Wednesday, January 10, 2018

KAZI ZA MIKONO ZAWASAIDIA WAKIMBIZI WANAWAKE KUPUNGUZA MAKALI YA MAISHA KAMBINI

https://3.bp.blogspot.com/-cq4Gkdq9ZS4/Wjn_H2dgQxI/AAAAAAAANso/dkGYWounc-sTOn0YUlWlWkpb9cfzNpG0wCLcBGAs/s640/IMG_0172.JPG
Baadhi ya wanakikundi Wanawake waishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko  Mkoani Kigoma wakifinyangavyungu mara baada ya kupata mafunzo kutoka shirika la IRC Amballinafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Wanawake hao licha ya kufanikwa kufinya vyungu hivyo huviuza kwa bei ya shilingi 200 kwa kimoja hali ambayo imekuwahaileti tija katika kazi yao.

https://3.bp.blogspot.com/-4cswTBvlJIA/Wjn_QynQdnI/AAAAAAAANss/xKv_HTNFjwMVLgrb7OcoO-grT98W3bW-QCLcBGAs/s640/IMG_0183.JPG
Mmoja wa wanakikundi wa ufinyanzi katika katika Kambi ya wakimbizi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma  Ambaye amepata mafunzo kutoka  tasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR) ambayo yanamuwezesha kutumia muda wake katika shughuli za mikono za uzalishaji. Ili kuhakikisha uendelevu wa vikundi mbalimbali vya wajasirimali ndani ya Kambi za wakimbizi kipato hafifu wanachopata baada ya kuuza bidhaa huingizwa katika mfuko wa kuweka na kukopa (VICOBA) wa kikundi ambao umeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wanakikundi kujiwekea akiba pamoja na kugawana faida inayopatikana kila mwisho wa mwezi. Kutokana na wateja kuwa ni watumishi/wadau mbalimbali wanaotembelea kambi hizi faida yao huwa ni finyu.

https://1.bp.blogspot.com/-aHR-LXODoZY/Wjn_R34o7PI/AAAAAAAANsw/c63x6_f2oz8JHJxLoKdNW9KmvctdGDnDQCLcBGAs/s640/IMG_0184.JPG
Mmoja wa Wakimbizi katika Kambi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma  Ambaye amepata mafunzo kutoka  tasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR). Wanawake hawa wenye uwezo wa kufinyanga vyungu hutumia baadhi ya siku kuwafundisha wanawake wenzao waishio ndani ya kambi hii ya wakimbizi na kwa njia hii elimu inawafikia wanawake wengi. Shughuli za uzalishaji mali/ujasiriamali husaidia kuwajengea wanawake uwezo wa kujikimu kimaisha. Elimu hii itawasaidia hata watakaporejea nchini mwao.

https://4.bp.blogspot.com/-IexY0tWQ4hA/Wjn_fYGtw2I/AAAAAAAANs4/gNHKFKoO8OgcGp1qHTOgBvYX5VSsZIhawCLcBGAs/s640/IMG_0207.JPG
Wanawake wa Kambi ya wakimbizi Mtendeli wakionyesha baadhi ya nguo za Watoto ambazo wamezifuma kutokana na uzi kwa kutumia mkono mara baada ya kupata mafunzo kutoka IRC. “Kabla hatujapata haya mafunzo kutokana na mazingira tnayoishi kwa sasa shughuli pekee tuliweza kufanya ni kupika na kufanya usafi wa maeneo ya nyumba/mahema lakini sasa tunatumia muda katika kujifunza vitu vya maendeleo.”

https://4.bp.blogspot.com/-LZAKsThSDjc/Wjn_kloxm2I/AAAAAAAANs8/o9rb1rVv_7gYeubTDUqgvbkNEPRj7LRTQCLcBGAs/s640/IMG_0228.JPG
Wanawake kutoka Kambi ya Wakimbizi Mtendeli  wakifuma Vitambaa kwa uzi kwa kutumia sindano ya mkono mara baada ya kupata mafunzo kutoka Tasisi ya IRC.
https://4.bp.blogspot.com/-qgkmySwkwPY/Wjn_nmaA3WI/AAAAAAAANtE/xfjcxrFyoAMeYgM3cn-NwBSUmVu5ClbCwCLcBGAs/s640/IMG_0224.JPG
Beatrice Emmanuel - Muwezeshaji wa Wanawake wa kutoka Shirika la IRC linalofadhiliwa na UNHCR, akimvisha mtoto Kofia iliyofumwa na mwanakikundi ndani ya kambi ya Mtendeli.

