Friday, January 5, 2018

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MPIGAPICHA ATHUMAN HAMIS

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Mstaafu wa  Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya wananchi wa Dar es Salaam katika mazishi ya aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa magazeti ya Serikali ya Habari Leo na Daily News Athuman  Hamis yaliyofanyika  katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Rais  Mstaafu  Dk. Jakaya Kikwete  katika mazishi hayo alikuwa ameongozana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harson Mwakyembe, Viongozi wa Serikali, Wahariri, wanaandishi  wa habari pamoja na wapiga picha za habari  katika  vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Mauti ya mpigapicha huyo yalimkuta jana katika Hospitali  ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Kabla ya mazishi hayo, nyumbani kwa marehemu  Athumani Hamis Sinza Madukani , Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya TSN, Dk.Jim Yonas amesema, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mbali ya kuguswa na kifo cha Athuman Hamis pia ameahidi  kuijengea nyumba familia ya marehemu itakayokuwa na vyumba vinne.

“Nilikuwa nazungumza na Mkuu wa Mkoa wetu wa Dar es Salaam na ameniambia kuwa ofisi yake itajenga nyumba ya vyumba vine kwa ajili ya familia ya marehemu Athuman Hamis,”amesema Dk Yonas.

Pia amemueleza marehemu Hamis kuwa enzi za uhai wake alikuwa mchapakazi hodari na licha ya kuwa na matatizo ya kiafya bado aliipenda kazi yake.

Amesema Athuman Hamis ameacha pengo kubwa katika tasnia ya habari na kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake hasa kwa wapiga picha wa vyombo vya habari nchini.
Akizungumza baada ya kumzika marehemu Hamis , Imamu wa Msikiti wa Sinza Maijiku Sheikh Mohamed Suileman amesema enzi za uhai wake Hamis alikuwa ni mcha Mungu na alipenda kufanya ibada.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema Athuman Hamis wakati wa uhai wake kabla ya kupata  kupata matatizo ya ajali alikuwa ni mtu mwenye kupenda kufanya ibada.

Rais Mstaafu ya Awamu ya Nne Dr. Jakaya  Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mpiga picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi katika maziko yaliyofanyika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo , Dr Harison Mwakyembe akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mpiga picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi katika maziko yaliyofanyika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
Rais Mstaafu ya Awamu ya Nne Dr. Jakaya  Kikwete  akiteta jambo na Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo , Dr Harison Mwakyembe  katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
Waombolezaji wakihuhifadhi  mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Waombolezaji wakiusaliwa Mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi  katika Msikiti wa Sinza Madukani
Mwenyekiti wa Chama cha Wapigapicha za Habari nchini, Mwanzo Milinga akiweka Udongo kwenye kaburi la aliykeuwa mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu , Gerson Msigwa akiweka Udongo kwenye Kaburi la aliyekuwa mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa Marehemu Athumani Hamisi Sinza Madukani Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiteta na Katibu wa Chama cha wapigapicha za Habari nchini Tanzania , Mroki Mroki nyumbani kwa Marehemu Athumani Hamisi Sinza Madukani Jijini Dar es Salaam

