WAITARA ;MIMI SIO MSALITI NIMEFATA MAENDELEO YA JPM

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mgombe Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Mwita Waitara  amesema yeye sio Msaliti Bali amechagua CCM  aweze kumalizia aliposhia ususani swala la barabara , Umeme na Maji katika jimbo  hilo

Waitara amesema hayo leo katika Mkutano wake wa Kampuni uliofanyika katika Kata ya kitunda.

"Naomba niwaeleze ukweli kuwa nilikuwa natumia nguvu sana  katika kufanikisha mambo ya Maendeleo yenu huku  kutokana na sehemu niliyokuwq hivyo sasa nimeamia  huku kila kitu ni mtelezo" alisema Waitara .

Alisema kuwa alikuwa qnapigwa marufuku kuongea na viongozi wa CCM lakini hao ndio wenye  mafungu ya Pesa na serikali jambo amblo mie nilikuwa kinyume nao kiasi cha kuanza kuniita Mimi Msaliti.

Alisema kuwa ajaanza kuitwa Msaliti leo  kwani walimuita Msaliti tangu  alivyokuwa ya kuwasaidia   na kuwaletea Maendeleo watu ambao  wamemwamini hili wapige hatua katika shughuli Zai za kila siku.

Alisema kuwa kwa  sasa unaweza kuzungumza na Waziri moja Kwa moja natayari Waziri wa Nishati  amemuakikishia kuwa Wakazi wote wa eneo hilo watapata  Umeme Kwa gharama za Rea.

Alisema kuwa katika swala la  barabara  na Maji tayari linqpatiwa ufumbuzi chini ya Serikali ya Chama Cha Mapunduzi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Juu ya CCM  Livingstone Lusinde aliwataka watu wa ukonga wasifanye makosa kwani sasa wanachqgua Mbunge wa  jimbo atakayefanya kazi na serikali na sio uchaguzi Mkuu.

Alisema CCM peke yake ndio inatekeleza ilani Kwa kupewa dhamana ya kuongoza dola hivyo wakichahua mgombea kutoka vyama vingine watakuwa wamejitafutia matatizo wenyewe 
 Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara akizungumza Wakazi wa Kata ya Kitunda katika moja ya Mikutano yake ya Kampeni
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akimwaga sera za CCM Namna gani Ilanai inatekelezwa kwa Wakazi wa Kitunda wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo Jimbo la Ukonga
 Mbunge wa Jimbo la Segerea , Bonnaha Kaluwa akizungumza na wakazi wa kitunda kuwataka wadumishe ujirani kw akumchagua Waitara wa CCM
 Mbunge wa Ilala , Mussa Hazzan Zungu akizungumza na Wakazi wa Kitunda na kuwaomba wamchague waitara kwa kuwa ni Msikivu .
 Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia akiwambaia wakazi wa Kitunda Jimbo la Ukonga kuwa kuhama kwa Waitara sio shida kwnai akuanza yeye kutaka kufata Maendeleo yaliyopo CCM
 Mbunge wa Ilala , Mussa Hazzan Zungu Akiserebuka na wkaazi wa kitunda kabla ya kupanda jukwaani .
 Wabunge waliohudhuria Mkutano huo wakisakata rumba linalopigwa na Bendi ya TOT PLUS
  Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara  Akicheza Ngoma ya Litungu kutoka Mkoani Mara
 Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara  akiagana na wapiga kura waliojitokeza katika Mkutano huo

Post a Comment

Previous Post Next Post