WAFANYABIASHARA WA WANYAMAPORI HAI NJE YA NCHI WAIOMBA SERIKALI IWASAIDIE

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia)    akifungua kikao cha    Wawakilishi wa Wafanyabiashara  ya Wanyamapori hai   kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara, kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina
 Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji  wanyamapori hai nje ya nchi, Enock Balilemwa  akizungumza kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina   akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  kufungua kikao  cha  Wawakilishi wa Wafanyabiashara  ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji  wanyamapori hai nje ya nchi, Fatuma Hamisi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani)    kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana  mjini Dodoma ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara
 Baadhi ya Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma kati ya Wizara na wadau hao lengo  likiwa ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga na  Wawakilishi wa Wafanyabiashara  ya Wanyamapori hai  kwenye kikao kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT

ELIMU BURE YAWABANA WAZAZI WALIOKUWA WAKIOZESHA WATOTO KATIKA UMRI MDOGO WILAYANI BAHI


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma

Serikali Wilaya ya Bahi  imehahidi kuendelea kushirikiana na Tasisi ya Msichana Initiative katika Mapambano yake ya kupinga ndoa za utotoni na  ukatili wa kijinsia kwa watoto wa Wilaya hiyo  hili waweze kufikia malengo kama ilivyo katika sehemu zingine hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Afisa  Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma , Daudi Kisagure alipotembelea mradi Msichana Cafe unaoendeshwa na tasisi ya Msichana Initiative katika kata kumi za wilaya hiyo.

"lazima niwaeleze ukweli tangu mradi huu wa Msichana Cafe uanzishwe na Msichana Initiative umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kwani tangu mwaka jana mara baada ya watu kupata elimu na kuelewa kesi za watoto kuolewa katika umri mdogo zimepungua sana kwani kwa tathmini ya awali kutoka kwa walimu wa kuu wanasema elimu iliyotolewa imepunguza kwa kiasi kikubwa kwa watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni "amesema Kisagure.

Ametaja kuwa hivyo uwepo wa tasisi hiyo kumeweza kusaidia sana kutoa uelewa kwa wazazi juu ya elimu kwa mtoto na kuwaelimisha juu ya haki za mtoto kuliko ilivyokuwa hapo awali ambapo watoto wengi walikuwa wakiripotiwa kuolewa na kushindwa kuendelea na masomo.

Ametaja kuwa tasisi hii imeweza kufanikiwa zaidi kwani kutokana na mpango wa elimu bure wa ulioanzishwa na Rais Dk John Magufuli umeweza kuondoa visingizio ambavyo apo awali vilikuwa kikwazo kwa watoto wa kike kwenda shule na badala yake kuozeshwa hili wazazi wapate mali.

kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Msichana Cafe, Paulina Mbabala amesema kuwa mradi huo wa kupinga mimba za utotoni umewasaidia sana mara baada ya kufanyiwa semina na kuchaguliwa kama wawakilishi wa kutoa elimu hivyo wameweza kuifikia jamii kubwa na kwasasa wameanza kupata kuelewa umuhimu wa mtoto wa kike kuendelea na masomo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Daudi Kisangire akizungumza jambo na wajumbe wa Msichana Cafe mara alipowatembelea katika eneo lao la kukutani kw aajili ya kujadili changamoto zinazowakabili katika mapambano ya ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni katika kata ya Kigwe.
Katibu wa mradi wa Msichana Cafe katika kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma,Miraji Adam akisoma Taharifa kwa afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo namna walivyofanikiwa kuwafikia wanafunzi na tasisi mbalimbali kutoa elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni.
Baadhi ya Wajumbe wa Mradi wa Msichana Cafe kutoka kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi wakisikiliza kwa makini Nasaha kutoka kwa afisa maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo.

TFC YAPAKIA TANI 200 ZA MBOLEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK. JOHN MAGUFULI


 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili jana na leo jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo,  Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji,  Sagar Shah na Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
 Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipakia mbolea hiyo kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda mikoani.
 Malori ya JWTZ yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
 Shehena ya mbolea hiyo ambayo inasafirishwa kwenda mikoani kwa wakulima
 Mbolea ikibebwa kuingizwa kwenye malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.
 Malori yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.

 Maghara ya kampuni ya Premium Agro Chem Limited yenye mbolea hiyo.

 Na Dotto Mwaibale


KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo. 

Waandishi wa Habari  jana na leo wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo hilo. 

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu juzi, waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori) ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). 

“Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba. 

Mkumba aliongeza kusema kwamba, kutokana na uzito wa agizo hilo lililotolewa na Rais Magufuli, wameongeza nguvu ya magari, yanayoelekezwa mikoa ya Katavi na Rukwa, ambako mahitaji ya mbolea hiyo ni makubwa kwa sasa. 

