Thursday, November 9, 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA (TPFNET)


Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameliagiza jeshi la la Polisi nchini, kuendelea kuwapa kipaumbele askari wa kike katika mafunzo mbalimbali hili waweze kukabiiana na  vitendo vya uhalifu mpya ambao umeanza kushika hatamu ukiwemo ugaidi, uchochezi, uhafidhina, wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao, utakatishaji wa fedha haramu, ujangili, usafirishaji wa dawa za kulevya na makosa mengine yanayovuka mipaka.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ame sema hayo le  jijini Dar es Salaam, alipokuwa kifunga  maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania(TPF NET)  katika viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini yaliyokuwa na kauli mbiu ‘Usalama Wetu ni Mtaji wa Maendeleo, Tokomeza Uhalifu Kuwezesha Uchumi wa Viwanda”.

 “Tumeona juhudi zenu kwa kuweza kudhibiti uhalifu katika maeneo yaliyokuwa korofi ila ni jukumu lenu pia kuhakikisha kuwa mnakabaliana na vitendo hivi vya uhalifu ili kuhskikisha havivurugi hali ya amani na kuhatarisha usalama wa nchi”amesema .

Ameweka wazi  kuwa ni wazi kwamba shughuli za kiuchumi zitafanyika kikamilifu iwapo nchi itakuwa tulivu na yenye amani na kwamba amani na utulivu huo ndiyo utaleta kuaminiana na kukubaliana miongoni mwa wananchi na wawekezaji, hivyo suala la ulinzi na usalama ni muhimu katika maendeleo na ustawi wa nchi.


“Changamoto hizi bado ni kubwa  mno kwa baadhi yetu yanayotuzunguka  kutokana na imani iliyojengeka kwa wananchi kuwa matukio haya. Mara nyingi yakifika polisi wengine hushauriwa kuyamaliza nje ya dola ili kuficha kile kinachoonekana kwamba ni aibu jambo hilo linapojuliaka na watu wengi na hivyo kumnyima mhanga haki yake kisheria” alisema.

Alisema pamoja na kwamba jeshi hilo limejenga madawati ya jinsia ili kukabiliana na tatizo hilo lakini kuna umuhimu wa kuzidisha utoaji wa elimu kwa jamii ili kuwaelewesha kuwa wasiwe waoga wala wasione aibu kuripoti matukio hayo.


Hata hivyo alisema, Serikali inajitahidi kuboresha jeshi la polisi kwa kuendelea kulipatia vitendea kazi na itazidi kufanya hivyo kulingana na bajeti iliyopo sambamba na kushirikiana na wadau wenye nia njema ya kuwasaidiia
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kufunga mahadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
  Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea Zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Ahmad Masauni wakati wa mahadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Ahmad Masauni akizungumza wakati wa mahadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride Maalum la Askari wa Kike Tanzania wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Inspector Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema akizungumza wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Askari wa kike nchini wakipita na bango wakati wa Maandamano Maalum kwenye mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
Askari wa kike wakiw akatika gwaride maalum wakipita mbele ya  Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Askari wa kike wakiw akatika gwaride maalum wakipita mbele ya  Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa askari wa kike kutoka kikosi cha usalama Barabarani jinsi wanvyofanya kazi wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,akipokea zawadi kutoka kwa muwakilishi wa Halotel Tanzania wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akionesha kitabu chwa muongozo juu ya Dawati la kijinsia wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa kituo cha Polisi Mpwapwa , Mrakibu Msaidizi wa Polisi , Mohamed Mhina wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
Wednesday, November 8, 2017

SERIKALI YAPATA MABILIONI YA SHILINGI KUTOKA ALMASI ILIYOKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA JNIA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Madini , Angela Kairuki amesema kuwa serikali inataraji kupata mrabaha Zaidi katika madini ya Almasi yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K Nyerere kutoka kwa Kampuni ya Williamson Diamond iliyokuwa ikikitaka kutoroshwa nchini kwenda nchini Ubelgiji.

Waziri kairuki amesema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wakati akitoa ripoti ya Wizara ya Madini juu ya mzigo huo wa Almasi kutoka kampuni ya Williamson Diamonds.

“tarehe 20/10/2017 almasi hizo zilisafirishwa kwenda ubelgiji na serikali ilituma maafisa wake kusimamia uuzwaji wa alamasi hizo ambapo tarehe 7/11/2017 almasi hizo ziliuzwa kwa dola za Marekani 10,261,227.76 hivyo thamani hii ni ongezeko la Dola za Marekani 2,069,582.77 sawa na asilimia 20.16%”amesema.

Amesema kutokana na ongezeko hilo baada ya almas kuuzwa serikali itapata mrabaha Zaidi ambao ni mwisho kiasi cha Dola za Marekani 124,174,.97 na ada ya ukaguzi Dola za marekani 20,695.83 ambayo jumla yake ni dola za Marekani 144,870.80 sawa na shilingi Milioni 325.525 hivyo jumla ya mapato yote ya serikali kutokana na mauzo ya almasi hizi ni Dola za Marekani 718,288.95
Aidha waziri kairuki amesema katika mzigo huo waliweza kuikuta Almasi moja yenye rangi ya pinki ambayo ni adimu kupatikana na yenye uzito wa karatani 5.92 na kuuzwa kwa dola za marekani 2,005,555.00 sawa na shilingi Bilioni 4.51 .

