UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM


Mwenyekiti  Umoja wa Vijana Wa CCM (UVCCM)  Mkoa wa Dar es salaam Bw. Mussa Kilakala watatu kutoka kulia, wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa uhamasishaji na chipukizi Wilaya ya Ilala Saady Khimji, na wakwanza upande wa kushoto ni Katibu wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, said Yassin said, wapili  kutoka kushoto ni Joan Kataraiya, wakiwa katika picha baada ya kuwasili ofisi ya CCM Wilaya ya Temeke, (Picha na John Luhende). 
MWENYEKITI Umoja wa Vijana Wa CCM (UVCCM)  Mkoa wa Dar es salaam Bw. Mussa Kilakala ameanza ziara kutembelea Wilaya za  Mkoa wa Dar es salaam ambapo leo ameanzia Wilaya ya Temeke  na  amekutana na kuzungumza  na  vijana na watumishi wa Manispaa  hiyo. 
Kilakala amesema kuwa  lengo la Ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi  na pia kuangalia Umoja wa Vijana unavyofanyika fanya kazi zake. 
Akizungumzia upande wa ujasiriamali ameipongeza  Wilaya ya hiyo  kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi waiopungua Elfu Moja na ameendelea kusema kuwa wajasiriamali hao ni lazima wapewe mitaji ili wautumie ujasiriamali wao katika kuzalisha,na Mwenyekiti anasema sehemu ya pekee ambayo wanaweza kuanzia kama Vijana ili kupata mitaji hiyo ni kutoka kwenye Halmashauri ambapo Vijana wanatakiwa wapewe asilimia 5% ya Mapato ya ndani na ni jukumu lao kama Umoja kutembelea Halmashauri na Idara mbalimbali ili wajue utekelezaji wa Ilani juu ya asilimia 5% hiyo na namna ambavyo Vijana wanaweza kunufaika nayo.
Hata hivyo  Kilakala amesema Mkoa wa Dar es salaam umezindua mfumo maalum wa kutambua Vijana wote,ujuzi wao pamoja na shughuli wanazofanya ili takwimu sahihi ziweze kuandaliwa na Vijana wote wanufaike sawasawa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva amewataka wa pokea vijana na hao na kuwa hakikisheni kuwa Ilan ya CCM katika Wilaya Temeke inatekelezwa ipasavyo na kwa upande wa usalama wameimeimarisha ulinzi na matukio ya uharifu yamepungua, na kwamba Halmashauri hiyo inatekeleza miradi ya maendeleo. 

Post a Comment

Previous Post Next Post