Alisema nusu saa baada ya tamko la Rais Magufuli, alipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage, akimtaka kuhakikisha wakulima kwenye maeneo husika wanatulia kwa kupokea mbolea. 

“Mbolea hii inapelekwa kwa wakulima kote nchini na itauzwa kwa bei elekezi ya szerikali, na ninawashukuru hawa wenzetu wa kampuni ya Premium Agro Limited kwa kuwa tayari kushirikiana kwa maslahi ya wananchi na Taifa letu,” alkisema Mkumba. 

Mkumba alisema wameamua kuingia makubaliano na kampuni binafsi ya Premium Agro Chem Limited, kupeleka mbolea hiyo kwenye maeneo hayo na mengineyo nchini yenye mahitaji, lakini akiamini kuwepo kwa unafuu kwenye maeneo mengine. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Primium Agro Chem Limited, Sargar Shah, alisema kwamba makubaliano na TFC ni kupakiwa kwa zaidi ya tani 1000 za mbolea hiyo kwenda katika mikoa ambayo wo hawana mawakala na kurahisha upatikanaji na pia kwa bei elekezi ya serikali. 

Meneja Biashara wa Primium Agro Chem Limited, ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia zoezi hilo Brijesh Barot, alisema wamejiandaa vizuri kufanya kazi hiyo mchana na usiku kwa nia ya kufikia malengo ambayo serikali imeyahitaji. 

Barot alisema kampuni hiyo tayari kuanzia mwezi Septemba, imesambaza kwa wakulima kupitia kwa mawakala wao zaidi ya tani 19,500 za mbolea ya kupandia aina ya Urea, ikiwa kwenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50. 

Barot aliongeza kusema kwamba, kampuni yake imeendelea kusambza na kuuza kwa wakulima mbolea zaidi kwa bei elekezi, licha ya kuwa tayari walimaliza kuuza tani 3,500 zilizoagizwa na serikali na kutakiwa kuuzwa kwa bei elekezi. 

“Sisi ni watanzania, wafanyabiashara wazalendo kwa nchi hii, hatutaki kufanyakazi kwa ajili ya kutafuta faida,badala yake tunaungana na Mheshimiwa Rais Magufuli, kuisaidia jamii kwa kufanya kazi ” alisema Barot.

WANANCHI WA LIWALE NA NACHINGWEA WALILIA BARABARA


 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akionesha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa watendaji wa Wilaya ya Liwale (hawapo pichani), ambapo utekelezaji wa miradi yote ya barabara hapa nchini umeanishwa humo wakati alipowatembelea kuona hali ya mtandao wa barabara katika wilaya hiyo, mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Sara Chiwamba.
 Mkuu wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Bi. Sara Chiwamba akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu hali ya mtandao wa barabara wilayani humo katika ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo, mkoani humo kukagua miundombinu hiyo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi. Rukia Muwango kuhusu nia ya Serikali ya kuhakikisha inafungua wilaya hiyo na wilaya jirani ya Liwale kwa kuwajengea barabara kwa kiwango cha lami, mkoani Lindi.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akisisitiza jambo kwa uongozi wa Wilaya ya Ruangwa wakati alipofanya kikao nao wilayani hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Joseph Mkirikiti.
 Muonekano wa sehemu ya barabara ya Ruangwa- Namichiga KM 22 ambapo Wakala wa Barabara mkoa wa Lindi wamepewa jukumu la kuhakikisha inapitika wakati wote.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Mzawa kutoka Kampuni ya Southern Link, Mhandisi Felix Aminieli, anayejenga Daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo katika mto wa Lukuledi, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw.Joseph Mkirikiti.
 Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Lindi, Mhandisi Isaack Mwanawima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua za ujenzi wa daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo katika mto wa Lukuledi, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.
Muonekano wa daraja la Nandanga ambalo lipo katika barabara ya Wilaya ya Luchelegwa-Ndanda inayounganisha wilaya za Ruangwa mkoa wa Lindi na Masasi mkoani Mtwara. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.

Wananchi wa wilaya ya Liwale na Nachingwea mkoani Lindi wameiomba Serikali kuhakikisha inaanza ujenzi wa barabara ya Liwale - Nachingwea (Km 129) kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mazao katika wilaya hizo. 

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, Mkuu wa wilaya ya Liwale Bi. Sarah Chiwamba amesema kuwa wanachi wake wanaamini kuwa Liwale itafunguka kibiashara na kiuchumi endapo itakuwa imeimarishwa katika mtandao wa barabara ambazo zitaiunganisha wilaya hiyo na wilaya jirani pamoja na nchi kwa ujumla.

