Friday, October 20, 2017

DC KIGAMBONI AZINDUA MPANGO WA DARMAERT NA VIFAA VYA MAWASILIANO WAKATI WA DHARULA NA MAAFA

 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa Mpango wa DarMaert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akikata utepe  kuashiria uzinduzi wa chumba cha Mawasiliano DarMaert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa utendaji kazi wa Uokoaji na Majanga
 Muwakilishi wa Benki ya Dunia, Erick Dikson akizungumza mara baada ya kukabidhi  vifaa kwa tasisi ya Dar Meart kwa ajilya Majanga na uokoaji
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akizungumza na kuahidi Kiwanja kwa ajili ya Kikosi cha Zima moto mkoa wa Dar es Salaam na mpango wa DarMaert na ghala kwa ajili ya kuwasaidia katika huduma za majanga.
 
 Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi amabye ni mkuu wa Wilaya ya Kigamboni

Sehemu ya Askari wa Jeshi la Zima Moto waliohudhuria uzinduzi wa mpango wa Dar Maert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa 

DC SINYAMULE APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KUTOKA TAWI LA NMB SAMENa Humphrey Shao, Globu ya Jamii . 

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule   amepokea Msaada wa  vifaa vyenye thamani ya Tshs. 10M  kutoka Benki ya NMB kwa  kwa ajili ya ujenzi wa Choo cha Wanafunzi wa Kike katika shule ya sekondari Kazita iliyopo kata ya Mhezi Same.

akizungumza wakati wa kupokea Msaada huo DC  Sinyamule  aliwashukuru NMB kwa vifaa hivyo vilivyojumuisha mabati, cement, mchanga, tofari, mawe, rangi na masink ya choo ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatioz la uhaba wa vyo vya watoto wa kike shuleni hapo. 

Dc Sinyamule aliwataka viongozi kuanzia bodi ya shule hadi Halmashauri kusimamia ujenzi wa vyoo hivyo na vikamilike kwa siku 45. Ili mwezi Novemba mwishoni tufanye uzinduzi wa vyoo hivyo. 

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya Aliwakumbusha fursa zilizopo Same kuwa ni pamoja na kufungua matawi mengine ya benki maeneo ya Ndungu na Mamba myamba kwani Wilaya inaendelea na uwekezaji mkubwa katika maeneo hayo. 

Naye meneja wa Benki hiyo Ndugu Mpimbi alieleza Benki hiyo ilivyoboresha huduma na kuwa ni benki inayoongoza kwa kurudisha faida kwa wateja katika mahadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja . alimaliza  kwa  kusema kuwa Kukamilika kwa vyoo hivyo kutafanya shule hiyo kutokuwa na upungufu tena wa vyoo jambo ambalo litasaidia sana watoto wa kike. 
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akipokea  Vifaa vya ujenzi na Saruji kutoka kwa Meneja wa NMB Wilaya ya Same.
Sehemu ya Vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Benk ya NMB W ilaya ya Same
akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Benki ya NMB Wilaya ya Same

Thursday, October 19, 2017

MWIGAMBA AIKIMBIA ACT NA KUHAMIA CCM

Aliyekuwa kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba Ameachana na Chama cha ACT wazalendo na kuamua kijunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) .

Mwigamba amewaeleza Waandishi wa Habari kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo bila kulazimishwa na mtu  yoyote hivyo yeye na baadhi ya wanachama wa ACT wametangaza rasmi kujivua uanachama wa ACT-Wazalendo na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“nimefikia uamuzi huo baada ya viongozi wa ACT-Wazalendo kuwa na maamuzi ambayo ni tofauti na lengo la kuanzishwa kwa chama akitolea mfano kuipinga serikali hata katika shughuli za maendeleo hivyo Uongozi wa sasa wa chama hiki unachepuka kwa kasi kubwa mno nje ya misingi ya chama na sasa chama kimebaki kuwa jahazi ambalo tanga lake limechanika”amesema Mwigamba.

ameongeza kwa kuwa baada ya kutangaza kujivua uongozi baadhi ya viongozi wa ndani ya chama waligeuka vichaa wakinitukana kila aina ya matusi na cha ajabu hata wale wanaofahamu na kuitetea misingi ya chama walitukanwa na viongozi wakiwepo na wamekaa kimya.


