Friday, February 2, 2018

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KUFANYA MASOMO YA UZALENDO NA MAADILI KUWA NI LAZIMA KILA KOZI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema Chuo chake kitaanza kutoa Somo la Uzalendo,Uadilifu na Maadili kuwa ni lazima katika kila kozi itakayotolewa na Chuo hicho.

Profesa Mwakalila amesema hayo leo alipokuwa akifungua Mhadhara wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana uliofanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere.

“Tutapitia mitaala yote hili kuweza kuongeza masuala ya maadili na Uongozi hivyo kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 Chuo chetu kitaanza kutoa Masomo ya Uongozi, Maadili na Uzalendo kama Masomo ya lazima katika kila kozi itakayotolewa chuoni hapa mitaala yote ipo katika hatua za mwisho na imefikishwa katika mamlaka zinazohusika hili ziweze kurejeshwa shuleni”

Profesa Mwakalila amesema kuwa utaratibu wa kutoa mada mbalimbali kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuhusu uongozi, Maadili na utaifa umeshaandaliwa .
Kwa upande wake mmoja wa watoa mada katika Mhadhara huo  Ibrahim Kaduma aliwakumbusha Vijana hao juu ya umuhimu wa kuwa Wazalendo kwa kuwasomea ahadi za Tanu kuwa kama Muongozo wa kutunza maadili katika kazi zao za kila siku.

Kaduma pia alitumia mahadahara huo kuwaambia Vijana juu ya umuhimu wa azimio la Arusha katika kujiletea misingi la Maendeleo hivyo kumuagiza kila kijana wa chuo hicho kwenda kusoma azimio hilo kwa umakini.

Kwa upande mtoa Mada Mwingine Samuel Kassori alizungumza juu ya uadilfu na kusema ni vyema viongozi wakalejea kusoma baadhi ya hotuba za Mwalimu na kusisitiza juu ya hotuba ile ya jisahiishe ambayo imezungumza namna ya Mwalimu Nyerere alivyoandika juu ya umuhimu kwa kila mmoja kujitathmini katika kazi za Serikali.

Amesema Viongozi wengi wameshindwa kumsaidia Rais John Magufuli matokeo yake wamekuwa wakifanya kazi kwa kukurupika bila ya kuwafikilia watanzania waliopo nyuma yao.
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho wakati wa Mhadhara wa wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Samuel Kassori  Mtoa Mada katika Mhadharawa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere  
 Ibrahim KadumaMtoa Mada katika Mhadharawa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere  
 Afisa Habari wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Evelyn Mpasha akizungumza jambo na Wanafunzi wa Chuo Hicho.
Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakifatilia Mhadhara wa wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Thursday, February 1, 2018

KUMBILAMOTO AKABIDHI KIFAA CHA KUPIMIA PUMU KWA AJILI YA ZAHANATI YA VINGUNGUTI

 Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akizungumza kabla ya kukabidhi kifaa cha kupimia pumu kwa watoto na watu wazima na Vifaa vya Kujifungulia katika Zahanati ya Vingunguti  ambayo Wanawake ufika hapo bila ya kuwa na Vifaa vya kujifungilia hivyo vitaweza kuwasaidia wale ambao awatakuwa na uwezo.
 Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara baada ya kupokea Vifaa hivyo na kuvikabidhi katika Zahanati ya Vingunguti
  Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akikabidhi kifaa cha kupimia Pumu kwa  Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, kwa ajili ya Zahanati ya Vingunguti.
 Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akikabidhi Vifaa vya Kujifungulia kwa ajili ya wajawazito  kwa  Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, kwa ajili ya Zahanati ya Vingunguti.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vingunguti, Sharif Mbulu akizungumza kushukuru mara baada ya kupokea Vifaa  kwa ajili ya Hosptali ya Vingunguti
Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto na  Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, wakikabidhi Mbuzi  kwa ajili ya  Madkatari na wauguzi wa Zahanati ya Vingunguti.

Tuesday, January 30, 2018

REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Tasisi ya Utafiti nchini Repoa leo imeongoza watafiti mbalimbali nchini katika Mkutano wa Watafiti Duniani ujulikanao kama "WHY THINKS MATTER"  Ambao umefanywa na watafiti wote Duniani kuanzia Saa tatu mpaka Saa tano.