"Naamini barabara hizi zikikamilika wilaya hii na mkoa wetu utaendelea kiuchumi kwani suala la miundombinu ya barabara imekuwa ni kilio cha muda mrefu katika wilaya yetu", amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Bi. Sarah amefafanua kuwa wananchi wengi katika wilaya hiyo ni wakulima, hivyo wamekuwa wakitumia miundombinu ya barabara kusafirisha mazao ya korosho na ufuta yanayozalishwa kwa wingi kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri huyo anayeshughulikia masuala ya Ujenzi, amewataka wataalamu wote wa masuala ya ujenzi nchini kupitia Sera ya Ujenzi ya mwaka 2003 ambayo itawasaidia kuwapa mwongozo katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma bora kwa jamii.

Ameongeza kwa wataalam wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuwa wabunifu katika ujenzi wa barabara zao ili kuondoa dhana potofu iliyopo dhidi ya usimamizi wa barabara kati yao na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

"TANROADS na TARURA shirikianeni katika kuhakikisha mnawajengea wananchi miundombinu iliyobora, kusiwepo na utofauti kati ya barabara mnazozisimamia", amesema Naibu Waziri huyo.

Ametoa wito kwa uongozi wa TANROADS mkoani Lindi kuhakikisha kuwa wanaboresha maeneo yote ya barabara ambayo ni korofi ili yaweze kupita kiurahisi katika kipindi chote cha mwaka. Naye, Meneja wa TANROADS mkoani Lindi, Mhandisi Isaack Mwanawima, amemhakikisha Naibu Waziri Kwandikwa kuendelea na mpango wa matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa mbalimbali katika mkoa huo.

Naibu Waziri Kwandikwa yupo katika ziara ya kikazi mkoani Lindi kujionea hali halisi ya mtandao wa barabara katika mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo kwenye mto Lukuledi katika barabara ya wilaya ya Luchelegwa- Ndanda inayounganisha wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi na Masasi mkoa wa Mtwara ili kujionea miundombinu yake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

DKT.KIGWANGALA AZINDUA KAMATI KUANDAA MWEZI WA URTIHI WA TAIFA LA TANZANIA

Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangala amekutana na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu shughuli za maandalizi ya Mwezi Maalum wa Maadhimisho ya urithi wa Taifa la Tanzania ili kukwepo na mwezi maalum wa kusherehekea Urithi wa Taifa la Tanzania

 Pamoja na mambo mengine, Kamati hiyo ya kitaifa inategemewa kuandaa utaratibu maalam kwa Watanzania wote ndani na nje ya nchi kushiriki kikamilifu  kupitia midahalo na programu mbalimbali za kielimu; matamasha mbalimbali yakiwemo michezo ya jadi; vyakula vya asili na vazi la Kitaifa.

Dk.Kingwangala amkutana na kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizundua rasmi kamati hiyo ya maandalizi ambapo pia wameamua kwa pamoja jina la maadhimisho hayo ambapo tayari wamekubaliana yatakuwa yanafanyika kila ifikapo Septemba ya kila mwaka.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa lengo la mwezi wa urithi huo wa taifa la Tanzania ni kutoa nafasi ya kuiweziwezesha jamii kuutumia urithi ambao taifa limejaliwa nao kama zao la utalii na hivyo kuchangia kiuchumi katika jamii na taifa kiujumla.

“Pia maadhmisho hayo yatatumika kuelimisha jamii kuhusu kumbukumbu tulizonazo na namna ya kuzitumia kikamilifu katika kuendeleza Taifa na kuboresha maisha yao. Kuzikumbusha jamii chimbuko la tabia, mila na desturi za watanzania

“Na kuzitambua na kuzienzi mila na desturi za makabila mbalimbali ya nchi hii pamoja na kuhakikisha kuwa matamasha yote ya utamaduni yanafanyika katika mwezi husika (mwezi wa urithi) ambao tumekubaliana iwe Septemba ya kila mwaka,”amesema Dk.Kigwangala.

Amefafanua kuwa lengo la wizara yake ni kuhakikisha wanaunganisha wadau katika kuthamini, kuendeleza na kuhifadhi uritihi wa taifa.Hivyo amehimiza taasisi zote za umma na binafsi zinazojihusisha na masuala ya urithi kujiandaa kikamilifu na kuunga mkono dhamira hiyo ili kufanikisha lengo hilo kwa manufaa ya Taifa letu.