Wednesday, October 18, 2017

KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA

                                  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Katibu Mkuu wa Chama Cha  Mapinduzi   Mkoa wa Dar es salaam, Saidi  kusalawe  amewataka  viongozi wa chama hicho kuvunja Makundi  na   kuacha kabisa swala la  maneno  ili  kufanikisha ushindi wa kishindo katika marudio  ya uchaguzi  wa Udiwani kata ya Saranga.


Kusilawe amesema hayo alipokuwa anaongea na wajumbe  wa halmashauli kuu ya wilaya ya ubungo  katika mkutano ulio wakutanisha viongozi hao  na kutumia mda huo kuwaasa  viongozi hao kuchagua kiongozi  bora na atakae  kubalika  kwa wananchi  ili  chama kiweze kupata  ushindi  wa kishindo kwenye marudio hayo ya uchaguzi.

 "  uchaguzi ni kama biashara  leo tuko  saranga,  mmepiga kula za maoni  jana,   kula zile zitakuja  kuwaambia  kuwa  saranga  tunakwenda na kuku au bata ,  tutakapo kwenda watatuambia ,  nikimaanisha  tunapaswa kumchagua mgombea  ambae  anafaa  na      anauzika  kwa  kwa jamii , kwani  ukiwa  umepita  na kuku  watu watakuuliza  iyo ni biashara ????  Lakini ukibeba bata  hakuna  atakae kuuliza kwakuwa wanajua  unaenda kufuga  hivyo hawaulizi bei   na sisi tufanye  uchaguzi  ambao utatupa  kiongozi  anae pendwa na  kukubalika  na  jamii  na majibu  tutapata  kesho kutwa amesema Kusilawe.

Aidha aliwaasa viongozi  kuwa na moyo wa  kutunza  vitu  na kulinda sana mdomo kwani wote tunajua mdomo ni jumba la maneno  kuna mda unaweza kuongea  kitu ambacho  kinajenga au kubomoa,  huku  akisisitiza kuwa  na weledi  wa kuchambua  mambo  punde unapo letewa  taarifa yoyote , alizidi  kueleza kuwa  kiongozi bora  hupaswi kuwa na maneno mengi,    kiongozi akipenda  kuongea sana  uyo sio   kiongozi  bali  ni kiwanda cha kuzalisha maneno.

Sambamba na hayo   aliwaonya makatibu  wa  matawi  kusimamia  vyema  vitega  uchumi  vyote  vya chama  kwa  umakini  kwani  kuna  baadhi ya makatibu  wamejibinafsishia  vitega uchumi  hivyk  na  kuvimiliki  kama vyao  kitu ambacho  chama  hakito kubali  wala  kufumbia  macho  vitendo hivyo vya wizi wa mali za chama.


Pia ndg  sadi  alitumia nafasi hiyo  kutoa onyo kali kwa  viongozi  ambao  hawapendi  kuvaa  sare za chama cha  mapinduzi  ccm  na  kuwataka waache mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo watajikuta kwenye matatizo ya kuitwa kunguru ikiwa na maana  ya  mamluki wa chama ambao  wanavujisha siri za chama   nahivyo  kujikuta kwenye kashfa zisizo na maana yoyote ,  alihoji kuwa  RAIS na MWENYEKITI  wa ccm Taifa mheshimiwa  JOHN  MAGUFULI   anafanya kazi  nzuri  hivyo hakuna aja ya kukificha chama  chako hivyo ni muhimu kwa wajumbe  kuvaa sale za chama .

