Thursday, February 8, 2018

RITA SASA KUTOA CHETI CHA KUZALIWA SIKU MOJA MUHIMBILI HOSPITALINa Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Wakala wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini(RITA),Imefanya Maboresho ya Kanzidata na mfumo wa usajili wa vizazi na kifo kupitia mradi wa maboresho ya Miundombinu ya TEHAMA.

Akizungumza na Wahandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Sifuni Mchome amesema kuwa lengo kuu la maboresho ni kuwezesha matukio ya vizazi na vifo kufanyika kwa ufanisi Zaidi na karibu zaidi na wananchi na kuimarisha miundombinu ya usajili ,usafirishaji taarifa ,uhifadhi wa taarifa pamoja na matumizi ya taarifa ndani nan je ya Wakala.

“Maboresho ya mfumo wa usajili yamezingatia mahitaji ya mkakati wa kitaifa wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu unaolenga kuboresha usajili wa matukio muhimu” amesema.

Amesema maeneo yaliyolengwa katika mradi huo ni kama yafuatavyo ni kuboresha miundombinu ya kanzidata , kuweka vituo 60 vya majaribio na madawati manne ya usajili RITA makao makuu , Maboresho ya mfumo wa kielektroninik wa usajili ,maboresho ya mfumo wa utafutaji wa taarifa za zamani na kuweka mfumo maalum wa kutoa namba za kuzaliwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,Sifuni Mchome akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya mfumo mpya wa usajili  wa Wakala wa Usajili ,ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kutumia TEHAMA
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili ,ufilisi na Udhamini (RITA),Emmy Hudson akitoa ufafanuzi juu ya mfumo wa usajili wa vizazina vifo kupitia mradi wa maboresho ya Miundombinu
Wadau na Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano  wa  Wakala wa Usajili ,ufilisi na Udhamini (RITA)

MTULIA AENDELEA KUSEMA KUWA SERA ZA MAGUFULI ZITAIBADILISHA KINONDONI

 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi Maulidi Mtulia akizungumza kuomba kura katika Mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera Livingstone  Lusinde akizungumza kumnadi mgombea mara baada ya kupokea waufuasi wawili kutoka CHADEMA ambao kwa hiari yao wenyewe wameamua kujiunga na CCM.
 Kampeni Meneja wa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi katika Kinyang'anyiro cha Ubunge Kinondoni, Iddi Azzan akizungumza wakati alipokuwa akimnadi mgombea wa Chama chake Maulid Mtulia.
 Wabunge wa Chama Cha Mapindzui wa Mkoa wa Dar es Salaam  wakifatilia mkutano wa Kampeni
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi Maulidi Mtulia akizungumza kuomba kura katika Mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wananchi wakifatilia mkutanowa Chama Cha Mapinduzi katika kata ya Makumbusho 

Wednesday, February 7, 2018

SALUM MWALIMU ASEMA PESA ZA MAENDELEO HAZINA CHAMA

 Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu akihutubia katika Mkutano wa Wananchi uliofanyika katika Kata ya Kigogo akiomba kura hili aweze kupata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni katika Uchaguzi Mdogo wa Marudio utakaofanyika February 16, 2018
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akumuombea Kura Mgombea Ubunge wa CHADEMA Salum Mwalimu katika Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Raound abot ya Kigogo .
 Waziri Mkuu Mstaafu, na Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Chadema , Fredrick Sumaye akihutubia Wananchi wa kata ya Kigogo katika Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Raound abot ya Kigogo.
 Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu , akiwa Juu ya gari  na kuwapungia mkono wakazi wa Kigogo mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuomba kura kwa Wananchi
Sehemu ya Wananchi wa kata ya Kigogo waliojitokeza kwa wingi katika Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...