Saturday, August 26, 2017

BRIGEDIA JENERALI MBUNGU AWATAKA ASKARI WA SUMA JKT GUARD KUWA MABALOZI WAZURI WA MAPAMBANO YA RUSHWA MAKAZINI

 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akizungumza na askari wa ulinzi binafsi wa kampuni ya Suma JKT wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya sita kwa askari wapya wa kampuni hiyo iliyopo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT). na kuwaasa kuwa mabalozi wazuri katika mapambano ya rushwa katika kazi yao na hasa katika ofisi watakazopangiw akufanya kazi
 Mkurugenzi wa kampuni ya Ulinzi ya Suma Jkt Guard Limited, Meja Alfred Mwaijande akizungumza kabla ya kukamribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya askari wa kundila sita wa Suma jkt
 Kaimu Mkuu wa chuo cha Uongozi JKT Kimbiji .Meja Josephat Songita akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya askari wa Suma Jkt Guard kundi la Sita
 Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Mafunzo wa Suma Jkt Guard ,Luteni Albert Masawe akizunguma namna mafunzo hayo yalivyoendeshwa kwa mgeni rasmi
 Askari wa Jeshi la Kujenga taifa akipiga ngoma wakati akiongoza gwaride la askari wa Suma Jkt Guard
 Askari wa kundi la sita wanaomaliza  mafunzo ya ulinzi binafsi kundi lasita la Suma Jkt Guard wakipita kwa mwendo w aukakamavu
 Askari wa ulinzi binafsi wa Suma Jkt Guard wakionyesha umahiri wao wa kuchez amchezo wa Karate mbele ya mgeni rasmi  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
 wakionyesha umahiri wao wa kuchez amchezo wa Karate mbele ya mgeni rasmi  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
    Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu  akiwasili katika uwanja wa kufunga kozi
 Askari wa ulinzi binafsi wa Suma Jkt Guard wakila kiapo cha uaminifu mbele ya  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akiwa katika picha ya pamoja na askari wa ulinzi binafsi wanaomaliza mafunzo yao 

Friday, August 25, 2017

Hivi Tshishimbi anajua kama ametupa BRN?