Alimalizia kwa kuwaasa wanachama wa chama hicho kuacha kuvaa nguo  zinazo wabana , vimini  na nguo ambazo zinaonesha  maumbile ya mtu jinsi yalivyo au kuvaa   nguo chini  ya makalio   kwani kufanya hivyo ni kukosa maadili.   pia kikao hicho kiliudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo  Mwenyekiti wa chama hicho  wilaya ya ubungo ,  katibu wa chama wilaya ya ubungo  ,  wajumbe  wa halmashauli kuu  wiaya ya  ubungo ,  madiwani n.k
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Sadi Kusirawe  akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Wilaya ya Ubungo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  Mkoa wa Dar es Salaam Sadi Kusirawe  akisalimiana  na wajumbe wa  halmashauri kuu wilaya ya ubungo
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzu(CCM), Wilaya ya Ubungo Mgonja Akimpoke katibu wa chama mkoa wa  Dar es salaa   Sadi  kusalawe
 Baadhi ya madiwani wa chama cha mapinduzi wakimsikiliza katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam
Kamati ya Watendaji   ya CCM  wilaya ya Ubungo wakiwa kwenye picha ya pamoja na  mgeni rasmi

LATIFA KANYANGA ASHEREHEKEA MAHAFALI YAKE YA KIDATO CHA NNE GREEN ACRES SEKONDARI

Afisa elimu Wilaya Ubungo, akizungumza wakati wa Mahafali ya 18 ya shule ya Sekondari ya Green Acres yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi Latifa Kanyanga akipokea cheti kutoka kwa mgeni Rasmi katika mahafali ya 18 ya kidato cha 4 katika Shule ya Sekondari ya Green Acres
Mwanafunzi Latifa Kanyanga akisoma Risala wakati wa Mahafali ya 18 ya Shule ya Sekondari ya Green Acres
Mwanafunzi Latifa Kanyanga  akicheza wakati wa mahafali ya 18 ya Sekondari ya Green Acres
Nasra Mushi akimlisha  keki Mama yake , Evelyn Kanyanga  katika Mahafali ya 18 ya shule ya sekondari ya Green Acres
Mwanafunzi Latifa Kanyanga akipokea Zawadi ya Laptop kutoka kwa Mama yake Evelyn Kanyanga mara baada ya Mahafali ya 18 ya shule ya Sekondari ya Green Acres
Ndugu na jamaa wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu 

DC SINYAMULE AFUNGUA TAWI LA TANESCO HEDARU

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule ameigiza  Tanesco Same  kuwafata wateja popote walipo hili kuongeza kasi ya huduma kwa kuhakikisha kuwa kila mahali wanapata Umeme.

Dc Sinyamule amesema hayo alipokuwa akizindua tawi la  Tanesco  Hedaru na Kisiwani katika Wilaya Same na kumbusha kuongeza ofisi maeneo ya milimani.

Kuhakikisha mkandarasi anayefanya kazi kuzingatia uimara wa nguzo hasa maeneo ya milimani pamoja na Kutengeneza mabango yanayoonyesha wateja tahadhari za kuchukua juu ya umeme ili kupunguza madhara ya vifaa na umeme kukatikakatika”Amesema Dc Sinyamule.

Amewataka Kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma kwa haraka na Kuanzisha na kuitangaza namba ya simu ya mkononi kwa ajili ya wateja.
Pia aliwakumbusha wateja kuongeza kasi ya kuweka umeme na  kulipia huduma za umeme pindi watakapohitajika kuunganishiwa.

Pia aliwakumbusha kuanza kutumia umeme kwa uchumi kwa kuanzisha viwanda vidogo na vya kati kwani serikali imekusudia kumaliza tatizo la umeme ifakapo 2021.

 Kwa Upande wake Meneja wa Tanesco Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Hiza amesema shirika limejipanga kusogeza huduma karibu baada ya ongezeko kubwa la wateja wanaotokana na mpango wa serikali  REA.

Hivyo aliwaomba wakazi wa Wilaya ya Same na Vitongoji vyake Kulipa bili kwa wakati na kutumia umeme kwa uangalifu ili kusiwepo umeme unaopotea bila sababu.

