MABINTI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA AJILI YA MANUFAA YA BAADAE

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu , Dkt Ave Maria Semakafu akizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi katik amaadhimisho ya siku ya Tehama kwa watoto wa kike Dunianai ambapo alitumia muda huo kuwaasa mabinti kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya manufaa yao ya badae na kuacha kutumia kwa matumizi ambayo yatawagharimu kwani picha katika mitandao azifutiki.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA), Dkt Raynold Mfungahema  akizungumza kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu katika Maadhimisho ya siku ya Tehama kwa Mtoto wa kike Duniani.


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu , Dkt Ave Maria Semakafu, akipata maelezo juu ya Teknolojia ya Ununuzi wa pedi mtaani kwa shilingi 200 au katika shule za sekondari hili kuweza kumsaidia mtoto wa kike.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu , Dkt Ave Maria Semakafu akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Masafa kutoka TCRA,Mhandisi Stella Bunyenza ni nmana gani gari hiyo inawez akufatilia masafa mbalimbali.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu , Dkt Ave Maria Semakafu akikabidhi zawadi ya Kompyuta kwa Mwanafunzi, Carina Manase aliyefanya Vizuri kwenye somo la ICT 
 Sehemu ya Wafanyakazi wa TCRA ambao ni  Wahandisi wa Kike wakiwa katika mkutano huo  wa Maadhimisho ya siku ya Tehama kwa Mtoto wa kike Duniani.
 Msanii Mrisho Mpoto na Mjomba bendi wakitoa burudani kwa watu waliofika katika Maadhimisho ya siku ya Tehama kwa Mtoto wa kike Duniani.
Sehemu ya Wadau  walioshiriki katika Maadhimisho ya siku ya Tehama kwa Mtoto wa kike Duniani.

Post a Comment

Previous Post Next Post