ABDUL MKEYENGE
PAPPY Kabamba Tshishimbi ndiyo habari ya town mazee (Dokii voice). Kiungo huyo aliyesajiliwa Yanga aliuhitaji mchezo wa juzi kutuonyesha yeye ni Mkongomani, lakini sio Nyoshi El Sadat wala Fally Pupa. Yeye ni Tshishimbi mwenye jukumu la kuurahisisha mpira. Ndiyo kazi yake, hana kazi nyingine.
Dakika 90 za mchezo wa Simba juzi zimetupa tofauti ya mchezaji wa kulipwa anayetakiwa kulipiwa Dola 2000 na mchezaji anayepatikana Mazense kwa mfuga mbwa.
Tshishimbi ni mchezaji wa kulipwa. Kila nilivyozitazama nyendo zake uwanjani dhidi ya Simba, kwa karibu nilimuona Patrick Mutesa Mafisango ndani ya mwili wake.
Kando ya usajili wa Gadiel na Youthe Yanga, Tshishimbi ndiyo usajili wangu bora. Yanga haijawahi kuwa na shida sana na kipa wala beki wa kushoto, lakini mara nyingi shida yao ilionekana kumkosa mchezaji aina ya Tshishimbi ambaye atakuwa na jukumu la kusimama mbele ya mabeki wanne kuwalinda.
Yanga ilimkosa mtu wa aina hii siku nyingi tu tangu wakati ule wa rafiki yangu Athuman Iddy alipoondoka na baadaye Frank Domayo kumfuata nyuma. Kazi za Tshishimbi zinafanywa na wanaume wachache wanaohesabika kwa vidole vya mkononi kama yeye. Hazifanywi na kila mchezaji.
Tshishimbi anacheza direct football. Sehemu ya kuuachia mpira anauachia, sehemu ya kutembea nao, anatembea nao, sehemu inayohitaji mapambano anapambana, sehemu anayopaswa ku'shoot ana'shoot. Modern football iko hivi, haina mambo mengi.
Muda huu ambao mashabiki wa Yanga wanaliimba na kulitaja mara nyingi zaidi jina lake kwenye vinywa mwao, hawalitaji kwa bahati mbaya, Tshishimbi anafanya kile alichoshindwa kukifanya Justice Zullu aliyeletwa kwa ajili ya kukata umeme, badala yake alisababisha shoti ndani ya nyumba na kusababisha hasara ya vyombo kuungua.
Tshishimbi ni box to box midfield anayetimiza vyema majukumu yake bila ya muingiliano wa kazi za wachezaji wengine uwanjani. Kila zuri lake na sifa anazomwagiwa muda huu liliko kaburi la Mshindo Mkeyenge linatikisika kwa furaha. Babu aliipenda Yanga na aliwapenda wachezaji wazuri ndiyo maana aliwahi kutoa fedha zake mfukoni kumsajili Leodegar Chilla Tenga na kumpeleka Yanga, lakini amefariki muda ambao Yanga imeondokewa na Niyonzima, lakini imemsajili Tshishimbi.
Kuwafanya viungo wa Simba wasione mashimo ya kupiga pasi za mwisho kwa washambuliaji wao si kazi ndogo. Ni Tshishimbi aliyewafanya viungo hao waonekane machachari na sio hatari. Mipira mingi ya hatari kuelekea langoni mwa Yanga ilifia miguuni mwake. Ni yeye aliyezima mashambulizi mengi.
Dunia ya leo inahusudu wachezaji wa aina hii. Wachezaji wanaovuja machozi, jasho na damu kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho wa mchezo kana kwamba hakuna mechi nyingine.
Kupitia ubora wa Tshishimbi ndiyo tunapata maana halisi ya mchezaji wa kulipwa anavyotakiwa kuwa uwanjani. Nimemuona kwenye mechi ya juzi na nimetosheka nae, sihitaji kumuona tena ili nijiridhishe zaidi. Huyu haji uwanjani kutuibia viingilio vyetu.
Hapa katikati Yanga walipigwa sana kwenye usajili wa wachezaji wa nje. Wachezaji wengi waliokuja walionekana wa kawaida. Mchezaji wa mwisho kuchukua fedha za bure na kutokomea nazo kusikojulikana ni Yusuph Garba.
Lakini kwa usajili wa Tshishimbi ambaye nimedokezwa nyuma ya dili lake kuna mtu wa kuitwa Shaffih Dauda (Pini Zahavi) na Shadaka yake, hapa lazima mchezaji awe mchezaji kweli sio mchezaji magumashi. Huwa namuamini Dauda. Ni kati ya watu wachache wanaofahamu masuala ya soka na wenye passion nalo.
Hapa kwa Tshishimbi Dauda ameitazama fursa na kuifanyia kazi. Wakati mwingine inataka moyo kuupenda mpira bila kupata kitu ndani yake. Hii inahitaji moyo wa yule hawafu mwenye nguvu kile kipande cha baba kilichopewa kazi ya kulala zizini ili kulinda ng'ombe wa mfalme wasiliwe na simba.
Licha ya kalamu ya babu iliyorithiwa vyema na mjukuu kumuona Tshishimbi akianza vyema kwa kucheza vizuri mechi ya kwanza ya kimashindano, lakini mwenyewe anajua kama alifanya vyema na kuwa gumzo nchini? Kama hajajua mfikishieni salamu zangu kwa kumwambia alichokifanya hapa kwetu kinaitwa Big Result Now (BRN), kitu papo kwa papo!

