Saturday, October 28, 2017

MGANGA MKUU AKANUSHA WATOTO 9 KUFARIKI KISA KUKATIKA KWA UMEMEMganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Wonanji Timoth amekanusha taarifa za kufariki kwa watoto 9 waliokuwa kwenye Incubator kutokana na katizo la umeme hapo jana hospitali ya Mt. Meru, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote.


Dkt. Timoth amesema kwamba watoto waliofariki walikuwa wanne na sio 9 kama inavyoelezwa kwenye taarifa iliyosambaa mitandaoni, na wamefariki kwa matatizo mengine lakini sio kukatika kwa umeme.

Dkt. Timoth ameendelea kwa kueleza kwamba moja ya sababu iliyofanya watoto hao kufariki ni mama kuchelewa kufika hospitali kujifungua kwa kuwa alijifungulia nyumbani, pamoja na hatari kubwa wanazopata watoto njiti.

WAZIRI MPINA ACHOMA NYAVU KUKOMESHA UVUVI HARAMU

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwasha moto kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu Mjini Kigoma leo.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akimimina mafuta ya taa kabla ya zoezi la kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu mjini Kigoma leo. Nyuma yake ni baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma watumishi wa umma na wanahabari wakishuhudia tukio hilo.
 Nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zenye dhamani ya shilingi milioni 31 zikiteketea kwa moto kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu nchini.

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelalini na moja kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi hilo katika serikali hii ya awamu ya tano.
Akiongea mara baada ya kuteketeza nyavu hizo hizo mapema leo, Mpina alionyesha kushangazwa na suala la uvuvi haramu kuwa sugu “kwa nini vita hii haina mwisho? Lazima yawezekana mbinu zinazotumika ni dhaifu ama silaha zinazotumika ni duni, ifike mahala suala hili  liwe historia”. Alisema Mpina.
Akitoa Maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizi zinafanyika, Mpina aliwataka viongozi hao wawe na jukumu la kulinda rasilimali za taifa ikiwa ni mapoja na Bahari, Maziwa na mito.
“kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu, niitaaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa wamejuruhiwa.” Alisisitiza Mpina.
Akiwa katika ziara ya Oparesheni Maalum ya Ondoa Mifugo kutoka katika mikoa ya mipakani na nchi jirani akiwemo Mkoani kigoma, Mpina Pia alitembea mwalo mpya wa Kibirizi Mjini Kigoma na kumtaka Afisa Mifugo na Uvuvi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kushughulikia changamoto za mitambo wa kugandisha barafu inayokikabili kikundi shirikishi cha rasilimali za uvuvi mwaloni hapo pamoja na suala la kuwauzia dagaa wafanya biashara wanaozisafirisha nje ya nchi. Waziri Mpina Pia alitembelea chuo uvuvi mjini Kigoma.
Zoezi la opareshini ondoa mifugo na kukomesha rasmi uvuvi haramu limeanza rasmi kwa viongozi wa Wizara husika wakiongozwa na mawaziri Luhaga Mpina na Abdalah Ulega kuingia kazini katika mikoa inayokabiliwa na changamoto hizo.

WAZIRI MWAKYEMBE AINGILIA KATI SAKATA LA MZEE MAJUTO KUDHULUMIWA MAMILIONI YA PESA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa Mzee Majuto amedhurumiwa pesa milioni 25 na kampuni ya filamu ambayo jina lake amelihifadhi na kudai atatumia hata mshahara wake kuhakikisha anawafunga watu hao.
Mwakyembe amesema hayo leo Oktoba 27, 2017 alipokutana na wasanii mbalimbali kujadili changamoto za kazi ya sanaa nchini na kusema katika vitu ambavyo atapambana navyo ni pamoja na watu wanaowadhurumu wasanii haki yao na kuwaibia kazi zao za sanaa.

