ELIMU BURE YAWABANA WAZAZI WALIOKUWA WAKIOZESHA WATOTO KATIKA UMRI MDOGO WILAYANI BAHI


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma

Serikali Wilaya ya Bahi  imehahidi kuendelea kushirikiana na Tasisi ya Msichana Initiative katika Mapambano yake ya kupinga ndoa za utotoni na  ukatili wa kijinsia kwa watoto wa Wilaya hiyo  hili waweze kufikia malengo kama ilivyo katika sehemu zingine hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Afisa  Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma , Daudi Kisagure alipotembelea mradi Msichana Cafe unaoendeshwa na tasisi ya Msichana Initiative katika kata kumi za wilaya hiyo.

"lazima niwaeleze ukweli tangu mradi huu wa Msichana Cafe uanzishwe na Msichana Initiative umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kwani tangu mwaka jana mara baada ya watu kupata elimu na kuelewa kesi za watoto kuolewa katika umri mdogo zimepungua sana kwani kwa tathmini ya awali kutoka kwa walimu wa kuu wanasema elimu iliyotolewa imepunguza kwa kiasi kikubwa kwa watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni "amesema Kisagure.

Ametaja kuwa hivyo uwepo wa tasisi hiyo kumeweza kusaidia sana kutoa uelewa kwa wazazi juu ya elimu kwa mtoto na kuwaelimisha juu ya haki za mtoto kuliko ilivyokuwa hapo awali ambapo watoto wengi walikuwa wakiripotiwa kuolewa na kushindwa kuendelea na masomo.

Ametaja kuwa tasisi hii imeweza kufanikiwa zaidi kwani kutokana na mpango wa elimu bure wa ulioanzishwa na Rais Dk John Magufuli umeweza kuondoa visingizio ambavyo apo awali vilikuwa kikwazo kwa watoto wa kike kwenda shule na badala yake kuozeshwa hili wazazi wapate mali.

kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Msichana Cafe, Paulina Mbabala amesema kuwa mradi huo wa kupinga mimba za utotoni umewasaidia sana mara baada ya kufanyiwa semina na kuchaguliwa kama wawakilishi wa kutoa elimu hivyo wameweza kuifikia jamii kubwa na kwasasa wameanza kupata kuelewa umuhimu wa mtoto wa kike kuendelea na masomo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Daudi Kisangire akizungumza jambo na wajumbe wa Msichana Cafe mara alipowatembelea katika eneo lao la kukutani kw aajili ya kujadili changamoto zinazowakabili katika mapambano ya ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni katika kata ya Kigwe.
Katibu wa mradi wa Msichana Cafe katika kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma,Miraji Adam akisoma Taharifa kwa afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo namna walivyofanikiwa kuwafikia wanafunzi na tasisi mbalimbali kutoa elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni.
Baadhi ya Wajumbe wa Mradi wa Msichana Cafe kutoka kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi wakisikiliza kwa makini Nasaha kutoka kwa afisa maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post