Friday, December 8, 2017

KUMBILAMOTO AGAWA JEZI KWA TIMU NNE ZILIZOINGIA NUSU FAINALI YA VINGUNGUTI SUPER CUP

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza kabla ya kugawa jezi kwa timu nne zilizofika katika hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya Vingunguti Super Cup yaliyoshirikisha timu 24 za Jijini Dar es Salaam
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto , akionesha moja ya jezi ya timu zilizofika hatu aya nusu fainali ya Mashindano ya Vingunguti Super Cup yaliyoshirikisha timu 24 za Jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Mashindano ya Vingunguti Super Cup Kombo Mbuya  akizungumza wakati wa hafla ya kugawa jezi kwa timu zilizofika nusu fainali
 Muandaaji wa Mashindano ya Vingunguti Super Cup , Spia Mbwembwe akizungumza wakati wa hafla ya kugawa jezi kwa timu nne zilizoingia nusu Fainali ya kombe hilo
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akikabidhi jezikwa kiongozi wa timu ya Freemason Fc ya Vingunguti, Sudi Rashid
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akikabidhi jezikwa kiongozi wa timu ya Guantanamo Fc ya Vingunguti ,Abdul Mgohela
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akikabidhi jezikwa kiongozi wa timu ya Msako FC ya Kigogo Kani Masumbola  wakati wa hafala ya kukabidhi jezi kwa timu nne zilizo ingia nusu fainala ya Vingunguti Super Cup
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akikabidhi jezikwa kiongozi wa timu ya Relini Fc wa Vingunguti Halidi Kitapagala
 Baadhi ya wajumbe wa timu zilizoingia Nusu Fainali ya Vingunguti Super Cup  wakisikiliza maneno ya viongozi wakati wa mkutano huo wa kugawa jezi
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa timu waliokabidhiwa jezi

KADA CHADEMA AANDIKA BARUA KWA CAG KUOMBA UKAGUZI MAALUM KATIKA MASUALA YA FEDHA YA CHADEMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Mimi Mackdeo Mackeja Shilinde mdau na Mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo tarehe 05 Desemba 2017, nimepeleka barua kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nikiiomba ofisi yake kufanya Ukaguzi maalum kwa chama chetu (SPECIAL AUDIT) kuhusiana na pesa za ruzuku na matumizi yake ili kuondoa utata unaokikumba chama chetu kwa kipindi kirefu sasa kuhusiana na masuala ya kifedha.
Nyote mnafahamu kwamba chama chetu ni miongoni mwa vyama vya siasa vinavyopokea pesa za ruzuku kutoka serikalini kila mwezi ambapo kwa chama chetu tunapokea zaidi ya
milioni 300 kwa mwezi.
Kadharika, nyote ni mashahidi kuwa pesa za ruzuku ni pesa zinazotokana na kodi za
wananchi wengi wao wakiwa walalahoi na hivyo ni vyema matumizi na usimamizi wake uwe wazi bila vificho.
Kuibuka kwa manung’uniko miongoni mwetu wanachama  kuhusiana na matumizi ya
Ruzuku ya chama chetu, ikiwemo viongozi wetu wa kitaifa na kanda mbalimbali za  chama,
kulipana mishahara minono, posho zisizozingatia mgawanyo rasmi na kuzagaa kwa taarifa ya kwamba mwenyekiti wa chama amekuwa akikidai chama zaidi ya shilingi bilioni saba (7,000,000,000/=) pesa anazodai kuwa alikikopesha chama kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na hivyo kwa zaidi ya miaka miwili sasa amekuwa akijilipa deni hilo jambo ambalo si sahihi na kinyume cha taratibu, kushindwa kupelekwa ruzuku mikoani na wilayani kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za chama ndiko kunakotusukuma kuomba uchunguzi maalum.
Mimi na  wanachama wenzangu kutoka mikoa zaidi ya kumi na mbili, tumekubaliana
kutafuta ukweli wa matumizi hayo ya pesa hizo za ruzuku kwa kutumia njia halali za kisheria ambapo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali ndio taasisi yenye mamlaka ya kufanya ukaguzi wa kimahesabu hasa katika pesa zinazotokana na umma.
Nakala ya barua hiyo tumeipeleka TAKUKURU na Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini.
Imetolewa na Mackdeo Makeja Shilinde

