Friday, April 20, 2018

JWAZIRI JAFO AFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU NA MADARJA YALIYOBOMOKA MANISPAA YA ILALA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema wizara yake kupitia wakala wa Barabara wa Serikali za Mitaa Tarura itafanya upembezi wa haraka hili kuwez akuhakikisha miundombinu ya barabara iliyoaribika  kutokana na mvua za Masiaka katika barabara za manispaa ya Ilala inarekebishwa haraka sana.

 

Waziri jafo amesema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea madaraja mawili yaliyo katika na maji ya kata ya Gongolamboto Ulongoni A na B  na Pugu Mnadani, ambapo yamesababisha watu kushindwa kuvuka kwa magari kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

“ Hili la ulongoni A litashughulkikiwa kwa haraka kutokana na laenyewe kuonyesha unafuu kidogo lakini Darja la ulongoni B na Pugu wataalamu watabidi wakachini hili waweze kujua ni namna gani yatajengwa hili yasiweze kupata tena madhara pindi mvua kubwa zinaponyesha”amesema Jafo.


 

 Aidha waziri jafoi aliwaomba wale wote waliojenga katika kingo za mto msimbazi kuanz akuondoka haraka kwani madhgara yake ni makubwa kama yalivyoonekana katika mvua hizi ambapo nyumba nyingi zimesombwa na maji na watua wana  pa kukaa.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiwa ameongozana na Viongozi waandamizi wa Manispaa ya Ilala kwenda kuanaglia bafrabra na Madaraja yaliyo athirika wakati wa Mvua.
 W Mkuuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo Sehemu ya Miundombinu iliyoharibika
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Viongozi Waandamizi wa Manispaa ya Ilala waliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema  wakati alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara za Halmashauri. 
Sehemu ya Draraja la Ulongoni A iliyochukuliwa na Maji ambayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo  alikwenda kukagua 

No comments:

Post a Comment

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa nj...