Saturday, June 17, 2017

HAKI ZA WATOTO INATAKIWA KUTEKELEZWA KATIKA KUJENGA TAIFA LENYE FURAHANa Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika amesema jamii inatakiwa kutekeleza haki za watoto katika kujenga taifa lenye furaha.

Lalika ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika  iliyoadhimimisha katika viwanja vya shule ya Msingi Mwanambaya wilayani Mkuranga mkoani Pwani, amesema kuna changamoto ya mimba katika wilaya na kufanya watoto wa kike wakose haki ya kupata elimu.

Amesema suala la mimba halitaweza kuvumilika kutokana na  kukosesha watoto wa kike kukosa elimu huku wazazi kushiriki vitendo hivyo kulipwa fedha na wale waliowapa ujauzito.

Dk. Lalika Amesema watoto wenye mahitaji maalumu wanatakiwa kuwa na miundombinu ya elimu rafiki kwani watoto wote ni sawa.
 Amesema watoto wanatakiwa kupewa ulinzi, pamoja na kupewa fursa sawa kwa mtoto wa kiume na kike na kuachana tamaduni za kutoa fursa ya elimu kwa mtoto wa kiume.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mtoto wa Afrika ni Maendeleo Endelevu 2030 Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa Watoto.
Kesi zote zinazohusiana na masuala ya mimba zisikilizwe katika mahakama za mwanzo kama kutokana na muongozo wa serikali kwa vyombo vinavyohusika kupeleka kesi hizo zianaze kusikilizwa kuanzia Juni 1.

Mtoto anatakiwa kufanya kazi zinazoendana na umri wake na sio za kumfanya mtoto atwete kutokana na kuwa Tanzania imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya umoja wa mataifa.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga, MhandisiMshamu Munde amesema  wazazi wametakiwa kuwa karibu na watoto kwa kila hatua kuwachia walimu  pekee yao hatuwezi kufika katika mtoto kuwa na elimu bora.

Munde amesema kuwa kwa michezo walionyesha ikiwemo Bunge la Watoto ni ishara kuwa walichosema ni kufanyia kazi.

Nae Afisa Maendeleo y Jamii Wilaya ya Mkuranga, Peter Nambuinga amesema wamepokea kesi kati ya kesi hizo zilisuluhishwa  na kesi 32 zilifikishwa mahakamani  na kupatiwa ufumbuzi.

Nambuinga amesema kesi za ubakaji na Ulawiti katika mwaka jana zilikuwa 12 ambazo zilishuhughulikiwa kwa wathumiwa kufikishwa mahakamani.

Mkuu wa Kitengo cha Dawati la jinsia na Watoto , Kulwa Kilongola Polisi wa Dawati la Jinsia,  amesema kuwa wazazi wa Mkuranga hawatoi ushirikiano pale polisi wanapotaka ushahidi wa jambo ambalo limetokea.

Katika maadhimisho ya siku Mtoto Afrika katika Wilaya ya Mkuranga wametoa msaada mbalimbali kwa watu  wenye mahitaji  maalumu ikiwemo kupatiwa watoto kadi huduma za Afya za (CHF) , Daftari, magodoro Baiskeli , mashuka.

Waliotoa msaada huo ni pamoja na Mke wa Mbunge wa Mkuranga, Mariam Ulega ambaye ametoa  vitu vyenye  thamani ya zaidi  ya sh. milioni moja.
Mariam amesema kuwa masuala yanayohusu watoto ni mengi hivyo yanahitaji ushirikiano katika kuanda taifa la leo la watoto.

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalila akizungumza katika siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

 .Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza katika siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
  Mke wa Mbunge  wa Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza katika siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika akimto matone  ya Chanjo ya vitamin A katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,  Steven Mwandambo akitoa maelezo juu chanjo vitamin A kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika  katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika akimkabidhi baiskeli mtoto mwenye Ulemavu , Kibibi Khamis katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika akimkabidhi  Godoro  mtoto mwenye Ualubino,Nasma Ally  katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 ehemu ya watoto wakiwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
MBUNGE WA KIBAHA MJINI KOKA, AIKABIDHI SERIKALI VIFAA VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH.MILIONI 400

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa tano kushoto) akipokea karatasi yenye orodha ya Vifaa vya kutolea huduma za Afya kutoka kwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kushoto kwake) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 400 iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya Mkoani, mjini Kibaha, leo mchana. Kulia kwa Waziri ni MKuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama.  
Makabidhiano yakiendelea......
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akikagua sehemu ya vifaa hivyo wakati akikabidhiwa na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kulia kwake).
Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya, iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mjini, Asumta Mshama.
**************************************************
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Koka, alisema kuwa alifanikiwa kupata msaada wa vifaa hivyo kutoka kwa rafiki zake waishio nchini Marekani, wakati alipokwenda katika shughuli zake za kibiashara, ambapo walimhakikishia kupata vifaa hivyo kwa kuchangia gharama za usafirishaji hadi kuingia nchini.

Baada ya uhakika huo Koke alitumia gharama zake kuwasafirisha baadhi ya wataalamu (Wazungu) kutoka nchini Marekani na kuja nchini hadi Mji wa Kibaha kwa lengo la kukagua na kujiridhisha juu ya uhitaji wa vifaa hivyo vya kutolea huduma za afya, ambapo alitumia jumla ya Sh. milioni 12.