Mwanachama Mwandamizi – CHADEMA,


Wednesday, December 6, 2017

REPOA; YASEMA RUSHWA IMEPUNGUA NCHINI KWA ZAIDI YA NUSU KWA WATANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Tanzania Dr Donald  Mmari  akizungumza   wakati wa Semina ya Matokeo ya Utafiti wa unaonyesha ni namna gani rushwa imezidi kupungua hapa nchini kwa Viashiria vya watu 7 kati ya 10 wanajua umuhimu w akupambana na Rushwa.
 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa,  akizungumza na Waandishi wa Habari walioshiriki kwenye Semina ya Matokeo jinsi Rushwa ilivyopungua nchini 
 Wadau walioshiriki katika Mkutano wa Matokeo kupungua kwa Rushwa nchini AFRO BAROMETER iliyoandaliwa na Repoa
 Mtafiti kutoka Repoa Nchini Stephene Mwombela akitoa mada juu ya Matokeo ya Utafiti wa kupungua kwa Rushwa nchini


Mtafiti Kutoka Repoa Nchini, Lulu Olan'g akizungumza na wadau waliofika katikautafiti wa Afro Barometer
 Wadau walioshiriki katika Mkutano wa Matokeo kupungua kwa Rushwa nchini AFRO BAROMETER iliyoandaliwa na Repoa


WANAHABARI WAFUNDWA JUU YA UMUHIMU WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI NA KUPIGANIA HAKI ZA WATOTO

Mwanaharakati wa Haki za Watoto nchini na Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative , Rebeca Gyumi  akizungumza na Wahariri na Waandishi waandamizi wa Vyombo mbalimbali vya Habari haki za Mtoto na   vita dhidi ya Ndoa za Utotoni zinazoendelea nchini
 Mtaalamu wa kupigania Haki za Watoto kutoka Taasisi ya Save The Children, Neema Bwaira akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo Mbalimbali vya Habari hapa nchini wakati wa Semina juu ya haki za Mtoto Jijini Dar es Salaam
 Mtaalamu wa Masuala ya Haki za Watoto kutoka nchini Thailand anayefanya kazi na Taasisi ya Save The Children nchini, Yui Mutomol  akitoa Elimu kwa Waandishi wa Habari waandamizi na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari Jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Waandishi Waandamizi na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa Makini wakati wa semina ju ya haki za Mtoto iliyoandaliwa na Taisisi ya Save The Children Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Waandishi Waandamizi  na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya habari waliohudhuria  Semina juu ya haki za mtoto iliyoandaliwa na Tasisi ya Save The Children nchini

Tuesday, December 5, 2017

RAIS MAGUFULI KUTEGUA KITENDAWILI CHA MALEZI YAKE DODOMA

USIKU wa Kitendawili unazidi kupamba moto ambapo Rais, Dk. John Pombe Magufulimnamo Desemba 8, mwaka huu anatafunga siri na malezi yake ya utotoni ambayo ndiyo yaliyomfanya leo hii awe mzalendo wa kweli wa nchi yake.

JPM ambaye atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ atafunguka kuhusu  maisha yake aliyoyapitia na kumfanya leo kuwa mzalendo wa kweli ndani ya Tanzania, na mwenye kuhimiza kila Mtanzania kuwa mzalendo wa kweli wa nchi yake.Siku hiyo, Watanzania watasikia kauli za viongozi mbalimbali wastaafu na walioko madarakani kuhusu harakati za Tanzania kupata uhuru, na kupinga kabisa ukabila licha ya Tanzania kuwa na makabila 120.

