Friday, February 23, 2018

UKAGUZI WA MAGARI MADOGO KUANZA MACHI MOSI, WAENDESHA BODABODA KUFUNGIWA KAMERA

Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii.

BARAZA la Taifa la usalama barabarani  limetangaza kuanza kwa ukaguzi wa magari madogo ya binafsi nchini nzima kuanzia Machi moja mwaka huu, huku likieleza kuwa linatafuta mfadhili atakayesaidia kufunga kamera kwenye baadhi ya makutano ya barabara ili kuwakamata bodaboda watakaofanya makosa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es saalam na mwenyekiti wa baraza hilo Mhandisi Hamad Masauni ambaye pia ni Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi wakati akielezea tathimini ya utekelezaji wa  mpango mkakati wa kudhibiti ajali za barabarani ambapo inaonesha ajali zimepungua. Akizungumzia kuhusu waendesha bodaboda amesema, baadhi yao wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani kwa kufanya makosa mbalimbali na baadhi ya makosa hayo ni kupita katika taa nyekundu, kutovaa kofia ngumu na kubeba abiria zaidi ya mmoja.

Hivyo amesema baraza limepanga kutoa elimu maalumu itakayosaidia kupunguza ajali na kuhakikisha wanaovunja sheria wanachukuliwa hatua.“Hatua hizo zitasaidia kuwajengea uelewa wa usalama barabarani watumiaji wa barabara na madereva wataogopa kufanya makosa barabarani na hivyo na kuwa na utii wa sheria bila shuruti.”

Pia amesema wamebaini kuwa, pikipiki nyingi zimesajiliwa kwa majina ya kampuni zinazouza pikipiki badala ya majina ya wamiliki wa pikipiki hizo kitendo ambacho ni kinyume na sheria na kimekua kikisababisha usumbufu katika ukamataji wa bodaboda.Hivyo, Masauni amesema pikipiki ambazo zitakamatwa na kubainika zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya jina la mmiliki wenye kampuni hizo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu wa magari madogo, Masauni amesema awamu ya pili ya mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani wamefanikiwa kukagua magari makubwa, magari ya abiria, magari ya mizigo na magari yanayobeba wanafunzi ambapo wamefanikiwa kufanya ukaguzi huo kwa asilimia 79.

Amesema hivyo awamu ya tatu ni kwa magari madogo ambapo amehimiza wenye magari kufanya ukaguzi huo ambao utafanyika kwa kipindi cha miezi miwili na baada ya hapo ambao watakabainika kutokuwa na stika zinazoonesha kutokaguliwa kwa magari yao watachukuliwa hatua.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani , Fortunas Musilimu amesema kuwa watu wote wenye magari kuhakikisha magari yao yanakaguliwa katika maeneo maalumu na kueleza wamekuwa makini kwa kuhakikisha gari inayobandikwa stika ni ile ambayo itakuwa imekaguliwa na si vinginevyo.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari(hawapo pichani), ambapo alitangaza kuanza rasmi kwa zoezi la ukaguzi wa magari binafsi mwanzoni mwa mwezi ujao.Wengine ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Fortunatus Musilimu na Mjumbe wa baraza hilo,Henry Bantu(kushoto).Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambapo ilitangazwa operesheni ya ukaguzi wa magari binafsi unaotarajiwa kuanza mwezi machi mwanzoni.Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Henry Bantu, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambapo ilitangazwa operesheni ya ukaguzi wa magari binafsi unaotarajiwa kuanza mwezi machi mwanzoni.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu(kulia). Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),Geoffrey Silanda, akijibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwake wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari(hawapo pichani).Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MANYANYA ASEMA VIWANDA UTASAIDIA KUKUA KWA KILIMO NCHINI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema uwepo wa viwanda nchini utachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa kuwahakikishia wakulima wanakuwa na soko la uhakika.
Mhandisi Manyanya ameyasema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza viwanda nchini lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA).

Amesema ili kufikia malengo hayo kunahitajika ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na Serikali  kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara.
"Tasisi za fedha mnatakiwa kuhakikisha mnatatua changamoto za wajasiriamali za ukosaji wa mitaji jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wengi wao, ili kuhakikisha tunafikia Tanzania ya viwanda" amesema.