Alimaliza kwa kusema kuwa anawakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea kuismamia kwa umakini rasilimali zetu za madini ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inanufaika ipasavyo.
 Waziri wa Madini Angela Kairuki akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ripoti ya faida iliyopata serikali katika Madini ya Almas kutoka mgodi wa  Wiliamson Diamonds Ltd iliyokamatwa uwanja wa ndege wa Jk Nyerere.
  Waziri wa Madini Angela Kairuki akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ripoti ya faida iliyopata serikali katika Madini ya Almas kutoka mgodi wa  Wiliamson Diamonds Ltd iliyokamatwa uwanja wa ndege wa Jk Nyerere.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini . Prof.Simon Msanjila akitoa ufafanuzi wa kitaalmu juu ya madini hayo yaliyouzwa huko ubelgiji.
 Kamishana wa Madini Mhandisi Benjamini Mchwampaka  akizungumzia juu ya madini hayo yanavyoweza kuliongezea pato taifa.
 Wahariri wa gazeti la Jamhuri Mkinga Mkinga na Deodatusi Balile wakiteta jambo katika mkutano huo

PAZIA LA MASHINDANO YA RIADHA YA KIGAMBONI MARATHONI LAFUNGULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mratibu wa Shindano la Kigamboni Marathoni,Dimo Debwe Mitiki akiwaonesha wana Habari Zawadi zitakazogawiwa kwa washindi wa mbio hizo zinazotaraji kufanyika Desemba 2 mwaka huu katika fukwe za Kigamboni jijini Dar es Salaaam
 Mratibu Mwenza wa Mbio za Kigamboni Marathoni , Juma Mtetwa akifafanua juu ya mbio hizo jinsi zitakazo fanyika na namna ya kujiandikisha kupitia Hospitali ya JPM Iliyopo Magomeni 
 Msemaji wa Chama Cha Riadha Nchini(RT), Tullo Chambo Akieleza namna chama hicho kilivyoshiriki katika kupima njia zote ambazo wakimbiaji watapita
 Mkurugenzi wa oparesheni wa kampuni ya uuzaji Viwanja ya Property International,George Obado akifafanua juu ya kampuni hiyo ilivyodhamini mbio ziytakazokimbiwa katika fukwe za Kimbiji Kigamboni.
 Meneja Masoko wa Hospitali ya JPM iliyopo Magoemni Jijini Dar es Salaam,Mja Abeid akileza namna hospitali hiyo itakavyoshiriki katika zoezi la upimaji wa afya kwa washiriki na kuuza fomu za wakimbiaji pamoja na kutoa huduma kwa watu watakaopata majeruhi
Waandaaji wa Mbio za Kigamboni Marathoni wakiwa katika picha ya Pamoma mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo

Tuesday, November 7, 2017

KITABU KICHOZUNGUMZIA UCHUMI WA DALADALA NCHINI CHA ZINDULIWA DAR ES SALAAM

 Mwandishi na Mtunzi wa Kitabu cha Taken For Ride,Dr Matteo Rizzo  akitoa ufafanuzi juu ya kitabu hicho kinachozungumzia biashara ya Daladala nchini mpaka kufikia kwenye mradi wa mabasi yaendayo Haraka, Mwandishi huyo ameonesha katika kitabu hicho namna biashara ya daladala nchini na katika Uchumi wa mtu mmojammoja wa madereva na Makonda.   
  Mwandishi na Mtunzi wa Kitabu cha Taken For Ride,Dr Matteo Rizzo  akitoa ufafanuzi  juu ya kitabu hicho kinachozungumzi masuala ya Daladala  na kugusia uchumi katika usafiri wa mabasi yaendayo haraka Dart.


Mtafiti Tasisi ya Utafiti ya Repoa , Dr Blandina Kilama akifafanua jambo mara baada ya kuwasilishwa kwa kitabu cha Taken to Ride kilichoandikwa na Mtafiti Dr Matteo Rizzo
 Mbunge wa Kigoma Mjini Zito Zuberi Kabwe akichangia mada wakati wa mjadala wa kitabu hicho uliofanyika katika ukumbi wa Repoa Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
 Mchambuzi wa masuala ya uchumi  nchini Profesa Honest Ngowi  Akichangia mada mara baada ya kuzinduliwa kwa kitabu hicho
  Baadhi ya watu walioshiriki katiika uzinduzi wa kitabu  kinachozungumzi masuala ya Daladala  na kugusia uchumi katika usafiri wa mabasi yaendayo haraka Dart.

