Friday, July 28, 2017

KIWANDA CHA NONDO CHA UNIQUE STEEL CHAJIPANGA KATIKA KATIKA UWEKZAJI KUHUDUMIA BOMBA LA MAFUTA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kiwanda cha uzalishaji wa nondo cha 
Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga kimesema kimejipanga kufanya uwekzaji mkubwa hili kuweza kutumia fursa ya uwepo wa ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Tanga mpka Uganda kutumia malighafi kutoka kiwandani hapo.

Hayo yamesemwa na Mhasibu Mkuu wa kiwanda hicho, Sikander Omar  alipokuwa  akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho Jijini Tanga.

 Omar amesema kuwa Wakati Serikali ikipambana kuhakikisha viwanda vinakua nchini, baadhi ya viwanda vilivyopo vimekuwa vikikumbana na changamoto mbalimbali zinazozuia uzalishaji kwa wakati.

"Moja ya changamoto hizo ni kukatika katika kwa umeme bila taarifa jambo linalotia hasara wakati wa uzalishaji. 
Mbali na hilo patikanaji wa mikopo kwa ajili ya kuwekeza zaidi imekuwa ni changamoto kwaoanapambana kukiboresha kiwanda hicho lakini umeme kutokuwa wa uhakika imekuwa changamoto".Amesema Omar.

Amesema kwa sasa wanazalisha hadi tani 60 za nondo ambazo nyingi huuzwa mkoa wa Arusha.
Akizungumzia changamoto zilizopo msimamizi wa kiwanda hicho, Jagjeet Singh alisema umeme unapokatika wakati wa uzalishaji inakuwa ni hasara kwao kwa kuwa mtambo wa kuyeyusha chuma hupoa na vyuma vilivyokuwa vinayeyuka ili kutoa nondo huganda.

 Kiwanda hicho ambacho kilikuwa cha Serikali na kuzinduliwa Julai 21, 1971 kilisimama na kuanza uzalishaji tena hivi karibuni baada ya kuchukuliwa na mwekezaji huyo.

Omar amesema hivi sasa wako katika mchakato wa kutafuta mkopo ili kukiongezea nguvu kiweze kuzalisha zaidi na kutoa huduma katika mikoa zaidi ya Tanga na Arusha ambalo ndilo soko kubwa lao lilipo kwa sasa.

 

 
 Mhasibu Mkuu wa kiwanda cha Nondo cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga, Sikander Omar akizungumza na Wandishi wa Habari waliotembelea kiwanda chake kuanagalia hali ya uzalishaji
 Watendaji wa kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga wakiwaonyesha waaandishi wa habari sehemu ya kuzalishia Nondo ambayo imesimama kutokana na matatizo ya Umeme
 Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi Boniface Meena akiangalia moja ya Nondo zinazozalishwa na Kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga

PROF MAGEMBE AWATAHADHARISHA WATU WANAOINGIZA MIFUGO HIFADHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Magembe alipokuwa akizungumza na Wahariri na Wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika semina ya mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA kwa wanatasinia hiyo ya habari.

Mhariri Mtendaji kutoka kampuni ya New Habari (2006) wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, The African na Bingwa, Absalom Kibanda (kushoto) akiuliza swali kwenye semina hiyo. Wengine ni baadhi ya washiriki wa semina hiyo kwa wahariri na wanahabari waandamizi.

