Thursday, December 21, 2017

LUKUVI ASITISHA MRADI WA PMM KUNUNUA NYUMBA ZA VINGUNGUTI NA BUGURUNI NA KUSEMA NI UTAPELI WA HALI YA JUU

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Vingunguti wakati alipoamua kusitisha zoezi la uuzwaji wa nyumba za Buguruni mpaka Vingunguti kwa Muwekezaji wa kampuni ya PMM ambaye amekuwa na mchakato wa kununua nyumba hizo kinyume cha utaratibu wa Serikali katika kufanya ununuzi huo na Tathmini
Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza na Wananchi wa Vingunguti wakati wa kusikiliza Kero za Wananchi juu ya mradi wa PMM 
Mkuu wa Wilaya ya  Ilala Sophia Mjema akizungumza wakati wa Mkutano wa Waziri Lukuvi na Wananchi wa Vingunguti juu ya mradi wa PMM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Akipata
Maelezo ya mradi wa ununuzi wa nyumba za Vingunguti

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani juu ya Mradi wa PMM Ulivyowazungusha wananchi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akishangiliwa na Wananchi wa Vingunguti mara kutangaza kuwa mradi wa PMM Autambuliwa na Serikali
Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  juu ya mradi wa PMM

Wednesday, December 20, 2017

PICHA MOJAWAPO YA MIAHANGAIKO YA MWANAMKE JIJINI DAR ES SALAAM

Mwanamke Mfanyabiashara ya Matunda akikatiza katika Barabara ya Garden  Avenue akiwa amembeba Mtoto bila ya kumfunika na kitu chochote wakati jua kali likiwaka hali inayoweza kuhatarisha afya ya Mtoto huyo ambaye atapigw anajua kwa muda mrefu.

SHIRIKA LA POSTA NCHINI LAZINDUA NEMBO MPYA YA SHIRIKA HILO YENYE KAULI MBIU YA TWENZETU

 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa  akizindua nembo mpya ya Shirika la Posta nchini ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam katika Kuboresha huduma za shirika hilo kuwa la kisasa.
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo mara baada ya kuzindua nembo mpya ya shirika hilo jijini Dar es Salaam leo
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akishuka katika mabasi mapya ya Shirika la Posta nchini mara baada ya kuzindua huduma ya mabasi ya shirika hilo ambayo yatakuwa yanabeba abiria na vifurushi
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, akizungumza mara baada ya kuzindua Nembo mpya ya  Shirika la Posta nchini
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo  akizungumza kabla yakumkaribisha mgeni rasmi kuzindua nembo mpya ya shirika la Posta nchini.
 Mjumbe wa bodi ya Shirika la Posta nchini, Khadija Khamis Shabani akitoa neno la shukrani mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa nembo mpya ya shirika la Posta nchini
 Muongozaji wa shughuli ya uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta nchini, Pascal Mayala akizungumza wakati sherehe hizo zikikiendelea.
 Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo pamoja na Posta Mkuu Hassana Mwang'ombe wakiongozana kwenda kukagua magari
Sehemu ya wafanyakazi wa shirika la Posta nchini wakiwa katika hafala hiyo ya uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta.

Rais Magufuli – “Ole wao Wanao Beza Takwimu za Nchi”


Na. Atley Kuni – OR TAMISEMI Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, ameweka jiwe la msingi kwenye jengo  la Ghorofa nne la Ofisi za  Taifa za Takwimu zilizopo Mkoani  Dodoma huku akionya vikali watu wanao potosha takwimu na kuwatisha watanzania.

Rais Magufuli amesema, wapo watu kwa Makusudi kabisa wamekuwa wakiupotosha umma juu usahihi wa takwimu mbali mbali za nchi bila kuwa na vyanzo sahihi vya takwimu ambao ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

“Mmesikia wenyewe hapa tumekuwa namba mbili kwa ubora wa takwimu katika nchi za Afrika, tukitanguliwa na Nchi ya Afrika Kusini, ametuambia mkurugenzi mkuu wa Takwimu Mama Chuwa, lakini wapo watu wengine sijui takwimu zao wanazitoa wapi na kuwadanganya wananchi” amesema Mh. Rais

Rais Magufuli ameiagiza Ofisi ya Taifa ya takwimu, kuitumia ipasavyo sheria ya takwimu namba 37 ya mwaka 2015 kifungu kupitia kifungu kidogo cha 3 hadi cha 5 ambacho kinawalenga wapotoshaji wa takwimu na kwakutumia kifungu hicho basi mtu anaweza kufungwa kati ya miezi sita hadi miaka mitatu au faini ya kati ya Mil. Moja hadi 10 au vyote kwa pamoja.

