SERIKALI KUANZISHA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE KISHERIA, WAZIRI KUPELEKA SHERIA BUNGENI BAADA YA MIEZI MIWILI IJAYO

3-min
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wadau (hawapo pichani) wakati alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo.
10-min
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi Prof. Ninatubu Lema alipokuwa akieleza jambo mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo.
9-min
Kamanda wa zimamoto na ukoaji viwanja vya ndege Tanzania Bara Bw.Juma Athumani akielezaa jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe(hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
8-min
Katibu wa Tughe Mkoa wa Dar es salaam Bi,Tabu Mambo,alipokuwa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
7-min
Mkurugenzi wa JNIA Bw.Paul Rwegasha ,alipokuwa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
6-min
Afisa Habari katika uwanja wa ndege Songwe Bi.Patania Asheri akielezaa jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe(hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
4-min
Afisa Uendeshaji wa TAA kutoka Mwanza Bw.Edger Mwankuga akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe(hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
2-min 1-min
Wajumbe mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika leo katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA WA FULLSHANGE.DODOMA
………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe amesema kuwa Serikali ipo mbioni kuanzisha Wakala waViwanja vya Ndege Tanzania ili kusimamia shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudhibiti viwango vya mafuta ya ndege.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa Baraza la Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini (TAA) Kamwelwe amesema kuwa wafanyabiashara wa mafuta ya ndege wanaendesha kazi hiyo wenyewe bila udhibiti wowote.
“Katika kuboresha mamlaka hii tupo mbioni kunazisha Wakala wa Ndege, na hii itasaidia kudhibiti masuala ya uuzaji wa mafuta, na mtakuwa mnatuuzia nyie, na mimi kama nitakuwa bado nipo baada ya miezi miwili mtasikia naisoma bungeni,” Kmamwelwe Amesema kiwanja cha Kimataifa cha KIA ambacho kinasimamiwa na Kampuni binafsi kitarudiswa serikalini na kuwa chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inatakayoanzishwa ili kisimamiwe na Mamlaka hiyo ya Serikali tofauti na sasa ambapo kiwanja hicho kinasimamiwa na Kampuni binafsi KADCO
“Unakuta mfanyabiashara wa mafuta ya ndege anajiendeshea tu biashara hana udhibiti, mahali pengine kuna ewura wapo? kwanini huku kwenye ndege msimamizi asiwepo? sasa ili kudhibiti hili mtakuwa mnauza mafuta ninyi na hii ni baada ya kuanzishwa kwa wakala,” alisema Kamwelwe
Hata hivyo Kamwelwe ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa inajenga uzio katika viwanya vya ndege ambavyo havina uzio, unatakiwa kuwepo wa nje na uzio wa ndani kwa lengo la kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama.
Waziri Kamwelwe aamesema kuwa Serikali inampango wa kuleta ndege mbili ambazo zitatumika kwa ajili ya mafunzo ya rubani huku akisema uwanja wa ndege Tanga ndio utatumika kwa kazi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka viwanja vya ndege Tanzania Rechard Magongela aliiomba serikali kuijengea uwezo taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa nyenzo za kufanyia kazi pamoja na kuajiri wafanyakazi wengine
Magongela aliomba kuongezewa mishahara na marupurupu mengine kwa watumishi wa mamlaka hiyo, huku akisema;“Usiwaone leo wamevaa suti lakini ukiwona siku za kawaida nyuso zao zimekunjamana kwani wana njaa,” alisema
Hata hivyo alisema kuwa wakati mamlaka hiyo inaanzishwa mwaka 1999 ilikuwa inakusanya sh, billion tatu lakini makusanyo hayo yameweza kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo hadi kufikia mwaka wa fedha 2017/18 walikusanya sh, 70 bilion kwa makusanyo ya ndani.
Naye Kamanda wa zimamoto na ukoaji viwanja vya ndege Tanzania Bara Bw.Juma Athumani aliiomba serikali kuboreshaji viwanja vya ndege pamoja na ununuzi wa ndege uende sambamba na kuboresha vikosi vya zimamoto na ukoaji katika viwanja vya ndege.

Post a Comment

Previous Post Next Post