Na Joachim Mushi, Tanga
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Magembe amewaonya wananchi walio jirani na hifadhi za taifa kuacha mara moja kitendo cha kuchanganya mifungo na wanyamapori kwani kitendo hicho ni hatari kubwa kwa afya za wananchi na mifugo yao. Alisema wanyamapori wana magonjwa mbalimbali na hatari kwa afya zetu hivyo kitendo cha kuchanganya mifugo na wanyamapori huamisha magonjwa kutoka huko na kuingia kwa wananchi wanapokula nyama.
Waziri huyo mwenye dhamana na Maliasili na Utalii alitoa onyo hilo jana jijini Mbea alipokuwa akifungua Mkutano na Semina ya mwaka kwa wahariri na wanahabari waandamizi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA). Alisema kitendo cha wafugaji kuchanganya wanyamapori na mifugo ni changamoto nyingine kubwa, hivyo kuwaomba waandishi wa habari kupitia vyombo vyao kutoa elimu kwa wafugaji. Alisema wanyamapori huwa na magonjwa mengine ambao kwao hayana madhara makubwa lakini yanapoingia kwa mwanadamu huhatarisha maisha yake kiafya.
"...Wananchi kuingiza mifugo yao mbugani hili ni tatizo kubwa, tunaomba mtusaidie...kwanza sheria zetu haziruhusu kabisa suala hili. Tusichanganye mifugo na wanyamapori hii ni hatari tunaweza kubeba magonjwa kule na yakawa na madhara makubwa kwetu...kuna magonjwa kama kimeta, TB na homa za vipindi ambazo zipo kwa wanyamapori zikija kwetu hizi ni hatari," alisisitiza Profesa Magembe.
Hata hivyo, Waziri Magembe alipongeza juhudi zinazofanywa na wanahabari kupitia vyombo vyao kwani wamekuwa msaada mkubwa kutoa elimu ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa matokeo ya wanahabari kutumia kalamu zao kutangaza utalii yanajionesha wazi kwa ongezeko la idadi ya watalii kutoka nchi mbalimbali kutembelea hifadhi zetu.
Aidha ameitaka TANAPA kuendelea kushirikiana na wanahabari kwa kufanya semina hizo kila mwaka ili kupata mrejesho juu ya kazi wanayoifanya, kwani vyombo vya habari ni fursa nzuri ya kutoa elimu kwa umma na kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo. Mkutano huo wa siku tatu ulioanza leo Julai 26 unatarajia kumalizika Julai 29, ambapo wanahabari watajifunza na kujadiliana masuala mbalimbali ya utalii na uhifadhi.
Idadi kubwa ya watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani bado wanamiminika kuja nchini Tanzania kutembelea vivutio anuai vya utalii. Alisema hali hiyo imebainika baada ya ziara aliyoifanya kutembelea hoteli mbalimbali za kitalii na kujionea namna zinavyopokea watalii mfululizo, huku baadhi zikiwa zimejaa na wateja kulazimika kuweka oda mapema kabla ya kuanza safari ya utalii.
"...Mimi nimetembelea kabla ya kuja hapa baadhi ya hoteli kwenye maeneo ya utalii kujionea, kweli hoteli baadhi zinawatalii wa kutosha kiasi kwamba zingine zimejaa...mteja ukienda bila ya kufanya 'booking' ya chumba huwezi kupata, hawana nafasi pia. Na watalii wanaokuja wanatoka kila upande, kimsingi ujio huo wa watalii kwa wingi ni mafanikio yenu wanahabari," alisema Waziri Prof. Magembe.
Alisema watu wa kupongezwa ni waandishi wa habari ambao kiasi kikubwa; ningekuwa na kofia hapa ningewavulia kwa heshima na kutambua mchango wenu kwa kazi hii," alisema.
Hata hivyo alisema bado suala la ujangili dhidi ya wanyamapori ni changamoto japokuwa kwa sehemu kubwa kuna tunaweza kujivunia mapambano na jitihada tulizozifanya kudhibiti hali hiyo. mabadiliko makndiyo wanaotumia kalamu zao kuutangazia utalii wetu.

sehemu ya washiriki wa Semina ya Wahariri na Wanahabari waandamizi kwa mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA.

sehemu ya washiriki wa Semina ya Wahariri na Wanahabari waandamizi kwa mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA. 

Mashindano ya Kigwangalla Cup 2017 yazinduliwa jimbo la Nzega vijijini

Mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za Kata zilizo ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini maalufu kama ‘Kigwangalla Cup’ yamezinduliwa rasmi jioni ya Julai 27, 2017 huku miamba 20 ikitarajiwa kuumana kumpata bingwa wa Jimbo hilo kwa mwaka huu.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliwataka wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo kuwa na nidhamu iliwaitumie michuano hiyo kama kipimo cha wao cha kuonesha vipaji vyao ili waonekane ngazi za juu.

“Mpambane kweli kweli. Kila mmoja wenu aoneshe uwezo wake wa kusakata kabumbu. Pia muzingatie nidhamu ya hali ya juu kwani michezo inaleta umoja na amani, inaimalisha afya ya miili yetu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akuzungumza na wachezaji katika ufunguzi wa michuano hiyo.

Dk. Kigwangalla pia alipata wasaha wa kukagua timu zilizofungua rasmi michuano hiyo kati ya Mizibaziba dhidi ya Nkiniziwa ambazo hadi kipyenga cha mwisho ziliweza kutoka droo ya bao 1-1. 
Dk. Kigwangalla alieleza kuwa, jumla ya Kata 19 za jimbo lake hilo zimeweza kutoa timu ilikushiriki michuano hiyo huku timu maalum ikiingizwa ambayo itajumuisha Madiwani wote kutoka Kata hizo ili kufanya jumla ya timu 20.

