Thursday, November 16, 2017

JK AWATAKA WASANII WA BONGO MOVIE KUJIONGEZA NA KUACHA KULALAMIKIA SERIKALI

 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati wa uzinduzi Televisheni  inayoshughulika na masuala ya filamu za Kitanzania kwa Wasanii wa Bongo Movie JTv ambayo itapatikana kupitia king'amuzi cha Star Times amabpo amewataka wasnii hao kujiongeza hili waweze kufanya kazi kama wasanii kutoka nchi za Magharibi.
 Waziri wa habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harisson Mwakyembe akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa Televisheni ya Jtv  itakayooneshwa kwenye king'amuzi cha Star Times
 Mkurugenzi wa Jtv, Jason Msimbe akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha  Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye uzinduzi wa televisheni yake
 Baadhi ya Wasanii walioshiriki katika uzinduzi wa Tlevisheni mpya ya Jtv ambayo itakuwa inaonesha filamu za kitanzania kupitia King'amuzi cha Star Times
 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiteta jambo naWaziri wa habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harisson Mwakyembe na Mkurugenzi wa JTv Jason Msimbe
  Baadhi ya Wasanii walioshiriki katika uzinduzi wa Tlevisheni mpya ya Jtv ambayo itakuwa inaonesha filamu za kitanzania kupitia King'amuzi cha Star Times
   Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Star Times mara baada ya uzinduzi wa Jtv
 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Mkurugenzi wa Star Times juu ya uwezekano wa kampuni hiyo kutoa ufadhili wa mafunzo ya vitendo kwa waandaaji wa filamu nchini  kwenda China
 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Star Times
Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii wa Bongo Movie walioshiriki uzinduzi wa Televisheni ya Jtv

Wednesday, November 15, 2017

MAKONDA AHAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MABAHARI NCHINI


Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na mabahari leo jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua mkutano wa  mabaharia hao.

Na Anna Chiganga .

Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda ameahidi kutatua changamoto zinazowakabili mabahari  kwa lengo la kuwawezesha mabaharia kupata kazi ndani na nje ya nchi.

Makonda ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa mkutano wa mabaharia  ulifanyika jijini Dar es Salaam, na kusema changamoto hizi zikitatuliwa zitaweza kutatengeneza fursa ya watu kupata kazi, kuheshimika na usalama wa mwajiriwa, uhakika wa kazi pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi.

"Naamini changamoto zote hizi ambazo nimeziona zipo kwenye makundi matatu ninaweza kuzitatua na tutaendelea kushirikiana na kuweka mikakati itayowawezesha mabaharia kunufaika, na niwahakikishie kwamba tutafanikiwa." Amesema

Changamoto hizo zimewasilishwa na mabahari kupita risala iliyosomwa na Aloyce Mpazi, ambapo.wamemwomba Mkuu wa mkoa wa Dar Makonda kuwasaidia kutatua changamoto hizi kikamilifu ili kuboresha  kazi za mabaharia

Aidha  Makonda amebainisha kuwa zikitokea nafasi za kazi kwa mabaharia watapewa kipaumbele ili waweze kulinda vyema rasilimali za nchi na kuepusha kusafirisha Mali za magendo na kusaidia kukuza uchumi wa taifa kwa kuweza kulipa kodi kikamilifu.

Pia amezungumzia suala la.upimaji afya bure litakaloanza November 19, mwaka huu litakalofanywa na madktari kutoka China na watafanya huduma hiyo bure kwa Siku saba na kuwaambia mabaharia ni fursa kwao kuweza kupima afya kwa lengo la kuchukua taadhari mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa.

"Nawataka wanachi wote wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupima afya bure November 19 itakayotolewa na madktari 381,kutoka  nchi ya china na ni fursa kwa ninyi mabaharia kupima afya zenu sitopenda kuona au kusikia Baharia au mkazi wa mkoa huu anaumwa ghafla tahadhari ni bora kuliko tiba". Amesema Makonda.

NAIBU MEYA MANISPAA YA ILALA OMARY KUMBILAMOTO AONGOZA KAMATI YA FEDHA NA UTAWAL KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO

Mchumi wa manispaa ya ilala (katikati) Ando Mwankunga akizungumza walipofanya ziara katika  ujenzi ofisi ya kata Mvuleni ambapo inaendelea kujengwa.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Enock Segesela,(kulia)  akielezea jambo.
Hii ndiyo ofisi ya kata ya Mvuleni inayoendelea kujengwa, ambapo ina chumba cha Mwenyekiti,ofisi ya chumba cha mtendaji kata,ukumbi wa mikutano,choo,pamoja na stoo ya kuifadhi vitu.