“Vyombo vya habari, Watu wa Mitandao, tusitafute takwimu zakupika tafuteni takwimu sahihi kutoka vyanzo sahihi” amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa, Maendeleo katika Nyanja zote hutegea takwimu sahihi.

Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya taarifa ya takwimu Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Taifa ya Takwimu Nchini Dkt. Albina Chuwa, alisema mpango uliopo mbele yao ni uboreshaji wa majengo, kusomesha wataalam, lakini pamoja na kuweka viwango bora vya ukokotoaji wa takwimu.

“Mhe. Rais tunajenga Jengo la Ghorofa moja pale mkoani Kigoma, nikuhakikishie kupitia wadau wetu wa maendeleo jengo hilo tutalikamilisha bila kuhitaji msaada wa serikali” alisema Dkt. Chuwa.

Chuwa amesema, mbali na kuendesha sensa ya taifa tangu mwaka 1967 wakati wa watanzania walipokuwa Mil. 13, Ofisi yao pia imeendelea na zoezi la sensa ya watu na makaazi kwa miaka tofauti na mwaka wa mwisho kufanya sensa 2012 watanzania walikuwa Mil. 45, huku akitoa makadiri ya watu Mil. 60 na zaidi ifikapo wakati wa Sensa ya 2022

Awali kabla yakumkaribisha Mh. Rais, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, alimwambia Mh. Rais kuwa wanawashukuru sana wadau wa maendeleo kwa jinsi wanavyozidi kushirikiana na Nchi ya Tanzania katika shughuli za maendeleo hasa  Benki ya  Dunia.

“Mhe. Rais kazi kubwa unayoifanya, wenzetu (World Bank) na wadau wengine wa Maendeleo wanaithamini sana na ndio maana wamekuwa bega kwa bega katika shughuli za Maendeleo alisema Mpango na kuongeza kuwa jengo linalojengwa Dodoma ni la pili, jengo la kwanza lipo Zanzibar na linategemewa kuzinduliwa mapema mwaka ujao.

Kwa upande wake Yasin Ringo Mtaalam wa ujenzi alimwambia Mh. Rais Jengo linalojengwa Mjini Dodoma, hadi kukamilika kwake litatumia Bil. 11.7
Akihitimisha Hotuba yake Mhe. Rais amezitaka taasisi zote nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bodi ya Taifa ya Takwimu ili kazi wanayoifanya iwe na ufanisi, huku akimuagiza Waziri wa Fedha kufatilia suala la Airtel kwani inaonesha kampuni hiyo ilikuwa mali ya TTCL.

Mbali na kufanya shughuli ya uwekaji wa jiwe la Msingi Mh. Rais hakusita kuongelea mambo mbali mbali yanayo husu uchumi wa nchi na kusema kuwa uchumi wa nchi umekuwa kwa kiwango cha aslimia 6.8 huku mfumuko wa bei ukishuka na kufikia asilimia 4.4 ambapo Tanzania imeongoza katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa na uchumi unaokuwa vizuri na kuwa miongoni mwa Nchi 5 zinazofanya vizuri barani Afrika katika suala la Ukuwaji wa Uchumi.


MPOTO ASEMA KUTUMA BARUA KUPITIA SHIRIKA LA POSTA NI UZALENDO

 Msanii wa Muziki wa kughani Kutoka Mjomba Band Mrisho Mpoto akiimba wakati wa uzinduzi wa wimbo nembo mpya ya Shirika la Posta Tanzania Mbali na kuimba mpoto alitumia muda huo kuwaeleza Watanzania juu ya kuwa wazalendo kwa kutumia Barua kama chombo pekee ya kuonyesha tahamani kwa mtu unayempenada na kumjali, Mpoto amesema kuwa apo zamani wahenga walitumia Barua kama chombo pekee cha kuonyesha namna gani mtu anamajali mwenzie hasa nayakati zile wakiwa wanasoma shule za bweni .
 Wasanii wa kundi la Mjomba Band wakitumbuiza wakati wa bendi hiyo ilipokuwa inaimba wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta nchini.
 Mpiga Drums Maharufu nchini James Kibosho akikaanga chipsi pamoja na Mjomba Band jijini Dar es Salaam leo
 Wanamuziki wakicharaza magitaa wakati wa Bendi ya Mrishoi Mpoto ilipokuwa inatumbuiza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya shirika la Posta nchini.
 Mpiga kinanda Maharufu nchini Erasto Mashine akipiga wakati wa Bendi ya Mrisho Mpoto ilipotumbuiza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta.
Msanii wa Muziki wa kughani Kutoka Mjomba Band Mrisho Mpoto akiimba na Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania 

JESHI LA POLISI LASEMA UHALIFU UMEPUNGUA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2016/2017

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi nchini limesema hali ya usalama nchini imezidi kuimarika katika kipindi cha mwaka 2016 /2017 kutokana na kupungua kwa matendo ya kiaharifu.

