URASIMISHAJI BANDARI BUBU KUINGOZEA TPA MAPATO


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko, amesema mpango wa kufufua bandari bubu ambazo zipo zaidi ya 250 nchi nzima utaongeza mapato ya mamlaka kwa kiasi kikubwa sambamba na kudhibiti bidhaa za magendo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake jijini Dar es Salaam Kakoko alisema jumla ya mapato ya bandari hizo yanakadiriwa kuweza kufikia theluthi moja au nusu ya mapato ya Bandari ya Dar es Salaam.
Bandari ya Dar es Salaam ambayo imefikia kuhudumia shehena za tani milioni 16.2 kwa mwaka inaingiza Sh  bilioni 70 kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za TPA za mwaka 2017.

Kakoko alisema zipo hatua kadhaa zinazochukuliwa katika mpango wa kufufua bandari bubu ikiwemo kuzianisha, kuwashirikisha wadau, kuzifanyia tathmini, kuandika ripoti ya kuanisha bandari zenye sifa za kuweza kufufuliwa na kisha kuipeleka kwa wizara husika kwaajili ya mapitio na kupitishwa.

Alisema kwa sasa zoezi la kuzitambua na kuzianisha zinaendelea na kwamba zoezi hilo linatarajia kukamika mwezi huu, "tunatarajia zoezi likikamilika tunaweza kupata bandari bubu zaidi ya 300."

"Tayari tumeshafanya vikao na wakuu wote wa mikoa na wilaya  ambazo zina bandari bubu na nusu ya viongozi wote wa vijiji na kata katika maeneo hayo tayari tumeshazungumza nao na zoezi hilo linaendelea," alisema Kakoko.

Alisema ushirikishwaji huo wa wadau umefanyika ili kupata ushirikiano katika utekelezaji wa usimamizi wa bandari hizo pindi zitakaporasimishwa na kutopata mapingamizi.
Kuhusu gharama za kuendesha bandari hizo pindi zitakaporasimishwa alisema kwa kiasi kikubwa hazihitaji gharama kubwa kwani zitakodishwa kwa halmashauri, vijiji au watu binafsi ili kuziendesha na kukusanya mapato kwa niaba ya TPA.

Akizungumzia faida za kurasimisha bandari bubu Kakoko alisema zaidi ya kuingiza mapato pia inasaidia kuondoa biashara za magendo, kuepusha uingizaji wa bidhaa zisizoruhusiwa, na uingizaji wa silaha kinyume cha sheria.

Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa mabadiliko makubwa yanayofanywa na TPA katika kuhakikisha bandari zinachangia kwa kiasi kikubwq ukuaji wa uchumi wa taifa.

"Tuliwahi kusikia Rais wa Rwanda Paul Kagame akisema angepewa bandari ya Dar es Salaam tu ingetosha kuendesha nchi bila kutegemea kitu kingine, na ni kweli kabisa kwasababu bandari ni fedha ndiyo maana serikali sasa imeamua kuwekeza katika uboreshaji wa miundombinu, mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, ulinzi na kuimarisha kitengo cha masoko, mahusiano na mawasiliano kwa umma," amesema.

Amesema pia wamewekeza katika kuongeza ujuzi kwa rasilimali watu kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu hasa katika matumizi ya tehama ambapo vijana wakitanzania wamepelekwa nje na wengine wqkipatowa mafunzo hapa nchini.

Ameongeza kuwa pia wametangaza nafasi za kazi kwà nafasi zilizokuwa wazi pamoja na kuweka nafasi nuingine mpya ambazo zimeonekana kuwa zinahitajika katika kuibadilisha bandari.
Alisema miradi mbalimbali ya upanuzi wa bandari mbalimbali nchini unaendelea katika mwambao wa pwani na katika maziwa makuu ambako magati mapya yanajengwa.

"Tumeona hapa bandari ya Dar es Salaam tayari gati namba moja imekamilika na wiki ijayo tunatarajia kupokea meli kubwa katika gati hiyo na gati ya magari inaendelea ikiwa imefkkia imefikia asilimia 65.
Alisema baada ya miradi hiyo ambayo yote inatarajia kuwa iwe imekamilika na wqtaanza ujenzi wa tunakwenda kujenga gati namba mbili na tatu pamoja 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya urasimishaji wa bandari Bubu na Umuhimu wake katika kukuza pato la Taifa.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali  wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko 

Post a Comment

Previous Post Next Post