Saturday, November 25, 2017

MJEA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WAISLAMU NCHINI

 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank,Bakari Kisuda  akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa  Afrika ya Mashariki (MJEA) kwa kushirikiana na kampuni ya KO Innovates zimeendesha  mafunzo kwa waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari vya Kiislamu hapa nchini.
Mwenyekiti wa MJEA, ABUOBAKARI FAMAU,amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari wanaotoka kwenye vyombo hivyo vya habari ili waweze kuendana na mazingira ya sasa ya tasnia ya habari.
FAMAU  ameongeza kuwa vyombo vya Kiislamu vina wajibu kubwa sana kwa jamii na hivyo kuna haja ya kukumbushana juu ya wajibu huo.
nae  Khadijah Omar amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwakutanisha waandishi wa habari wa vyombo vya Kiislamu na kubadilishana uzoefu.
Zaidi ya washiriki 25 wamepatiwa mafunzo hayo ambayo yatafanyika Novemba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Tangaza House jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank,Bakari Kisuda  akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa  Afrika ya Mashariki (MJEA)
Waandishi wa Habari wa Mashirika ya Kislamu nchini wakifatilia hotuba ya mgeni Rasmi kwa makini

POP UP YA SWAHILI FASHION WEEK YAWA GUMZO KWA WANA MITINDO

 Mwanamitindo wa kampuni ya African Doll akimuonyesha nguo ndugu John Ulanga katika Swahili Fashion week Pop Up iliyofanyika Nyumbani kwa Balozi wa Italy jijini Dar es Salaam
 Mwanamitindo,Diane Kapela kutoka Naled Fashion Tanzania akiweka sawa bidhaa zake katika Pop Up ya Swahili Fashion Week iliyofanyika Nyumbani kwa Balozi wa Italy
 Mwanamitindo Maharufu nchini Martin Kadinda, akichagua nguo za Mwanamitindo Kulwa Mkwandule katika Pop Up ya Swahili Fshion Weeek iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Italy
 Mwanamitindo Manca Mushi akiuza bidhaa zake za mikoba na nguo kutoka kwa moja ya wateja waliofika katika Pop Up ya Swahili Fashion Week
Mwanamitindo Rebecca Mwaipopo  akiwaonyesha wateja wake  nguo wakati wa Pop Up ya Swahili Fashion Week iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Italy jijini Dar es Salaam

KUMBILAMOTO; VIJANA MUUNGENI MKONO RAIS MAGUFULI AMEFANYA MAKUBWA

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na umoja wa Vikundi vya Jogging Vingunguti mara baada ya kumaliza uasafi wa mwezi katika juhudi za kumuunga mkona Rais John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania iwe s
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akiongoza zoezi la Usafi katika mtaa wa Miembeni kata ya Vingunguti kama agzio la Rais lilivyotaka kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi watu kufanya usafi
 Afisa Ugavi wa Manispaa ya Ilala,Vicent Odero akitoa shukrani kwa umoja wa Vikundi vya Jogging Vingunguti kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Mwisho wa Mwezi
 Afisa usafishaji wa Manispaa ya ilala Cosmas Mwaitete akihahidi kuwaongezea vifaa zaidi vya kufanyia usafii umoja wa wakimbiaji mbio za pole Vingunguti
 Mtangazaji wa kituo cha Radio cha east Afrika  Zembwela akionyesha kwa vitendo namna ya kufanya usafi katika mitaa ya vingunguti mara baada ya kualikwa na Naibu Meya.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akitoa uchafu kwenye mitaro ya mitaa ya Vingunguti
Sehemu ya wana kikundi wakikimbia kabla ya kuanza kwa usafi wa mazingira kata ya VINGUNGUTI

WANAFUNZI ZAIDI YA 700 WAHITIMU MAFUNZO YAO CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MNMA


 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir akihutubia wakati wa kutunuku vyeti kwa wahitimu wa Ngazi ya Shahada na Astashahada wa chuo hicho kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof . Shadrack Mwakalila  akizungumza juu ya mipango ya chuo hicho wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika katika jengo la utamaduni la MNMA Kigamboni jijini Dar es Salaam.