Dk. Kigwangalla alizitaja baadhi ya Kata zinazochuana kwenye michuano hiyo ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata, Sanzu,Lusu, Milambo Itobo, Magengati,Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi.
Kata zingine ni Kata za Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.

Awali kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo wa ufunguzi, Madiwani wa Kata zote waliweza kukabidhiwa baadhi ya vifaa kwa timu zao sambamba na hilo wananchi waliweza kufurahia michezo mbalimbali ikiwemo ile ya jadi hasa mchezo wa asili wa bao la Kinyamwezi, kucheza drafti, kukimbiza kuku, michezo ya mbio kwa Wazee huku mchezo wa mbio kwa watu wenye vitambi ukitia fola kwenye ufunguzi huo, uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Nkiniziwa iliyopo kwenye Kata hiyo ya Nkiniziwa.

Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wachezaji wa Kata ya Nkiniziwa wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
 Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na timu ya Kata ya Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
 Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wachezaji wa timu za Kata za Nkiniziwa na Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1. 

DC Babati awataka wakulima kuunga mkono jitihada za watafiti wa mbegu


Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi akizungumza na wakulima na watafiti wa Mradi wa utafiti mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA), katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati.

Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kulia) juu ya shamba la majaribio ya mbegu chotara za mahindi zinazostahimili magonjwa na ukame (WEMA), katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea.

Mtafiti wa Mradi wa WEMA, Ismail Ngolinda (kulia) akimtembeza mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kushoto) ndani ya shamba la majaribio katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi akitembelea shamba la majaribio ya mbegu chotara za mahindi zinazostahimili magonjwa na ukame (WEMA), katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea.


Mtafiti wa Mradi wa WEMA, Ismail Ngolinda (kwa kwanza kulia) akijibu maswali ya baadhi ya wakulima ndani ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea.

Mahindi ndani ya shamba la utafiti shirikishi na wakulima la Mradi wa WEMA lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati.

Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano na uratibu Mradi wa WEMA, Bw. Temu akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo akijibu maswali ya wakulima (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea shamba la utafiti shirikishi wa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA).

Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati, Cade Mshamu (wa pili kulia) akizungumza na wakulima na watafiti wa Mradi wa utafiti mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA), katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati.

Baadhi ya wakulima na wageni anuai wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati.

Mkulima akiuliza swali kwa watafiti katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Maendeleo ya Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Jackson Nkuba (kulia) kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabaan Husein (kulia) akizungumza kwenye hafla hiyo.

Na Joachim Mushi, Babati
MKUU wa Wilaya ya Babati, Raimond Mushi amewataka wakulima kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo wakiwemo watafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame, magonjwa (WEMA) ili waweze kuendesha kilimo chenye tija na kuachana na kilimo cha kujikimu ambacho hakiwezi kuwapa maendeleo.
Alisema kilimo cha sasa kinapaswa kuendeshwa kisayansi na kufuata ushauri wa kitaalamu, ambapo ni pamoja na kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti kulingana na mahitaji ya maeneo ya wakulima. Mh. Mushi ametoa ushauri huo mjini Babati alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima wilayani Babati ambapo pia alitembelea shamba la utafiti shirikishi wa mbegu za mahindi unaotekelezwa na watafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA).
Alisema wakulima wakitaka kufanya kilimo cha manufaa hawana budi kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti na kupendekezwa na wataalamu wa kilimo kutumika katika maeneo yao. "...Tuwe macho na mbegu tunazonunua ili tuweze kuvuna mazao ya kutosha, wakulima sasa lazima tubadilike tusiendeshe kilimo cha kujikimu tu...mkulima huwezi kuendelea kwa kufanya kilimo cha kujikimu, tunataka ulime upate chakula na ziada kisha uuze mazao kukuza uchumi wako na ubaki na akiba," alisema Raimond Mushi.
Alisema serikali ya awamu ya nne imedhamiria kufanya uchumi wa viwanda hivyo wakulima wanakila sababu ya kufanyia kazi ushauri wa wataalamu wa kilimo ili waweze kuzalisha mazao ya kutosha yatakayotumika kama mazao ghafi kwenye viwanda na kunufaika zaidi.
"Tunapolima sasa tulime kisayansi na kwa malengo, tutumie maeneo yetu vizuri ili tuweze kuzalisha mazao ya kutosha," alisisitiza Mkuu wa Wilaya, Raimond Mushi na kuongeza eneo la kilimo kwa sasa linapungua kutokana na ongezeko la idadi ya watu nchini hivyo kuna kila sababu ya kutumia eneo dogo linaloleta matokeo makubwa na manufaa kwa mkulima.
Alisema serikali imedhamiria kuleta mabadiliko kwa wakulima ndio maana inawawezesha wataalamu kama WEMA na kuwaunga mkono shughuli za utafiti kwa maendeleo ya wananchi hawa wakulima. "Sisi hapa Babati tunangoja kwa hamu matokeo ya utafiti ili tuweze kuyafanyia kazi...tuleteeni mapema tutasimamia na kuhamasisha wakulima wetu kutumia mbegu za WEMA," alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Maendeleo ya Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Jackson Nkuba alisema Serikali ipo tayari kushirikiana na makampuni yatakayojitokeza kuzalisha mbegu za WEMA na zingine bora zinazofanyiwa utafiti ili wakulima wazipate kirahisi, hivyo kutoa rai kujitokeza kwa wingi.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Babati, Bw. Mushi, viongozi mbalimbali katika tukio hilo wakiwemo wakulima kwa pamoja walitembelea shamba la utafiti shirikishi wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA) lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini na kujionea mbegu zilizofanyiwa utafiti wa WEMA na kujionea matokeo ya utafiti.

