ABDUL Mteketa: Nimefika daraja la MAGUFULI kabla sijafa




Na. Mwandishi Wetu
-KILOMBERO
MBUNGE wa zamani wa Kilombero, Abdul Mteketa (CCM), ametimiza azma yake ya kutembelea daraja jipya la Magufuli lililopo Wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Akizungumza leo baada ya kutembelea daraja hilo, alisema yeye alikuwa ni moja ya viongozi waliopigania ujenzi wa daraja hilo ukamilike haraka wakati Rais Dk. John Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya tatu.
“Kama unavyojua katika maisha yangu ya kuumwa pengine nisingeliona hili daraja. Lakini leo nimefika na kuona kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli.


Abdul Mteketa akiwa katika daraja la Magufuli leo hii
“Watu wa Kilombero, Ulanga na Malinyi tunamshukuru kwa dhati kiongozi wetu mpendwa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kulijenga taifa letu na kuleta maendeleo kwa kasi.
“…tayari umekamilisha ujenzi wa daraja na ameshaweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Kidatu hadi Ifaraka- Ulanga, sasa ametufuta machozi watu wa Kilombero-Ulanga na kwa dhati ninampongeza Rais Magufuli,” alisema Mteketa
Akizungumza hali yake ya kiafya, alisema anamshukuru Rais Magufuli kwani kwa sasa hali yake imeimarika baada ya kupata msaada wa matibabu.
“Awali nilikuwa na atembetea kwenye wheel chair  lakini kwa sasa ninaweza alau kusimama kwa msaada wa magongo.  Sina la kusema zaidi ya kusema asante Rais Magufuli nasi Watanzania tunakuombea kwa Mungu akupe afya njema ili uweze kuongoza taifa letu kwa upendo kama unavyofanya sasa,” alisema

Post a Comment

Previous Post Next Post