KESI YA KINA MBOWE NA WENZIE YARUSHWA MPAKA SEPT 27 MWAKA HUU

NA EUNICE SHAO

Kesi dhidi ya vongozi tisa wa  (Chadema) akiwamo Freeman Mbowe wanaokabiliwa na mashtaka 13 likiwemo la uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  itatajwa Septemba 27, 2018

Washtakiwa walipaswa kusomewa Maelezo ya awali leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri lakini imeshidikana kwa sababu mshtakiwa wa tano, Esther Matiko hakuwepo mahakamani na mdhamini wake alieleza kuwa anatatizo la kiafya kwenye mfumo wa uzazi.


Pia  Wakili Peter Kibatala anayewatetea washtakiwa hao, aliieleza  mahakama kuwa mshtakiwa Peter Msigwa ambaye ni mbunge wa Iringa mjini alikuwa akitetewa na wakili Jeremiah Mtobesya ambaye amejitoa.

Aidha, mshtakiwa Peter Msigwa aliiomba Mahakama kuandikia hati ya wito (Summons) Mahakama ya Iringa kwa kuwa muda mwingi yupo katika Mahakama ya Kisutu na yeye bado ana kesi kwenye mahakama hiyo.

Pia ameiomba mahakama impatie  muda wa wiki tatu ili aweze kutafuta wakili mwingine,

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Mbali Mbowe na Msigwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Post a Comment

Previous Post Next Post