Aidha aliwaomba wakazi wa eneo hilo Kuchukua tahadhari za usalama pamoja na kutunza miundombinu na Kutoa taarifa haraka kunapotokea tatizo/ uharibifu
 Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Tanesco Hedaru wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule  akizungumza na wadau mara baada ya kufungua ofisi ya Tanesco Hedaru
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akiwa katika picha ya pamoja Wafanyakazi wa Tanesco Hedaru

REPOA REPORT ; TANZANIA YAZIDI KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI

 Mtafiti Kutoka REPOA, Dk . Lucas Katera,Akiwasilisha   ripoti ya Nafasi ya nchi katika kufanya Biashara Duniani iliyotolewa na World Economic Forum na Repoa
 Mkurugenzi wa Repoa nchini, Donald Mmari, akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Nafasi ya Tanzania  katika kufanya Biashara Duniani
 Baadhi ya Watu waliohudhuria Uzinduzi wa Ripoti hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Repoa
 Mtafiti kutoka Repoa. Dk Blandina Kilama akizungumza mara baada ya kuwasilishwa Utafiti huo 
 Prof .Sufian Bukurura kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akichangia mada mara baada ya kuwasilisha kwa ripoti .
 Mtafiti Kutoka Repoa Prof.Paschal Mihyo akichangia mada  mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Nafasi ya Tanzania  katika kufanya Biashara DunianiKatibu wa Kwanza wa sera na Uchumi  kutoka ubalozi Uholanzi Nchini, Eugene C.M Gies  akichangia mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Nafasi ya Tanzania  katika kufanya Biashara Duniani
 Baadhi ya watu walioshiriki katika  uwasilishwaji kwa ripoti ya Nafasi ya Tanzania  katika kufanya Biashara Duniani

Kamishena wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Roselyn Akombe ajiuzulu


Na Mashirika ya Kimataifa.

Kamishna wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu, siku saba pekee kuelekea Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika Octoba  26 mwaka huu.

Akombe ametoa tangazo hilo akiwa jijini New York nchini Marekani, na kusema kuwa hawezi kuendelea kufanya kazi katika Tume hiyo, aliyoielezea kugawanyika.

Aidha, amedokeza kuwa mazingira ya sasa ya kisiasa hayawezi kuruhusu kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

“Siwezi kuendelea kufanya kazi, katika mazingira kaa haya, kila dalili zinaonesha wazi kuwa Uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki,” alisema Akombe akiwa Marekani.

Bi Akombe aliondoka nchini Kenya  siku ya Jumanne, kwenda Dubai kushuhudia uchapishwaji wa karatasi za kupigia kura lakini akaamua kwenda nchini Marekani, ambako pia ni raia wa nchi hiyo.

Kujiuzulu kwa Bi. Akombe, ni pigo kwa Tume hiyo ambayo ilikuwa inamtegemea kuzungumza kwa niaba yake na kuitetea mara kwa mara.

"Tume ijitokeze wazi, iwe na ujasiri na kusema kuwa Uchaguzi huu hauwezi kuwa huru na haki katika mazingira haya," aliongeza Akombe.

Amesema pia alikuwa anapata vitisho kuhusu maisha yake na huenda asirejee nchini Kenya katika siku za hivi karibuni.


Suba Churchil, kiongozi wa mashirika ya kiraia amesema hali hii inaendelea kuzua wasiwasi kuhusu Uchaguzi huo uliopangwa kufanyika wiki ijayo.

Monday, October 16, 2017

DC SINYAMULE ; AMEWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDONa Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule  amewataka Vijana kuwa wazalendo hili kuweza kuyaenzi yale yote yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi cha uhai wake .

hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule alipokuwa akitoa mada  kwa vijana iliyohusu  "Kijana na Uzalendo"  kwa Vijana wa Ukwata zaidi ya 1000 wa Wilaya ya  Same na uzinduzi wa Kitabu kilichohusu Maisha ya Mwalimu Nyerere.

