Wednesday, November 29, 2017

Dkt,Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu.


Na Agness Francis,Blogu ya Jamii

Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dkt Faustine Ndugulie,awataka wakazi wa  wilaya hiyo pamoja na wananchi wengine  kutoka sehemu mbali mbali  kujitokeza  kwa wingi katika kuhudhuria  tamasha la Kigamboni Marathon,ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika  hapa Jijini Dar es Salaam.

Dr. Ndugulile amesema hayo leo katika Ofisi  zake Jijini Dar Es Salaam kuwa mbio hizo ambazo huleta manufaa kwa mwanadamu  ambazo hujenga  afya na mwili  pamoja pia na kukutana na  watu mbali mbali wapya na kubadilisha mawazo  ili kuleta mafanikio katika Wilaya hio mpya.

 Ndugulile amesema hayo  ametanabaisha kuwa mbio hizo za Kigamboni Marathoni zitakazo fanyika siku ya jumamosi  Disemba 2 mwaka huu kuanzia saa 12 asubui katika Halmashauri ya Wilaya hiyo ya Kigamboni

Ambapo Mbio hizo zenye kiomita 21,10 hadi 5 zitakazoanzia  darajani,feri  kuelekea kibuguni hadi kumalizikia katika ofisi za afisa wilaya ya kigamboni .

Pia amemalizia kwa kusema kuwa wanachi waendelee kujitokeza katika zoezi zima la kujaza fomu ambazo zinapatikana katika ofisi za  Mkuu wa wilaya wa Kigamboni  ilikushiriki mbio hizi za kilomita 20,10 mpaka 5
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndungulile  akizungumza juu ya kuwakaribisha wakazi wa Dar es Salaam kufika katika mbio za Kigamboni Marathoni

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndungulile akipokea fulana kw ajili ya kushiriki Mbio za Kigamboni Marathoni 

MBUNGE WA ILEJE JANET MBENE AZINDUA NAMBENE CUP

 Mbunge wa Wilaya ya Ileje, Janet Mbeneakizungumza wakati wa Uzinduzi wa Nambene Cup inayoshirikisha timu za Wilaya nzima kutoka kila Kata ambapo Mbunge huyo ametoa ufadhili wa Jezi na Zawadi ya Mshindi wa kwanza mpaka wa tatu wafungaji bora.
 Mbunge wa Wilaya ya Ileje, Janet Mbeneakizungumza wakati wa Uzinduzi wa Nambene Cup inayoshirikisha timu za Wilaya nzima kutoka kila Kata ambapo Mbunge huyo ametoa ufadhili wa Jezi na Zawadi ya Mshindi wa kwanza mpaka wa tatu wafungaji bora.Mbunge wa Ileje  akisalimia timu zilizojitokeza kushiriki Nambene Cup aliyoiandaa katika Wilaya yake kama hatua za kukuza michezo na kuleta Umoja kwa Jamii
 Wachezaji wa Timu Mbalimbali zinazoshiriki Nambene Cup wakiwa uwanjani wakijandaa kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi
 Wacheaji wa timu zilizoshiriki uzinduzi wa Nambene Cup wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi
Mbunge wa Ileje Janet Mbene akifurahi wa na Watoto waliofika katika uzinduzi wa Nambene Cup

