SERIKALI YASAINI MKATABA WA KUWAKOPESHA WATUMISHI WA UMMA MITUNGI YA GESI NA VIFAA VYAKE


 Na Mwandishi wetu
Serikali imesaini mkataba na Kampuni ya Gesi ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa umma.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni juhudi za Serikali za kutaka  kupunguza matumizi ya mkaa pamoja na kuni kwa lengo la kutaka kuhifadhi misitu ambayo imekuwa ikitumika  kama nishati.

Mkataba huo ulisainiwa jana  Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo na   Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan na huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Mej. Gen. Gaudence Milanzi akishuhudia tukio hilo.

Mbali na kusaini mkataba huo, TFS na Kampuni ya Mihan Gas zilizindua kampeni ya kukopesha mitungi ya gesi na  vifaa vya vyake kwa Watumishi wa Umma.


Awali, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi  aliwahimiza watumishi kuchangamkia fursa hiyo ya  kukopa mitungi na vifaa hivyo kwani itasaidia katika kuokoa misitu.

“Hili ni tukio kubwa hasa kwa wale ambao ni watunzaji wa mazingira katika kuwezesha jamii kuanza kutumia  nishati mbadala.’’ Alisema

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu  zaTanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo,alisema upatikanaji wa huduma hiyo ni jitihada za kuhakikisha matumizi ya mkaa yanapungua

Aliongeza kuwa nishati mbadala ndo njia pekee itakayosaidia jamii kuachana na  matumizi ya mkaa na kuni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni hiyo,Hamisi Ramadhani aliishukuru Serikali kwa kuikubalia kampuni hiyo kusambaza gesi kwa watumishi.  
Akizungumzia namna watumishi watakavyonufaika na mpango huo,  Mkurugenzi Mtendaji , Ramadhani alisema kampuni imetenga fungu ambalo litarahisisha ukopeshaji wa vifaa hivyo na kila Mtumishi atapewa nafasi ya kuweza kulipia mwezi mmoja mara baada ya kuanza kuitumia gesi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo (kushoto)  akiwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano kati ya  Serikali na Kampuni ya Mihan Gas wa  kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kushoto) akizungumza na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati)   mara baada ya  mkutano  wa utiaji  saini wa mkataba wa makubaliano na Serikali wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa. Kulia ni Eng. Christopher Bitesigire wa Wizara ya Nishati.    

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS), Profesa  Dos  Santos Silayo (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na   Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia)  mara baada ya kusaini mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma   
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi  akizungumza kabla  ya  utiaji saini mkataba  kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS), Profesa  Dos  Santos Silayo akizungumza kabla ya  utiaji saini mkataba  kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Santos Silayo (kushoto)  na   Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia) wakionesha  hati ya makubaliano mara baada ya utiaji saini mkataba  kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi walioshiriki kwenye mkutano wa utiaji saini kati  ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi  pamoja na watumishi mara baada  ya zoezi la utiaji saini mkataba  kati ya Serikali  na Kampuni ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa kukamilika katika mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma              

Post a Comment

Previous Post Next Post