"Mwl. Nyerere alivyokuwa mzalendo na mpaka sasa ndiye Mtanzania wa kwanza aliyeonyesha Uzalendo wa kiwango cha juu kabisa akifuatiwa na Rais wetu wa sasa Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli hivyo nyie Vijana Mnapaswa kuenenda kama viongozi wetu hawa wanavyotutaka hili tuwe na Taifa la Wachapakazi na Wazalendo" amesema Sinyamule. 


katika Uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Kijana kwa ajili ya kuelimusha vijana wa kike kujitambua na kuchukua hatua muhimu kwa ajili ya mustakabali wao wa baadaye  kinachokwenda kwa jina la  " A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".


Mara baada ya kuzindua kitabu hicho mkuu wa Wilaya hiyo aliweza kununua vitabu 51 na kuagizwa visambazwe kwenye shule zote 51 za Sekondari Wilaya ya Same, viwekwe maktaba ili wanafunzi waweze kuvisoma 

Aidha Dc Sinyamule alimpongeza  mwandishi wa kitabu hicho Elihuruma kwa uandishi huo na kumtaka aendelee kuandika vitabu vingi zaidi kwa faida ya Vijana na watanzania kwa ujumla.
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
Wanafunzi wa UKWATA wamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Same juu ya mada ya Uzalendo

DC SINYAMULE AONGOZA MAZOEZI KWA WAKAZI WA WILAYA YA SAME

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya ISame mkoa wa Kilimanjaro , Rosemary Sinyamule ameongoza mazoezi ya wakazi wa Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya utamaduni waliojiwekea watumishi na wakazi wa eneo hilo kila ifikapo mwisho wa wiki.

Dc Sinyamule amesesma kuwa mazoezi yamekuwa ni utamaduni hivyo wananchi hao upata fursa ya kujumuika na viongozi wao katika siku ambazo sio za kazi na kuweza kupata nafasi ya kuzungumza mambo ya kawaida yanayohusu maisha yao ya kila siku katika mfumo wa kawaida . 
" leo wananchi wamepata fursa muhimu ya kusikiliza maelekezo ya afya kutoka na  umuhimu wa mazoezi kutoka Kwa mganga Mkuu wa Wilaya ya Same . Dr. Andrew ambaye aliwataka wakazi wa eneo hilo kutunza afya  kwa kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki hili kuweza kujiepusha na magonjwa yasiyokuwa ya lazima" amesema Dc Sinyamule.


DC Sinyamule ameongeza kuwa  katika kuadhimisha wiki ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayat Mwl Julius Nyerere ni kila mmoja kuona namna anavyomuenzi kwani alikuwa Mazalendo na alipigania Uhuru akiwa katika umri mdogo hivyo  kuwasisitiza Vijana kufanya yale yote yaliyofanywa na Mwalimu katika harakati zake. 


DC Sinyamule alimaliza kwa kuwashukuru wananchi wa Same Kwa kuendelea kujitokeza Kwa wingi. Pia aliwakumbusha kila mmoja kujipangia ratiba ya mazoezi kila siku. na si kungoja siku moja Kwa mwezi.

 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akiwa katika picha ya pamoja na Wanachi waliojitokeza katika Mazoezi Wilaya ya Same.
Wakazi wa Wilaya ya Same wakiwa katika Mazoezi ya Pamoja yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Rosemary Sinyamule 

KATIBU WA CCM KATA YA SINZA SALUM KALI; AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI TAWI LA SINZA" A"

Na Ripotawetu wa Globu ya Jamii

Katika kuazimisha kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo  cha hayati Baba  wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Chama Cha Mapinduzi(CCM)  katibu wa chama wilaya ya ubungo ,  Salum  kali  ameweka jiwe la Msingi kwa ajili ya   ujenzi wa ofisi za chama katika tawi la sinza "A"  


Akiutubia wanachama walio  jitokeza  katika shughuli  hiyO  kali amesema, Baba wa taifa  alitengeneza  heshima kwa  Mtanzania  aheshimu  kwanza  maadili ya taifa lake ndio aweze  kuheshimiwa na watu wengine.

aidha kali amesema kuwa ,  Mwalimu Nyerere  aliamini ndani ya  chama  cha mapinduzi  CCM ndiko  kunapo patikana  viongozi bora  ambao wana uwezo  wa kufanya  kazi  kwa umakini pasipo  malumbano wala fujo  kama tunavyo  ona kwa wenzetu  wa pembeni.

