Dhamana ya mbowe na wenzake imekwama,wataendelea kukaa mahabusu hadi April 3

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru viongozi wa sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kuletwa mahakamani hapo Jumanne Machi 3, ili kutimiza masharti yanayowataka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Sh milioni 20 kwa maandishi.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria ambapo Jamhuri wamewasilisha nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kutoa dhamana kwa washtakiwa hao.
Wakili Mkuu wa Serikali, Fatma Nchimbi andiye amewasilisha nia ya kupinga washtakiwa hao kupewa dhamana hoja iliyopingwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala.
Baada ya mabishano hayo, Hakimu Mashauri alisema: “Hoja ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa kuwapa dhamana washtakiwa hao, imewasilishwa mapema na inatoa amri washtakiwa hao waletwe Jumanne ili kutimiza masharti ya dhamana kwa kuwa leo hawapo mahakamani.”

“Nikitoa dhamana wakati washtakiwa hawapo haina maana zoezi zima lisimame.” -Hakimu 

“Leo washtakiwa hawajafikishwa mahakamani na nimetoa masharti ya dhamana, hivyo kutoa dhamana na washtakiwa wakiwa bado hawajasaini ilo zoezi bado halijakamilika.” -Hakimu 

“Hivyo kwenye hatua ya sasa ni mapema mno kwa upande wa mashtaka kuwasilisha hoja za kukata rufaa wakati bado mchakato haujakamilika.” -Hakimu

“Mahakama inatoa remove order waje mahakamani April 3,2018 na wadhamini wao ili waje kukamilisha masharti ya dhamana.” -Hakimu

Post a Comment

Previous Post Next Post