AWAMU YA PILI YA SPORTPESA SUPER CUP KUZINDULIWA

Na Mwandishiwetu, Jiji la Dar es Salaam

Dar es Salaam, Alhamisi 17, 2018. Awamu ya pili na mashindano yanayohusisha timu bora za Afrika Mashariki-SportPesa Super Cup yanatarajiwa kuanza Juni 3-10, 2018 nchini Kenya kwenye uwanja wa Kimataifa wa Moi uliopo Kasarani.

Timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo kutoka Tanzania ni timu zinazodhaminiwa na SportPesa ambazo ni Simba, Yanga, Singida United pamoja na JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi kutoka Zanzibar), wakati kutoka Nairobi timu zitakazoshiriki ni Gor Mahia, AFC Leopards na Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Dar es Salaam ambapo pia walikuwepo wawakilishi na viongozi kutoka TFF pamoja na viongozi wa timu za Simba, Yanga na Singida United Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas alisema “michuano hii kuleta chachu na kumpata bingwa kwa upande wa Africa Mashariki”

“Matayarisho ya mwaka huu yamefanyika mapema na ukiangalia muda wa kupewa na taarifa mpaka kuanza ni zaidi ya mwaka mmoja, hivyo basi hakuna sababu kwa timu zetu za Tanania zisifanye vibaya zaidi ya mwaka jana kwani matayarisho yamefanyoka mapema na kwa hali hiyo timu zikifanya vibaya tutakuwa na sababu za kuwalaumu”

“Kutakuwa na jumla ya timu nane za Afrika Mashariki na mshindi wa michuano hiyo atacheza na 
moja kati ya timu iliyoshiriki ligi kuu uingereza, Everton”
Timu zitakazoingia robo fainali kwenye mashindano haya watapata kiasi cha dola za kimarekani 2,500, nafasi ya nne timu itapata kiasi cha dola 5000, wakati nafasi ya tatu na wa pili dola 7,500 na 10,000 kila mmoja.
Timu itakayoshinda itazawadiwa kiasi cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kuchuana na timu ya Everton katika uwanja wa Goodison Park.

“Napenda kuwatakia kila la kheri timu zetu tatu zinazokwenda kutuwakilisha jijini Nairobi, natumaini zitatutoa kimasomaso kwa kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana, wataiwakilisha nchi yetu vilivyo kwa kucheza kwa uweledi na nidhamu” alimaliza Ndugu Tarimba
Kwa upande wa timu ya Simba Ndugu Said Tulliy alisema “Napenda kuchukua nafasii hii kuwataarifu wanasimba kuwa tunakwenda kushiriki mashindano kama timu shindani na si timu shiriki na tunajua mwaka jana tulipata nafasi kama hii lakini tuliipoteza na tusingependa kitu kama hicho kijirudie. Tumeona faida yake kutokana na jinsi wenzetu waliopita ni jinsi gani walivyofaidikakupitia mashindano hayo”

“Kama timu tumejiandaa na tuko tayari kuhakikisha tunalinda heshima ya Simba Sports Club na heshima ya Tanzania, tunakwenda na kikosi kamili ili kuhakikisha tunachukua ubingwa ili tuweze kushindana na timu iliyopangwa”

“Tunathibitisha kuwa tutashiriki mashindano haya kwa sababu ni mashindano muhimu, tuko tayari kwa ajili ya mashindano na timu yetu nzima na tuko tayari ya kushinda” alimaliza Ndugu Said Tulliy

“Changamoto ya mashindano iko pale pale lakini kwa mwaka huu nia yetu kuu ni kuchukua ubingwa ili kuleta heshima kimataifa” Charles Boniface Mkwasa Yanga

“Kwanza napenda kuwashukuru SportPesa kwa sababu wamefanya timu yetu kujulikana kwenye kila kona ya nchi, moja kati ya wadhamini wetu wa nguvu ambao tunajivunia sana kutoka kampuni hii. Jambo kubwa tutakaloenda kulifanya kwenye michuano hii kimsingi kwa mwaka huu tumeweza kushirikishwa mapema ili tuweze kujipanga sisi kama timu lakini kikubwa zaidi ikumbukwe kuwa Singida United ni timu pekee iliyofanikiwa kufika nusu fainali kwa hapa Tanzania na mwaka huu tunaamini tutachukua kombe”

Kwa watanzania na watu wa Africa mashariki tunaombawatuunge mkono timu yetu. Ningependa kuwaomba SportPesa kuhakikisha kanuni na sheria za mpira wa miguu zinafatwa ili michuano hii iweze kumalizika vizuri”–Shabani Mande Singida United
Tunapenda kuwashukuru SportPesa kwa kututambua na kutupa nafasi ya kushiriki katika michuano hii na napenda kuwaahidi hatutawaangusha ingawa hii itakuw mara ya kwanza kushiriki.” Maalim Masoud, Katibu wa klabu, JKU.

KUHUSU SPORTPESA SUPER CUP
SportPesa Super Cup ni mashindano ya mwaka yanayohusisha timu bora kutoka Afrika Mashariki kwa wiki moja mfululizo.
Lengo kuu la mashindano hayo ni kuongeza chachu ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na kati, kuwapa fursa vijana kuonyesha na kufichua zaidi vipaji vyao.
Kama kampuni yenya matawi nchi mbali mbali duniani yenye lengo la kuunganisha wapenda soka duniani na kuonyesha maana ya mpira wa miguu kwa nchi za Afrika na inawakilisha nini.

 Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti  wa SportPesa Tanzania Tarimba Abbas akizungumza na Waandishi wa habari juu ya awamu ya pili ya Mashindano ya Super Cup
 Kiongozi wa Klabu ya Simba, Said Tully akizungumzia umuhimu wa Mashindano hayo ya SportPesa Super Cup
 Katibu wa Mkuu wa Yanga , Charles Boniface Mkwassa akizungumzia timu yake ilivyojipanga katika Mashindano hayo

Post a Comment

Previous Post Next Post