 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir akikabidhi zawadi kwa Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mwaka wa masomo 2017
 Baadhi ya wahitmu wa Shahada ya Maendeleo ya Jinsia ya MNMA Wakiwa wanasubiri kutunukiwa shahada zao wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dare s Salaam
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 12 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  ZanzibarMashavu Ahmad Fakir  akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi waliofanya Vizuri

Thursday, November 23, 2017

WAZIRI MHAGAMA AKABIDHI PIKIPIKI KWA TASISI YA IOGT INAYOJIHUSISHA NA MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki kwa Tasisi ianyojiusisha na kutoa eleimu juu ya Mapambano ya Dawa za kulevya ya IOGTkatika ofisi za Kamishna wa Mamlaka ya kupambana na Dawa .
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akikabidhi Pikipiki kwa kiongozi wa IOGT Taifa Wellngton Kyumba  katika ofisi za Mamala ya kupambana na Dawa jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akisalimiana na Vijana wa IOGT Waliofika katika hafla ya kukabidhiw apikipiki katika ofisi za Mamlaka ya Dawa jijini Dar es Salaam
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kupambana na Dawa nchini,Rogers Siang'a akisalimiana na kiongozi wa IOGT Taifa Wellngton Kyumba  katika ofisi za Mamala ya kupambana na Dawa jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi waliopata mafunzo ya Dawa za Kulevya wakieleza madhara ya dawa hizo mbele ya Waziri Jenista Mhagama

WADAIWA SUGU WA KAMPUNI YA TTCL WAPELEKWE MAHAKAMANI- NAIBU WAZIRI MHANDISI NDITIYENaibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya 
kampuni ya simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea makao makuu ikiwa ni mara ya kwanza na kuwataka kuwachukulia hatua wale wote wanaodaiwa madeni sugu. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt Mary Sassabi.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara makao makuu ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL) na kuwataka kuwachukulia hatua wadaiwa sugu ikibidi kuwapelekea mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza mbele ya menejinenti ya TTCL, Mhandisi Nditiye amesema kuwa wale wanaodaiwa na hawafuati taratibu za kulipa madeni wanatakiwa wapelekwe mahakamani na zaidi wadaiwa hao bado wanaendelea kutumia huduma za TTCL.

Mbali na hilo, Mhandisi Nditiye amesifia huduma ya Conference Video Call kwani itasaidia kupunguza gharama kwa serikali na itaruhusu watu kufanya mikutano kupitia njia ya mawasiliano na sio kukutana kama ilivyokuwa zamani.

"Huduma hii ya Conference Video Call itasaidia kupunguza gharama kwa serikali ambapo awali ilikuwa unatakiwa kuwakusanya viongozi wote 
Kuja katika mkutano ila kwa huduma hii unaweza kuzungumza nao wakiwa huko huko waliko," amesema Mhandisi Nditiye.

Afisa Mtendaji Mkuu wa 
 kampuni ya simu Tanzania (TTCL)
 Waziri Kindamba  akielezea namna kampuni yao ilivyowez akukusanya deni la bilioni 6.8 kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka kwa wadaiwa sugu huku akimuelezea 

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye namna Conference Video Call inavyoiweza kufanya kazi.


Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa 
 kampuni ya simu Tanzania (TTCL)
 Waziri Kindamba amesema kuwa kwa sasa TTCL inatekeleza mpango mkakati wa mageuzi ya kibishara na ni mahsusi kwa mabadiliko ya kuwa kiongozi wa huduma za mawasiliano na TEHAMA katika soko la Tanzania.

Kindamba amesema wanamatumaini kuwa mchakato wa kupata sheria mpya ya kampuni ya TTCL kuja kuwa Shirika la Mawasiliano iliyopitishwa na bungeni wiki iliyopita unaweza kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli.