Hayo yamesemwa mapema jijini  Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz alipokuwa akitoa hali ya usalama nchini kwa vyombo mbalimbali vya habari vilivyofika katika Makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

“hali ya usalama nchini kwa ujumla ni ya kuridhisha sana takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba 2016 makosa makubwa ya jinai yarilipotiwa yalikuwa ni 68204 ikilinganishwa na makosa ya jinai yaliyoripotiwa 2017 kuwa 61410 na kufanya kupungua kwa asilimia 9.4” amesema DCI Boaz.

Ametaja kuwa makossa dhidi ya ubinadamu ambayo yanajumuisha makossa ya mauaji , kubaka ,kulawiti, wizi wa watoto ,kutupa Watoto kunajisi pamoja na usafirishaji binadamu yaliyoripotiw akatika kipindi cha 2016 yalikuwa 11,513 ukilinganisha na makosa yaliyoripotiwa 2017 kuwa ni 11620 ambayo ni ongezeko la makossa 107 sawa na asilimia 0.9.

Ameongeza kuwa katika kundi hilo makossa ambayo yameonekana kuongezeka ni ni kubaka na kunajisi ambapo kwa mwaka 2016 hadi kufikia novemba makossa ya kubaka yarililipotiwa  yalikuwa 6985 ikilinganishwa na makosa 7460 ambayo yameripotiwa mwaka huu.

Ameongeza kuwa makossa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, wizi wa magari ,uvunjaji ,wizi wa pikipiki, 2016 yaliripotiwa makossa 34830 wakati mwaka huu 2017 yameripotiwa 29677 pungufu ya makossa ya 5153 sawa na asilimia 14.8.
DCI ametoa wito kwa wananchi kuwa wepesi kutoa taharifa pindi wanapoona viashria vyovyote vya uhalifu katika maeneo ya makazi au maeneo ya baiashara.
 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ropert Boaz akizungumza na Waandishi wa habari juu ya hali ya uslama nchini katika kipindi cha Mwaka 2016/2017 na kutaja kuwa uhalifu umepungua kiasi katika baadhi ya makosa.
 Baadhi ya Viongozi wa jeshi la Polisi walishiriki katika mkutano huo wa Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini kinachozungumzwa.
 Baadhi ya Viongozi wa jeshi la Polisi walishiriki katika mkutano huo wa Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini kinachozungumzwa
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa hali ya usalama nchini katika kipindi cha mwaka 2016 /2017.

Tuesday, December 19, 2017

UNHCR YAWAWEZESHA WAKIMBIZI WENYE MAHITAJI MAALUM KUKABILIANA NA CHANAGAMOTO ZA MAISHA NDANI YA KAMBI YA NDUTA WILAYA KIBONDO MKOANI KIGOMA

Ujumbe wa Wanahabari na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)  Wakiwa na Maofisa wa Shirika la Help Age International wakizungumza na Kikongwe cha Miaka 80 ambaye anapata huduma za kijamii kutoka UNHCR Kupitia  Shirika la Help age ndani ya Kambi ya Wakimbizi ya Nduta Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma. Wazee na Walemavu katika Kambi hizo za wakaimbizi wamekuwa na Changamoto kubwa ya kuweza kujipatia mahaitaji ya kila siku na kufanya shughuli zingine za kuwaingizia kipato hili waweze kujikimu hivyo UNHCR Kupitia Mashirika Saidizi imekuwa ikitoa  Msaada kwa makundi hayo maalum
Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) wa Masuala ya Ustawi wa Jamii, Grace Atim akionyesha Jiko la Mafuta ya taa linalotumiwa na  Kikongwe wa Miaka 80 ndani ya nyumba yake iliyopo ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nduta Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma jiko hilo limekuwa msaada kwake kwani hawezi tena kutembea umbali mrefu ndani ya kambi kwenda kutafuta nishati ya kupikia.
 Mmoja wa walemavu waishio ndani ya kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambaye ana uwezo wa kufanya kazi za useremala, akieleza namna ambavyo Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kwa kushirikiana na Help Age International walivyomuwezesha kuendeleza shughuli hizo kwa lengo la kuweza kijikimu kimaisha baada ya kujengewa uwezo. 