TAZAMA HAPA MASTAA WA MUZIKI NA FILAMU NCHINI WALIVYOCHIZIKA NA MECHI YA SIMBA NA YANGA

 Msanii wa filamu anyekuja kwa kasi nchini Gabo Zigamba akifatilia kwa makini mchezo wa Watani Simba na Yanga huku yeye akiwa katika upande wa timu anayoikubali Simba
 Msanii wa Michezo ya kuigiza kutoka Tamthilia ya Rangi ya Chungwa Ndende akiwa amezubaa mbele ya Mashabiki wenzie wa timu ya Simba wakati mchezo ukiendelea
 Mzee wa kuoga maji ambaye amejipatia umaharufu kupitia Mashindano ya Ndondo Cup akiwa katika Jukwaa la Simba
 Mwanamuziki wa wa Muziki wa Bong Fleva Hamisi Mwijuma (Mwana FA) Akiwa amesimama kushuhudia mikwaju ya penati inavyopigwa Vizuri
 Msanii wa Vichekesho Haji Mboto na Mau Fundi wakiwa katika jukwaa la Yanga wakiangalia mpira kwa staili ya aina yake
 Salama yanga kama kawaida yake akiwa amejipaka rangi mwili mzima kukoleza mbwembwe za ushabiki wake
 Mashabiki wa Yanga wakiwa  katika staili ya aina yake ya kubeba ungo
 Shabiki wa Yanga akiwa amevaa chupi kubw ainayosema Bosi anauniwi  katika mchezo huo wa watani
 Msanii wa filamu nchini, Jacob Stephene akiwa katikati ya Mashabiki wa Simba
Gabo akishangaa mara baada ya mikwaju ya penati kumalizika 

NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI KUTAMBUA MAENEO YASIYOENDELEZWA NA YASIYOMIKILIWA KIHALALI


Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali .
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya wakati alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Busega mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, (kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Tano Mwera.
Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao Wilayani Busega(hawapo pichani).


Na Stella Kalinga, Simiyu

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri nchini, kuyatambua na kuyatolea taarifa maeneo yanayohodhiwa na watu bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara iweze kuchukua hatua stahiki.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo utakaonufaisha vijiji vinne vya kata ya Lamadi.

Mhe.Mabula amesema Halmashauri zinapaswa kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha sheria na kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili yaweze kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi mengine yenye manufaa zaidi kwa jamii.

“Maeneo yote yaliyohodhiwa ambayo hayajaendelezwa na ambayo pengine hayakupatikana kihalali, ni jukumu la Halmashauri kuyatambua na kuleta taarifa zake Wizarani ili Wizara iweze kuchukua hatua ya kuweza kuyarudisha katika matumizi kwa Umma na yaweze kufaidisha watu wengi zaidi badala ya mtu mmoja” amesema Naibu Waziri Angelina Mabula

Aidha,Naibu Waziri Mabula amebainisha sababu zilizopelekea Mwekezaji Hermati Pateli kufutiwa hati ya eneo hilo na Serikali kuwa ni udanganyifu wa Uraia pamoja na upatikanaji wa hati ambao haukuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Naibu Waziri huyo amesema eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji huyo isivyo halali ambalo limefutiwa hati miliki limegawanyika katika ploti mbili, ploti Namba 01 na Namba 02 Block C lenye ukubwa wa hekta 7.62 na Block Namba 03 C hekta 5.45.

Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji wa Lamadi kutoka Kampuni ya EAU Consult, Baraka Felix amesema Tanki la Maji litakalojengwa katika eneo hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 3000 kwa siku.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya amesema Mradi wa Maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo hilo utawanufaisha wananchi wa Vijiji Vinne vya Kalago, Lamadi, Lukungu na Mwabayanda.

Mradi huu wa maji unaojengwa katika eneo hili lililokuwa linamilikiwa isivyo halali na Mwekezaji Pateli, utagharimu kiasi cha Yuro milioni 2.8, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2019.

Thursday, August 24, 2017

Mambo Sita (6) Mazito waliyoibua LHRC Leo,Sakata la Lissu,Bomoa Bomoa Laguswa,wakemea mauaji na Bomoa Bomoa

Katika kuisimamia na kulinda haki za binadamu nchini Tanzania Kituo cha sheria na hakiza binadamu Tanzania LHRC, Leo wameibuka na kukemea mambo kadhaa yanayoendelea nchini kwa sasa huku wakiitaka serikali kuyafanyia kazi kwa haraka kwani kuyaacha ni kuendelea kuminya haki za binadamu nchini,
Nchini Tanzania kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa kukiripotiwa mambo kadhaa ikiwemo Bomoa bomoa ya maeneo mbalimbali nchini kupisha shughuli za maendeeo,kamata kamata ya wanasiasa na kuminywa na democrasia nchini.Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na -------