Kampuni ya TTCL imeweza kukusanya takribani bilioni 6.8 za madeni ndani ya miezi mitatu ambapo awali deni lilikuwa ni Bilioni 10.7.

Kwa sasa, TTCL imeweza kuboresha huduma zake kwa takribani mikoa 18 ikiwemo Unguja na Pemba pamoja na kutumia teknolojia za kisasa za 2G, 3G, 4G na FMC pia kuwa na huduma za TTCL PESA.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa anaongea na wafanyakazi wa kampuni ya simu (TTCL) kutoka Dodoma kwa njia ya Conference Video Call. 

NAIBU WAZIRI AFANYA ZIARA YA GHAFLA KATIKA KIVUKO CHA KIGAMBONI

AM.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa amefanya ziara katika kivuko cha Kigamboni na kujionea namna mashine mpya za kieletroniki zilivyoweza kufungwa na kumtaka  mhandisi aanze kuzifanyia majaribio kabla ya mwaka huu kuisha ili Januari 2018 zianze kutumika.

Akizungumza baada ya kumaliza ziara yake na kujionea namna wafanyakazi wanavyotoa huduma kwa abiria wanaofika kwa ajili ya usafiri kwa kivuko kutoka Kigamboni na Kivukoni, Naibu Waziri Kwandikwa amesema kuwa amefurahishwa na huduma zinazotolewa na zaidi amezungumza na baadhi ya wananchi na wote wameonekana kufurahishwa. 

" Nimezungumza sehemu mbalimbali na kujionea namna watoa huduma wanavyotoa huduma zao kwa abiria na pia nimezungumza na takribani wananchi kumi wanaotumia usafiri wa kivuko na wote wameonekena kufurahishwa na huduma zenu ,"alisema Naibu Waziri Kwandikwa.

Katika ziara yake ameweza kuzungumza na wahudumu wanaokatisha tiketi na kuwauliza changamoto wanazokutana wakati wa ukatishaji tiketi, ametembelea na kupanda kivuko cha MV KAZI ambacho ni kipya pamoja na kuona namna Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) wanavyofanya shughuli zao za kila siku.

Amesema, kama serikali wanahakikisha watumiaji wa kivuko hicho wanapata huduma bora na zinazostahili ikiwemo usalama wa safari zao za kila siku.


Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na mhudumu wa kukata tiketi katika kituo  cha Kivukoni wakati alipofanya ziara kuangalia namna abiria wanavyopata huduma zao, juu akikata tiketi ya kuingia ndani.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake katika kivuko cha Kivukoni na Kigamboni na kujionea uendeshaji wa huduma bora kwa abiria kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na Mhandisi wa kivuko Ally Daudi na akipewa maelezo ya maendeleo ya vivuko vyote vilivyopo chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akikagua mashine za kieletroniki za tiketi zilizofungwa katika Kivuko cha Kigamboni na Kivukoni wakati wa ziara yake iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wananchi wakizungumzia baadhi ya kero ndogo ndogo wanazokutana nazo pia huduma bora wanazozipata.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akiwa ziarani katika kivuko cha Kivukoni na Kigamboni iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Zainab Nyamka.TAMBWE KAMILI GADO, YANGA KUENDELEA KUWAKOSA TSHISHIMBI, NGOMA NA KAMOSOKU


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo katika Uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wa raundi ya 11 ya ligi kuu Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons ya Jijini Mbeya.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Chamazi kutokana na mabadiliko yaliyofanya na bodi ya ligi baada ya Uwanja wa Uhuru kuwa na shughuli za kijamii.

Katika mazoezi hayo, mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe aliyekosekana uwanjani kwa kipindi kirefu toka kuanza kwa ligi msimu huu leo amejumuika na wenzake na kufanya mazoezi kikamilifu kwa mara ya kwanza pamoja na wenzake ikiwa ni baada ya muda mrefu.

Kurejea kwa Tambwe katika mazoezi ya pamoja chini ya Kocha George Lwandamina  kuna uwezekano  kwenye mchezo wa wiki hii akajumuishwa kwenye mchezo dhidi ya TZ Prisons siku ya Jumamosi.

Kocha wa Yanga, Mzambia George ‘ Lwandamina amesema kwamba kati ya majeruhi wake wanne, wengine ni Tambwe pekee amefanya mazoezi ukiachilia  kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji, Donald Ngoma nna kiungo Papy Kabamba "Tshishimbi" ambapo alikosa mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Mbeya City.


Lwandamina amesema kwamba inaonekana Tambwe amerudi imara kabisa na leo alionyesha yuko fiti kwa kucheza kwa nguvu na kupiga mashuti ya kusisimua. Tambwe alifanya mazoezi mepesi ya kukimbia peke yake juzi na jana Uwanja wa Uhuru, kabla ya leo kuungana na wenzake kwa program kamili ya mazoezi.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itaendelea Ijumaa, wenyeji Ndanda FC wakiwakaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Jumamosi, Yanga wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Singida United watakuwa wenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Namfua, Singida.


Mechi nyingine za jumamosi, Mbao FC wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar wataikaribisha Stand United Uwanja wa kambarage Shinyanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Maji Maji Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. 
Jumapili Simba SC watakuwa wenyeji wa Lipuli ya Iringa Uwanja wa Azam, Complex na mzunguko wa 11 wa Ligi Kuu inayoonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam TV utakamilishwa Jumatatu ijayo kwa mchezo mmoja kati ya wenyeji, Azam FC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

AZAM YAMNASA MKALI KUTOKA GHANA
UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unayofuraha kuwajulisha kuwa imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Bernard Arthur, akitokea Liberty Professional ya Ghana.

Arthur amesaini mkataba wa miaka miwili kujiaunga na matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex, na zoezi zima limefanikishwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed, aliyekuwepo nchini Ghana kukamilisha usajili wake.

Usajili wa Arthur, 20, ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo, anayekuja kuziba pengo la straika mwingine, Yahaya Mohammed, aliyeondoka kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya WAFA (Ghana) na Asec Mimosa ya Ivory Coast, anaungana na washambuliaji wengine wa timu hiyo katika kukiongezea makali kikosi hicho, ambao ni Mbaraka Yusuph, Wazir Junior, Yahya Zayd, Shaaban Idd pamoja na wale waliopandishwa kutoka Azam B, Paul Peter na Andrea Simchimba.

Liberty Professional ni moja ya kitovu kikubwa cha kutoa mastaa wa baadaye nchini Ghana, wachezaji waliotesa barani Ulaya waliowahi kupiatia hapo ni nyota wa zamani wa Chelsea, Michael Essien, Sulley Muntari (Pescara, Italia) na Asamoah Gyan (Kayserispor, Uturuki).

Azam FC inamatumaini makubwa kuwa usajili wa nyota huyo, utaweza kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji na kutatua tatizo la ukosefu wa mabao linaloonekana, hii ikitarajia kuendeleza mbio za kuwania taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania walizozianza vema hadi sasa.

Aidha uongozi kwa ujumla na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, unaendelea kutoa pongezi kwa mashabiki wa timu kwa moyo wanaoendelea nao wa kuisapoti timu hiyo, kwa hakika kila mmoja amejionea namna nguvu na umoja wao wa kuishangilia timu unavyozidi kuwapa hamasa wachezaji na kupata matokeo bora kwenye kila mchezo.
Wasifu wa Bernard Arthur

Arthur aliyekuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya vijana ya Ghana chini ya umri wa miaka 20 (Ghana U-20), ni mmoja wa washambuliaji bora kwa sasa katika Ligi Kuu nchini Ghana (GPL), msimu huu akifunga jumla ya mabao 11, tisa akifunga ndani ya ligi hiyo na mawili (Kombe la FA).

Moja ya sifa zake kubwa ni uwezo wa kumiliki mpira na kuwatoka mabeki wa timu pinzani kwa spidi, kukaa na mipira na kusambaza kwa wachezaji wenzake, kutumia vizuri miguu yote miwili, uwezo wa kupiga mashuti kwenye eneo lolote la ushambuliaji pamoja na kusaidia ukabaji pale timu pinzani inapokuwa ikishambulia.

