mara baada ya kupata futari

Tuesday, June 6, 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA ;SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MIFUMO YA ELIMU KWA WATU WOTE

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vifaa vya kufundishia kwa watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko Ilala jijini Dar es Salaam.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri mkuu wa Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imejipanga kuboresha Elimu nchini kwa kuongeza bajeti ikiwemo ununuzi wa vifaa na walimu katika shule zenye mahitaji maalum.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua na kukabidhi vifaa vya elimu vya kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini vyenye thamani ya bilioni sita kutoka shirika la Global Partner ship.

“Vifaa hivi vitakwenda katika mikoa yote 26 nchini kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo itanufaisha shule za Msingi 213 kati ya shule 408 na sekondari 22 kati ya shule 43 zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum” amesema Waziri Mkuu Majaliwa .

Amesema kuwa pia serikali imenunua vifaa vya kufundishia kwa walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum ikiwa ni kielelezo cha kutimiza ahadi za Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata elimu bila ya kujali mapungufu yake.

Amesema mapungufu ya kimwili kiakili sio mwisho wa kufikia malengo kwa watoto wetu kwani bado wapo watumishi serikalini ambao wanamahitaji maalum na bado wanafanya vizuri katika kazi zao.

Waziri mkuu Majaliwa amesema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya walimu na kutoa mafunzo ya kitaaluma hili waweze kuendana na mabadiliko ya mitaala nchini.

Wizara iakikishe inasimamia na kuwachukulia hatua  wazazi wote ambao wanaficha watoto wenye mahitaji maalumu na kushindwa kwenda shule na kumuagiza waziri wa tamisemi atoe waraka katika Halmashauri ziweze kuwahudumia watotoambao wapo kwenye shule za kawaida hili waweze kupatiwa vifaa.

Ametoa wito kwa watoto Wazazi na walimu kuwa na nidhamu ya hali ya juu hili kuleta umaana  wa vifaa hivi.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wengine waandamizi wa serikali na wawakilishi wa mashirika yaliyofafadhili vifaa hivyo wakikata utempe kuashiria uzinduzi wa vifaa vya watoto wenye mahitaji Maalum
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia namna vifaa hivyo vinavyofanya kazi kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko
 Waziri Mkuu Kassim majaliwa akipunga mkono kuwasalimia watu waliofika katika shrehe hizo za uzinduzi wa vifaa vya kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalum.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akitoa Salaam za Mkoa wa Dar es Salaam akimwakilisha RC .Paul Makonda katika hafla hiyo ya uzinduzi wa vifa avya kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
 Waziri Mkuu Kassim majaliwa akisalimiana na Naibu Meya wa Ilala , Omary Kumbilamotowakati akiwasili katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko
 Waziri Mkuu Kassim majaliwa akisalimiana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam ,Saad Kusirawe wakati akiwasili katika shule ya Msingi uhuru Mchanganyiko
 Wanafunzi wa shule ya Msingi umoja wakitoa burudani ya Makirikiri
 Wanafunzi wa uhuru Mchanganyiko wakitoa burudani mbele ya waziri mkuuu

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...