SAKATA LA TANAPA KUJERUHI WANANCHI
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Kaimu mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Henga ameyataja mambo ambayo wameamua kuishinikiza serikali kuyaangalia kwa jicho la Tati kuwa ni pamoja na Operation inayoendeshwa na TANAPA kulinda hifadhi ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakijeruhiwa na askari wa eneo hilo akiwemo kijana mmoja ambaye wamemtaka kwa jina la Pormoson Losso mwenye umri wa miaka 23 ambaye iliripotiwa kuwa alijeruhiwa kwa risasi na askari wa TANAPA kwa madai ya kuwa eneo la hifadhi,ambapo LHRC wamelitaka shirika hilo kuhakikisha kuwa linalinda haki za binadamu wakati likiendesha mazoezi yake kwani kutokufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.

BOMOA BOMOA KIMARA
Sakata lingine ambalo LHRC wamelijadili ni kuhusu Bomoa bomoa inayoendelea ikiendeshwa na TANROADS katika barabara ya morogoro kupisha upanuzi wa barabara ambapo inasadikika kuwa mpaka sasa wakazi zaidi ya elfu moja wamebaki bila makazi maalum,huku wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto ambao wamaweza kupata madhara makubwa kwa hatua hiyo.
Sakata hilo limewafanya LHRC kuitaka serikali na taasisi zake kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria na haki za binadamu wakati wa uendeshwaji wa zoezi hilo,ili kuepuka madhara zaidi ambayo yanaweza kujitokeza.
WAKUU WA WILAYA NA MADARAKA YAO
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zikiwahusisha baadhi ya wakuu wa wilaya kutumia nafasi zao kuwaweka ndani baadhi ya wananchi na viongozi wa kisiasa kwa makosa mbalimbali na wengine wakiwa bila makosa jambo ambalo limezua mjadala mpana nchini Tanzania.

Sakata ambalo kwa sasa limekuwa likijadiliwa sana ni kuhusu Mkuu wa wilaya ya chemba Simon Odunga kumcharaza viboko mzazi wa mmoja wa watoto walioshambulia gari lake na kuvunja vioo kwa mawe,pamoja na lile tukio la mkuu wa wilaya ya hai Gelasius Byakanwa kuagiza jeshi la polisi kumuweka ndani mwalimu Erasto Mhagama wa shule ya secondary lerai kwa kosa aliloliita utovu wa nidhamu la kushinda kutaja jina la mkuu huyo wa wilaya na kushindwa kutaja nafasi ya ufaulu wa shule hiyo kitaifa kwa mwaka 2015.

Kwa kuzingatia matukio hayo LHRC wameitaka wizara ya nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwaonya wakuu hao wa wilaya kwani matukio hayo yamekuwa yakiongezeka na hakuna sheria inayowaruhusu kufanya hivyo nchini.
POLISI NA MAUAJI YA WAHALIFU
Kufwatia matukio kadhaa ya polisi kuwaua Raia ambao wamekuwa wakiripotiwa kama wahalifu LHRC imeitaka serikali kuwapa mafunzo polisi ya kuwaweka kizuizini wahalifu badala ya kuwaua kwa kuwa hakuna shEria inayoruhusu kufanya hivyo na uwezo wa kuwakamata wanao.

MIILI INAYOOKOTWA UFUKWENI
Kutokana na kuwepo kwa Taharuki kubwa miongoni mwa Taifa baada ya kuripotiwa kuokotwa ka miili ya binadamu kadhaa inayoelea katika mito na bahari ya hindi bila kujulikana ni watu gani na ni nani anayewaua huku miili hiyo ikiwa imefungwa katika viroba,kituo hicho kimeitaka Ofisi ya upelelezi wa makosa ya jinai DPP kufanya uchunguzi wa miili na matukio hayo ili kutoa taarifa sahihi ambayo itawatoa hofu wananchi,kwa kuwa vitendo vya mauaji ya kinyama kwa binadamu kama hayo ni uvunjifu mkubwa wa sheria na haki za binadamu na watanzania wana haki ya kufahamu matukio hayo yanafanywa na watu gani ili kurudisha amani mingoni mwa watanzania.