Aidha alisema kuwa vifaa hivyo vilichelewa kutokana na uhitaji kutoka mataifa mengine yaliyokuwa yakipata matatizo na magonjwa ya mlipuko, na hivyo kampuni hiyo ya Project Cure, kulazimika kughairisha kusafirisha kuja nchini na kutoa kipaumbele kwa mataifa hayo yaliyokuwa yakipata matatizo kwanza.

Mbali na Mbunge kuchangia kiasi cha Sh. milioni 12, pia Halmashauri ya Mji wa Kibaha pia ilichangia kiasi cha Sh milioni 32, zilizosaidia kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchini Marekani hadi kuwasili nchini. Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa hii leo vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 400.
Sehemu ya vifaa hivyo.......
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka, wakitoka kutembelea katika Wodi ya Wazazi, katika Kituo cha Afya Mkoani, leo mchana wakati alipofika kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya vyenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 400. 
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Chumba cha Maabala cha Kituo cha Afya Mkoani, Farida Chagulaga, wakati waziri huyo alipotembelea chumba hicho na kukagua taratibu za ufanyaji kazi, alipofika kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kutolea huduma za afya.
Naibu  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Chumba cha Maabala cha Kituo cha Afya Mkoani, Farida Chagulaga, wakati waziri huyo alipotembelea chumba hicho na kukagua taratibu za ufanyaji kazi, alipofika kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kutolea huduma za afya.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa pili kushoto) Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kushoto kwake) Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama (kushoto) wakikabidhi karatasi ya orodha ya vifaa vya kuhudumia wagonjwa kwa Madaktari wa Kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha, wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 400.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa tatu kulia) Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kulia kwake) Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama (wa pili kulia) na baadhi ya waganga wa Kituo cha Afya cha Mkoani Kibaha, wakikagua badhi ya Vitanda vya wagonjwa, baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya kutolea huduma kwa wagonjwa vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 400. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Kituo cha Afya Mkoani, mjini Kibaha.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiimba wimbo maalumu kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya Asumta Mshama (kulia), Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, alipokuwa akizungumza na wananchi wa mji wa Kibaha, Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Mkoani (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Vifaa vya kutolea huduma za afya kituoni hapo
Dkt. Kigwangala, akizungumza wakati wa hafla hiyo.....
Baadhi ya wananchi wakimsangilia mgeni rasmi wakati akitoa hotuba yake katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa mji wa Kibaha baada ya hafla hiyo. 
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na baadhi ya wanachi waliohudhuria hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na baadhi ya wanachi waliohudhuria hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na baadhi ya wanachi waliohudhuria hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na Diwani Selina.
Wasanii wa Kikundi cha Malaika Dance, cha Kibaha wakitoa burudani katika hafla hiyo

DC MJEMA AWAONYA WALE WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI MBONDOLE

Mkuu wa  Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na Waandishi wa Habari na kuwatahadharisha wale wote ambao wamekua wakichochea migogoro ya Ardhi katika Mtaa wa Mbondole kwa Muhaya eneo kata ya Msongola jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya amesema atawachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotoa taharifa za uongo kuwa hukumu ya kubomolewa eneo hilo limetoka hivyo watu hao wanatakiwa waondoke wakati hukumu hiyo inataraji kutoka tarehe 28 June 2017.

 aidha ametoa wito kwa wakazi wa Mbondole kuwa wapole na kuacha kufata maneno ya Matapeli ambao wamekuwa wakiwadanganya kuwa eneo hilo hukumu imetoka na kutaja kuwa mtu anayewatisha wanatakiwa wamwambie awaonyeshe hukumu iliyo tayari hivyo kama ana hukumu wamlete ofisini kwake hili  taratibu za kisheria zifuatwe.


Sehemu ya mji Mbondole  kwa Muhaya ambayo mtu mmoja amejitokeza na kusema eneo hilo lake na kuwadanganya kuwa hukumu ya mahakama imetoka hivyo wanatakiwa waondoke
Wananchi wa Mbondole wakiwa wameshika mabango na kuandamana kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa  hukumu ya kubomolewa imetoka

Wakazi wa Mbondole wakiwa wameshika bango kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa  hukumu ya kubomolewa imetoka  mahakamni hivyo waondoke eneo hilo
Sehemu ya Wananchi wa Mbondole ambao walikusanyika na kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa  hukumu ya kubomolewa imetoka  mahakamani  hili waondoke katika eneo hilo

AZANIA BENKI YAPATA FUTARI PAMOJA NA WATEJA WAKE

 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Azania ,Charles  Itembe akizungumza na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Aznia Benki Mawasiliano Tower.
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Azania ,Charles  Itembe, akisalimiana na watoto wa kituo cha Yatima cha Vingunguti wakati wa wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Aznia Benki Mawasiliano Tower.
 Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara Benki ya Azania , Othman Jibrea akiwa katika picha ya pamooja na baadhi ya Watoto wa Kituo cha watoto yatima kutoka Vingunguti
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akipakua futari katika futru iliyoandaliwa na benki ya Azania.
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Azania ,Charles  Itembe, akiwa na wateja wa benki hiyo
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akipata futari iliyoandaliwa na benki ya Azania
 Sehemu ya wateja wa beni hiyo wakichukua futari
 Sehemu ya wateja wa benki hiyo wakipata futari na wafanyakazi wa benki ya Azania
 Watoto wa kituo cha Watoto Yatima Vingunguti wakipata futari  wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Aznia Benki Mawasiliano Tower.
 Wafanyakazi wa benki ya Azania wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Aznia Benki Mawasiliano Tower.
baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki ya Azania wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Aznia Benki Mawasiliano Tower.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...