Saturday, August 5, 2017

AfDB YASISITIZA WELEDI KWA WANAFUNZI WANAOFADHILIWA NA BENKI HIYO CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA

Benny Mwaipaja-WFM, Arusha

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, amewataka wanafunzi 45 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia, wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia kilichoko mkoani Arusha, kusoma kwa bidii na maarifa ili waweze kuzisaidia nchi zao kuinua sekta ya viwanda kwa njia ya utafiti na ubunifu wa teknolojia mbalimbali

Dkt. Weggoro ametoa rai hiyo alipotembelea Chuoni hapo ili kuangalia utekelezaji wa programu ya miaka mitano ya kuboresha masuala ya rasilimali watu inayofadhiliwa na Benki yake kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 8.2

Alisema kuwa Benki yake imeamua kuwekeza fedha nyingi katika eneo la Sekta ya elimu ya juu katika nyanja ya ufundi ili kuwapata vijana wa kutosha watakaoziba pengo lililopo na kuweka misingi mizuri ya maendeleo ya baadae hasa katika matumizi ya teknolojia na sayansi.

 “Nimefurahi sana kuona wanafunzi wanasoma na wana ari kubwa na kwamba fedha tulizozitoa zinatumika vizuri, tunadhani hata baada ya mradi huu wa  miaka 5 kukamilika, Benki itaweza kusaidia zaidi ufadhili wa fedha na vifaa” Alisema Dkt. Weggoro.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Joram Buza, ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kwa ufadhili huo, hatua iliyoongeza udahili wa wanafunzi katika chuo hicho.

“Mwaka wa masomo wa 2014/2015, Chuo kilidahili wanafunzi 7 pekee kutokana na changamoto wafadhili lakini baada ya ufadhili wa AfDB na Benki ya Dunia, wanafunzi wameongezeka hadi kufikia 135 jambo linalotia matumaini” alisema Pro. Buza.

Bi. Mwanaisha Mkangara na Bw. Alexander Mzura, wanaosomea shahada ya uzamivu katika masuala ya uhandisi na mifugo, kupitia ufadhili wa AfDB, wamesema kuwa masomo yao yatawaongezea ujuzi wa namna ya kufanya utafiti wa kihandisi na kuvumbua chanjo mbalimbali za mifugo.

AfDB inafadhili wanafunzi 45 ambapo 42 kati yao wanatoka Tanzania, huku Uganda, Kenya na Ethipia zikitoa mwanafunzi mmoja mmoja. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro akizungumza kuhusu umuhimu wa vijana wenye weledi wa kitaaluma katika kukuza uchumi, alipokutana na wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha (hawapo pichani) wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia) akiwa na Mkutano na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza, alipotembelea chuo hicho kuangalia mradi wa kuwafadhili wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake.


 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) alipotembelea Chuo hicho, ambapo aliwasisitiza kusoma kwa bidii ili kuhimili ushindani katika soko la ajira.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia), na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza wakizungumza jambo baada ya kumalizika kwa mkutano na wanafunzi wa chuo hicho wanaofadhiliwa na AfDB.
 Afisa wa Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia Dawati la AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge (kulia) na Meneja wa Mradi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wa ufadhili wa wanafunzi katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Arusha, Bw. Julius Lenguyana (kushoto), wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu ufadhili wa AfDB katika mradi wa miaka 5 kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.
 Meneja wa Mradi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha, Julius Lenguyana (kulia) akimuongoza Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) alipowasili chuoni hapo kuangalia utekelezaji wa mradi wa ufadhili wa wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake kwa miaka mitano katika Chuo hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (mbele wa pili kushoto),  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza (kulia kwake), Mshauri wa Mkurugenzi huyo Bw. Amos Kipronoh Cheptoo (kushoto kwake) na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia Dawati la AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na  wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA UGANDA MPAKA BANDARI YA TANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pongezi na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Chongoleani kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma ya msanja na Mama Janeth Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja vya Chongoleani kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.
 Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza kuhutubia katika  sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania ambapo aliwaahidi Rais Magufuli na Rais Museveni kuwa wataulinda mradi huo kwa faida ya nchi hivi mbili na Afika Mashariki kwa Ujumla.

 Baadhi ya wananchi wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la  kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja vya Chongoleani kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakielekea kuweka jiwe hilo la msingi.

Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali mara baada ya kutumbuiza.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akihutubia katika viwanja vya Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga. PICHA NA IKULUR

UN YAZUNGUMZA NA VIJANA WA TEMEKE KUHUSU MALENGO YA MILENIA Ofisa kutoka Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa Tanzania ,Didi Nafisa akizungumza na Vijana wa Mtandao wa Vijana Temeke(TEYODEN), Juu ya Malengo ya Milenia kwa vijana na mambo yaliyopewa vipaumbele katika malengo hayo
 Katibu mkuu wa Mtandao wa Vijana Temeke(TEYODEN),Yusufu Kutegwa akizungumza juu ya namna Mtandao huo unavyofanya kazi kusaidia Vijana
 Baadhi ya Vijana walioshiriki Mkutano Huo wakisikiliza kinachozungumzwa kutoka kwa watoa mada
 Balozi wa Malengo ya Dunia kwa Vijana kutoka chuo cha Uhasibu Arusha ,Gloria Nassary akizungumza na Vijana wa Temeke juu ya Vipaumbele vitano vya Kibinadamu katika Malengo ya Milenia
  Balozi wa Malengo ya Dunia kwa Vijana kutoka chuo cha Mtakatifu Agustino ,Julius Kitingati akieleza namna Vijana wanavyoweza kufanikisha malengo hayo kwa Sera ya Viwanda hapa nchini

Sehemu ya Viana walioshiriki katika mkutano huo ulioandaliwa na TEYODEN  Kwa kushirikiana na umoja wa Mataifa

NMB YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 10 KUFANIKISHA TAMASHA LA USALAMA BARABARANI AGOSTI 12 MWAKA HUU

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema jijini Dar es Salaam juu ya Tamasha la Usalama barabarani linalotaraji kufanyika Agosti 12 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi mbalimbali ya Wasanii watu maharufu na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi na Mauzo ,Omary Mtiga  NMB imetoa Vifaa Vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya Kufanikisha Tamasha la Usalama Barabarani Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi na Mauzo ,Omary Mtiga  NMB imetoa Vifaa Vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya Kufanikisha Tamasha la Usalama Barabarani Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni Akipokea Fulana kutoka kwa Meneja Masoko wa Azam Omary Kuwe
 Meneja wa Mwanamuziki Mahiri wa Bongo Fleva Diamond Platnum, Salam Mendez akizungumza juu ya uwepo wa mwanamuziki huyo katika Tamasha la Usalama Barabarani la Twenzetu Taifa.
 Msanii Mkongwe wa Maigizo nchini , Suzan Lewis Mharufu kama Natasha akizungumza jambo juu ya masuala ya usalama barabarani kuelekea tamasha hilo agosti 12.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa  Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Kampuni ya Binslum ya hapa nchini Tanzania

Sehemu ya Wanahabari na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakifatilia mkutano huo kwa makini juu ya Tamasha la Twenzetu Tifa katika masuala ya usalama barabarani

ZOLA WAZINDIUA DUKA LAO JINGINE JIJINI DAR ES SALAAM

 .  Akizungumza wakati uzinduzi wa Duka hilo Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea ametoa wito kwa Taasisi za Serikali ambazo hazina huduma za umeme hasa vijijini kushirikiana nao ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa kwenye vituo vya afya ili kuwasaidia wagojwa pamoja na kinamama wajawazito.
  
Amesema kuwa kampuni hiyo inayotoa umeme wa ZOLA hapa nchini imeshatoa huduma hiyo kwenye vituo vya Polisi pamoja na vituo vya huduma za afya na umeme upo vizuri.

Hata hivyo amesema kuwa utakapo nunua  mtambo wa umeme wa ZOLA  utatengenezewa mfumo wa umeme katika nyumba yako kwa bei nafuu na wengine kwani huduma zao zinalingana na maisha ya Mtanzania.

