Skip to main content

Posts

Showing posts from February 11, 2018

MWAKIBINGA AONGOZA WAISLAMU KAWE KUPELEKA KILIO CHAO KWA RAIS MAGUFULI

Mwanaharakati na Mzawa Kawe James Mwakibinga akizungumza na wakazi wa Kawe wakati walipokuwa wakitoa ombi lao kwa Rais Magufuli kupitia Waziri Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuingilia kati mgogoro wa kiwanja namba 196 kilichojengwa Msikiti ambapo mmoja ya mfanyabiashar anataka kubomia Msikiti huo


 Mwanaharakati na Mzawa Kawe James Mwakibinga akizungumza na wakazi wa Kawe wakati walipokuwa wakitoa ombi lao kwa Rais Magufuli kupitia Waziri Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuingilia kati mgogoro wa kiwanja namba 196 kilichojengwa Msikiti ambapo mmoja ya mfanyabiashar anataka kubomia Msikiti huo  Katibu wa Msikiti huo akitoa tamko la Msikiti kutangaza kuwa awakubaliani kamwe na maamuzi ya Mahakama kwani haki aikutendeka katika utekelezwaji wa hukumu yao ya kutaka msikiti huo uvunjwe
Sehemu ya Waandishi wa Habari na Wakazi wa Kawe wakifatilia kwa Makini Mkutano wa Msikiti wa Kawe ukwamani kupinga kubomolewa Msikiti wao na Wafanyabiashara.

HAKI ELIMU YASEMA WAZAZI WENGI WANAWATELEKEZA WATOTO WENYE UONI MASHULENI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Tasisi ya Haki Elimu imesema kuwa tafiti ya Tathmini ya Mafunzo na ushirikishwaji wa Wanafunzi wenye Changamoto za uoni katika shule jumuishi hapa nchini  umetoa majibu kuwa watoto wengi wenye matatizo hayo wamekuwa wakitelekezwa  mashuleni na wazazi wao.
hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la Haki Elimu, John Kalage alipokuwa akisoma ripoti hiyo kwa wadau na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari.
Amesema kuwa lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kutathimini iwapo mazingira ya shule jumuishi za kuanzia Msingi Mpaka Sekondari yanakidhi mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na kama sera na mikakati ya elimu inakidhi mahitaji tofauti ya wanafunzi wakati w akujifunza na kufundishwa.
"utafiti huu ambao umefanyika katika mikoa tisa ya Tanzania baraambayo ni Dodoma , Iringa , Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga,Tabora na Tanga hivyo ni matumaini yangu kuwa utafiti huu utatoa taswira ya hatua tuliyofikia kama taifa katika utekelezaji wa sera n…

VANESSA MDEE ATETA NA WATOTO WA BAGAMOYO KUPITIA AMANI PROJECT

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bagamoyo
 Msanii wa Muziki wa Bongofleva, Vanessa Mdee amesema jamii inawajibu wa kuwajengea uwezo wa kujitambua katika umri mdogo hili kuwa na taifa ambalo litakuwa na Usawa wa kijinsia na Amani.

Vanessa amesema hayo wakati alipokuwa akifungua Mradi wa Amani Project unaoendeshwa katika Shule nne za mkoa wa Pwani Wilaya Bagamoyo na Tasisi ya Msichana Initiative . "amani Project inaweza kubadilisha maisha ya kijana wa kitanzania kwani waswahili wanasema Samaki mkunje angali mbichi hivyo wanafunzi wanapopata fursa kama hii inawasaidia sana katika kutunza amani iliyopo hpa nchini, kwani imezoeleka siku zote kuwa watoto wa kiume kuwa ndio wanafanya vitu vile vyenye mafanikio lakini mradi huu upo kwa ajili ya kutengeza usawa baina ya wavulana na Wasichana"Amesema Vanessa.

 kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Msichana Initiative Rebecca Gyumi amesema mradi huu unalengo kuhamasisha masuala ya usawa kijinsia upendo na akili ya kihisia kwa …