"Nilipopita Tanga nilikutana msanii nguli wa filamu Mzee Majuto nilikwenda kumjulia hali na bahati nzuri saizi anaendelea vizuri, Mzee Majuto akaniomba kitu kimoja na kuniambia naumwa nahitaji pesa lakini nimeshafanya kazi na kampuni hii akanionyesha na kuwa ameshatengeneza filamu zaidi ya 100 na kampuni hiyo kwa mkataba wa kulipwa fedha ndogo tu shilingi milioni 25 lakini huu ni mwaka wa  pili hajalipwa hata senti tano sasa hayo ndiyo mambo ambayo sifurahii, nimeshapeleka taarifa kwa hiyo kampuni tukutane Dar es Salaam na Dodoma asipokuja tunajua njia za kumsafirisha kwenye kalandinga mpaka Dodoma, huu ni wizi kama wizi wa kwenda kumchomolea mtu mfukoni" alisisitiza Mwakyembe

Waziri Mwakyembe aliendelea kufafanua kuwa kwa sasa yupo tayari kutumia pesa zake mfukoni kuhakikisha Mzee Majuto anapata haki yake kwa kazi mbalimbali alizofanya na kampuni hiyo.

"Mzee Majuto alikwenda Mwanza na familia kupokea ule mzigo, meneja kwa kumuheshimu akamfuata na kumwambia hiyo cheki hata senti tano hakuna na cheki iliyobaundi ni kosa la jinai, tunachezea watu hivi. 

"Mzee Majuto ameacha familia yake, amekaa Mwanza zaidi ya miezi sita anahangaika kuzipata hizo pesa, na mimi niko tayari nitatumia hata mshahara wangu twende mahakamani tufunge watu tumeshachoka huko ni kudharau watu" alisema Mwakyembe

Mwezi Agosti Waziri Mwakyembe alimtembelea msanii nguli na mkongwe wa filamu nchini Mzee Majuto nyumbani kwake ambapo alikwenda kumjulia hali baada ya kupata taarifa kuwa anaumwa.

Tigo Kukabidhi Nyenzo za Kidigitali shule ya sekondari wasichana Machame


 
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa akikata utepe kuzindua rasmi maabara yenye nyenzo za elimu ya kidigitali ya Tigo eSchools kwa shule ya sekondari wasichana Machame jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo. 
 Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa (aliyekaa kulia)akipata maelezo ya matumizi ya kujisomea vitabu kwa njia ya mtandao kupitia Tigo eSchools toka kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari wasichana Machame, Delynes Laurian mara baada ya kampuni ya Tigo kukabidhi huduma hiyo shuleni hapo jana. 
Mtaalam wa tovuti toka Shule Direct, Emmanuel George akielezea jambo kwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Gelacius Byakanwa wakati wa uzinduzi wa Tigo eSchools shule ya wasichana Machame leo. Wengine nyuma kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda kaskazini, Henry Kinabo, mwalimu mkuu wa shule ya Machame, Asteria Massawe. 
Umati wa wanafunzi wa shule ya wasichana Machame Machame wakiwa wanashuhudia uzinduzi wa Tigo eSchoolsl mapema jana.

NAIBU WAZIRI MGALU AZURU KITUO CHA UMEME ZUZU, DODOMA

HABARI
Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), wakati Naibu Waziri alipotembelea Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Kulia ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu. 
Na Veronica Simba - Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo eneo la Zuzu mjini Dodoma, leo Oktoba 28, 2017.

Akiwa amefuatana na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, Naibu Waziri Mgalu, ametembelea Kituo hicho ili kujionea utendaji kazi wake.

Akitoa malelezo kwa Naibu Waziri, Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina amesema kuwa, Kituo hupokea msongo wa umeme wa kilivolti 220 katika njia tatu ambazo ni Mtera, Iringa One na Iringa Two. Aidha, ameongeza kuwa, Kituo kina transfoma mbili za kupoza umeme ambapo kila moja ina uwezo wa kutoa megawati 24 za umeme hivyo kufanya jumla yake kuwa megawati 48.

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme kwa Mkoa wa Dodoma, Meneja Temu ameeleza kuwa kwa sasa huduma ya nishati hiyo muhimu imerejea katika maeneo yote baada ya jitihada za Shirika hilo katika kutatua matatizo yaliyojitokeza hivi karibuni.