"Mwalimu Nyerere  aliamini  viongozi wa ccm  pekee ndio wanao weza  kusimamia  amani ya nchi hii na ndio kitu ambacho  mpaka sasa chama cha mapinduzi  kinaendelea kufanya  kupitia Rais   wa  Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli" amesema Kali.katibu kali amesema  Baba wa Taifa   alitengeneza  upendo  huku akidumisha  amani  kubwa  ambapo  mataifa  mengi  walikuwa  wakimtumia Mwalimu  Nyerere  kwa kutafuta  Amani  katika nchi zao  na wengi  kuja  kusoma na kujifunza Tanzania  ili  waweze   kwenda kusaidia  nchi zao,  alitolea mfano moja ya nchi ya Msumbiji  na nyingine  nyingi  ambazo  zilikuja  kujifunza nchini  kwetu.

Aidha ameongeza kuwa  sisi leo tunashindwa  kukumbuka  maadili na misingi ya Baba  wa taifa  aliyo  iweka  akiwa na nia ya  kutuunganisha  watanzania  wawe kitu kimoja,  pia waipende nchi  yao ,  wapende  maendeleo ya taifa  lao ili tusonge mbele.

Pamoja na hayo katibu  kali  alizidi  kusema Baba  wa Taifa  aliamini mno kwenye  uaminifu,  uadilifu na uwajibikaji  huku  akiwatilia  mashaka  wale wote  walio kuwa  wanataka  kwenda  ikulu  kwani alichokua anaamini Baba wa Taifa  kuwa  URAIS  ni utumwa  ila  alishangaa kuona watu  wanagombania  kwenda ikulu. 

Adha katibu kali  alisema  walio  zaliwa  mwaka 1974  watakumbuka  ilikuaje , lakini  watu  wanasahau  sana , sasa ivi  vijana  wa Kitanzania  wanabeza  Taifa  la TANZANIA   linalo  ongozwa na ccm, kwa kusema maisha magumu , huku  vijana hao wakiwa wamekaa na kazi  hawataki kufanya  badala yake wamekuwa wakilala mika kwenye mitandao  kuwa maisha magumu  aliwaomba vijana na kuwasihi kufanya kazi kwani akuna kitu kinacho kuja bule na wasipende  kudanganywa .

Alimalizia kwa kusema  kwa mwendo wa  wa mwenyekiti wake wa chama cha mapinduzi CCM  ambae pia ni Rais   wa Tanzania  ana uhakika  kabisa  mpaka  kufikia  mwaka  2020  upinzani Tanzania  utabaki  kuwa ni  mavumbi  kwani  haoni  kazi zozote ambazo  wabunge wa upinzani  wakifanya  zaidi ya vurugu  na kwamba hata wakifanya   bado wanatekeleza  irani ya chama cha  mapinduzi ccm  alitoa  rai kwa wana ccm wote  kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi Baba wa taifa kwa vitendo

 Katibu wa chama akizindua jiwe la msingi la  ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Sinza "A"  Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM)  Salum  Kali akishiriki ujenzi wa ofisi za chama kata ya Sinza A
 Katibu wa jumuia ya wazazi mkoa wa rukwa ndg chollaje nae alishiriki ujenzi huo
 Katibu wa wilaya akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  kata ya sinza Shafii Diwani
 Katibu wa wilaya akiwa kabidhi kadi wanachama wapya walio jiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kutoka vyama mbalimbali
 Mmoja wa wazee wa Chama Cha  Mapinduzi  Wilaya ya Ubungo Bi siwema  akitoa nasaha kwa wanachama wenzake
Viongozi wa jumuia ya umoja wa wanawake (UWT)  kata ya Sinza   wakishangilia

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa nj...