 Naibu Meya katika Manispaa ya ilala (kushoto) Omary Kumbilamoto pamoja na diwani wa kata ya segerea Edwin Mwakatobe   wakikagua Kisima cha maji katika kata ya segerea
Diwani wa kata ya Segerea kushoto akielezea kuhusu mradi wa maji unavyotekeleza na umekaribia kukamilika.Hapa ni katika daraja la Segerea ambapo diwani wa kata hiyo akielezea changamoto zinazotokea wakati mvua inanyesha ambapo wakazi wa maeneo hata wanakumbwa na adha ya maji kujaa na kuingia katika makazi yao.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Kamati ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imefanikiwa kutekeleza  asilimia 98 ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokusudiwa kutekeleza katika awamu ya kwanza ya mwaka fedha wa 2017/2018 katika kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba kutumia Sh bilioni 1.2 kati ya Sh bilioni 2.5 zilizotakiwa kutumika.

Hayo yamesemwa leo na Mchumi wa manispaa hiyo Ando Mwankuga baada ya kufanyaamesema ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuweza kujionea kile walichopanga kuwa kimetekelezwa kwa ufanisi, na baadhi ya miradi imekamilika na mingine ikiendelea kutekelezwa kikamilifu.


Amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo kuna changamoto mbalimbali ambapo miradi mingi inaanzishwa lakini haikamiliki  kwa wakati ambapo miradi hiyo hufanyika kutokana na vyanzo mbali mbali vya fedha za ndani na ruzuku ya serikali  na kukuta mradi ni mkubwa kuliko kiwango cha fedha,l kilichopo,pia amewaomba madiwani kupitisha bajeti kulingana na miradi ili kutatua changamoto ya miradi kutofanikiwa. 


Aidha amewashukuru madiwani katika manispaa ya ilala kwani ni watu makini na wanaelewa kile wanachokifanya na pia wanakosoa na kutoa changamoto vizuri kwa lengo la kuleta maendeleo katika mispaa hiyo

Miradi iliyokaguliwa ni Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mvuleni kata ya Msongola, Ujenzi wa Barabara ya Segerea hadi Bonyokwa, Ujenzi wa Kisima na Miundombinu ya maji Mtaa wa Segerea pamoja na Jengo la DMP liliopo ndani ya maanispaa hiyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni NaibuMeya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amesema kuwa wataalamu waliokabidhiwa miradi wamefanya kazi kwa kuzingatia maadili na uadilifu na kuchangia kukamilika kwake.

Naye Diwani wa Kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe amesema miradi iliyotekelezwa kwenye kata hiyo imetokana na fedha zilizotengwa na kutumika ipasavyo.   

Afisa Mtendaji Kata ya Msongola Enock Segesela, ameishukuru Manispaa kwa kujenga Ofisi ya Serikali za Mtaa ya Mvuleni kwani awali walikuwa wamepanga katika fremu na kulipa kodi

MAVUNDE AFUNGUA KONGAMANO LA VIONGOZI VIJANA BARANI JIJINI DAR ES SALAAM


 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Viongozi Vijana Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo ambao umehudhuliwa na Vijana Zaidi ya 100 kutoka Mataifa mbalimbali  ulikuwa ukijadili namna ya fursa zilizopo kwa Vijana katika kutumia rasilimali za nchi zao kama Viongozi katika kujiletea maendeleo
 Mratibu wa kongamano hilo kutoka Tasisi ya The Open Society Initiative for Eastern Africa,Adam Anthony akizungumza kablaya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua kongamano hilo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akiwa meza kuu pamoja na Mratibu wa kongamano hilo kutoka Tasisi ya The Open Society Initiative for Eastern Africa,Adam Anthony na Balozi wa Uholanzi nchini Lianne Houben
 Balozi wa Uholanzi nchini Lianne Houben, akitoa neno kwa vijana kama mfadhili wa kongamano hilo lililowaleta Viongozi Vijana zaidi ya 100 kutoka bara la Afrika
 Msanii wa Muziki wa kughani na mshahiri maharufu barani Afrika , Mrisho Mpoto akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nini Vijana wanatakiwa kufanya hili waweze kuwa Viongozi bora katika mataifa wanayotoka

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde , akipiga Selfier na Vijana walioshiriki Mkutano huoVijana walioshiriki Mkutano wa Viongozi Vijana Barani Afrika wakifatilia mada mbalimbali zinazoendelea katika kongamano hilo
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Vijana walioshiriki kongamano la Viongozi Vijana Barani Afrika