Mhandisi Manyama, amesisitiza ikiwa taasisi za fedha zitasaidia kukuza uchumi kupitia viwanda maana yake itakuwa chachu ya kukuza kipato cha wawekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani.

“Kuna changamoto kadhaa katika taasisi za fedha ambazo ni lazima zifanyiwe kazi kwa sababu wafanyabiashara wengi wanapokopa fedha kwa mfano kununua mashine wanatumia muda mrefu kutafuta ushauri. Niwaombe kuwasaidia kuwapa ushauri pale mnapowakopesha,"amesema Mhandisi Manyanya
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Geofrey Simbeye, ameishauri Serikali  kuanzisha benki maalumu zitakazosadia kutoa mikopo ya kuanzisha na kuendeleza viwanda kama imekusudia kufikia uchumi wa kati unaotegemea sekta hiyo.
Pia Simbeye amesema licha ya ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kuonesha Sh. trilioni 16.3 zilitolewa kwa sekta binafsi ni alisimia 9.8 tu ya fedha hizo iliyoelekezwa sekta ya uzalishaji huku kiasi kikubwa kikielekezwa kwenye biashara.
“Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Charles Kimei, amezungumza mambo mengi, lakini ninachosisitiza ni lazima tuwe na mfumo mpya, kwa sababu kama fedha zilizokopeshwa kwa private sekta ni Sh.trilioni 16.3, kwa mujubu wa taarifa ya BoT.

“Na ripoti ya Benki Kuu hiyo hiyo, inaonesha katika hizo ni asilimia 9.8 tu ndizo zimekwenda kwenye viwanda. Sasa tunajiuliza kwa ‘rate’ hiyo tutafika kwenye viwanda? Amehojia Simbeye.
Amesema benki za kibiashara zimekuwa zikiangalia zaidi wapi zinapata faida ambapo mikopo inaweza kurudi haraka, ambapo mikopo mingi imekuwa ikielekezwa kwenye biashara ambako watu wengi hukopa ili kuagiza bidhaa za biashara na kujenga nyumba tofauti na uwekezaji wa viwanda ambao ni wa muda mrefu.
“Sasa tunajiuliza swali je, tutaendelea kutegemea benki hizi za kibiashara katika kuendeleza viwanda hapa Tanzania? Tunatakiwa kufikiria nje ya boksi nini tufanye.
“Kujenga uchumi wa viwanda nchini Tanzania ni sawa sawa na projecti ya kitaifa yaani ni project ya kujenga Taifa ndiyo itakayotulepeka kwenye uchumi wa viwanda na kama tunaichukua kama project ya kitaifa lazima tuje na mfumo tofauti wa kuiwezesha,” amesema Simbeye.
Amesema mchakato wa ujenzi wa viwanda unapaswa kuchukuliwa kama unavyochukuliwa mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (standard gauge) ambapo Rais amesema anazo zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3.5 za kujenga mradi huo kuanzia Dar es Salaam hadi makao makuu ya nchi Dodoma.
Amesema hivyo ni vema kuwa na chombo maalumu kitakachokuwa kikitoa mikopo ya maendeleo hasa sekta ya viwanda ili kuwezesha kufikia lengo la uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
“Hakuna kiwanda kinaanzishwa kikae miaka mitano, kiwanda ni project za milele na milele, wewe mwanzishaji utakufa lakini kile kiwanda kipo, kwa hivyo vinahitaji uwekezaji wa muda mrefu.
“Tatizo hapa wanaangalia faida zaidi lakini tukiwa na ‘industrial development bank’ kama TIB ni kama una-empower watu kuanzisha viwanda,” amefafanua Simbeye.
Ameongeza sensa ya maendeleo ya viwanda ya mwaka 2013 iliyozinduliwa mwaka 2016 inaonesha Tanzania ina jumla ya viwanda 49,242 lakini viwanda vikubwa ni 1,322 tu. "Hivyo ni vema kujiuliza kwanini viwanda vidogo ndiyo vingi na kwanini visianzishwe viwanda vikubwa".
Amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa mitaji, hivyo ni vema kusaidia kuanzishwa viwanda vingi vikubwa vitakavyosaidia pia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vitakavyokuwa vinazalisha malighafi kwa za viwanda vikubwa na kutoa ajira nyingi kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki ya Tanzania, Dk. Charles Kimei, amesema licha ya taasisi za fedha kuwa na jukumu la kusaidia upatikanaji wa fedha kwa watu bado kuna changamoto nyingi nchini ikiwamo wafanyabiashara wengi wazawa kutoaminika katika taasisi za fedha hususani za kigeni.
Dk. kimei amesema kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wajasiriamali wadogo na wa kati taasisi za fedha nchini zinapaswa kuongeza ushirikiano na wajasiriamali hao badala ya kufikiria viwanda vikubwa tu.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi  Stela Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA)  kuhusu wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Nchini na Mwenyekiti wa  jumuiya ya Mabenki , Charles Kimei  akichokoza mada  wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  Tasisi ya Sekta Binafsi Nchini(TPSF),Geoffrey Simbeye, akichokoza mada wakati wa kongamano la kujadili umuhimu wa mabenki na sekta binafsi katika maenedeleo ya Viwanda.
Naibu Mkuu wa Chuo  Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dr.Thomas Ndaluka  akitoa neno kwenye Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania. 
 Mhadhiri wa Chuo Cha MNMA, Binto  akitoa mada ya Ujasiliamali ktika Uwekezaji wa Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Mkurugenzi wa Uchumi ,Utafiti na Sera , Benki kuu ya Tanzania Johson Nyela  akichangia jambo wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori akiwa ameketi pamoja na Washiriki wengine wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.


Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof Shadrack Mwakalila wa kwanza kulia akiwa ameongozana na  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi  Stela Manyanya (Katikati) pamoja na  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Nchini na Mwenyekiti wa  jumuiya ya Mabenki , Charles Kimei 
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi  Stela Manyanya  wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Thursday, February 22, 2018

MWIJAGE MGENI RASMI KONGAMANO LA VIWANDA MNMA


Na Humphrey Shao, Globu Ya jamii
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano kuhusu Maendeleo ya Viwanda Tanzania   litakalo fanyika katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  February 23 Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo  Afisa Habari wa chuo Hicho 

Evelyn Mpasha amesema kuwa Kongamano hilo kubwa litawaleta karibu wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo ya Viwanda nchini.

“Kongamano hili litaangazia Masuala ya Maendeleo ya Uchumi , Uwekezaji Endelevu  katika Viwanda, Ujasiliamali katika Uwekezaji katika Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi” amesema Mpasha.

 Kwa upoande mmoja wa watoa mada katika kongamano hilo Binto Mawazo amesema kongamano hili ni sehemu ya juhudi za chuo kushiriki katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuipeleka Tanzania katika uchumi wa Viwanda .


Binto amesema kuwa MNMA kama chuo ni wadau Muhimu sana katika kukiwezesha wananchi kufika malengo ya Rais kuipeleka nchi katika  uchumi wa kati. 

WATAALAMU WA ICT WAKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI ULINZI WA SHERIA YA MITANDAO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Cyber Tanzania, Samson Mwele akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwa ahilo kwa wataalamu wa Masuala ya ICT Tanzania juu ya kupambana na uhalifu wa mitandaoni.
 Mratibu wa Kongamano la Ulinzi wa Mtandaoni,Inocent Mungy, akizungumza wakati wa kongamano hilo lilipokuwa lianaendelea.
 Sehemu ya wataalamu wa Masuala ya ICT nchini wakifatilia kwa Makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wadau wengine.
Sehemu ya Wadau wakiwa katika Mkutano ulinzi wa Sheria ya Mtandao nchini