Akihitimisha ziara yake katika Kituo hicho, Naibu Waziri Mgalu amewasisitiza viongozi wa TANESCO kuhakikisha huduma ya umeme wa uhakika inaendelea kutolewa kwa wateja katika maeneo yote.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia) kuhusu utendaji kazi wa Kituo hicho. Wengine pichani (kutoka kushoto) ni Msaidizi wa Naibu Waziri, Ngereja Mgejwa, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akiangalia kwa makini, kupitia Kompyuta, namna umeme unavyopokelewa katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu, Dodoma na kusambazwa kwa wateja. Anayetoa maelezo (kulia) ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina. Katikati ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akimwonesha Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), namna umeme unavyopokelewa kituoni hapo na kusambazwa kwa wateja.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia). Wengine pichani ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (wa pili kutoka kulia), Msaidizi wa Naibu Waziri, Ngereja Mgejwa (wa pili kutoka kushoto) na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (wa pili kutoka kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), wakati Naibu Waziri alipotembelea Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Wengine pichani ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Bosco Mgina (kulia) na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akiwa katika ziara ya kukagua Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma. Kulia ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia), alipotembelea Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Kushoto ni Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akikagua Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina.

SHIRIKA LA HAKI ELIMU YASHIRIKIANA NA JAMII KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU.

 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel,Arusha)
 Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii

Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakijiandaa kwenda kupaka rangi madarasa katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii
  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana

Mmoja wa wazazi shuleni hapo akishiriki zoezi la umwagiliaji wa maua katka maadhimisho ya huduma kwa jamii iliyoratibiwa na Shirika na Haki Elimu

Wafanyakazi wa Haki Elimu wakiwa wananendelea na zoezi la upakaji rangi shule hapo jana
Aliyeshika ndoo nyekundu ni Abraham Lazaro kutoka  Idara ya Habari na uchechemuzi akiwa na mfanyakazi mwenzake wakiendelea na zoezi la umwagiliaji  katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamiiMwanafunzi shuleni hapo akiwa amebeba ndoo kwaajili ya kubebea maji kwaajili ya shughuli ya umwagiliaji shuleni hapo jana

Meneja Idara ya Huduma, fedha na Utawala Daniel Luhamo akichimba shimo la kuhifadhia taka ngumu shuleni hapo

Mfanyakazi wa Haki Elimu Raphael akiendelee na shughuli ya upakaji rangi

Rose Mwenda Mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu kutoka Idara ya Ushiriki na Uwajibikaji wa jamii akipaka rangi bati katika shule ya Mukulat iliyopo Mkoani ArushaMwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari  Mukulat Stella Massawe akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa HakiElimu John Kalage, zawadi  iliyotengeneza katika klabu yao ya wanafunzi ya Njoo Tuzungumze
Mkuu wa Miradi HakiElimu - Boniventura Godfrey akibeba ndoo za kuchotea maji kwaajili ya umwagiliaji

Baadhi ya wazazi wakisalimia katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na tunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu


Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri   akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini John Kalage kwa kutambua umuhimu wa elimu Nchini
 Picha ya pamoja
Na Pamela Mollel,Arusha

Shirika lisilo la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mwingi  kwakutafuta maji.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.

Shirika hilo la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat  watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya kifugaji.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii  ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora

Ameiomba jamii kushirikiana na mashirika yasyoyakiserikali kupungumza changamoto  yanaozikabili shule za msingi na sekondari na kuitaka jamii kuhakikisha wanatunza miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi walikuwa wanapata shida kwa usafuri umbali mrefu kutafuta maji.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha miradi shirika la haki elimu Boniventura Godfrey  amesema kwa kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchni tayari wameanzisha mpango maalumu wa kuzisaidia shule za msingi na sekondari 127  katika wilaya ishirini na mbili kwa kuwasaidia miradi ya maji,uwekaji wa umeme wa jua ,ukarabati wa madarsa,na upelekaji wa vifaa vya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kuapata elimu katika mzngira bora.


Awali wakizungumzi miradi hiyo wanafunzi wa shule ya sekondari Mukulat  Stella Massawe wamelishukuru shirika la haki elimu kwa uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo kwa kuwa mradi huo wa maji utawapungumzia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa kusafuri umbali mrefu kwa kutafuta maji pamoj na kutumia muda wa masomo hivyo ,kupungua kwa changamoto hizo kutapunguza suala la utoro kwa wanafunzi. 

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa nj...