Arthur alianzia soka lake katika timu ya Mighty Cosmos kwenye eneo alilozaliwa na kukulia la Dansoman nchini Ghana, akiwa kijana mdogo mwaka 2005-2010.

Cosmos aliyoanzia soka lake Arthur, pia wamewahi kucheza nyota wengi wa soka la Ghana wakiwamo nahodha wa zamani na timu ya Taifa ‘Black Star’, Stephen Appiah na Michael Essien.

Mbali na kucheza Liberty, mshambuliaji huyo pia amewa kucheza kwa mabingwa wa msimu uliopita nchini Ghana, WAFA huku pia akiwahi kutolewa kwa mkopo kujiunga kwa vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosa.

Nyota huyo anavutiwa na staa wa Ghana, Asamoah Gyan, ambaye ndiye mfano wake wa kuigwa (role model), ambapo anapenda siku moja wacheze naye pamoja katika timu Taifa.

Wednesday, November 22, 2017

PB Bank Plc, Multichoice kuwapatia Watanzania DStv kwa Mkopo

  Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini.[/caption]   [caption id="attachment_82799" align="aligncenter" width="500"] Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini.[/caption]   [caption id="attachment_82796" align="aligncenter" width="500"] Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kusaini makubaliano rasmi na Benki ya TPB ambapo sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Multichoice Tanzania, Salum Salum.[/caption]   [caption id="attachment_82797" align="aligncenter" width="500"] Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakisaini makubaliano ya ushirikiano, ambapo kwa sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Nyuma yao ni mashahidi kutoka pambe zote mbili.[/caption]   [caption id="attachment_82798" align="aligncenter" width="500"] Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakisaini makubaliano ya ushirikiano, ambapo kwa sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Nyuma yao ni mashahidi kutoka pambe zote mbili.[/caption]   [caption id="attachment_82795" align="aligncenter" width="500"] Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kusaini makubaliano rasmi na kampuni ya Multichoice Tanzania inayotoa huduma za DStv, sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja sasa wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande.[/caption]

WAZIRI MWIJAGE AWATAHADHARISHA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOWAKWAMISHA WAWEKEZAJI

Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charlse Mwijage akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Jengo la usambazaji wa Vifaa vya ujenzi na Saruji linalojengwa na umoja wa Wafanyabiashara wa Kichina Barani Afrika CNBM kwa thamani ya Dola za kimarekani Bilioni 56  Katika Mtaa wa Buguruni Mivinjeni Jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charlse Mwijage akiongoza zoezi la uwekaji wa mchanga katika sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi katika Uzinduzi wa ujenzi wa eneo la Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi katika kutoka kwa umoja wa Wafnyabiashara wa kichina Afrika CNBM
 Balozi wa Serikali ya China ya China nchini Tanzania , Ke Wang akihutubia  wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi kwa jengo la uuuzaji wa bidhaa za ujenzi kutoka kwa umoja wa Wafanyabiashara wa kichina nchini CNBM
 Mwenyekiti wa bodi ya Umoja wa Wafanyabiashara wa kichina , CNBM GROUP COLTD, Dr Zhiping Song  akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuweka jiwe la Msingi
 Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote ,Hemendra Raithatha  akitoa salam za Kiwanda chake juu ya jengo hilo la usamabazji wa Vifaa vya Ujenzi .

 Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charlse Mwijage akiasaini katika ubao wa wageni 
 Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charlse Mwijage, akiteta jambo na Balozi wa China,Ke Wang mara baada ya kumaliza kuweka jiwe la Msingi
 Baadhi ya Wananchi walioshiriki katika Zoezi la uwekajiwa jiwe la Msingi
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa kichina waliohudhuria katika zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la Msingi
 Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charlse Mwijage akiwa katika picha ya Pamoja na Wanachama cha Mapinduzi waliohudhuria uzinduzi huo

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...