Dr Mmari amesema kuwa Mkutano huo unafanyika na nchi 170 Duniani amabpo mwaka huu wanazungumzia Umuhimu wa Tasisi za Utafiti wa Duniani ambapo  kwa sasa kumekuwa na Changamoto ya ukuwaji wa teknolojia na watu kupotosha tafiti kutoka na hali ya kisiasa.

"siku hizi kuna changamoto ya mitandao ya kijamii taharifa zinasambaa haraka  na taharifa zingine azina ukweli wowote na kusababisha viongozi wakaziamini na kuzitumia katika utungaji wa sera na kuendesha shughuli mbalimbali za Serikali , hivyo ikaonekana kuwa ni muhimu mwaka huu wakazungumzia tafiti ambazo zimefanyiwa kazi kisayansi" Amesema Dr Mmari.

amesema umuhimu wa Watafiti umeweza kusaidia katika kufanya Maendeleo ya kweli hivyo nashawishi Watanzania waweze kuendelea kufanya tafiti ambazo zinaweza zitatumika kwa ajili ya mipango ya Maendeleo ya Serikali na Wadau Mbalimbali.

Amemaliza kwa kusema kuwa si vyema watafaiti wakafanya tafiti ambazo zinawekwa  tu kwenye makabati pasipo kuwa na Matokeo yoyote kwa Taifa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti Nchini,REPOA, Dr Donald Mmari  akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Tafiti Duniani ambao kwa Tanzania ulifanyika katika Ofisi za Repoa na kuitwa jina la Umuhimu wa Tafiti Duniani
 Balozi wa Swideni Nchini, Katarina Rangnitt akizungumza wakati wa Mkutano wa Watafiti Duniani(WHY THINK TANKS MATTER) uliofanyika katika Tasisi ya utafiti ya Repoa kwa hapa nchini.
 Mtafiti Kutoka Tasisi ya Utafiti ya Repoa,  Dr Blandina Kilama akizungumza wakati wa mkutano huo wa watafaiti Duniani.
 Baadhi ya Maprofesa walioshiriki Mkutano huo wakiongozwa na Profesa Mwesigwa Baregu wa kwanza kulia Pichani.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano huo wakisikiliza Mada Mbalimbali kutoka kwa watafiti  na Wadau mbalim,bali.

KUPASUKA KWA BOMBA LA MAJI LAZUA TAHARUKI TABATA

 Wakazi wa Tabata Chang'ombe wakiwa wanashangaa Bomba la Maji lililopasuka kutokana na Ukarabati unaoendelea katika barabara hizo ambazo zinajengwa na Tarura, ukarabati wa barabara hizo utasaidi kuwaunganisha wakazi wa Tabata Chang'ombe na Kisukulu bila kuzunguka njia ya Bima.
 Sehemu ya Barabara ya ianayokarabatiwa na Wakala wa Barabara nchini Tarura eneo la Tabatra Chang'ombe .

Monday, January 29, 2018

Uchaguzi Dodoma, mabondia 5 kupelekea michuano ya Jumuya ya Madola.

Na Agness Francis Globu ya Jamii. 
Katibu mkuu  BFT Makore Mashaga amesema kuwa  Katika kujiandaa na michuano ya kuelekea Jumuiya ya Madola wataelekea Mjini Dodoma ili kufanya mashindano ambayo yatakuwa ya kujipima uwezo kati ya mabondia hao 13.

Akizungumza hayo leo katika ofisi zao Temeke Jijini Dar es Salaam  Katibu huyo amesema kuwa  licha  ya kujianda  vema katika  michuano hiyo wameona ni vizuri kufanya Shindano ili  kupima na kuona viwango vya mabondia hao ili kuweza kujua wamefikia kiwango gani na  makocha waweze kurekebisha makosa kabla ya  kwenda kwenye michuano hiyo ya Jumuiya ya madola. 

Ambapo mazoezi  hayo yalianza mwezi wa 4 wakiwa mabondia 30 ikiwa mpaka sasa wamebaki 13 kutokana na Mchujo mara  baada ya kumaliza mazoezi. 