Amesema kuwa umeme wa ZOLA unaweza kutumika katika vifaa mbalimbali kama kuchaji simu, mashine za kunyolea, televisheni pamoja na kuwasha taa sita za ndani.  
Pia ukinunua vifaa vya ZOLA utapata dhamana(Warrant) ya miaka mitano endapo kifaa chochote kitaharibika mteja utatengenezewa bila gharama yeyote ile. 
Katikati ni Meneja Masoko  wa ZOLA Tanzania, Irene Mbowe akikata utepe kuzindua Duka linalouza  na kutoa huduma za ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Mkuu wa kitengo cha mauzo wa ZOLA, John Amach na Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea wakishrikiana kukata utepe kuzindua duka hilo.
 Duka la ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko  wa ZOLA Tanzania, Irene Mbowe akipata maelekezo na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimealeo katika uzinduzi wa Duka jipya ambalo linatoa huduma mbalimbali za umeme wa ZOLA jijini Dar es Salaam leo.
 Mfanyakazi wa kampuni inayotoa huduma ya umeme wa ZOLA akitoa maelekezo kwa baadhi ya wateja waliofika dukani hapo Mwenge  jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzindu wa duka hilo.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Steve Kimea wa ZOLA akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya uzinduzi wa duka hilo ambalo watakuwa wanatoa huduma pamoja na kuuza vifaa mbalimbali vitakavyotumika kupata umeme wa ZOLA.

Friday, August 4, 2017

MAOMBI YA DHAMANA YA MANJI KUSIKILIZWA AGOSTI 7

Mfanyabiashara Yusuf Manji akirudishwa mahabusu baada ya kesi yake ya maombi ya dhamana kuahirishwa hadi Agosti 7mwaka huu.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Leo imeahirisha kesi maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na   Mfanyabiashara maarufu Tanzania Y usuf Manji, hadi Agosti 7 mwaka huu kwa kuwa Jaji Isaya Arufani anayesikiliza kesi hiyo anaudhuru.

Kesi hiyo imeahirishwa na  Msajili wa Mahakama kuu, Siani..
Hata hivyo kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, upande wa Mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Paul Kadushi akisaidiana na Simon wankyo wamesilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu.
Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana, na kwamba upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ya dhamana kwa kutumia vifungu ambayo siyo sahihi kisheria na pia viapo walivyo viwasilisha vina dosari kisheria.
Hata hivyo, kwa kuwa Jaji husika anayesikiliza kesi hiyo hayupo, kesi hiyo itakuwa tena Agosti 7 (Jumatatu).

Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Julai 5 mwaka huu aliposomewa Mashtaka ya uhujumu uchumi.

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Farces Salaam Leo imeahirisha kesi maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na   Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji, hadi Agosti 7 mwaka huu kwa kuwa Maji Isaya Arufani anayesikiliza kesi hiyo anaudhuru.
Kesi hiyo imeahirishwa mbelw ya Msajili wa Mahakama kuu, Siani.
Hata hivyo kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, upande wa Mashtaka ukiongizwa na Wakili wa Serikali Paul Kadushi akisaidiana na Simon wankyo wamesilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu.
Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana, na kwamba upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ya dhamana kwa kutumia vifungu ambayo siyo sahihi kisheria na pia viapo walivyo viwasilisha vina dosari kisheria.
Hata hivyo, kwa kuwa Jaji husika anayesikiliza kwai hiyo hayupo, kesi hiyo itakuwa tena Agosti 7 (Jumatatu).

Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurgenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa hati ya maombi hayo, Manji anadai kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo  na kwamba ameambatanisha vyeti vya daktari katika maombi yake.

Katika kesi ya msingi,  Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri ya mbalimbali ya JWTZ isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.

Mbali na Manji, washtakiwa wengine ni,  Ofisa Rasilimaliwatu Deogratias Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo msaidizi, Thobias Fwele (43)

MSIGWA ATOA SOMO LA KUTAMBUA KUTAMBUA BIDHAA FEKI ZA NISHATI JADIDIFU NCHINI


WANANCHI WAHIMIZWA KUTUNZA FEDHA NA KUTAMBUA ALAMA ZA USALAMA


Makamanda wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Lindi wamewataka wananchi kutunza vizuri fedha zao ili kupunguza uharibifu unaoliongezea taifa gharama za kutengeneza fedha zingine.
Aidha, viongozi hao wameelezea umuhimu wa wananchi kutambua alama za usalama wa noti zetu ili kuepuka kuangukia mikononi mwa matapeli na kupata hasara.

Viongozi hao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, SACP Renatha Mzinga, Mkuu wa Magereza wa Mkoa, Bw. R. Nyange, na Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Mkoa wa Lindi, Bw. Nsiima Wema walisema hayo baada ya kutembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika maonesho ya Wakulima kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi.

