Vyama visivyokuwa na Ruzuku vyaitaka Chadema iache kuingilia wagombea wake.

Katibu Mkuu wa Chama cha AFP Taifa, Rashid Mohamed akizungumza na waandishi wa habari  kupinga Tamko la ubalozi wa Marekani kuhusu uchaguzi wa Igunga na kutaka Chadema isiwaingilie kwenye maamuzi yao

NA Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Umoja wa vyama visivyokuwa na Ruzuku nchini ikiwemo chama cha AAFP, DP pamoja na Chama cha Demokrasia Makini wamelaani vitendo vya wagombea wa vyama hivyo kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kulalamikia tume ya uchaguzi kutotenda haki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge kwenye jimbo la Korogwe vijijini.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo, Katibu mkuu wa chama cha AAFP Rashid Mohamed Rai amesema kuwa baada ya kukagua fomu ya mgombea wa chama chake alibaini kuwa kuna baadhi ya tozo ambazo mgombea huyo alikuwa hajalipia licha ya kutumiwa fedha hizo na baada ya hapo akalalamika kuwa miongoni mwa watu ambao fomu zao hazijapokelewa wakati alikuwa hana vigezo na fomu yake ingekataliwa kwasababu hakulipia fedha za baadhi ya ada za uchaguzi.
“Kuna baadhi ya  magenge ya matapeli ambao wamevamia hivyi vyama kwa nia tofauti, kuna watu wanachukua fomu kwa nia ya kugombea wanaweka mfukoni halafu baada ya muda wanaanza kulalamika ukimwambia lete fomu uangalie unakuta yeye mwenyewe hakujaza fomu aliiweka tu” alisema
“Mfano mzuri ni Mgombea wangu, hata ile hela ya uchaguzi ya tume hakulipa halafu siku ya uchaguzi ananiambia fomu haipokelewi na mkurugenzi hayupo mpaka mida ya saaa 9 nauliza wenzake pale wananiambia bado mgombea huyo hajafika eneo la kurudisha fomu, anaingia pale saa 10 na yeye anaungana na hao wanaolalamika kuwa wamefamnyiwa ubaya” aliongeza Rai.
Amebainisha kuwa uchukuaji wa fomu na urejeshaji ni tofauti lakini baadhi ya watu walikuwa wakidanganya ili kutengeneza mazingira ya kugombanisha tume na vyama vya siasa kwa nia mbaya, ambapo CHADEMA waliungana na Mgombea wao na kuanza kutumia maneno makali akilalamikia tume jambo ambalo ni uongo.
“Kama hata ada hakulipa lakini na eye anaungana kwenye mkutano wa  Chadema halafu anatoa povu hapo unajua kabisa kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwaambia wasirudishe fomu” aliongeza Rai kwenye taarifa yake
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa chama cha DP Abdul Mluya amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa mgombea wake majira ya saa saba akilalamika kuwa hamuoni mkurugenzi lakini baada ya hapo alikuja kupata kipande cha video ya mgombea wake akiwa kwenye ofisi ya Chadema akilalamika wakati CHADEMA haina mahusiano mazuri na chama cha DP.
“Sisi DP na Vyama wenza ambavyo havina ruzuku tutaungana  wakati tukienda kwenye uchaguzi wa Monduli kushiriki uchaguzi wa marudio lazima tupite korogwe tuonane na mkurugenzi tukajue tatizo lilikuwa ni lipi kisha tutatoa tamko pamoja au chama kimoja kimoja” alisema Mluya
Aidha amebainisha kuwa  kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwapigia simu wagombea wa vyama hivyo wanaoshiriki uchaguzi wa marudio kwenye Jimbo la Monduli, wakiwatishia na kuwaambia wajiunge na vyama vyao na wawaunge mkono na kusema kuwa vyama hivyo vitaenda kushughulika na kuhakikisha wanakabiliana na watu hao wenye nia mbaya ya kugombanisha tume na Vyama Vyao.





Post a Comment

Previous Post Next Post