Saturday, August 19, 2017

M-KOPA YAFUNGA UMEME JUA WENYE THAMANI YA Tshs 4,959,000. KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWINYI MKURANGA PWANI

 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi boksi la Vifaa vya umeme wa jua kma ishara ya makabidhiano ya mradi wa umeme uliojengwa katika shule ya Sekondari ya Mwinyi Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kamati ya shule iliyoongozwa na Mwalimu Mkuu Martin Chuwa Mtendaji kata .Juma Difa na Afisa Elimu Iddi Mdoe
 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi zawadi kwa Mtendaji kata .Juma Difa mara baada ya kukabidhi mradi wa Umeme jua katika shule ya Sekondari ya Mwinyi

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kampuni ya vifaa nishati jadidifu vya Jua ya M-Kopa imefunga vifaa vya Umeme jua katika Shule ya Sekondari  ya Mwinyi iliyoko Mkuranga mkoa wa Pwani vyenye thamani ya shilingi Tshs 4,959,000.
akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja Msaidizi wa kampuni ya M-Kopa Nchini, June Muli amesema kuwa wameameamua kutoa msaada huo ka sehemu yao ya kurudisha wanachokipata kwa jamii hivyo waliona matatizo ya shule zisizokuwa na Umeme.

"Kuna Changamoto kubwa sana ya kusoma katika shule amabzo azina umeme hali inayofanya wanafunzi wanaochukua masomo ya Sayansi kushindwa kuifunza vizuri katika maabara zao na hata wakati wa usiku kuhsindwa kujisomea hivyo sisi kama M-Kopa tumeweza kuchangia upatikanaji wa vifaa hivi mpka kuahakisha umeme unawaka shuileni hapa tunamini sasa vijana wetu wataweza kujifunza na kufaulu vizuri"amesema June Muli.

ameongeza kuwa katika tafiti yao kwa wazazi wamebaini kuwa asilimia 92% ya watoto wanaosoma katika shule zenye umeme ufanya vizuri Darasani kuliko wale wanaosoma kwenye giza .

kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwinyi ,Martin Chuwa amewashukuru kampuni hiyo kwa kuweza kutoa Msaada huo ambao utasaidia kuinua taaluma ya shule hivyo na kusema kuwa anawashukuru kwa kuchagua shule hiyo kuwa ya kwanza kufikiwa na mradi huo ambao unalengo la kuboresha elimu nchini  

ROLI LAPINDUKA NA KUACHA BARABARA ENEO LA KIMARA TEMEBONI

 Roli la Mafuta likiwa limepinduka mara baada ya kuacha barabara ya Mororogo na kuanguka pembeni katika eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leo
Roli la Mafuta likiwa limepinduka mara baada ya kuacha barabara na kuanguka pembeni katika eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leo

Friday, August 18, 2017

KUBENEA ZAIDI YA MILIONI 90 KUKARABATI SHULE ZA MSINGI KATA YA MAKUBURI

 Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na Wanafunziwa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Makuburi wakati alipokwenda kukagua ukarabati wa Madarasa wa shule hiyo unaotokana na mfuko wa jimbo na fedha za Halmashauri ambapo jumla ya fedha zaidi ya Milioni 88 zimetolewa na Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya ubungo na Milioni 17 Kutoka Mfuko wa Jimbo wa  mbunge huyo
 Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na Wanafunziwa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Makuburi wakati alipokwenda kukagua ukarabati wa Madarasa wa shule hiyo unaotokana na mfuko wa jimbo na fedha za Halmashauri ambapo jumla ya fedha zaidi ya Milioni 88 zimetolewa na Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya ubungo na Milioni 17 Kutoka Mfuko wa Jimbo wa  mbunge huyo
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaaa wa Mwongozo , James Gointamile(CCM)   akimuonyesha Mbunge wa Ubungo , Saed Kubenea (CHADEMA), Baadhi ya Vigae ambavyo vilikuwa vinavuja katika madarasa matatu ya Shule ya Msingi Makuburi mara baada ya Mbunge Huyo kutoa Milioni 17 kwa ajili ya kununua bati mpya za kisasa kuezeka shule hiyo.
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akionyesha Sehemu ya Paa ambayo inavuja inatarajiwa kuzibwa hivi karibuni na Mabati amabyo yametolewa kwenye fedha za mfuko wa Jimbo
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiangalia sehemu ya Shimo la choo cha Matundu 12 knachotaraji kujengwa na fedha za Halmashauri ya Manispaa ya ubungo mara baada ya Choo cha shule hiyo kutokuwa katika hali nzuri
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akizungumza na Watendaji wa Mtaa na Diwani wa kata ya Makubuli, Hanifa Chiwili kwenye darasa ambalo liko juu ya chemba ya kuhifadhia maji ya mvua ya shule hiyo hili kuzuia Mmong'onyoko kwa Madarasa Mengine

