DALADALA ZA KIMARA MATOSA ZATISHIA KUGOMA SIKU YA JUMATANO WIKI HII

Na  Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Madereva wa Magari na Bodaboda zinazofanya safari kutoka Kimara Mwisho kwenda Matosa wametishia kugoma siku ya Jumatano endapo Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kufanya marekebisho ya barabara hiyo hili waweze kupita vizuri.

Akizungumza Globu ya Jamii Dereva wa Noah Paulo Tarimo amesema kuwa barabra hiyo imekuwa na mashimo makubwa sana kwani wamewafata viongozi wa Serikali ya Mtaa na Diwani waweze kuwasaidia lakini awajapata ufumbuzi wa Tatizo lao ambalo limekuwa likichangia kuharibika kwa magari.

"Sisi kama Madereva tunapata tabu sana katika kazi yetu maana hii njia  inaharibu sana magari lakini askari wa usalama barabarani wanakuja kutusummbua kwa kutukamata kuwa sisi tunamagari mabovu jambo ambalo linawakera sana madereva"amesema 

Nae Dereva Mwingine wa Bodaboda katika njia hiyo Rajabu Yusufu amesema kuwa ubovu wa barabra hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa nauli kwa nyakati za jioni kutokana na kuwa na msongamano mkubwa unaosababishwa na mashimo.

amesema kwa kawaida njia hiyo ikiwa safi ni mwendo wa Dakika kumi mpaka Matosa lakini sasa gari zinatumia nusu saa kufika eneo husika jambo ambalo limekuwa liwakwaza watu wengi kutokana na matatizo ya njia.
 Magari ya yakipita kwa shida katika Barabara ya Kimara  Matosa  amabyo imechimbika na kuwa na Mashimo kama andaki ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo ambao kwa sasa utumia zaidi ya nusu Saa kupita hapo
 Magari ya yakipita kwa shida katika Barabara ya Kimara  Matosa  amabyo imechimbika na kuwa na Mashimo kama andaki ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo ambao kwa sasa utumia zaidi ya nusu Saa kupita hapo

Post a Comment

Previous Post Next Post