RPC Mzinga alisema taifa linaingia hasara kubwa kutengeneza noti zinazotokana na uharibifu unaofanywa mara kwa mara na wananchi.

“Mimi nilikuwa najua pesa chafu zinarudishwa Benki Kuu na kufanyiwa recycling na kurudishwa kwenye mzunguko; kumbe tunapata hasara. Kwa elimu hii niliyoipata, nawashauri wananchi kwa ujumla watunze fedha zetu, kwa sababu zinapoharibika ni hasara kwa taifa,”alisema RPC Mzinga.
Mkuu wa Usalama wa Taifa mkoani Lindi, Bw. Wema alieleza kwamba amefurahishwa sana kwa kupata elimu kuhusu alama za usalama za noti zetu na kuahidi kutumia elimu hiyo kuwafundisha wengine.

“Kikubwa zaidi kilichonivutia ni namna ya kutambua pesa halali na pesa zisizo halali. Kwa ajili ya kukosa uelewa wananchi wengi wanalizwa kila siku kwa kupewa pesa zisizo halali kwa kuwa hawajui kuzitambua. Elimu niliyoipata itanisaidia niwaambie na wenzangu mtaani kwamba pesa halali iko hivi na isiyo halali iko hivi,” alisema Bw. Wema.

Mkuu wa Magereza wa Mkoa, Bw. Nyange, aliwashauri wananchi wanapofikia umri wa kustaafu wajiepushe kuwekeza katika biashara wasizozijua ili kuepuka hasara na badala yake wawekeze katika dhamana za serikali zinazotoa faida ya uhakika bila wasiwasi wowote wa kuingia hasara.

“Watu wanapostaafu mara nyingi wanajiingiza kwenye miradi mbalimbali…ambayo hawana ujuzi nayo; hawajui hata hasara zake, ili mradi wanaona mtu fulani ana biashara ya magari, ana mabasi, basi naye anajiingiza huko matokeo yake anapata hasara au mwingine anajiingiza kwenye mashamba na wakati mwingine jua mwaka huo linakuwa kali, moja kwa moja mazao yanakufa, inafikia hatua mtu anaweza hata kujiua…kumbe fedha ile unaweza ukawekeza kwenye dhamana za serikali, ukaendelea kupata faida na pesa yako ikabaki kuwa salama,” alisema.

Viongozi hao wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoani Lindi walitumia takriban saa nzima wakipata elimu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Benki Kuu na jinsi zinavyoendana na Kauli Mbio ya Maonesho ya Wakulima ya mwaka huu isemayo: Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati.

Maonesho ya Nane Nane kitaifa mwaka huu yalifunguliwa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Bw. George Simbachawene tarehe 1 Agosti, 2017, ambaye pamoja na mambo mengine aliwataka wakulima, wafugaji na wavuvi kuongeza tija kwa kuzalisha mazao na bidhaa kwa njia za kisasa.
Waziri Simbachawene alihimiza kilimo na ufugaji wa kisasa na kuwataka wavuvi kuanzisha ufugaji wa kisasa kwa kujenga mabwawa badala ya kutegemea mitego katika mito, maziwa na bahari, ambako hakuna uhakika wowote wa kipato.Maonesho kama haya pia yanafanyika katika ngazi ya kanda katika kanda za Mashariki, Kati, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini.

SERIKALI YASISITIZA UHIFADHI SHIRIKISHI KATIKA HIFADHI ZA TAIFA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo makani amesema  jukumu la uhifadhi wa Maliasili za taifa sio la Serikali pekee kwakua Maliasili hizo ni urithi wa taifa na kila mwananchi anapaswa  kujua kuwa ana jukumu la kulinda urithi huo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Makani amesema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mshiri, Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa ajili kuona changamoto za uhifadhi na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi.

Alisema askari pekee na mitutu ya bunduki haitoshi kulinda maliasili hizo kutokana na ukubwa wa maeneo yaliyopo ukilinganisha na rasilimali zilizopo. "Rasilimali hizi zipo kwa faida ya kila mwananchi, tunawaomba muendelee kuiunga mkono Serikali katika kulinda Maliasili tulizonazo, tunahitaji kufanya uhifadhi shirikishi, utalii uimarike na nchi yetu ipate mapato zaidi tuweze kufikia uchumi wa kati", alisema Makani.