 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akizungumza na Walimu wa shule ya Msingi Makuburi mara baada ya kutembelea chumba cha Walimu


 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Akiwa katika korido za shule msingi Makuburi
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiagana na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makuburi

Tuesday, August 15, 2017

LUKUVI AKABIDHI HATI ZA KIMILA 2100 KATIKA KIJIJI CHA NYANGE WILAYA YA KILOMBERO

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii , Kilombero
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaonya wale wote watakao chukua hati za Kimila na kuwauzia watu waliopo miji sehemu ya maeneo hayo ambayo yamepimwa na Serikali na kusema kuwa  Serikali haitawatoza kodi wananchi wanaomiliki ardhi za kimila badala yake maofisa ardhi wawatoze kodi wenye hati za miaka 99 za kumiliki mashamba makubwa ya biashara.
 
Hayo yamesemwa jana na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa hatimiliki za kimila zaidi ya 2000  katika Kijiji cha Nyange wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro  kupitia Mradi wa Uwezeshaji Umilikishaji Ardhi (LTSP).

Lukuvi amesema  hatimiliki hizo zipo kwa lengo la kulinda ardhi ya vijiji husika na kwamba walanguzi wa ardhi hawatapata nafasi kwa kuwa ardhi iliyopimwa haitaweza kununulika kwa mtu ambaye sio wa kijiji hicho.

Amesema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya udalali wa ardhi lakini kutokana na ulinzi uliowekwa katika hatimiliki hizo, hawataweza kwa kuwa ardhi haitanunulika.

"Hili ni agizo kutoka kwa Rais Dk John Magufuli kwamba wananchi wote watakaopatiwa hatimiliki za kimila wasitozwe kodi isipokuwa wale wenye mashamba makubwa ya biashara ambao watatozwa kila ekari Sh 1,000.  Kwa kuwa hamtalipa kodi, basi fedha hiyo muitumie kuzalisha zaidi kwa manufaa yenu ya baadae," alisema Lukuvi na kuongeza;

"Ardhi iliyopangwa na kupimwa hata kama ardhi ni ndogo  inathamani kubwa zaidi ya mtu mwenye eneo kubwa ambalo halina hatimiliki."
Alisisitiza kuwa wananchi waliopewa hatimiliki za kimila wanakopesheka hivyo, benki zote zifungue milango na kuwapatia mikopo stahiki ili kuendeleza mashamba yao na kujiunua kiuchumi.

Alieleza kuwa maofisa wa serikali wanapaswa kueleza namna ya kuzalisha mazao mengi kuliko awali na kwamba ardhi isibadilishwe matumizi kama ni ya kilimo au ufugaji itumike kama ilivyotakiwa.

Lukuvi amesema katika miaka hiyo wanatarajia kutoa hati za kimila 300,000 kwa wananchi na kwamba kwa sasa asilimia 20 pekee ya ardhi ndio imepimwa na kupangwa.
LTSP ni mradi wa majaribio wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Mashirika ya maendeleo ya Denmark kupitia Shirika la DANIDA, Sweden kupitia Shirika la SIDA na Uingereza kupitia Shirika la UKaid kwa Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga mkoani Morogoro.
Mradi huo umeanza kazi ya kupima, kubainisha mpango wa matumizi ya ardhi Julai mwaka jana.

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi ,akizungumza na Wakazi wa Kijiji Cha Nyange Kabla ya kuanza zoezi la Ugawaji hati za Kimila kwa wakzi wa Kijiji Hicho ambao wamepimiwa kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akiwa na Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Masijala ya Kijiji Cha Nyange ambayo itakuwa inatunza kumbukumbu ya hati
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi  akimkabidhi hati yake Mkazi wa Kijiji Cha Nyange , Bibi Clesencia Namuhoni  wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard  akizungumza na wakazi wa kijijii cha nyange juu ya umuhimu wa kumiliki hati za kimila katika kujiendeleza kiuchumi  wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 

 Mratibu wa Programu ya Godfrey Machabe mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi  na Wageni kutoka balozi mbalimbali wakisaini Vitabu vya wageni mara walipowasili katika kijiji cha Nyange Wilaya ya Kilomber
 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA
 Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Morogoro Mch Getrude Rwakare akiuhutubia  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk .Kebwe Stephene Kebwe, akihutubia  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA
  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA


 Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Nyange Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro  wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Lukuvi na Wadau wa Maendeleo
Wafanyakazi wa mradi wa mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Lukuvi na Wadau wa Maendeleo

TASISI YA HUMANITY ACTION FOR CHILDREN FOUNDATION YATOA VIFAA KWA WALEMAVU

 Mwanzilishi wa Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation , Rahma Mohamed Abdalah akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa ...