POLEPOLE AHITIMISHA KAMPENI ZA UDIWANI VINGUNGUTI



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

 Kampeni za  udiwani kata ya Vingunguti Zimefungwa leo katika uwanja wa Msikatetamaa, ambapo pole pole alikuwa mgeni rasmi nakuwaeleza makutano hao kuwa chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Dr John Pombe Magufuli kimefanikiwa  mambo mengi ya maendeleo  ambapo hata wapinzani wamekosa hoja za msingi.


 "Watu wenye akili zao vijana na kama Kumbilamoto na akinamama mtatiro wameona Mazuri ya CCM na kuamua kumuunga mkono Rais, nami na waaomba  kesho siku ya jumapili tarehe16/2018 wakazi wa Vingunguti mpigieni kura Omary Said Kumbilamoto mapematu tuwetumeshinda Jina lake kwenye karatasi litakuwa nambambili"amesema


 Viongozi wengine waliomwombea kura Kumbilamoto ni pamoja na mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu , Bonna Kaluwa, wa Segerea, Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Dar es salaam Frank Kamugisha na Julius Mtatiro aliyejiunga na CCM akitokea CUF  na Wenyeviti saba wa Mitaa ya kata hiyo.

Katika hatua nyingine Diwani wa kata ya Buguruni kwa mnyamani Shukuru Dege leo amejivua uanchama wa Chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM, ambapo amesema ameamua kujiunga na CCM kwa kuwa CUF imepoteza mwelekeo na pia ameamua kuunga mkono serikali ya awamu ya tano.

Pamoja na hayo Mgombea wa kata hiyo Omary Said Kumbilamoto amesema amefurahishwa na wananchi wa kata hiyo kwa kumuunga mkono na kuwaomba tena kesho kumpigia kura kwa wingi iliaendeleekuwatumikia  akiwa CCM na kuwaletea maendeleo.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwisho wa Kampeni za Mwisho Udiwani kata ya Vingunguti
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa , Humphrey Polepole akimnadi mgombea wa Udiwani wa kata ya Vingunguti Kupitia CCM , Omary Kumbilamoto
 Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Vingunuti Omary Kumbilamoto akiomba Kura kwa mara ya mwisho wakati w akuhitimisha kampeni
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo kupitia  Chama Cha Wananchi CUF ,Sharifu Mbulu akizungumza mara baada ya kurejea CCM katika mkutano wa kufunga kampeni Vingunguti
 Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza Jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika Mkutano wa kuhitimisha Kampeni Vingunguti
 Aliyekuwa Diwani wa Mtoni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam , Benard Mwakyembe akizungumza wakati wa Mkutano wa kuhitimisha Kampeni kat aya Vingunguti




Post a Comment

Previous Post Next Post