“Nichukue fursa hii kuwaomba wajumbe wateule kushirikiana ili kutekeleza lengo hili ili kuendeleza juhudi za kukuza sekta ya utalii kwa manufaa ya Taifa letu. “Ingawa najua kuwa sote tuna majukumu mengine ya kitaifa, ushirikiano wa wanakamati wote pamoja na watendaji wa Wizara yangu ndio utarahisisha ufanisi wa kazi hii. Niwahakikishie mimi na watendaji wa Wizara yangu tutakuwa nanyi bega kwa bega ili kufanikisha kazi hii,”amesisitiza.

Amefafanua urithi huu wa Taifa ni miongoni mwa vivutio vya utalii kwa kuwa ni vielelezo vya historia, utamaduni na ustaarabu wa jamii katika hatua mbalimbali za maisha. “Urithi huu huonesha na kuikumbusha jamii husika chimbuko la tabia, mila na desturi ambazo inazitumia katika nyanja za uchumi, siasa, teknolojia na elimu.

“Jamii yoyote ile inatambuliwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa kutokana na urithi wake. Kwa sababu hiyo, tuna kila sababu ya kuendeleza urithi huu tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu,amesema.

Hivyo kwa kutambua umuhimu huo wa kuuenzi, kuutangaza na kuutumia uritihi wa Taifa la Tanzania kama kivutio cha utalii na kumbukumbu za Taifa, Wizara yake imeona ni vema kukwepo na mwezi maalum wa kusherehekea Urithi wa Taifa la Tanzania .
 Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo  akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania katikati ni Mjumbe wa Kamati hiyo  na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG.
 Waziri wa Maliasili na Utalii  Dkt.Hamisi Kigwangala akizungumza katika mkutano na  Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania uliofanyika leo kwenye chuo cha Utalii cha Taifa Posta jijini Dar es salaam leo kushoto ni Dkt. Aloyce Nzuki Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasoli na Utalii.
 Mjumbe wa Kamati hiyo  na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Jokate Mwegelo.
 Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa  Simiyu Anthony Mtaka akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania wanaofuatia katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa mama Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Jokate Mwegelo na Imani Kajula
 Wajumbe wa kamati hiyo kutoka kulia ni Wema Sepetu na Dkt. Sebastian Ndege pamoja na wajumbe wengine

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA ATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa anaingia katika mapango ya Amboni, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea  mapango hayo mwishoni mwa wiki.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  ( kushoto )  akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said  wakipatiwa maelezo na  Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha mapango ya Amboni, Jumanne Mabule, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea  mapango hayo mwishoni mwa wiki.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  ( kushoto )  akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said  wakipatiwa maelezo na  Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha mapango ya Amboni, Jumanne Mabule, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea  mapango hayo mwishoni mwa wiki.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  ( kushoto )  akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said wakioneshwa mchoro ambao ni mfano wa  mnyama chui uliotokea baada ya mabadiliko katika miamba  ndani ya mapango ya Amboni na  Mhifadhi Mkuu wa Kituo hicho,  Jumanne Mabule, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwenye mapango hayo mwishoni mwa wiki.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga( katikati) akiwa anatembezwa ndani ya mapango ya Amboni na Mhifadhi Mkuu wa Kituo hicho, Jumanne Mabule, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwenye mapango hayo mwishoni mwa wiki.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  ( wa pili kulia )   akioneshwa mchoro ambao ni mfano  wa uwanja wa ndege uliotokea baada ya mabadiliko katika miamba  ndani ya mapango ya Amboni na  Mhifadhi Mkuu wa Kituo hicho,  Jumanne Mabule, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea  mapango hayo mwishoni mwa wiki.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea  mapango ya Amboni  wakati  alipotembelea mapango hayo mwishoni mwa wiki.  

MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NA IDARA ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba akiongoza kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara.Kushoto  meza kuu ni Katibu Mkuu wa wizara, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Hassan Simba Yahya.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, akizungumza  na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa   wizara na idara zilizopo chini ya wizara.Kulia ni Waziri wa wizara hiyo, Dk. Mwigulu Nchemba. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Utawala na Fedha  wa Jeshi la Polisi, Kamishna Albert Nyamhanga,  akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara ya polisi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna Musa Ali Musa.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk. Juma Malewa akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara ya magereza  kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara yake  kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa  Idara  Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(Nida), Alphonce Malibiche, akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara yake  kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MASAUNI AKUTANA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri(kulia) kuhusu ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea zawadi kwa niaba ya wizara kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo  kuhusu ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri, akipeaa mikono  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) wakati akimkabidhi zawadi baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...