Akitaja miongoni mwa faida hizo, Makani alisema maliasili za misitu husaidia upatikanaji wa mvua, kuweka mazingira bora kwa ajili ya kilimo na upatikanaji wa hewa safi. Kwa upande wa faida za kiuchumi alisema sekta hiyo kupitia utalii inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimi 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

Kwa upande wao Wananchi wa kijiji hicho ambacho kinapakana na Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro waliiomba Serikali iwalegezee masharti waweze kuingia na waume zao pamoja na vijana wao wa kiume katika eneo la Nusu Maili lililopo ndani ya hifadhi hiyo waweze kusaidiana kazi ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni.

Akitoa ombi hilo mbele ya Mhandisi Makani, mkazi wa kijiji hicho, Theresia Mtui alisema wanawake wa vijiji jirani na hifadhi hiyo wanaruhusiwa kuingia ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni kavu lakini wanaume hawaruhusiwi.

Alisema wapo tayari kuhifadhi na kulinda mlima huo “Tunaomba mturuhusu na mtupe angalao miaka miwili au mitatu ya majaribio muone tutakavyolinda msitu huu”, alisema Mtui.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Estomi Benjamin Moshi alisema “Ombi letu turuhusiwe kuingia na kukata majani tu katika eneo hili, tupo tayari kuilinda hifadhi hii kwa taratibu tutakazopewa”.

Akijibu ombi hilo Naibu Waziri Makani alisema, ombi hilo litaenda kufanyiwa kazi kwa ushirikiano kati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wakuu wa Wilaya zinazozunguka eneo hilo la hifadhi ambazo ni Moshi, Rombo, Hai na Siha, Wizara ya Maliasili na Utalii na TANAPA ambapo wananchi watapewa mrejesho wa ombi lao hilo.

Sheria za uhifadhi zinakataza mtu yeyote kuingia na kulisha mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kisheria ikiwa ni pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu, kutokana na umuhimu wa eneo hilo kwa wananchi wanaolizunguka na katika jitihada za Serikali kujenga uhifadhi shirikishi, Mwaka 2014 Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kilimanjaro iliruhusu wanawake pekee kuingia ndani ya eneo hilo umbali wa mita 800 kutoka kwenye mpaka wa hifadhi hiyo kwa ajili ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni, wanaume walizuiliwa kutokana na kujihusisha na uharibifu wa eneo hilo. 

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Betrita Loibooki alisema hifadhi hiyo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kukabiliana na ujangili ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hakuna tukio lolote la ujangili wa tembo lililoripotiwa katika hifadhi hiyo.

Betrita alisema katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la uwekaji wa vigingi vya mipaka kwenye maeneo ya hifadhi ili kuepuka migogoro na wananchi alisema jumla vigingi 290 vimewekwa kwa ushirikiano na wananchi kuzunguka hifadhi hiyo kwa urefu kwa kilomita 123 sawa na asilimia 100 ya lengo lililokusudiwa.

Nae mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia alisema ili uhifadhi uimarike ni lazima uwepo ushirikiano wenye tija kwa Serikali, Wananchi na Hifadhi huku akitoa rai ushirikiano huo uimarishwe kwa maslahi ya pande zote.

 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia (kulia) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi.
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia kwake), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto) na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (kulia). 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akisikiliza na kujibu kero mbalimbali za wapagazi wanaopandisha mizigo ya watalii katika mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akikagua moja ya kigingi cha mpaka wa Hifadhi ya Taifa mlima Kilimanjaro na kijiji cha Kifuni wilayani Moshi jana, jumla ya vigingi 290 vimesimikwa kuzunguka hifadhi hiyo ambayo ni sawa na asilimia 100 ya lengo lililokusudiwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia), Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia (wapili kulia) na Mhifadhi Mkuu wa KINAPA, Betrita Loibooki (wa nne kulia) wakiangalia mfereji unaotiririsha maji kutoka hifadhi ya mlima Kilimanjaro katika kijiji cha Kifuni wilayani Moshi jana wakati wa ziara ya kutatua changamoto za uhifadhi wilayani humo. 
 aibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mhifadhi Mkuu KINAPA, Betrita Loibooki na nyuma yake ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia) namna mfumo wa ukusanyaji mapato unavyofanya kazi katika Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mtango Mtahiko (kulia), Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (wa pili kulia) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia (wa nne kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mtango Mtahiko (kushoto), Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (wa pili kushoto) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia). (Picha na Hamza Temba - WMU).

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...