Saturday, January 20, 2018

PSPTB YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU WA UGAVI NA MANUNUZI WA CHUO CHA TIA

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniava amewataka wanafunzi wanaosoma masula ya Ununuzi na Ugavi katika chuo cha Uhasibu TIA  Kuwa Wazalendo pindi wanapofika katika maeneo yao ya kazi hili waweze kuwa mfano bora kwa Taifa.

Dc Lyaniva ameyasema hayo laeo alipokuwa akifungua mafunzo ya Masuala ya ununuzi na Ugavi iliyoandaliwa na Bodi ya PSPTB kwa wanafunzi wa Chuo cha TIA ambao wanasoma masuala ya manunuzi.

"Msiwe na mawazo ya kufikiria kupata pesa za haraka haraka pindi mnapopata kazi kwani mkiwa na moyo huo mtaangukia katika makosa ya uhujumu Uchumi jambo amablo watu wengi wa taaluma yenu wameangukia Polisi"amesema Dc Lyaniva.

Napenda kuwambia kuwa Maadili Uzalendo ndio nguzo ya Msingi  katika kufanya kazi ndio Maana Rais wetu Dk John Magufuli ameweza kubadilisha mambo mengi katika nchi kutokana na uzalendo wake
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu cha TIA Kampasi ya Dar es Salaam wanaosoma Masula ya Manunuzi wakati wa Semina Maalum iliyoandaliwa na bodi ya Wataalam wa Manunuzi PSPTB
 Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Wataalam wa Manunuzi nchini, Godfred Mbanyi akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha uhasibu cha TIA ambao walikuwa wanapata Semina Maalum juu ya masula ya Manunuzi
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu TIA, Mugisha Kamala akizungumza kwa ajili ya kuwakaribisha wageni na Mkuu wa Wilaya ya Temeke katika Semina hiyo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi
 Mwenyekiti wa PSA katika Chuo cha TIA, Baraka Selemani akizungumza na juu ya umuhimu  wa klabu za PSA katika chuo hicho na vyuo vingine vinavyotoa kozi ya Manunuzi
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Nhini(TIA), Furahini Mmbakweni akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wakati wa Semina hiyo
 Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu nchini(TIA) juu ya umuhimu wa wataalamu wa manunuzi kuzingatia maadili pindi wanapokuwa kazini.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akiagana na baadhi ya watendaji na wataalamu wa masuala ya Manunuzi na Ugavi
Sehemu ya Wanafunzi waliohudhuria Mafunzo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi kutoka PSPTB yaliyoendeshwa katika Chuo cha uhasibu TIA
 Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo Cha TIA Wakifatilia mafunzo ya Ununuzi na Ugavi yaliondeshwa na PSPTB Katika Chuo cha Uhasibu TIA

Friday, January 19, 2018

KUMBILAMOTO APOKEA NILU MIFUKO 90 YA VIROBA VYA NILU KUTOKA TOL

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kupokea Mifuko 90 ya Nilu kutoka kiwanda cha Tanzania Oxygen Limited ambapo Nilu hiyo itatumika kwa ajili ya kupaka katika shule mbalimbali zinazojengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akipokea viroba vya Nilu ambavyo vitatumika kupaka katika shule zilizopo katika Manispaa ya Ilala.
Karani kutoka kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL),Dorothy Katala  akimuonyesha Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, Idadi ya Viroba vya Nilu anavyotakiwa kuchukua .
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, akisimamia upakiaji wa Viroba vya Nilu kwenye gari hili iweze kufika panapo husika.

Thursday, January 18, 2018

WAZIRI UMMY AMEWATAKA MADAKTARI NA WATAALAMU WA TIBA KUFUATA MUONGOZ WA WHO KATIKA UTOAJI WA DAWA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  amewataka Madaktari na watendaji wa Wizara hiyo kufuta maelekezo ya shirika la Afya duniani (WHO), kutumia kwa umakini mkubwa dawa za antibiotiki ili kudhibiti kuenea kwa usugu wa vimelea vya magonjwa ya kuambukiza.


Waziri Mwalimu amesema hayo Dar es Salaam leo alipokuwa akizindua Kitabu cha Muongozo wa Matibabu nchini na orodha taifa ya Dawa Muhimu.