Tuesday, February 20, 2018

THE LAUNCH PAD YATUMIA TASISI TATU KUWAELEZA VIJANA UMUHIMU WA NIDHAMU MAHAA PA KAZI

 Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa Tasisi ya Launch Pad Tanzania, Henry Kulaya, akizungumza na Vijana waliofika katika mafunzo ya siku mbili ya Ujasiliamali na Kuongeza Maharifa ya kuweza kuajirika katika tasisi mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Niajiri Platform, Lillian Madeje akizungumza na Vijana namna ya kuweza kuandaa Cv zao hili ziweze kuwasaidia kupata ajira kw aurais kupitia Mtnadao wake wa Niajiri Tanzania.
 Mkurugenzi ya Tasisi ya kuwezesha Vijana ya Empower Limited, Miranda Naiman akieleza namna tasisi yake ilivyojikita katika kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi katika kipindi hiki ambacho Dunia inapitia changamoto ya uhaba wa ajira.
  Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa Tasisi ya Launch Pad Tanzania,Carol Ndosi akichangia jambo katika mjadala wa kuongeza maharifa kwa vijana hili waweze kupata ajira kwa uraisi hili waweze kujikwamua kiuchumi
 Mmoja wa Vijana walioshiriki katika Kongamano hilo akieleza jambo juu ya umuhimu wa Vijana kuwa na Maadili kazini
 Sehemu ya Vijana waliokuwa katika makundi wakifanya kazi ya kujadili namna ya kuwa na maadili mahala pa kazi kunavyoweza kusaidia kukua kiuchumi na kupandishwa cheo.
Vijana walioshiriki kongamnao la Vijana Ujasiliamali na kuongeza maharifa hili waweze kuajirika katika mashirika mbalimbali lililoandaliwa na Tasisi ya The Launch Pad

Monday, February 19, 2018

Dk 30 ZA ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE


Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Ilikuwa siku ya feb 17 ambapo Msanii wa Muziki wa BONGO Fleva Aslay Isihaka alivyoweza kubadilisha Histori aya kimziki katika Maisha yake kwa kuweza kufanya shoo kubwa ya Mapenzi na Muimbaji Mwenzie Nandy ambae ameshirikiana katika nyimbo nyingi.

Licha ya usiku huo kufikiriwa kuwa wa nyimbo za Mahaba mambo yalikwenda tofauti kwa nusu saa nzima pale Aslaya alipopanda jukwaani na kibao cha “Angekuwepo” wimbo ambao aliumba kwa ajili ya kumkumbuka Mama yake Mzazi.

Aslay ambaye aliimba kisha kuishia kati na kwenda kumsogelea Mama Mzazi wa Nandy na kusema kuwa “natamani muda huu Mama yangu muda huu angekuwa hapa lakini sio mapenzi yangu natamani namimi ningekuwa kama Nandy naimba Mama yangu anaona hivyo nikuombe Mama Nandy kuanzia leo uwe mama hili niweze kupata faraja kama anayopata mwanao” alisema Aslay .

Maneno hayo ambayo yaliteka hisia za watu wengi na kumfanya Mama yake Nandy kuamka na kwenda Mbela kucheza na Aslay kisha watu wengi kuinuka kwenda kumwambia mwanamuziki huyo aendelee kuimba na kuacha kulia.

Aslay ambaye aliendelea kuimba wimbo huo huku akiwa amekaa chini na uzuni mkubwa na kutengeneza Simanzi kubwa ndani ya ukumbi wa Escape One kwa zaidi ya Dk 30 Jambo ambalo liliwafikirisha watu na kusema kuwa Mama ni wa muhimu kuliko kitu chochote
 Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi Kipya Aslay Isihaka akionyesha kidole juu kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotekea katika maisha yake.
 Aslay akimuomba   Mama yake Nandy  kuwa Mama yake wa kumlea wakati anaimba wimbo wake angekuwepo
 Aslay akicheza na Mama yake Nandy  mara baada ya kukubali kuwa Mama Mlezi
 Mmoja wa Mashabiki wakinyamazisha Aslay asilie wakati anaimba wimbo angekuwepo
Mashabiki wa muziki wakiwa wamesimama kwa Huzuni mara baada ya Aslay kuimba wimbo huo