Viongozi hao wa zamani watakuwa wamekaa chini kwenye mikeka ya asili na vigoda, na kuelezea namna serikali na viongozi wake walivyoweza kuondoa mambo ya ukabila ambao bado unazitesa nchi nyingi za Afrika.

Akizungumza na TBC katika Kipindi cha Tanzania Mpya, Mrisho Mpoto amesema kuwa;

“Rais, Dk. Magufuli atapata fursa ya kueleza maisha yake ya utoto na namna alivyoweza kusimama katika mstari ambao kila mmoja kwa sasa akiangalia matendo yake anaona rais kweli ni mzalendo wa kweli.

“Tutakuwa na Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na wote watapata fursa ya kueleza mawili machache kuhusu namna walivyoweza kuwa wazalendo wa kweli wa nchi yao.

 “Tumeomba protocol zisiwe kali sana kwa upande wa Watanzania na viongozi ili watu wafunguke, tunataka Rais wetu atuambie kwa nini ni mzalendo wa kweli, kwa nini ana uchungu na Watanzania wa chini ambao ni wanyonge zaidi. Kwa nini anahamasisha kuwa Tanzania ya Viwanda?

 Mpoto aliongezea kuwa: “Tutakaa kwenye mikeka na vigoda, tutakula ugali wa muhogo, kisamvu na madafu, Majaliwa pale, Mama Samia pale, ukumbi wenyewe umetengenezwa kama kuna vijiji na mitaa, Mhe atapita pale kwenda kusalimia kijiji cha jirani watuambie tu wamewezaje kuondoa suala la ukabila, nchi za wenzetu wanapigana kila siku. Hakika tuna kila sababu ya kuwa wamoja na kuimba wimbo mmoja wa Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’.”

 Usiku wa Kitendawili umeanzishwa na msanii Mpoto baada ya kuachia wimbo wake‘Kitendawili’ na kuamua kuanzisha usiku huo, kwa ajili ya kuwakutanisha wadau na kujadili kuhusu Uzalendo.

Baada ya uzinduzi, kampeni hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati, Julis Kambarage Nyerere, na itakuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali kupaza sauti kuhusu uzalendo.

Kampeni ya uzalendo itazungumzia kudhibiti na kukomesha mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa umma, kupunguza tuhuma za rushwa, ufisadi, ubadhilifu wa mali za umma na kuongeza hali ya kufanya kazi na Uzalendo.

Monday, December 4, 2017

HDIF YAFUNGA RASMI MASHINDANO YA MWISHO YA MAWAZO CHALLENGE

 Kiongozi msaidizi wa HDIF  Joseph Manirakiza akifungua rasmi mshindani hayo ya mwisho kwa timu 12 za  Madkatari wanafunzi  wanaoshindanishwa ili kupata timu 10 zitakazo pata seed fund toka HDIF.
 Timu ya Afya Plus ikitoa huduma ya kufanya Vipimo vya urefu, uzito BP na Kisukari katika eneo la tukio.
 Moja ya timu zilizofika fainali toka mchakato huu ulipoanza na mawazo zaidi ya 350 mpaka kufikia 12 iliyoingia fainali 

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA DODOMA

 Usiku wa Kitendawili kufufua upya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dr John Pombe Magufuli anataraji kuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ utakaofanyika Ijumaa hii Disemba 8 2017 kupitia ‘Usiku Wa Kitendawili’ mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

akizungumza na Waandishi wa habari Msanii  wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ndio wataouratibu usiku huo wa Kitendawili kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Sanaa utamaduni na Michezo.

Usiku wa Kitendawili ulianzishwa baada ya msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kuachia wimbo ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo.

Akiongea na wadau wa sanaa katika Maandalizi ya Kampeni hiyo ya Kitaifa itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, Mrisho Mpoto amesema kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza ndani ya Taifa letu.