Amesema muongozo huo wa tano kutolewa, umezingatia kuimarisha huduma katika ngazi za Zahanati na Vituo vya Afya ambapo dawa ambazo hazikuwepo kwenye muongozo wa awali sasa zimeainishwa.


"Baadhi ya dawa hizi ni zile za Katibu magonjwa ya Kisukari, Ukimwi, Kifua kikuu, Malaria... Wizara itaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa kuajiri wataalamu wenye ujuzi stahiki, "amesema.


Amesema katika muongozo huo, dawa za antibiotiki zimegawanywa katika makundi matatu yaan 'ACCESS','WATCH'   na 'RESERVE'.


"Atibiotiki za kundi la kwanza zimeainishwa kutumika katika ngazi zote za kutolea huduma nchini, antibiotiki kundi la pili haziruhusiwi kutumika ngazi ya zahanati na vituo Afya bali zitatumika katika ngazi ya hospitali za halmashauri, "amesema.


Ameongeza kuwa, Antibiotiki kundi la tatu zitatumika katika ngazi ya hospitali za rufaa za kanda, hospitali ya taifa na hospitali maalum.


"Nasisitiza tuzingatie mgawanyo huu pale tunaponunua au kuagiza dawa Bohari Kuu ya Dawa ( MSD), "amesema.


Amefafanua kuwa, matumizi ya muongozo huo wa matibabu na orodha ya taifa ya dawa utarahisisha ununuzi wa dawa kwa MSD  kwani vituo vya vituo vya kutolea huduma vitaweza kufanya makadirio ya manunuzi ya dawa na kuimarisha upatikanaji wake katika vituo vya kutolea huduma.


Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Mohamed Bakari Kambi, amewataka wataalamu kuwa mstari wa mbele kutumia muongozo huo na kutoa mapungufu wizarani ili kuboresha.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kabla ya kuzindua Kitabu cha Muongozo wa Matumizi ya Dawa Muhimu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitabiu cha Muongozo wa Matumizi ya Dawa Muhimu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na Watendaji wengine wakionyesha kitabu kinachonyesha muongozo wa matumizi ya Dawa Muhimu

MAMA SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA


 
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii Dar es Salaam

Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania  wote nchini kutunza miradi ya kutunza mazingira na miundombinu inayojengwa katika Mitaa yao  bila kujali vyama vyao.
Pia  amewataka wananchi kuhakikisha wanaitunza miundombinu hiyo ikiwemo mifereji ili kuepukana na mafuriko yanayotokana na mvua.

Samia aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoa wa Dar es Salaaam ambapo leo amehitimisha kutembelea miundombinu ya kuhifadhi Mazingira katika Wilaya ya Ilala na Mtoni Wilaya Temeke na hapo kesho anataraji kujadili na wadau juu ya changamoto za kutatua mafuriko jijini Dar es Salaam.

 “maendeleo ya nchi  na athari za mabadiliko ya tabia nchi hayana vyama hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha wanatunza miradi hiyo na mazingira kwa ujumla  na nawataka Madiwani wote mnahakikisha Wananchi wanatunza miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata zao na kuwachukulia hatua mara moja watu wote wanaohujumu miundombinu hii”Amesema Suluhu.

Amesema kuna athari kubwa kwa mambo yanayofanywa na Wananchi  wenyewe ikiwemo uharibifu wa mitaro, utiririshaji wa majitaka katika mitaro haswa kipindi cha mvua na kuathiri watoto wetu, kutuathiri sisi wenyewe na viumbe vinavyotuzunguka

Amesema kutiririsha kinyesi kwenye mitaro au kipindi cha mvua sio utamaduni wetu watanzania, hivyo naomba mitaro hii utumike kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwa pamaoja na kufanya usafi katika nyumba zetu na mazingira yanayotuzunguka

Ametaja kuwa  wajibu wa kila serikali kuhakikisha wananchi wake wanaishi salama na ndiyo sababu Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali ikiwemo kujenga miradi ya maendeleo.Tuna wajibu wa kutunza usalama wenu ila pia usalama wako unaanza na wewe mwenyewe

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesemamiradi mingi itaendelea kutekelezwa katika jiji  la Dar es Salaam  ili kunusuru  athari zinazojitokeza ikiwemo  hofu kwa wananchi na kusimama kwa shughuli za kiuchumi kwakuwa jiji hilo ni kitovu cha maendeleo.