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Dk. Akwilapo afungua mkutano wa wadau wa elimu

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akifungua mkutano wa 9 kwa wadau wa sekta ya elimu nchini ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT). Mkutano huo umeanza leo New Dodoma Hoteli, Mkoani Dodoma. Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao akizungumza leo kwenye mkutano wa 9 wa wadau wa sekta ya elimu nchini ulioandaliwa na TenMeT. Mkutano huo wa siku tatu umeanza leo New Dodoma Hoteli, Mkoani Dodoma. Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo mara baada ya kufungua mkutano wa 9 kwa wadau wa sekta ya elimu nchini ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania Dk. Mkonongwa Mhadhiri UDSM akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.

Wahanga wa Soko la Sido Mbeya walipwa na Bima.

Na Oyuke Phostine.
Zaidi ya wafanyabiashara themanini waliokata bima wamelipwa fidia yenye thamani ya kiasi cha fedha cha takribani TZS 1,538,653,057.08 kupitia kampuni za bima zilizosajiliwa kisheria kutoa huduma hapa nchini baadaya wafanyabiashara hao kupatwa na janga la bidhaa zao kuungua katika soko la sido Mbeya mwezi Agosti mwaka huu.

Kamishna wa Bima nchini Dr. Baghayo Saqware akitoa elimu ya bima kwa wafanyabiashara wa soko la Sido Mbeya juu ya namna bima linavyosimamiwa na kurekebiwa na Mamlaka ya Bima nchini (TIRA) sambamba na zoezi la kutoa hundi kwa wahanga amewashauri wafanyabiashara nchini kutumia huduma za bima ili kukinga biashara zao dhidi ya majanga yasiyotarajiwa.

“Na kwa bahati nzuri mfano mzuri na halisi wa faida ya kukata bima ili kukinga biashara zenu uko miongoni mwa wenzenu hapa. Janga ni jambo lisilo na hodi wala taarifa hivyo ni vyema na busara kujikinga nalo kupitia mifumo ya bima” alisema Dr. Saqware.

Pia Dr. Saqware aliwataka watanzania kuondokana na dhana hasi pamoja hofu iliyojengeka siku za hivi karibuni kuhusu huduma za bima kwa sababu sekta hii inasimamiwa kikamilifu na Mamkala ya Bima na makampuni yote yanayofanya shughuli hizo yamesajiliwa na (TIRA) na yanawajibika kisheria kutoa huduma zinazokidhi viwango.  

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Amos Makalla, amesema kwa sababu Mamlaka ya bima ni chombo cha ushauri kwa Serikali kuhusu masuala ya soko la bima, ni imani yake kuwa wananchi sasa hawatasita kukata huduma za bima. Na iwapo kutakuwa na msigano kati ya makampuni ya bima na wateja anaamini Mamlaka iko tayari kuutatua kwa faida ya uchumi wa taifa.

“Soko lilipoungua ni zaida ya Tsh. 14 bilioni ziliteketea, hivyo kama wafanyabiashara wote wangekuwa na bima angalau wangeweza kunufaika kwa kupewa fidia” alisema Mh. Mkalla.

Pia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameyataka makampuni ya bima nchini kwenda na kasi ya Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za bima nchini kwani imelenga kuwakwamua wananchi dhidi ya umasikini.
Pamoja elimu iliyotolewa Mamlaka ya Bima nchini inayataka makampuni na wataalamu wa bima nchini kuongezeni huduma na elimu kwa wananchi, na pia walipe madai ya bima haraka bila usumbufu ikiambatana na lugha nzuri kwa wateja.

Naye Bw. Erasto Sanga mmoja wa wahanga moto katika soko la sido ametoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kukata bima kwa sababu imekuwa ni mkombozi wa biashara zake kwani mara zote tatu alizounguliwa na bidhaa zake bima imekuwa ikimunufaisha kwa kumrejesha kwenye biashara.
“Mara ya kwanza moto uliunguza bidhaa zangu mwaka 2006 katika soko la Mwanjelwa nilipata hasara kwasababu sikukata bima baada ya hapo nilikata bima na mar azote tatu nilipounguliwa nililipwa fidia na kampuni niliyokata bima kwao” alisema bw. Sanga.