Monday, November 6, 2017

EFM MZIKI MNENE YATEKA WAKAZI WA KIBAHA NA VITONGOJI VYAKE

 Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Mshiriki wa Coke Studio Afrika kutoka Lebo ya Wasafi, Rayvan akitoa Burudani  kwa wakazi wa Kibaha katika tamasha la Efm Mziki Mnene mkoa wa Pwani
 Mtangazaji wa kipindi Cha Genge Pido na Mc Wa Efm Mziki Mnene akiwa na Mashabiki wa kipindi hicho katika Tamasha la Mziki Mnene Kibaha  mkoa wa Pwani
 Msanii wa Bongo Fleva nchini Msami Baby akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani

Msanii Mkongwe wa Muziki wa Hip Pop nchini Squizer akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 Msanii Mkongwe wa Muziki wa Hip Pop nchini Squizer akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 RDJ Mamy kutoka kipindi cha Joto la Asubuhi cha Efm Radio  akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 RDJ X5 akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 Msanii Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva nchini Prince Dully Sykes  akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 Msanii Muziki wa Singeli nchini Majid Migomba  akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 Mashabiki na wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 Msanii  wa Muziki wa Hip Pop nchini Billnas akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 RDJ Spur  akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
 RDJ Autrun akitoa Burudani kwa wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani
  Mashabiki na wakazi Kibaha katika Tamasha la Efm Mziki Mnene  Mkoa Pwani

Sunday, November 5, 2017

JUKWAA LA KATIBA KWENDA MAHAKAMANI KUDAI MAANDAMANO

 JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata), limesema kuwa litalifikisha jeshi la Polisi Mahakamani, kudai haki ya kikatiba kufuatia kuzuiwa kufanya maandamano ya amani.

Shauri hilo litaongozwa na jopo la mawakili wakiongozwa na Dk. Rugemeleza Nshala kudai haki hiyo. 

Mwenyekiti wa Jukata Hebron Mwakagenda alisema jana jijini Dar es Salaam, kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kuzuia maandamano yaliyotakiwa kufanyika Oktoba 30mwaka huu.

Alisema barua kutoka jeshi hilo ikielezea kwamba maandamano hayo yataathiri mitihani ya Kidato cha nne inayoendelea nchini, kutojibiwa barua na Ikulu ya kukubaliwa ili rais apokee maandamano hayo, ni sababu ambazo hazina msingi.

"Hadi Leo hatujapata majibu ya barua iliyotumwa Ikulu kwa Rais, juu la ombi ingawa lakini jeshi limetuandikia barua kutuzuia, kabla ya kukataliwa au kukubaliwa na Rais," alisema Mwakagenda.

Alisema Jukata lilipanga kufanya maandamano hayo ili kuunga mkono jitihada ya Rais John Magufuli katika kusimamia rasilimali za taifa, kupiga vita rushwa pamoja na kukumkumbusha kuendeleza mchakato wa Katiba mpya.

Pia maandamano yalilenga kufikisha ujumbe wa wananchi kwa rais kuhusu haja ya serikali kurejesha mchakato huo, ili ipatikane katika uongozi wa awamu ya tano.

Mwakagenda alisema wanatatajia mahakamani itaeleza kwa namba gani wananchi wanapaswa kutumia haki ya kikatiba.

"Ibara ya 107 (A) (1) inasema ..Mahakama ndio yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakamani," alisema.

Alisema mahakama pia itatoa tafsiri ya mahakama kuhusu namna jeshi la polisi linavyotumia vifungu 43 (3) na 44 vya sheria ya jeshi la polisi ya mwaka 2002.

"Taarifa za kiintelijensia kwamba kuna viashiria vya uvunjifu amani havina ukweli, mahakama itatuamulia," alisema Mwakagenda.

ASKOFU MALASUSA AONGOZA MAELFU YA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KATIKA IBADA YA MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA

 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa  akiongoza  Maelfu ya Waumini wa KKKT wa Dayosisi hiyo katika Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.


Naibu Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mission na Uinjilisti Mchungaji, Boniface Kombo akiongoza Lutrijia wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.
 Mchungaji Lewis Hiza akisoma somo la pili wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengezo ya Kanisa la KKKT iliyoadhimishwa na Dayosisi ya Mashariki  na Pwani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Mchungaji Muke Najua  kutoka nchini Afrika kusini akitoa mahubiri wakati  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa hilo iliyofanyika  Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Kundi la watoto zaidi ya 4000 waliopata Ubarikio wa Kipaimara wakati wa Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa la KKKT Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Wachungaji mbalimbali wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani wakito ubarikio kwa Vijana wa kanisa hilo amabo wamepata kipaimara leo  katika Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.
 Wachungaji mbalimbali wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani wakito ubarikio kwa Vijana wa kanisa hilo amabo wamepata kipaimara leo  katika Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa.
Waumini wa Kanisa la KKKT wakiwa katika  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Watoto wa Shule ya Jumapili wakiwa katika alaiki   wa Kanisa la KKKT wakiwa katika  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa akiwa katika Maandamano ya kuingia Uwanjani wakati wa Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa wakati wa Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa
 Waziri Mkuu wa Zamani Fredrick Sumaye akiwa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ibada ya miaka 500 ya  Matengenezo ya Kanisa

Waumini wa Kanisa la KKKT wakiwa katika  Ibada ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO UCHINA

Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maharufu kama China International Beauty Expo African Hall,Rex Chan akizungumza na Waanddishi w...