Amesema kuwa Dar es Salaam imekuwa aitamaniki wakati mvua zinanyesha hivyo kwa sasa zinafanyika juhudi za makusudi ili kuweza kuinusuru mji huu na mafuriko yasiyokuwa na lazima.
 Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wakazi wa Dar es Salaam leo wakati alipotembelea ujenzi wa Mitaro ya kutiorisha maji ya Mvua katika kata ya Ilala na Mtoni. 
  Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiangalia mfereji wa kutiririsha maji wa malapa
  Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akimpa Maelekezo Diwani wa kata ya Mtoni Benard Mwakyembe  alipotembelea mfereji wa kutiririsha maji ya mvua katika kata hiyo
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba  akizungumza na wakazi wa Dar es Salaam kablaya kumkaribisha Makamu wa Rais 
aziriMtaro wa kutirisha majai ya Mvua uliopo kta ya Buguruni Malapa uliojengwa na  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira   
 Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwaaga wakazi wa Dar es Salaam
 Wakazi wa Dar es Salaam waliofika kumsikiliza Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan

Wednesday, January 17, 2018

WACHUUZI WASEMA BEI YA BIDHAA SOKO LA ILALA INARIDHISHA

 Muuzaji wa Vitunguu katika Soko la Ilala Boma akichambua Vitunguu kusubiri wateja ambapo Vitunguu hivyo kwa Sasa anauza kwa kilo moja ni Shilingi 2000/- za Kitanzania .
 Muuzaji wa jumlajumla wa Ndimu katika Soko la Asubuhi la  Ilala Boma  akimuhudumia mmoja wa wateja wake ambapo kwa sasa anauza ndimu mmoja kwa shilingi  kwa bei ya jumla
 Wauzaji wa ndizi katika Soko la Asubuhi la Ilala Boma wakipatana amabpo ndizo katika soko hilo uuzwa kwa shilingi 125 kwa bei ya jumla
 Mchhuzi wa Magimbi akipanga bidhaa hiyo katika Soko la Asubuhi ya Ilala Boma
 Mmoja wa Mama akiwa amebeba Makabichi yake mara baada ya kununua bidhaa hiyo katika Soko la Ilala Boma ambapo Kabichi moja leo imeuzwa kwa Shilingi 300
Mama akichagua  Makabichi yake mara baada ya kununua bidhaa hiyo katika Soko la Ilala Boma ambapo Kabichi moja leo imeuzwa kwa Shilingi 300

WAJUKU WA MUASISI WA TANU WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI WASIDHULUMIWE NYUMBA YAO

 Mjukuu wa Mwasisi wa TANU Iddi Tosiri, Iddi Maulid akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu kudhulumiwa Kiwanja kilichopo Mtaa wa Ukami Kariakoo ambapo mmoja wa Mwanamke wa Kigogo anataka kuwadhulumu nyumba hiyo hivyo kuiomba Serikali ya Rais Dr John Pombe Magufuli iwasaidie
Mtoto wa Mwasisi wa TANU Iddi Tosiri, Maulid Iddi akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu kudhulumiwa Kiwanja kilichopo Mtaa wa Ukami Kariakoo

MAKAMU WA RAIS AWATAKA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA HILI KUJIEPUSHA NA MAJANGA YATOKANAYO NA MABADILIKO YA TABIA NCHINa Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dar es Salaam
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka  watanzania kuchana na  vitendo vya uharibifu wa mazingira  ili kujiepusha  na Madhara yatokanayo  na mabadiliko ya tabia nchi.