CHEMBA WAKOSA HUDUMA ZA AFYA KWA MIAKA MINNE


WANANCHI wa Kijiji cha Magasa, Kata ya Mrijo wilayani Chemba, wamekosa huduma za afya kwa muda mrefu, licha ya jengo la zahanati yao kukamilika kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Wakizungumza na Ripota wa Jijiletu  mwishoni mwa wiki, wananchi hao walisema wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita saba hadi vijiji vya Soya na Mrijo kufuata huduma za afya, jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwao.
Jengo hilo ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi na baadae Serikali kumalizia, linadaiwa kukaa kama pambo kijijini hapo bila huduma zozote, licha ya ujenzi wake kukamilika tangu 2014.
“Jengo letu tangu limekamilika linazaidi ya miaka minne, pia tumeletewa daktari hapa alikuja kuripoti, tuliambiwa baada ya mwezi mmoja atakuja kuanza kazi, tumesubiria hadi leo hatujamwona,” alisema Ramadhan Rajabu.
Mwananchi mwingine Hamisi Kijaji alisema kinachowaumiza zaidi ni pale wajawazito wanavyopata shida, kwani wanatumia usafiri wa baiskeli na mikokoteni na wakati mwingine wanapoteza maisha njiani kutokana na ubovu wa barabara.
Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Mussa Ninga, alikiri kukosekana kwa huduma hiyo na kueleza watumishi wawili wameripoti kijijini hapo, lakini waliondoka katika mazingira ya kutatanisha.
Ninga alimtaja daktari mmoja kwamba aliripoti kijijini hapo Novemba 28, mwaka jana akitokea Kituo cha Afya Makorongo, lakini aliondoka bila taarifa ambapo hadi sasa haijulikani alipo.
“Awali tuliletewa mtumishi anaitwa Prisca alikuja 28/10/2016 na saini yake ipo ofisini kwenye kitabu alipokuja kuripoti, baadae tuliambiwa ameondolewa kwa sababu ya vyeti feki,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Idd Baba, alisema zahanati hiyo imegeuka mzigo kwake, kwani amefanya jitihada kufuatilia ngazi za juu lakini hajapata majibu ya kuridhisha.
“Kila siku mara leo mara kesho, naletewa daktari mara tunaambiwa ni feki, naanza tena kufuatilia nikaletewa mwingine mara nikasikia naye amehamishwa,” alisema.
Diwani wa Kata ya Mrijo, Hamisi Msakati (CCM), alikiri wananchi hao kupata shida licha ya jengo kukamilika muda mrefu na kueleza kuwa alipofuatilia wilayani kuhusu watumishi aliambiwa zahanati hiyo haijasajiliwa.
“Mwaka jana walileta doctor mwingine alikuja akaripoti nikapata na barua, lakini mazingira aliyoondokea ni ya kutatanisha. Nilipofuatilia wilayani Mganga Mkuu wa Wilaya akaniambia hii zahanati haijasajiliwa.
“Nilimwambia kuna watumishi wawili mmewaleta kule, wakati mnafanya hayo hili la usajili mlikuwa hamlijui? Kwa kweli sikupata majibu ya kuridhisha, hayatoshelezi hata kwa akili za kawaida,” alisema.
Mwandishi alilazimika kumtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Dk. Semistatus Mashimba,  ambaye alishangazwa na taarifa hizo na kuahidi kuchukua hatua mara moja ili wananchi hao wapate huduma.
“Hili ndiyo nalisikia kutoka kwako, kwanza nikushukuru kwa kunipa taarifa hili nalifuatilia kuanzia sasa, yaani hata diwani ameshindwa kufika ofisini kwangu hata simu ameshindwa kunipigia tukalimaliza?
“Miaka minne watu hawapati huduma na jengo limekamilika kama ni usajili taratibu zake zipo wazi kinachokwamisha ni nini? Uzembe huu hauwezi kuvumiliwa,” alisema Dk. Mashimba.

THE LAUNCH PAD YAWANOA VIJANA MABALIMBALI JUU YA MAHARIFA YA KAZI NA UJASILIAMALI

 Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw Makbel akizungumza juu ya mpango wa uanagenzi ulivyoweza kuwasaidia Vijana wengi kuingia katika sekta rasmi na kuweza kushindana na wasomi wengine ambao walipata ujuzi katika mfumo wa kawaida.
 Mwakilishi wa Tasisi ya Vijana Think Tank akizungumza namna Vijana wanavyotakiwa kufikiri zaidi hili waweze kujikwamua katika wimbi la kukosa ajira kwa kusema kuwa kila mwaka kundi la Vijana wasiokuwa na ajira wanavyoongezeka
 Mtaalamu wa Masula ya ushauri wa kujikwamua na ajira kutoka Shirika la kazi Duniani ILO, Comoro Mwenda akitoa somo ya namna vijana nini waweze kufanya hili kufikia malengo yao ya kuajiriwa au kujiajiri popote pale duniani
 Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Launch Pad Tanzania, Caroline Ndosi akizungumza wakati wa akiongoza Meza ya mjadal awakati wa kongamano la kuwajengea Vijana uwezo wa ujasiliamali na kuweza kuajirika katika Tasisi mbalimbali.
Sehemu ya Vijana kutoka sehemu mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Kongamano la Kuongeza Maharifa ya ujasiliamali na kuajirika lililoandaliwa na Tasisi isiyo ya Kiserikali ya The Launch Pad