PSPTB IMESEMA WOGA WA WANAFUNZI UMEPUNGUZA UDAHILI KATIKA MITIHANI YA BODI HIYO

Na Humphrey Shao Globu ya Jamii
BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imesema kuwa udahili wa wanafunzi wanaofanya mitihani ya bodi hiyo umepungua kutokana na woga wa wanafunzi hao na kwamba somo la hesabu limekuwa tatizo kubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo, Godfred Mbanyi alisema kuwa lengo la bodi hiyo ni kudahili wanafunzi waliochukua kozi ya ununuzi na ugavi 2,000 lakini tangu mwaka 2016, udahili umekuwa ukishuka.
Amesema kuwa katika mtihani uliofanyika mwaka 2016, walifanya udahili kwa wanafunzi 1,519, waliofanya mtihani ni 1,442, waliofaulu 660 na wanafunzi 745 wanarudia mitihani huku wanafunzi 37 ambayo ni sawa na asilimia 2.6 walifeli.
Alifafanua kuwa udahili wa mwaka huu ulifanyika kwa wanafunzi 1,964 na kwamba wanafunzi 1,578 ndio waliofanya mitihani na 653 wamefaulu mitihani hiyo.
‘’Kutokana na masomo ya ugavi kuhusisha somo la hesabu, kumekuwa na matokeo hafifu kwa wanafunzi wetu wanaofanya mitihani hii ya bodi na tatizo hili limetokea hata mwaka jana. Sababu za watu kufeli masomo haya ni kwa sababu hawapendi hesabu,’’ alisema Mbanyi.
Aliongeza kuwa ‘’Wanafunzi wengi wanaofanya mitihani wanakuwa na background mbaya katika somo la hesabu hivyo tunaendelea kuweka msisitizo kwenye vituo vya maandalizi. Lakini woga wa wwanafunzi unachangiwa na kuwa na mtaala mpya wa mitihani ulioanza Novemba 2016  ambao haukuwepo na unautaratibu mpya wa ufaulu hivyo wanafunzi waliogopa.’’
Pia alisema kuwa somo la  viashiria vya hatari  katika ununuzi na ugavi  ambalo linalenga kutambua na kuainisha viashiria ili kuviepuka wakati wa mchakato wa ununuzi na kwamba masomo ya kujifunzia (case studies) watahiniwa walifeli.
‘’Udahili umepungua lakini tumeweka mikakati ya kutembelea vyuo vyote vikuu na vinavyotoa masomo ya ugavi na ununuzi kwa ngazi ya shahada na stashahada kuwahamasisha kufanya mitihani ya bodi ili watambuliwe na waongezeka,’’ alisisitiza Mbanyi.
Alieleza kuwa bodi hiyo imewataka wanafunzi wanaotaka kufanya mitihani hiyo kupitia katika vituo vya kutolea mafunzo vilivyosajiliw na bodi kwa kuwa sababu za wanafunzi kufeli mitihani hiyo inachangiwa na kutojiandaa vizuri.
Kwa mujibu wa Mbanyi, PSPTB imeweka mkakati wa kuwa na vitabu maalumu ya kufundishia vya aina moja vitakavyotumika katika vyuo vyote nchini na mitihani ijayo itakayoanza wawe wameanzisha vitabu hivyo ili kuondoa mkanganyiko katika kufundishia.
Mbanyi alisema watahakikisha kuwa wataalamu wanaozalishwa wanakuwa na mtazamo wa kufikia uchumi wa viwanda kwa kusoma masomo ya sayansi na hesabu na kwamba utaalamu wa ununuzi na ugavi utaleta matokeo chanya kufikia uchumi huo.
‘’Vyuo vinavyoongoza kwa kuleta wanafunzi wengi ni Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU),  Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Chuo cha Biashara (CBE) na vyuo vinavyochangia ni Chuo cha Jordan Morogoro na Chuo cha Usafirishaji (NIT),’’ alifafanua.
Alisema kuwa vyuo vilivyopo Zanzibar pia vimekuwa vilileta watahiniwa kwa ajili ya kufanya mitihani hiyo ya bodi ili kuingizwa katika orodha ya wataalamu wa masuala ya ununuzi na ugavi.
Kaimu Mkurugenzi wa bodi  ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi  akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wanatangaza matokeo ya wanafunzi waliofanya mitihani ya bodi hiyo mwezi wa Novemba mwaka jana.
Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini Mkutano huo ambao ulikuwa wa kutangaza matokeo na mwenendo wa matokeo ya Mitihani kwa wanafunzi wanaokuja kujiandikisha.

WIZARA YAHAHIDI KUSHIRIKIANA NA KINA BABU SEYA KATIKA KURUDI KWENYE MUZIKI WAO

 Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Studio ya Wanene na Wasanii Nguza Viking , Papii Nguza(Papii Kocha ) kwa ajili ya kurekodi mziki wa Live katika Studio Wanene.
 Msanii wa Muziki wa Dansi Gunza Viking akizungumza na Waandishi wa  Habari mara Baada ya kufanya Mazungumzo na Uongozi wa Wanene Studio na Naibu Waziri.
 Mwanamuziki wa Muziki wa Dansi Papii Kocha akaizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea Studio za Wanene na kufanya Mazungumzo  mkurugenzi wa Studio na Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Juliana Shonza
  Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, akiteta na Mkurugenzi wa Wanene  Studio wakati wa mazungumzo  ya kuweza kufanikisha wasanii hao kurekodi katia Studio hizo
Wasanii   wa  muziki wa Muziki wa Dansi Papii Kocha na Gunza Viking wakiwa wanatoka katika Studio za Wanene Mikocheni Dar es Salaam

Tuesday, January 2, 2018

HAPI ASEMA RUSHWA IMECHANGIA WAKANDARASI KUJENGA BARABARA CHINI YA KIWANGO

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Alli Hapi akionyesha sehemu  Udongo ambao ni matakataka ambayo yalikuwa chini ya barabra ya Msasani CCBRT amabyo imekuwa ikimeguka kila siku kutokana na mkandarasi wa awali alikuwa akijenga juu ya udongo wenye Taka ana kusababishia hasara serikali kila Mwaka.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Alli Hapi akiwaonya wakazi wa Tandale kwa Tumbo juu ya utupaji taka katika mitaro ya Maji iliyopo pembeni mwa barabara amabyo imejaa maji taka nakuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Alli Hapi akionyesha barabara ya Magomeni Kondoa inayokarabatiwa na Wakala wa Barabara nchini Tarura  mara baada ya kuwa na Mashimo mengi na kufanya kushindwa kupitika
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Alli Hapi akichota sehemu ya udongo ulikuwa ukisumbua barabara ya Msasani CCBRT ambao ulikuwa umechanganyika na Taka.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Alli Hapi akikagua barabara ya kuelekea Sleepway Masaki Jijini Dar es Salaam ambayo imeharibika na Mashimo Makubwa na sasa inakarabatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.


BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...