BENKI I&M YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA KUWAPA UJUMBE MZITO



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Benki ya I&M imeandaa futari Maalum kwa ajili ya wateja wake wa Dar es Salaam katika kuadhimisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza wakati wa futari hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki I&M Baseer Mohamed amesema kuwa anawashukuru wateja wa benki hiyo kwa kuendelea kuwapa ushirikiano wa kibiashara ambao umeifanya benki hiyo kuendelea kusimama vyema.

“Mwezi wa Ramadhani unajulikana kama moja ya kati ya nguzo za Dini ya Kislamu na Benki ya I&M kwa kutambua umuhimu wake katika Jamii imeandaa futari hii kama sehemu ya matendo yanayopaswa kufanywa na wanajamii katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani” Amesema Baseer

Baseer  amesema kuwa benki itaendelea kutekeleza mkakati wake wa kibishara wa mwaka 2018 na kuhakikisha kuwa inaendelea kupata ukuaji ni endelevu na kutaja kuwa wamejipanga kuanzisha huduma mpya ya pamoja na kutanua wigo wetu wa utoaji huduma kupitia njia mbadala za utoaji wa huduma za kibenki. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki I&M Baseer Mohamed akizungumza na Wateja wa benki hiyo waliofika katika futari iliyoandaliwa na Benki yake katika Mwezi hu Mtukufu wa Ramadhani
  Mkurugenzi wa bodi ya Benki I&M,Alan Mchaki  akitoa neno la Shukrani kwa  wateja waliofika katika futari hiyo


 Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja Ndabu Swere akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya huduma za benki hiyo katika kipindi cha mwak 2018.

Sehemu ya Wateja wa Benki ya I&M Wakifatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo
 Wateja wa Benki I& M wakipakua futari mara baada ya swala katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
 Wateja wa Benki I& M wakipakua futari mara baada ya swala katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki I& M wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya  futari katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Post a Comment

Previous Post Next Post