MAMA SALMA KIKWETE MAMLAKA KUTOA HAKI KWA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete amezitaka mamlaka zinazojihusisha na utoaji haki, kuwasaidia wanawake kupata haki zao pindi wanapofungua mashauri ya kudai matunzo ya watoto.
Mama Salama amesema ahayo juzi Jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wanawake wanaolea watoto peke yao Single Mothers lililoandaliwa na kituo cha Radio cha Efm na Tv E.

amesema kuwea ni vyema wanaume kutambua majukumu yao ya kulea watoto kwani ni matakwa ya sheria watoto kulelewa na wazazi wote na sio kuwatelekeza  na kusema  watoto wanatakiwa kupata malezi mema  na ya upendo.

"Wanawake wanatekesa wanapotafuta haki zao  kutokana na unyonge na umasikini waliokuwa nao hivyo haki itendeke ili wanawake watembee kwa kujiamini katika nchi yao," amesema Mama Salma.
Aliongeza kuwa watoto wana haki ya kupata malezi mema kutoka kwa wazazi wote, elimu na afya ili kukua vizuri kiakili na kijamii.

"Ukiona wanawake wanatupa watoto jiulize kuna nini, bila tatizo hawawezi kutupa mtoto kwani anauma sana na ndio maana wengine wanapojifungua wanawaviringisha na kuwaweka mahali pazuri  akijua kwamba lazima watu watapita na kumuokota na kwamba atalelewa vizuri," alieleza.
Alisisitiza kuwa wanaume wanapaswa kutambua mazingira ya wake zao pindi wanapokuwa wajawazito na wawatunze, kuwathamini na kuwajali watoto.

Mama Salma alisema wasiwaachie malezi wanawake pekee kwani hakuna mtoto asiye na baba.
Pia alisema kuwa kampeni hiyo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi inayofanywa na Kituo cha Redio Efm na TV E inapaswa kuungwa mkono kwani ndio muelekeo wa Siku ya Wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8.

Naye, Mhariri wa kituo hicho cha redio, Scholastica Mazura alisema ni wakati wa kutoa elimu kwa vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
Alisema wanawake wengi wanaishi nje ya ndoa zao  kwa sababu mbalimbali na hivyo tatizo la malezi ya upande mmoja kuwa kubwa nchini.

Alieleza kuwa wanawake wamekata tamaa kwani wapo ambao wametelekezwa nao wanatelekeza watoto lakini wengine wanawalea kwa shida ili wapate malezi bora.
"Tuwacheke wanaume wanaokimbia majukumu yao na kuwaachia wanawake pekee kwa kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa kwani mnauwezo mkubwa wa kulea nasi tutawasaidia ili mjikwamue kiuchumi," alisema Mazura.

 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa Kongamano la Single Mothers lililoandaliwa na Efm na Tv E 
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete Akicheza na Wanawake waliojumuika katika Tamasha la Sinle Mothers lililoandaliwa na Efm Radio kwa kushirikia na Tv E
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wanawake walioshiriki Tamasha la Sinle mothers wakati anaingia ukumbini
 Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige akizungumza na kuwatia moyo wanawake hao na kusema pia hata yeye ni Single Mothers na bado maisha yanenda
 Mhariri wa kituo hicho cha redio Efm na Tv E, Scholastica Mazura akizungumza  na vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akipoke Zawadi kutoka kwa Meneja Tukio wa Efm na Tv E , Jesca Mwanyika.
 Mbunge wa Viti Maalum Rita Kabati akizungumza na wnawake wanaolea Watoto peke yao juu ya umuhimu wa kumtegeea Mungu hili kufanikiwa
 Waziri Mstaafu na Mbunge , Hawa Ghasia akieleza ugumu wa kulea mtoto peke yako na kuwatia moyo wanawake wote waliotelekezwa
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Efm Radio na Tv E ambao ni Single Mothers 

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...