Mama Samia amesem hayo mapema jijini Dar es Salaam leo katika ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa kuta za kingo za bahari jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Tanzania imeharibu mazingira yake kwa kiasi kikubwa hali inayofanya sehemu kubwa ya maeneo yote kuwa na hali tofauti na tulivyotegemea na kutolea mfano mji wa Dodoma ambao watu wamekata miti yote hali iliyosabababisha eneo hilo kuwa jangwa kiasi cha kusababisha maafa pindi mvua zinaponyesha.
Ametaja kuwa  mikoa mingi ambayo ilikuwa na baridi sasa hivi imekuwa ikiongoza kwa joto sawasawa na mikoa iliyopo Pwani kwa mfano mikoa ya Kilimanjaro kila ukiangalia utabiri wa hali ya hewa unaambiwa ina nyuzi joto 32 hadi 33, kiasi ambacho awali haikuwahi kufikia hapo. .

Amesema kuwa adhabu yote hii na  athari tunazoziona sasa inatokana na uharibifu huo mkubwa wa Mazingira .

“Napenda kutumia mfano anaotumia Papa Francis kuwa ukimkosea mwanadamu utakwenda kulia kanisani ama Msikitini utasamehewa lakini ukiyakosea mazingira hayana msikiti wala kanisa yatakuadhibu mpaka utakaporudi kuwa rafiki tena” Amesema Makamu wa Rais .
Amesema nasi tumeharibu mazingira kwa kukata miti, kuchimba mchanga katika fukwe ambapo matokeo yake bahari imepata nguvu ya kula ardhi yetu hivyo turekebishe tulipoharibu ili kurudisha urafiki huuAmesema kwa mkoa wa Dar es Salaam wakazi wake wamekuwa wakitupa takataka katika mitaro na ikiziba inaleta madhara ya mafuriko hivyo hii ni hasara kwa taifa kwa kuwa tunatumia muda mwingi kutoa pole na anayepewa pole hutegemea uende na chochote umsaidie kama mahindi na fedha

 Ameongeza kuwa baada ya kutembelea miradi mbalimbali Ijumaa atakutana na wadau wa mazingira wa mkoa wa Dar es Salaam kupanga mikakati ya kuokoa mazingira.

Naye Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alisema pamoja na kuwa Tanzania haichangii kiasi kikubwa katika uharibifu wa mazingira lakini ni wahanga wa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Athari hizi zinaathiri moja kwa moja uchumi wan chi kutokana na kuathirika kwa kilimo, utalii na uvuvi, hivyo tunaendele na miradi mbalimbali ya kukabiliana ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kingo za bahari maeneo mbalimbali,” amesema Makamba.

Kwa upande wake mtaalamu wa miradi kutoka wizara hiyo,Fred Manyika alisema miradi hiyo inayofadhiliwa na mfuko wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi(Adoptation Fund) inagharimu dola za Marekani Milioni 5.8.

“Fedha hizi zimefanya ujenzi wa ukuta wa kingo za bahari katika eneo la kigamboni na ule wa jirani na Ocean Road jijini hapa,” alisema Manyika.

Aliongeza kuwa miradi mingine inajengwa katika manispaa za Ilala na Temeke inayogharimu dola za marekani 900,000.

“Miradi hii inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya kuzuia bahari kubomoa ardhi, kupanda mikoko na kurudishia matumbawe chini ya bahari na kutoa elimu kwa wananchi,” alisema Manyika.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alisema pamoja na kuwa serikali kuu inamipango yake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi mkoa huo pia unapanda Mikoko iliyoharibiwa.

“Tunapanda mikoko eneo la Mbweni manispaa ya Kinondoni ambapo ekari tano tayari zimepandwa na Tundwi Songani ekari 40,” alisema Makonda
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wakazi wa Kigamboni wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa ukuta wa Kingo ya Bahari ya Hindi kwa upande wa Kigamboni na upande wa Barabara ya Barack Obama Jijini Dar es Salaam ambapo alitumia muda huo kuwaasa Watanzania kutunza Mazingira hili kuweza kuepuka majanga yanayotokana na Mabadiliko ya Tabia nchi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Dezo Civil Controctor Premji Pindoria namna ya ujenzi wa ukuta huo unavyofanyika  kwa kuzingatia mahitaji ya watu watakaotumia fukwe hizo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akitoa kitambaa chake kufuta kiti cha kukalia ambacho kimejengwa kando ya ukuta wa kukinga fukwe ya Bahari ya Hindi upande wa Kigamboni.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira , January Makamba akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais hili aweze kuzungumza na Wakazi wa Kigamboni wakati alipotembelea fukwe za Bahari ya hindi
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza juu ya umuhimu wa kingo hizo kwa wakazi wa Dar es Salaam wakati wa ziara  ya kikazi ya Makamu wa Raisi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akitembea katika ukuta wa kingo ya Bahari uliojengwa kandokando mwa Bahari ya hindi Kigamboni
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akitembea katika ukuta wa kingo ya Bahari uliojengwa kandokando mwa Bahari ya hindi Kigamboni
 sehemu ya wadau na wanafunzi waliofika kusikiliza hotuba ya  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan,
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa wakati alipowasili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi kukagua kingoi za bahari

