Friday, November 3, 2017

WANAWAKE BARANI AFRIKA WAKUTANA TANZANIA KUJADILI AMANI YA BARA LA AFRIKA

 Aliyekuwa katibu Mkuu wa Mkutano wa Beijing , Getrude Mongela akizungumza wakati wa mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
Mhasisi wa Mkutano wa Wanawake juu ya  Amani na kutatua matatizo Barani Afrika, Dr Basirat  Nahibi akizungumza juu ya suala la wanawake wa bara la Afrika kukutana kujadili na kuanda upatanishi juu ya mgogoro wa kisiasa unaondelea nchini Kenya.


Waziri wa Viwanda, Biashar na Masoko Kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Balozi Amina Salum Ali akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Muuandaaji wa mkutano huo kwa hapa Tanzania , Khadija  akimkabidhi kitabu Aliyekuwa katibu Mkuu wa Mkutano wa Beijing , Getrude Mongela
Mwanahabari Mwanamke mkongwe nchini Radhia Mwawanga akichangoa hoja katika mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
Mjumbe wa mkutano huo Madam Fanta Dissa Berthe akichangia jambo mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
Mhariri wa jarida la mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika, Fatma Othman Moma akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leoBaadhi ya Viongozi Wanawake walioshiriki Baadhi ya Viongozi Wanawake walioshiriki mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo wakifatilia mada zinazo endelea kwa Makinimkutano huo  wakifatilia mada zinazo endelea kwa Makini
Baadhi ya Viongozi Wanawake  walioshiriki mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo wakifatilia mada zinazo endelea kwa Makinimkutano huo  wakifatilia mada zinazo endelea kwa Makini
Picha ya Pamoja ya Baadhi ya Viongozi Wanawake  walioshiriki mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo wakifatilia mada zinazo endelea kwa Makinimkutano huo  wakifatilia mada zinazo endelea kwa Makini

TAMASHA LA SITA LA WATU WENYE ULEMAVU LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM,

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akimkabidhi Cheti cha Shukrani Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, kutoka kwa Shirikisho la Vyama vya wenye ulimavu Tanzania, SHIVYAWATA, wakati wa Tamasha la Sita la Watu wenye Ulemavu, lililofanyika kwenye ukumbi wa LAFP, Makumbusho jijini Dar es Salaam, leo Nov 2, 2017. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akizungumza wakati wa Tamasha hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Taifa, Ummy Nderiango.
Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, akizungumza wakati wa Tamasha hilo.
Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, akionyesha Cheti alichokabidhiwa katika Tamasha hilo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tamasha hilo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tamasha hilo.
Wakipasha misuli baada ya mazungumzo ya muda mrefu
Salamu.......
Paleeee, umeona eeeh....

PROFESA MWAKALILA WATAKA WANAFUNZI MWALIMU NYERERE KUACHANA NA SIASA WAKIWA SHULENI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo kigamboni,Profesa , Shadrack Mwakalila  ameagiza wanafunzi wa chuo hicho waliojiunga katika mwaka wa Masomo wa 2017 kutojiusiha na masuala ya siasa pindi wanapokuwa chuo na badala yake wazingatie katika suala zima la taaluma hili waweze kupata kile kilicho wapeleka chuoni hapo.

Profesa Mwakalila amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Mwaka wa kwanza juu ya nini wanatakiwa kufanya wakiwa chuoni hapo na kutambua nini cha msingi kilichowaleta.

"Hapa sio mahali pakufanya Siasa ni sehemu mliyokuja kuchua taaluma kamwe msikubali wanasiasa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmepoteza lengo ambalo limewaleta hapa katika kufanikisha malengo yenu ya kitaaluma"amesema Profesa Mwakalila.

Profesa Mwakalila ameongeza kuwa kama wanavyojua chuo hicho kimetokana na Mhasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius .K. Nyerere hivyo wanapaswa kufuata maadili na kuwa waadilifu hili kuweza kumuenzi mhasisi wa Taifa ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa sehemu hiyo iweze kupika viongozi wenye maadili mema kwa Taifa hili.

alimaliza kwa kutoa wito kwa wote waweze kukazana katika masomo yao hili waweze kuwa alama ya chuo hicho pindi wanapomaliza masomo yao na kufika hapo kwao isiwe majuto.

