Na Sophia Mtakasimba(TaSUBa)
Mchezo wa kuigiza wa jukwaani unaofahamika
kwa jina la Afrika zinduka, umetikisa tamasha la kumi la kigoda cha Mwalimu
Nyerere lililoendelea katika ukumbi wa Nkuruma
wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mchezo huo uliobeba ujumbe wa namna Bara la Afrika linavyoteseka na umasikini
mkubwa ile hali lina utajiri mkubwa wa
mali asili , ardhi na madini umetungwa , umeongozwa na kuchezwa na Kikundi cha “Bagamoyo
Players” cha Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili kuchagiza
ujumbe wa tamasha la mwaka huu uliosema “wimbi la uporaji wa rasilimali Afrika
wanyonge wanajikwamuaje”
Akizungumza katika siku ya pili ya Tamasha
hilo Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama
, amesema kuwa igizo hilo limeakisi namna halisi ya maisha ya sasa ya muafrika
hivyo ni wakati wa kuzinduka.
“Wenzetu wa TaSUBa wametuambia Afrika
Zinduka ,sasa huu ndio wakati wetu wa kuzinduka na kuona namna Afrika inaweza
kunufaika na rasilimali zake.” Alisema bi Mlama
Tamasha la kigoda cha kitaaluma cha
Mwl,nyerere ambalo kwa mwaka huu
limetimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake limefanyika kwa siku tatu kuanzia
tarehe 11-13 Aprili ambapo mada
mbalimbali kuhusu masuala ya kijamii zimejadiliwa .
Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionyesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionyesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionyesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
washiriki wa tamasha wakifuatilia igizo la Afrika Zinduka