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan,  akiwa ameketi juu ya kiti  Saruji kilichotengenezwa kwenye kingo za fukwe ya bahari ya Hindi akiwa pamoja na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira , January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Sehemu ya Makada wa Chama cha Mapinduzi wakifatilia kwa Makini utekelezaji wa Ilani wa CCM kwa Vitendo


Tuesday, January 16, 2018

WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO UHABA WA MADAKTARI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 

WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  amesema kuwa kuna changamoto ya uhaba wa madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kwa ajili ya kupata huduma katika hospitali hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati anamalizia ziara yake kwenye hospitali hiyo ambapo amesema pamoja na kuridhishwa na huduma ambazo madaktari wanazitoa kwa wagonjwa katika hospitali hiyo lakini bado kuna changamoto ya uhaba wa madaktari.

"Nimeridhishwa na huduma katika hospitali hii na nimpongeze Mganga Mfawidhi na uongozi  wa Wilaya  kwa kazi nzuri wanayoifanya licha ya kwamba bado tunafahamu kuna changamaoto katika sekta ya afya.

"Madaktari wa Amana kwa siku wanahudumia wagonjwa 800 , hivyo tunachangamoto ya uhaba wa madaktari na kwa kuwa kuna nafasi za ajira 52,000 zimetangazwa tunaamini sekta ya afya tutapewa mgao unaostaili ili tuwe na wataalamu wa masuala ya afya wa kutosha,"amesema Waziri Mwalimu.

Mbali ya changamoto ya uhaba wa madaktari, Waziri Mwalimu ameendelea kuwasisitiza wagonjwa umuhimu wa kuwa na kadi za bima ya afya kwani humfanya anayekuwa nayo kuwa na uhakika wa kupata matibabu kwa gharama nafuu.

"Ifike wakati kila mwananchi awe na kadi ya bima ya afya kwani milango imefunguka na kilichobaki ni kuendelea kuona umuhimu wa kuwa nayo,"amesema Waziri Mwalimu.

Wakati huohuo ametoa onyo kwa watumishi wote wa hospitali za Serikali ambao watabainika kujihusisha na tabia ya kuuza dawa ambazo zimetolewa na Bohari ya Dawa(MSD)ambazo zinatolewa bure waache mara moja.

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akizungumza na wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu wakati alipofanya ziara ya kukagua hospitali hizo mara baada ya Rais Dk John Pombe Magufuli kuagiza Hospitali hizo zianze kusimamiwa na Wizara ya Afya.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Amana, Dr Meshack Shimwela  akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu, akikagua katika ubao wa Matangazo  ambao unaonyesha namna ya watu wanatakiwa kuhudumiwa katika hospitali hiyo.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza na Wanawake ambao wamejifungua katika  Hospitali ya Rufaa ya  Amana
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akipokea maekezo kutoka kwa  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Amana, Dr Meshack Shimwela juu ya ujenzi wa jengo jipya la kuhudumia wagonjwa
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akizungumza na Mmoja ya Wamama ambao wamelzwa na Watoto wao katika wodi mpya iliyojengwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda .


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akikagua Dawa zilizopo katika Bohari ya Dawa ya Hospitali ya Rufa aya Amana Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akizungumza na Madaktari ndani ya Wodi ya watoto katika Hospitali ya Amana.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akikagua Majengo ya Hospitali ya Amana.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...