Pia ni muda mwaafaka kwa Serikali za Mkoa nchini kushirikiana kwa pamoja kuwadhibiti wahalifu katika shughuli za bima kwa sababu kuna wahalifu wachache wanauza bima feki hususani za magari. Hili linaweza fanikiwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Mahakama katika kuharakisha upatikanaji wa haki za wakata bima.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akitembelea soko la bima akiwa na Kamishana wa Bima nchini Dr. Baghayo Saqware (Kulia), Mwenyekiti wa soko na Kamana wa mkoa wa Mbeya Mpinga 
 Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuliza Bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bi. Consolata Gabone akitoa historia fupi ya soko la SIDO.
 Kamishna wa Bima Nchini Dr. Baghayo Saqware akiongea na wafanyabiashara wa soko la SIDO Mbeya (hawako pichani) kuhusu umuhimu wa Bima kwa biashara zao.
 Wafanyabishara wa soko la SIDO Mbeya wakimsikiliza Kamishna wa Bima nchini Dr. Baghayo Saqware alipokuwa akielezea umuhimu wa Bima kwa biashara zao.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akimkabidhi Bw. Mohamed Omary Magayu mfanyabiashara wa Soko la SIDO Mbeya mfano wa hundi ya ya fidia aliyolipwa baada ya kukata bima.

Tuesday, November 14, 2017

PROF KAMBI AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA WADAU WA SEKTA YA AFYA NCHINI

 Mganga Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof  Mohamemed Kambi  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la  nne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambalo lilipata fursa ya kujadili jinsi ya kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya Afya Tanzania.
 Rais wa Kongamano laNne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini, DK Omari Chilo akizungumza kabla ya kumaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la nne la wadau wa sekta hiyo lililofanyika Jijini Dar es Salaam leo.
Kiongozi Mkuu wa  HDIF, David McGinty akizungumza katika Mdahalo wa mabadiliko ya Sayansi Ubunifu na Sera katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya wakati waKongamano la nne la wadau wa Sekta ya Afya nchini

Mratibu wa wa Kongamano la 4 la Sekta ya Afya nchini Dr Peter Maduke akizungumza wakati wa kongamno hilo likiwa linaendelea katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Madaktari waliohudhuria Kongamano la Nne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini
 Meneja wa Tanzania kutoka kampuni ya Sproxil, Ashok Maurya, akimueleza mmoja wa wadau wa Sekta ya Afya namna ya mradi wa huduma ya simu za mkononi katika sekta ya Afya unavyofanya kazi.
 Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka HDIF, Hannah Mwandolomo akitoa ufafanuzi kwa wadau waliofika katika banda la maonesho ya programu hiyo wakati wa Kongamano la nne la wadau wa sekta ya Afya nchini lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa  Mkuu wa programu ya  DTREE International,Erica Layer akizungumza na wadau wanaofadhiliwana mradi wa HDIF wakati wa Kongamano la 4 la sekta ya Afya nchini

Monday, November 13, 2017

SHIRIKA LA FOUNDATION FOR CIVILI SOCIETY WAPANGA KUSAIDIA WATOTO WANAOTIBIWA MOI

Katika kuhakikisha kuwa wanaisaidia Jamii inayowazunguka shirika lisilo la kiserikali la The Foundation Foundation for civil Society limejipanga kuwasaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatikana katika Taasisi ya mifupa MOI jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa shirika hilo kuadhimisha siku yao maarufu ya “GIVING TUESDAY” ambayo hutumia siku hiyo kuisaidia jamii.

Akieleza mikakati ya kuadhimisha siku hiyo kwa mwaka huu mwakilishi kutoka shirika hilo Ndugu Karin Rupia amesema kuwa baada ya kuona changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wanaohudumiwa katika taasisi hiyo wameamua kuitumia siku hiyo kuwasaidia watoto hao huku akiwataka watanzania kuwaunga mkono katika kutekeleza Jukumu hilo.

Mwakilishi huyo amesema kuwa shughuli hiyo itafanyika kwa siku mbili ambapo siku ya kwanza itakuwa tarehe 25 Novemba ambapo wataitumia kuchangia damu kwa ajili ya watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ,zoezi ambalo litafanyika ndani ya taasisi hiyo ya Mifupa MOI kuanzia saa tatu asubuhi hadi majira ya mchana

Katika zoezi la pili litafanyika tarehe 28 Novemba ambayo ndiyo siku maalum ya Jumanne ya kutoa “Giving Tuesday” ambapo katika siku hiyo shirika limejipanga kusaidia watoto katika kuwapatia mahitaji mbalimbali ambapo shughuli kubwa itakuwa ni kuwasaidia watoto kupata upasuaji ambapo amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa wanasaidia watoto mia moja kupata huduma hiyo ya upasuaji.pamoja na kuwadaia vifaa mbalimbali vitakavyosaidia katika kwa watoto hao ambapo watanzania wametakiwa kujitolea kuchangia kwa kasi ili kusaidia shirika hilo kufikia malengo hayo.