Alisema mambo ambayo yatayozingatiwa katika kampeni hiyo ni pamoja na kudhubiti na hatimaye kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma, kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka ufisadi, ubadhilifu wa mali za Umma pamoja kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.

“Usiku wa Kitendawili utatumika kama jukwaa la kuwaleta pamoja watanzania pamoja na viongozi wao ili kukumbushana kuhusu wajibu na kujadili mustakabali wa Taifa. Kutakuwa na vivutio mbalimbali pamoja na wimbo maalumu kutoka kwa wasanii maalumu Mwaka Huu,” alisema Mpoto.

Aliongeza,”Tumekuja kuunadi Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ kwasababu tunaamini Uzalendo na Utaifa lazima uwepo ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kuunga mkono juhudi za Raisi Dkt. John Pombe Magufuli za kujenga Taifa lenye Uzalendo, Utu, Weledi na Uadilifu uliotukuka. Mimi ni mzalendo ndio maana hata kwenye hizi harakati nipo toka nimetoa wimbo wangu wa kwanza, ukiangalia nyimbo zangu zote ni za kuonganisha jamiii 120 za watanzani,”

 “Naamini kwenye kufanya kazi ambayo itawafanya watanzania pamoja na kizazi kijacho kitambue kuna watu ambao walifanya kazi kubwa kwenye hili taifa, kuacha alama ambazo haziwezi kufutika katika maisha ya historia ya nchi hii, kwa sababu hivi vyote ambavyo vinaenda kufanywa ni kufufua upya na kuiweka pamoja mitazamo ya watanzania ili kujenga Taifa la Wazalendo na Wachapakazi kuiga nyayo zilizoachwa na hayati Baba wa Taifa,” alifafanua zaidi.

Mpoto amesema lengo kuu la maadhimisho hayo kuambatana na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa kuanzia mwaka 2018 ni kutumia jukwaa hilo kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kujenga na kuendeleza Utaifa.

Alisema baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo wiki hii huko Dodoma, itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni chini ya Uwenyekiti wa Mkuu wa Mkoa na  Wilaya.

Sunday, December 3, 2017

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MHANDISI MASAUNI NA WAZIRI BARANDAGIYE WA BURUNDI KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI NDUTA NA MTENDELI MKOANI KIGOMA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao. Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani   na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (hayupo pichani). 
 Waziri wa Mambo ya Ndani   na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
 wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma wakinyoosha mikono juu baada ya kuulizwa  wangapi wanataka kurudi nchini kwao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara ikiwa ni ziara ya kikazi ya naibu waziri kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani   na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika uwanja ulipofanyika mkutano wa hadhara uliowahusisha wakimbizi   wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma. Ziara hiyo lengo lake ni kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani   na Mafunzo ya Uzalendo kutoka serikali ya Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakiagana baada ya kumaliza kuzungumza na wakimbizi   wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma. Ziara hiyo lengo lake ni kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi  wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nduta na Mtendeli, mkoani Kigoma, baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara ikiwa ni ziara ya kikazi kukagua zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi hao katika nchi yao

WADAU WATAKIWA KUJITOKEZA KUSAIDIA KITUO CHA ELIMU YA WATU WAZIMA KIGAMBONI

 Mratibu wa Elimu Kata ya Kigamboni Angelina Gaswaswa akipokea maelezo kutoka kwa Mmoja wa waratibu wa kituo cha kutoa elimu ya watu wazima  Mastidia Mbeo
 Mwenyekiti wa  Serikali ya Mtaa wa Kigamboni, Abdul Habibu  akizungumza wakti alipotembelea kituo hicho cha kutoa elimu ya Watu wazima cha Kigamboni
 Wanafunzi wanaopatiwa elimu ya Watu wazima wakiimba wimbo mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kigamboni akiwa katika picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Shule ya elimu ya watu wazima ya Kata ya Kigamboni

SPORTPESA KUDHAMINI TIMU YA WABUNGE LA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI.Dar es Salaam, Tanzania Desemba 02, 2017. Kampuni ya michezo ya kubashiri ijulikanayo kama SportPesa Limited imeidhamini timu ya mpira wa miguu na kikapu ya Bunge la Tanzania ambao wanatarajia kushiriki mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki mnamno Desemba 3, 2017 katika uwanja wa Taifa, Temeke Dar es Salaam.

 Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Peninsula House    Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji SportPesa Tanzania Mr. Tarimba Abbas alisema “Tulivyosikia kuwa haya mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki kwa mwaka huu yatafanyika nchini kwetu tuliona ni vyema kuwa wazalendo kwa kuidhamini timu ya mpira wa miguu na pete kwa kutoa vifaa mbalimbali vya michezo kama Jersey, bibs, soksi, pamoja na mipira. SportPesa ni kampuni ya kubashiri michezo mbalimbali ikiwa na kengo kuu la kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini na ndiyo maana tulianza kwa kudhamini timu za mpira wa miguu za Simba, Yanga na Singida United.

“Mbali na hapo tutatoa tracksuits kwa ajili ya wabunge wote 160 wanaoshiriki katika mashindano hayo siku ya ufunguzi ambapo wabunge hao watafanya maandamano kutoka ukumbi wa PTA SABASABA kuelekea Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuanza michezo mbalimbali ya ufunguzi.”

“Tunapenda kuwapongeza na kuwatakia kila lakheri timu ya Bunge la Tanzania katika mashindano haya na tunaamini wataiwakilisha vizuri nchi yetu” alimaliza Mr. Tarimba

Naye Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya wabunge Mh. William Ngeleja alianza kwa kusema “tunapenda kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa kwa ushirikiano wao waliouonyesha na kutusapoti katika kuhakikisha timu zetu za mipira wa miguu na pete zinapata vifaa vya michezo kama vile jezi, mipira na soksi.

“Tunatarajia kuanza rasmi mashindano yetu siku ya jumapili tarehe 03, desemba 2017 ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali za ufunguzi huo ikiwemo kukimbia, kuvuta kamba, mpira wa pete, mpira wa wavu pamoja ja mpira wa miguu”.

“Michezo hii itahusisha wabunge kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi. Timu zetu za mpira wa miguu na mpira wa pete zitacheza na timu ya wabunge wanaoiwakilisha nchi ya Burundi siku ya jumatatu tarehe 04 desemba 2017, alimaliza Mh. Ngeleja.

Mashindano haya yatafunguliwa kwa michezo ya riadha pamoja na kuvuta kamba huku wengine wakijiandaa na Jumatatu ambapo timu za mpira wa miguu, Pete, pamoja na mpira wa wavu wakijiandaa kwa siku iliyofuata.
Mashindano ya mpira wa miguu yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo uwanja huu uliofanyiwa marekebisho makubwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa na kukabidhiwa kesho kabla ya ufunguzi wa mashindano hayo.

WAZIRI JAFO ;KUMSOMESHA MTOTO NI IBADA KUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza wakati Mahafali ya Shule Mikocheni Islamic ambapo aliwaasa wazazi kuwataka kuwekeza katika kuwapatia wtoto elimu ya Duniani na dini hili waweze kuja kuwa watumishi waadilifu baadae pindi wanapokuja kuwa viongozi wa Umma.
 Katibu wa Shule ya Mikocheni Islamic akizungumza kablaya kumakaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo katika mahafali ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic Jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akikagua Maonesho ya kisayansi ya shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakati wa mahafali ya Darasa la Saba ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
 Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Msingi ya Mikocheni Islamic wakionyesha Umahiri wao wa kuimba Kaswida mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kitengo cha Sayansi na walimu wao wa shule ya Msingi Mikocheni Islamic.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...