REPOA YAZINDUA MATOKEO YA NA FAIDA ZA UTUMAJI WA FEDHA KWA MTANDAO KATIKA KUMUWEZESHA MWANAMKE KIUCHUMI


 Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa kiuchumi nchini(NEEC),Bengi  Issa akizungumza wakati alipokuwa akifungua Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu iliyofanyika katika ukumbi wa Tasisi ya utafiti nchini REPOA Jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na IDRC na TASAF.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya utafiti ya REPOA ,DK .Donald Mmari akizungumza kabla ya kumakribisha mgeni rasmi hili aweze kufungua Warsha ya Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu
 Muwakilishi wa tasisi ya IDRC Kutoka nchini Canada ,Dr Arjan  De Haan akizungumza na na wadau waliofika katika warsha hiyo namna tasisi yake ilivyousika katika tafiti za kumuwezesha mwanamke kiuchumi kupitia mtandao wa simu.
 Mtafiti kutoka Tasisi  ya Utafiti ya REPOA , Dr.Abel Kinyondo akizungumza na wadau walioshiriki Warsha ya  Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu ambapo alipata fursa ya kuwaeleza wadau faida na changamoto ya huduma hiyo katika mradi wa TASAF.
 Mtafititi kutoka Tasisi ya Utafiti ya REPOA, Dr. Blandina Kilama  akitoa neno la ukaribisho kwa wadau waliofika katika Warsha ya  Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu iliyoandaliwa na REPOA kwa kushirikiana na IDRC na TASAF
 Washiriki wa warsha hiyo wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa Warsha  Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu
 Washiriki wa warsha hiyo wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa Warsha  Faida za kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kupitia mpango wa matumizi ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu

Tuesday, November 28, 2017

HAROUN MDOE AAPISHWA KUWA DIWANI WA KATA YA SARANGA KUPITIA CCM

 Diwani Kata ya Saranga Haroun Mdoe akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni,Boniface Lihamwile  katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
 Diwani Kata ya Saranga Haroun Mdoe kwa tiketi ya CCM, Akisaini hati ya kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni,Boniface Lihamwile  katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
  Diwani Kata ya Saranga Haroun Mdoe kwa tiketi ya CCM, akipokea Ilani ya CCM kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo John Kayombo hili aweze kwenda kutekeleza ilani ya Chama hicho
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo John Kayombo, akionyesha Ilani ya CCM inayotekelezw ana Serikali ya awamu ya tano ya Dk John Pombe Magufuli
 Diwani Kata ya Saranga Haroun Mdoe akiwasili katika ofisi za Manispa aya Ubungoa kiwa na msafara mkubwa wa wanachama wa CCM

HIACE YAGONGA BASI NA KUSABABISHA MAJERUHI ENEO LA KIBAMBA JIJINI DAR ES SALAAM


 Gari aina ya Tyota Hiace na Basi aina ya Scania linalo julikana kw ajina la Safari Njema yakiw ayamegongana katika Barabara ya Morogoro eneo la Kibamba kwa Mangi mara baada ya Hiace kuhama njia na kulifata basi lilipokuwa likajiribu kulipita Roli na kusababisha Mejeruhi waliopo ndani ya Hiace hiyo.
 Majeruhi waliokuwa ndani ya Hiace hiyo wakiwa wamelala chini mara baada ya gari yao kwenda kugonga Basi la Safari njema
  Majeruhi waliokuwa ndani ya Hiace hiyo wakiwa wamelala chini mara baada ya gari yao kwenda kugonga Basi la Safari njema

  Dereva wa Hiace iliyogonga basi akiw amebebwa na Roli kwa ajili ya kuwahishwa Hospitalai ya Tumbi Kibaha mara baada kzimia hapo hapo na kupoteza fahamu

 Askari wa usalama Barabarani akiandika Pf 3 Kwa Majeruhi wa Hice iliyogonga Basi la Safari Njema eneo la Kibamba kwa Mangi jijini Dar es Salaaam leo
Majeruhi waliokuwa ndani ya Hiace hiyo wakiwa wamelala chini mara baada ya gari yao kwenda kugonga Basi la Safari njema

Monday, November 27, 2017

WANAUME WATAKIWA KUWA CHACHU YA MABADILIKO KATIKA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NCHINI

 Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia, Theodosia Mhulo kutoka WLAC Akifungua maadhisho hayo katika ofisi za REDESO zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo alitoa wito kwa wana harakati kuanza kuwatumia Wanaume kama chachu ya mabadiliko katika vita ya ukatili wa Kijinsia nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi isiyo ya kiserikali ya REDESO, Abeid Kasazi akizungumza kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi kufungua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani kote yaliyofanyika katika ofisi za Tasisi hiyo zilizopo kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri kutoka  REDESO, Brigitha  Sedekia akitoa somo juu ya ukatili wa kijinsia  kwa watu waliofika katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
 Sehemu ya wageni waalikwa walikuwa wamekaa Meza kuu wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani
 Kundi la Muziki la Wakimbizi linalojulikana kwa jina la Bana ba Zambe wakitoa Burudani wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani
 Sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...