 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam,Profesa. Shadrack Mwakalila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho wa Mwaka wa kwanza ambao wamechaguliwa katika muhula wa Masomo 2017 kwa ngazi ya Cheti, Astashahada na Shahada juu ya umuhimu wa kufuata Maadili.
 Mshauri  wa Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akikazi jambo juu ya kuwa na maadili shuleni
 Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila
  Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila
 Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila

Thursday, November 2, 2017

AMREF HEALTH AFRICA YAZINDUA MRADI WA HAMASA KATIKA UZAZI WA MPANGO MIKOA 24

 Mkurugenzi mkazi wa Amref Health Africa, Dr. Florence Temu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Health  Afrika kwa mikoa 24 nnchi nzima hili kuweza kusaidia sekta ya Afya kwa   msaada wa Serikali ya Uholanzi.
 Mfamasia wa kitengo cha afya ya uzazi na Mtoto kutoka kutoka Wizara ya Afya Wanawake jinsia na Watoto, Machumu Mayeye akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa masuala ya afaya ya uzazi na mtoto
 Meneja mradi wa Masuala wa hamasa na Tiba kwa ajili ya afya ya uzazai na Uzazi wa mpango kutoka Amref Africa, Dr. Sarafina Mkuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam.
 Mfamasia wa kitengo cha afya ya uzazi na Mtoto kutoka kutoka Wizara ya Afya Wanawake jinsia na Watoto, Machumu Mayeye akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Hamasa na Tiba kwa Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango.
 Baadhi ya Wadau walioshiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Afrika kwa  msaada wa Serikali ya Uholanzi.
 Baadhi ya Wadau walioshiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Afrika kwa  msaada wa Serikali ya Uholanzi.

Baadhi ya Wadau walioshiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Afrika kwa  msaada wa Serikali ya Uholanzi.wakiwa katika picha ya pamoja

Wednesday, November 1, 2017

BASHE ASEMA MIMI SIO KIONGOZI WA NDIYO MZEE


Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amefunguka na kusema wakati anaomba kura na Mhe. Rais Dkt. Magufuli mwaka 2015 alimwambia kiongozi huyo kuwa yeye hawezi kwenda bungeni na kuwa kati ya wale wabunge wa kusema 'Ndiyo' mzee.

Bashe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wananchi wa jimbo la Nzega akiwaeleza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika miaka miwili jimboni hapo toka alipochaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 25, 2015.

"Mimi nikienda Bungeni nikisimama naposema nasema kweli kwa sababu kiapo cha CCM kinasema 'daima nitasema kweli unafiki kwangu mwiko' huo ndio msimamo wangu na siku naona kura na Mhe. Rais nilimwambia Rais jukwaani kwamba Mhe. Rais mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee bali mimi naenda kutimiza wajibu wangu na wajibu wangu ni kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali" alisema Bashe

Aidha Mbunge huyo alisema ataendelea kubaki na msimamo wake huo wa kuisimamia serikali labda mpaka wazee wa jimboni kwake wamshauri vinginevyo ili na yeye akiingia akae kimya avute pesa na kutulia kimya.

"Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM huwezi kumuachia mtoto wa jirani kutatua matatizo ya ndani ya nyumba yenu na huo ndiyo msimamo wangu lakini wazee mkisema baba eeh wewe nenda kawa mzee wa ndiyo mzee, zikija vuta saini nenda zako mtaani basi nitafanya hivyo kwa sababu nitakula good time kama wabunge wengine" alisisitiza Bashe

Mbali na hilo Bashe amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa wanapoelekea mwaka wa 2020 kuwa changamoto ya maji, umeme itakuwa historia jimboni hapo na kusema katika suala la elimu watahakikisha wanafika kiwango ambacho watajivunia. 

RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL Makonda leo amezindua zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema ujenzi wa Ofisi hizo utaenda kwa kasi ya hali ya juu chini ya Vijana wenye morali ya kazi kutoka JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.

Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani, Taa za kisasa na Umeme.
Akizungumza Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti RC Makonda amesema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika Mazingira mazuri yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.

Aidha RC Makonda amesema kama Walimu wakiboreshewa Mazingira ya kufanya kazi itasaidia kukuza ufaulu.

RC Makonda amepongeza Walimu kwa kuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa Darasa la saba ikitokea nafasi ya nne mwaka jana na kuwahimiza kukamatia nafasi hiyohiyo.
"Rais Magufuli ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi" Alisema RC Makonda.

Amewataka Viongozi kuacha Siasa kwenye mambo ya Msingi yanayolenga kuleta maendeleo kwakuwa Maendeleo hayana chama wala ubaguzi wa Dini.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar es Salaam Lazaro Mambosasa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule ambapo Wote kwa pamoja wamepongeza hatua ya RC Makonda kujenga ofisi za Walimu.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...