WARAMI WAMVAA MBOWE WAMTAKA ASIIPANGIE KAZI MAHAKAMA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuishukia mahakama kuwa haimtendei haki, Watetezi wa Rasilimali za taifa Wasio na Mipaka (WARAMI) wameibuka na kupinga vikali kitendo hicho kwa kusema Mahakama aingiliwi wala aipangiwi hivyo ni vyema wakaicha ifanyekazi kwa weledi .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa Tafiti wa Warami,  Philipo Mwakibinga, alisema kitendo kilichofanywa na Mbowe cha kulalamika kwa vyombo vya habari kuhusu kesi ambayo bado ipo mahakamani, ni fedheha na kuidhalilisha Mahakama.
Amesema Mbowe kupitia tamko lake alidai kuwa kuna viashiria ambavyo vinaonyesha kuwa mahakama inaingiliwa na dola huku akijua kwamba si kweli na kwamba mahakama ni mhimili unaotenda kazi zake kwa uhuru.
 “Si mara ya kwanza kwa Mbowe kuingilia uhuru wa mahakama hasa pale anapoona kuwa kusa analoshtakiwa nalo linaweza kumtia hatiani kwa mujibu wa sheria,” alisema Mwakibinga na kuongeza Mbowe anafanya hivyo kwa nia ya kupata huruma ya watanzania.
“Jana (juzi) kupitia tamko lake alisema kuwa dola inaingilia mahakama ili kuishinikiza yeye ashindwe. Utagundua kwamba huku ni kuvunja sheria na taratibu ambazo tumejiwekea. Tunafahamu kwamba suala lililopo mahakamani halipaswi kuzungumzwa katika public (hadharani) likiwa bado linaendelea mahakamani,” amesema Mwakibinga.
 amesema Mbowe kupitia vyombo vya habari alitoa kauli za uchochezi na kulitisha Taifa kwa kusema kuwa yatatokea yale yaliyotokea nchini Uganda.
“Kwanini Mbowe anatumia vibaya uhuru wake wa kujieleza, je anahaki miliki ya nchi hii? Kwanini ameanza kuitilia shaka mahakama kwamba haitamtendea haki,”
Amesema pamoja na Mbowe kudai kuwa wameonewa kuhusu sakata la kifo cha Mwanafunzi Akwilina ambacho kilitokea wakati wa maandamano yao, watu wanajua kuwa kifo hicho kilisababishwa na wao kwa mazingira yeyote.
“Mbowe ndiye aliyehamasisha watu kwenda kufuata barua za mawakala kwa maandamano tena yasiyo na kibali, lakini pia Mbowe amenukuliwa akisema kwamba wapo tayari kubeba majeneza zaidi ya 200, sasa yawezekana hilo jeneza moja lilikua kati ya hayo aliyosema,” amesema.
Amesema endapo Mbowe na wafuasi wao wasingeenda kufuata barua kwa maandamano hakuna machafuko ambayo yangetokea na kwamba kifo cha Akwilina kisingetokea.
“Ukijaribu kuangalia mwenendo mzima wa tukio hilo Mbowe anaona kabisa anayo hatia na ndiyo maana anakimbia na kusema anaonewa huku akilalama suala  la wakili wake kujitoa ambalo kimsingi ni kawaida endapo wakili anaona atafedheheka kutetea watu ambao wana hatia, alitaka wakili afanye nini?” amehoji.
“Hawa ndio ambao kwa miaka yote wamekuwa wakilalamika mahakama zetu zinachelewesha kesi, leo hii mahakama zimeongeza ufanisi na kujitahidi kusikiliza mashauri kwa haraka wao wanadai kesi inapelekwa haraka,” amesema .

Aidha alitoa wito kwa vyombo vya usalama nchini kumchukulia Mbowe hatua za kisheria kutokana na kutoa matamko ya kichochezi licha ya kuwa ni mshtakiwa wa kesi ya uchochezi.

Post a Comment

Previous Post Next Post