 
 Mmoja wa wazee wanaowezeshwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia taasisi ya Help Age Interanational jinsi ya kusuka viti vya asili akipokea maelekezo kutoka kwa Afisa wa Masuala ya Ustawi wa Jamii (UNHCR), Grace Atim. Lengo la kutoa mafunzo mbalimbali kwa nadharia na vitendo kwa wakimbizi waishio ndani ya kambi za wakimbizi ni ili kuwawezesha kuwa na shughuli za kujiongezea kipato pindi watakaporejea katika nchi zao.
Watumishi wa Shirika la Help Age International wakiwa wanaingia katika moja ya nyumba ya Mkimbizi mwenye mahitaji maalumu ndani ya kambi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma. Watumishi hao wamekuwa wakitembelea nyumba za watu wenye mahitaji maalum kila siku hili kubaini ni changamoto gani wanakabiliana nazo ndani ya kambi hiyo 


Baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wakimsikiliza mwalimu katika kambi ya Wakimbizi ya Nduta Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma
--

Monday, December 18, 2017

Vijana wahamasishwa kuanzisha viwanda mara wanapomaliza elimu ya juu

Said Mwishehe,blogu ya jamii

MWENYEKITI wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(TID) Profesa Apollinaria Pereka amewataka vijana  wasisite kuanzisha viwanda nchini  kupitia elimu ya ufundi waliyoipata kwenye taasisi hiyo kwa manufaa ya taifa.

Pia  amesema  wasiogope changamoto watakazokumbana nazo na badala yake wawe wabunifu katika uanzishaji wa bidhaa zao.

Prof Pereka amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye Mahafali ya 11 ya DIT ambapo amefafanua ,Serikali imejipanga kupiga vita umasikini, hivyo vijana ni vema wakaanzisha viwanda ili wajiajiri wenyewe.

Amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kulijenga taifa na kuanzisha viwanda endelevu.

Ameongeza nchi yenye maendeleo makubwa ni ile yenye ujuzi wa ufundi,na wanaotumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya uwanzishaji wa viwanda.Pia amesema kwa sasa  DIT imefikisha miaka 60 tangu ianzishwe  na imefanya kazi kubwa kueneza elimu ya ufundi nchini.

“Utimizaji wa miaka 60 ya DIT imeenda sambasamba na serikali ya awamu ya tano ya kuanzisha viwanda nchini kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi ,hivyo tutakwenda sambamba na serikali hiyo ili kutimiza azma ya Rais, Dk. John Magufuli,"amesema 

Awali Mkuu wa chuo hicho Profesa Preksedius Ndomba,amesema  Serikali ya awamu ya tano inalenga kuleta maendeleo ya viwanda vidogo,vya kati na vikubwa.

"Hivyo vijana wajiunge katika vyuo vya ufundi ili kuweza kupata ajira na kuanzisha viwanda vyao wenyewe.

“Elimu ya ufundi ina umuhimu mkubwa katika serikali hii ya awamu yatano kwa sababu ya uwanzishaji wa viwanda nchini, vijana mjifundishe ufundi sanifu kwa ajili ya manufaa yenu wenyewe”amesisitiza  Profesa Ndomba.

Ameongeza DIT ipo sambasamba na Serikali katika kufanikisha  uanzishwaji wa viwanda, hivyo wapo makini katika utoaji wa elimu yao ili vijana wao wakimaliza wawe wasanifu wazuri katika viwanda vinavyokuja na kwamba wataendelea kupia watalaamu .

Mwenyekiti wa Baraza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT)Process  Apollinaria Pereka akizungumza kwenye Mahafali ya 11 ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu  876 wamehitimu ngazi mbalimbali za kitaaluma za Stashahda, Shahada na Shahada za Uhandisi na Teknolojia.

KUMBILAMOTO AKABIDHI PIKIPIKI KWA KUNDI LA VIJANA WAJASILIAMALI VINGUNGUTI

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto akizungumza na Wakazi wa Vingunguti juu ya namna alivytokeleza ahadi zake kwa kata hiyo alizohahidi wakati wa uchaguzi kablaya kuchaguliwa katika kipindi cha Miaka miwili iliyopita
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto akikabidhi pikipiki kwa kikundi cha Vijana wajasiliamali kinachojulikana kwa jina la Watoto Pori hili iweze kuwasaidi akatika kutunisha mfuko
 Kundi la Vijana wajasilimali wa Kata ya Vingunguti lijulikanalo kama Watoto pori wakifurahi mara baad aya kupokea pikipiki yao aiana ya Boxer kutoka kwa  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto
Wananchi waliofika katika mkutano wa  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamaoto alipokuwa akitoa maelezo ya nini amefanya ndani ya Miaka miwili na kukabidhi pikipiki kwa watoto pori

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa nj...