Ili kushiriki katika zoezi hilo la kuchangia damu kwa ajili ya ,kuwa unaweza kupiga simu namba 0762767237.
Video ikifafanua kuhusu siku hiyo ya Jumanne ya kutoa “Giving Tuesday”

Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii.

Na Lusungu Helela- MNRT

Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Utalii wameombwa kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deograsius Mdamu, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam  na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi   Sehemu ya Maendeleo  ya Utalii katika Wizara hiyo , Bi. Uzeeli Kiangi  katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu mwanzoni mwa mwezi Julai kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma akiwa ameitumikia Wizara kwa kushika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema  ‘’ Watumishi ni kiungo muhimu katika kumsaidia Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutekeleza majukumu yake, ni matumaini yangu kuwa mtampa ushirikiano katika hili’’

Amesema kupitia  ushirikiano huo  utasaidia kupelekea Wizara kutimiza azma ya kufikia watalii milioni 8 na fedha za kigeni dola bilioni 20 kila mwaka kufikia mwaka 2025

Aidha, Bi.Kiangi aliwataka watumishi kuzingatia miiko ya kazi zao kwa kutojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa wanapotimiza majukumu yao, la sivyo serikali hii ya awamu ya tano haitawaacha salama.

‘’Wakati wa utumishi wangu nilijitahidi kukwepa kupokea rushwa kwa kuwa sikujua huyu anayetaka kunihonga katumwa na nani na kwanini anipe rushwa wakati natimiza majukumu yangu jihadharini na watoa rushwa’’ alisisitiza

Katika hatua nyingine,  Bi. Kiangi aliwataka  watumishi wenye tabia ya kujituma kufanya kazi pale tu wanapohisi kazi hiyo ina malipo wajirekebishe mara moja kwa kuanza kufanya kazi zote zenye malipo na zisizo na malipo kwani zina umuhimu katika kuwajenga kitaaluma.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu alisema Idara yake imejipanga kufanya kazi kwa kasi zaidi na kuendeleza yale ambayo Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Kiangi aliyokuwa akiyapigania kwa ajili ya maendeleo ya utalii.

‘’Wizara inatambua mchango wako tangu ulipoajiriwa mwaka 1984, tunakuahidi tutakutumia pale tunapohitaji utaalamu wako ili kuhakikisha Wizara inafikia malengo iliyojiwekea’’ alisisitiza

Kwa upande wake, Afisa Utalii Mwandamizi, Josephat Msimbano  wakati  amesema Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa utumishi wake alikuwa ni kiongozi aliyeichukia rushwa na yeyote aliyethubutu kutaka kumhonga ili ahudumiwe kwa minajili ya kupindishwa kwa sheria  aligonga mwamba.

Naye Afisa Utalii, Domina Moshi  amesema kwa upande wake, Bi Uzeeli Kiangi alikuwa ni mshauri mzuri, alikua zaidi ya mama na alipenda watumishi wajiendeleze kielimu na ndiye aliyemfanya aende masomoni nchini kujiendeleza kielimu.

Bi. Uzeeli Kiangi kastaafu kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma akiwa ameihudumia Idara ya Utalii katika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33 ambapo aliajiriwa mwaka 1984 kama Afisa Utalii Daraja la tatu ambapo alipandishwa madaraja hadi kufikia Afisa Utalii Mwandamizi daraja la kwanza mwaka 2007.

Mwaka huo huo alipandishwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Leseni na Uthibiti kwa kipindi cha miaka mitano. Pia, mwaka 2013 hadi julai 2017 alikuwa Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii

 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam  na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (katikati)  katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa Utalii Domina Moshi (kushoto)  

 Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza jijini Dar es Salaam  na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii  katika hafla fupi ya kuagwa kwake baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akimkabidhi moja ya  zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma  
 Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akiwa na Afisa Utalii, Nina Kisando (katikati) wakiwa wanatabasamu huku  wakionesha moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki  baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu. 
 Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii wakimsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria ya  Utumishi wa Umma.
 Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akikata keki katika katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma tayari kuwalisha Watumishi wa Wizara. Kushoto kwake ni Marygoreth Mushin a Kulia kwake ni Mary Msekela.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...