KAMATA KAMATA YA WANASIASA
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimeelezwa kusikitishwa kwake na vitendo vya kuminywa kwa democrasia nchini na haki za kisiasa na kiraia, ambapo hali hii imejitokeza kwa kuwanyanyasa wabunge na viongozi hasa wa vyama vya upinzani, ikiwa ni pamoja na kamata kamata ya viongozi hao inayoendelea bila kufwata sheria za nchi,misingi na haki za binadamu.

Akitolea mfano sakata la kukamatwa mara kwa mara kwa Mbunge wa singida mashariki Mh Tundu Lissu,ambapo kwa sasa amekamatwa Tarehe 22 mwezi huu akiwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa shughuli zake kwa tuhuma za uchochezi na baadae kupekuliwa nyumbani kwake.
Wabunge wengine walokumbwa na kadhia hiyo ni Ester Bulaya mbunge wa Bunda,Godbles Lema mbunge wa Arusha mjini ambaye alikamatwa kwa kosa la kuzidisha muda wa mkutano kwa dakika saba na maadae kuachiwa.
LHRC wameitaka serikali kutoa nafasi kwa vyama vyote kufanya kazi kwa usawa bila kuingiliwa kwani Tanzania ipo katika mfumo wa vyama vingi na ni haki ya kikatiba kwa wanasiasa kuendesha shughuli zao.

JAMBO LINGINE KUBWA LITAKALO KUWEPO KWENYE TAMASHA LA JINSIA MWAKA HUU

TGNP Mtandao katika kutambua nafasi ya wanajamii imetoa nafasi maalum kwa  watu waliofanya mambo makubwa kwenye jamii yao na mchango wao haukutambulika, hivyo watapewa nafasi ya kuadithia simulizi zao mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata.


Hayo yalizungumzwa jana kwenye semina ya jinsia na maendeleo (GDSS) ilifanyika mapema  kwenye ukumbi wa mtandao huo Mabibo jijini Dar es salaam.

Akiongoza semina hiyo afisa programu wa TGNP Mtandao Bw. Deogratius Temba alisema kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kusherekea mafanikio na kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye harakati zao.

Amesema kuwa Wametoa nafasi hiyo kwa wanajamii na washiriki wa semina za  jinsia na maendeleo kuwapa nafasi ya kusimulia stori za maisha yao kwa wale waliopitia magumu mpaka kufanikiwa na kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri katika harakati za jinsia na maendeleo.

Kwa washiriki wa semina za jinsia na maendeleo na wanajamii kwa ujumla watapata nafasi ya kushiriki kwenye mjadala wa wazi na baadae kushiriki kwenye warsha  ndogo ndogo zitakazofanyika kwenye tamasha hilo.
Aidha ameongeza kuwa  kwenye warsha hizo kutakuwa na mada mbalimbali zinazoongoza kila warsha kama mjadala wa Maji, Elimu, Ardhi, Mazingira Madini, Mabadiliko ya tabia ya nchi, Afya na mengine mengi.

Amesisitiza kuwa warsha hizo  zitaongozwa na idara mbalimbali za serikali pamoja na mashirika rafiki na Mtandao wa Jinsia(TGNP) kama TAMWA, MEWATA, WLAC, Plan International, Haki elimu, Mfuko wa wanawake, Haki ardhi, VIWATA  na mashirika mengine mengi.

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 789 LEO AUGUST 24,2017..CHAGUA HAPA UNAYOTAKATANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi za Umma mbalimbali Serikalini, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 789. Kwa Maelezo zaidi tembelea www.ajira.go.tz

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Tano Mwaka 2017 Awamu ya PiliTAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda kuwajulisha wananchi juu Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa Awamu ya Pili kwa mwaka 2017. Wanafunzi hawa wataanza muhula wa kwanza wa masomo tarehe 24 Agosti, 2017 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa
kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 08 Septemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, atakuwa amepoteza nafasi.
Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, inabidi ku-download fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi awamu ya pili mwaka mwaka 2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais –TAMISEMI
23 Agosti, 2017
XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Tafadhali bofya chini Kujua Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano kwa Awamu ya Pili kwa mwaka 2017.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...