WANAWAKE WAONGOZA KATIKA BIASHARA YA SAMAKI PWANI YA TANGA

 Wachuuzi wa Samaki  wakiwa wanaelekea ndani ya Maji kwa ajili ya kununua Samaki maharufu kma Uono ambao wanapendwa sana katika mji wa Tanga kwa ajili ya kulia Ugali na kutafuna wakati wa chai asubuhi

 Wachuuzi wa Samaki wakiwania Samaki katika moja ya jahazi lililoingia na mzigo kutoka  katika kina kirefu mara baada ya kusubiri muda mrefu
 Mchuuzi wa Samaki akingi katika maji kwa ajili ya kununua Samaki katika Majahazi yaliyofika katika ufukwe wa Sahare
 Mchuuzi wa Samaki akingi katika maji kwa ajili ya kununua Samaki katika Majahazi yaliyofika katika ufukwe wa Sahare
 Wavuvi wakiondoka kwenda kuvua mapema leo Asubuhi katika pwani ya Jiji La Tanga
 Mchuuzi wa Samaki akingi katika maji kwa ajili ya kununua Samaki katika Majahazi yaliyofika katika ufukwe wa Sahare
 Mkazi wa Jiji la Tanga akichagua Samaki kutoka wauzaji wa soko la Sahare jijini TangaThursday, July 27, 2017

WANAHABARI WAJADILI UMUHIMU WA UHIFADHI NA UJIRANI MWEMA JIJINI TANGA

 Mkurugenzi wa Utalii na Masoko  kutoka Hifadhi za Taifa Tanzania, Ibrahim  Mussa akizungumza wakati wa Mjadala juu ya uhifadhi na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari Waandamizi katika mkutano wa Mwaka wa TANAPA.
 Katibu wa Jukwaa la Wahariri , Neville Meena  akinyosha Mkono kwa ajili ya kuhitaji kuchangia juu ya nini kifanyike hili Waandishi wa habari waweze kuripoti habari za utalii wa hapa nchini katika nyanja ya kimataifa.
 Mwenyekiti wa MisaTan , Salome Kitomari  akichangia jambo katika mkutano wa Mwaka wa Wahariri na wanahabari waandamizi katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Jiji la Tanga
 Ofisa anaeshughulikia masuala ya Ujirani mwema kutoka TANAPA, Ibrahim Ninga akitoa somo kwa Wanahabari nini Mamlaka yake imefanya katika kuakikisha hakuna migogoro baina ya hifadhi na Majirani
 Mhariri wa gazeti la Jamhuri ,Jackton Manyerere akichangia juu ya umuhimu wa wadau wa utalii sasa kutumia mkoa wa mara ambao upo jirani na Hifadhi ya serengeti utumike kama kituo cha kupokelea Watalii kuliko Arusha hivi sasa
 Mdau Lilian Timbuka na Sara Kibonde wakaijadili jambo mara baada ya kukutana kwenye mkutano wa Wahariri na waandishi wa waandamizi

 Mrataibu wa mradi Misitu ya Hifadhi ya Mazingira  Asilia Tanzania, Gerald Kamwenda akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) ,Prof Dos Santos Silayowakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wahariri na Waandishi Waandamizi Jijini Tanga ulioandaliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA)
Washiriki wengine wakifatilia mkutano huo kwa makini

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...