Katibu huyo amesema kuwa katika  Mashindano hayo wamealika wageni kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Mikoa yote hapa Nchini,  Afrika Mashariki na nje ya Bara ambapo mashindano hayo yatafanyika tarehe 25 mwezi wa 2  mpaka  tarehe 2 mwezi wa 3.

"Kati ya mabondia13 watachaguliwa 5 ikiwa mataifa mengine wanapeleka  washiriki 10 ila tunaomba angalau   tupeleke watu 8 Ili kukari bia angalau kufikia uwiano wa Nchi   nyingine"Amesema Katibu Mashaga. 

AidhaKocha BFT David Yomba Yomba amesema kuwa  mandalizi ni mazuri wachezaji  wote wamekamilika kila idara na wananguvu za kutosha na wanaamini watafanya vema katika mazoezi ya kuelekea michuano ya jumuiya ya Madola.
 Karibu Mkuu BFT Makore Mashaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi yanayoendelea kuelekea Michuano ya Jumiya ya Madola leo katika ofisi zao Temeke Jijini Dar es salaam.
Kocha BFT Davidi YombaYomba akizungumza na waandishi wa habari huku akijiitapa kuwa vijana wake wapo vizuri kabisa tayari kwa mpambano leo katika ofisi zao Temeke Jijini Dar es Salaam

MSEMAJI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI ATEMBELEA CHANNEL TEN

 Mwandishi wa habari na mtangazaji mwandamizi wa African Media group Ltd inayosimamia Vyombo vya utangazaji Channel ten na Magic Fm, Bw. Kibwana Dachi akifafanua jambo kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.
 Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja (katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtangazaji mwandamizi wa Channel Ten na Magic fm, Kibwana Dachi katika studio za Channel Ten, (kushoto) ni Damian Muheya na Nasibu Mgosso (kulia) wakiwa ni Maafisa habari wa Jeshi hilo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.
 Mkuu wa Kitengo cha kurusha matangazo Channel Ten, Bw. Abdallah Lugisha akitoa ufafanuzi jinsi mitambo ya kurusha matangazo inavyofanya kazi kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja akiwa ameambatana na Maafisa habari wa Jeshi hilo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.
 Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja akijibu swali kutoka kwa mtangazaji wa Magic Fm Salma Msangi katika kipindi cha Busati wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018. Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

DALADALA ZA KIMARA MATOSA ZATISHIA KUGOMA SIKU YA JUMATANO WIKI HII

Na  Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Madereva wa Magari na Bodaboda zinazofanya safari kutoka Kimara Mwisho kwenda Matosa wametishia kugoma siku ya Jumatano endapo Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kufanya marekebisho ya barabara hiyo hili waweze kupita vizuri.

Akizungumza Globu ya Jamii Dereva wa Noah Paulo Tarimo amesema kuwa barabra hiyo imekuwa na mashimo makubwa sana kwani wamewafata viongozi wa Serikali ya Mtaa na Diwani waweze kuwasaidia lakini awajapata ufumbuzi wa Tatizo lao ambalo limekuwa likichangia kuharibika kwa magari.

"Sisi kama Madereva tunapata tabu sana katika kazi yetu maana hii njia  inaharibu sana magari lakini askari wa usalama barabarani wanakuja kutusummbua kwa kutukamata kuwa sisi tunamagari mabovu jambo ambalo linawakera sana madereva"amesema 

Nae Dereva Mwingine wa Bodaboda katika njia hiyo Rajabu Yusufu amesema kuwa ubovu wa barabra hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa nauli kwa nyakati za jioni kutokana na kuwa na msongamano mkubwa unaosababishwa na mashimo.

amesema kwa kawaida njia hiyo ikiwa safi ni mwendo wa Dakika kumi mpaka Matosa lakini sasa gari zinatumia nusu saa kufika eneo husika jambo ambalo limekuwa liwakwaza watu wengi kutokana na matatizo ya njia.
 Magari ya yakipita kwa shida katika Barabara ya Kimara  Matosa  amabyo imechimbika na kuwa na Mashimo kama andaki ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo ambao kwa sasa utumia zaidi ya nusu Saa kupita hapo
 Magari ya yakipita kwa shida katika Barabara ya Kimara  Matosa  amabyo imechimbika na kuwa na Mashimo kama andaki ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo ambao kwa sasa utumia zaidi ya nusu Saa kupita hapo

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...