DC SINYAMULE AIPONGEZA TAKUKURU SAME

Na Mwandishi wa Globu ya Jamii Same
Mkuu wa Wilaya  Same Rosemary Senyamule, ameipongeza Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) Wilaya ya Same kwa kumkamata katibu wa Baraza la ardhi la kata ya Mamba Myamba kwa kosa la Kuomba, Kushawishi na  Kupokea hongo ya Tshs. 200,000/= kinyume na kifungu cha 15 cha sheria na. 11/2007. Dc Sinyamule amesema kuwa Rushwa hiyo ilipokelewa kutoka kwa mteja wake ili ampe nakala ya hukumu na mwenendo wa shauri lilikuwa limesikilizwa katika baraza la Kata. “Rushwa imepelekea kutoisha kwa migogoro Mingi  ya ardhi maeneo mengi hivyo nawapongeza sana wananchi kwa kutoa taarifa za dhamira hii mbaya na ninaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa mara wanapoona viashiri au dhamira ya rushwa." Amesema Sinyamule
Dc Sinyamule amewasisitiza TAKUKURU kuendelea kuwakamata wote wanaochafua jina la Serikali kwa kunyima haki wananchi na kutaka rushwa  hivyo watu hao awapaswi kuvumiliwa wala kuwaonee haya, ili kazi hii nzuri mliyoifanya iwe…

SERIKALI IMESEMA ITAENDELEA KUIMARISHA MFUMO WAKE WA UTOAJI DAWA

Na Mwandishiwetu Serikali imesisitiza kwamba itaendelea kuimarisha mifumo yake ya utoaji huduma za dawa kutokana na ukweli kwamba baadhi ya dawa zinatumika kwa wanyama na binadamu na kuleta usugu wa ugonjwa husika kwa mgonjwa na  gharama kubwa kwa taifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na watoto,Dr Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa siku nne wa Jukwaa la kudhibiti usambazaji na uzalishaji wa bidhaa za madawa Afrika ambapo nchi 18 zipo nchini kujadili namna bora ya kudhibiti madawa yasiyo na viwango katika soko ili kuimarisha na ustawisha afya za wananchi wake.
“Tanzania ni moja ya nchini iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa dawa feki kwa Afrika nzima na mamlaka ya dawa na vipodozi nchini ina maabara za kisasa na watalaamu wa kutosha wa kuweza kufanya ukaguzi wenye ubora na viwango vya kimataifa,” amesema Ndungulile
Ameongeza kwamba Tanzania imeweza kujitosheleza kwa dawa za kutosha na zenye viwango vya kimat…

WADAU MBALIMBALI WAKUTANA KUJADILI MADHARA YATAKONAYO NA NDOA ZA UTOTONI

Mwanasheria  na Wakili wa Masuala ya haki za Watoto, Gebra Kambole akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Wadau  wanaopinga ndoa za utotoni katika mkutano Maalum ulioandaliwa na Tasisi ya Msichana Initiative  Dar es Salaam, katika Mkutano huo wadau wameweza kujadili na kupitia Rufaa iliyowekwa na Mwanasheria Mkuu juu ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu kuwa Mtoto wa Miaka 15 awezi kuolewa.
 Afisa Mawasiliano wa , Eileen Mwalongo, akizungumza jambo kuhusiana kupinga ndoa za utotoni wakati wa kikao cha Wadau kujadili Rufaa ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya Hukumu ya kesi ya kupinga ndoa kuanzia miaka 15.
 Sehemu ya Wadau walioshiriki katika kikao cha Wadau kupinga Rufaa ya Mwanasheria Mkuu kupinga hukumu ya Mahakama kuu juu ya ndoa kuanzia miaka 15.
 Sehemu ya Wadau walioshiriki katika kikao cha Wadau kupinga Rufaa ya Mwanasheria Mkuu kupinga hukumu ya Mahakama kuu juu ya ndoa kuanzia miaka 15 wakimsikiliza Mwanasheria Gebra Kambole.