Saturday, March 3, 2018

JUKWAA LA WANAWAKE TANESCO LACHANGIA DAMU HOSPITALI YA TUMBI KIBAHA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kupitia jukwaa la wanawake wa shirika hilo leo kwa umoja wao wamekusanyika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani , Tumbi Kibaha na kujitolea Damu kwa ajili ya Wanawake wanaojifungua na majeruhi kadhaa wanaotibiwa katika Hospitali hiyo.

akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja wa Tanesco Kanda ya Pwani, Martin Maduhu amesema wafanyakazi wa shirika hilo wameamua kujitolea kwa moyo wao mara baada ya kundi la umoja wa Wanawake kufikiria kutoa mchango huo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

"Sisi tumekuwa tukiwaangazia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kuakikisha kuwa wanapata umeme wa uhakika lakini tumegundua umeme bila afya auna faida hivyo kupitia jukwaa hili tumeweza kuja kujitolea damua hili iweze kuwasaidia Mama zetua mabo ujifungua hapa na kumaliza damu nyingi pamoja na majeruhi."amesema Maduhu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi amesema wazo hilo limekuja mara baada ya kushauriana na wenzao wa pwani na kuona umuhimu wa damu katika Hospitali iyo ambayo upokea watu wengi kuliko kawaida kutokana na barabara ya Morogoro kuwa na mikasa mingi ya ajali.

amesema kuw ahuo ni mwanzo tu kwa jukwaa hilo lakini wamejipanga kutoa msaada zaidi katika jamii hili kuaakikisha kuwa wao kama watanzania wanaona kila mmoja anakua kiuchumi na afya.

Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha,Dkt Briceson Kiwelu, aliwashukuru wafanyakazi hao wa Tanesco na kusema kuwa ni mara chache sana kuona kundi kubwa kama hilo linakuja kujitolea damu katika hospitali hiyo hivyo uwe uwe mwanzo na isiwe mwisho.

amesema kuwa uzuri wa damu inayotolewa na kundi kubwa la watu kutoka katika shirika hilo asilimia 70 huwa ni nzima kutokana na watu wake wengii huwa wanafika wakiwa tayari wamejitathmini na kuchangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa damu safi kwa muda mfupi.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchangiaji Damu kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco lilipoamua kujitolea kutoa Damu kwa jili ya Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoa wa pwani kama Sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
 Meneja wa Tanesco Kanda ya Pwani, Martin Maduhu akizungumza jinsi gani Tanesco inavyoweza kuwaangazia wananchi maisha yao kwa kushiriki katika utoaji damu kwa ajili ya kuwezesha wajawazito na watu wanaopata ajali waweze kupata matibabu haraka katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha,Dkt Briceson Kiwelu akitoa neno la ukaribisho kwa wafanyakazi wa Tanesco wa Dar es Salaam na Pwani waliojitokeza kwa wingi kujitolea Damu kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayo adhimishwa Marchi  8  mwaka huu
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi akiwa katika Maandalizi ya utoaji wa Damu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha.
Mmoja ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco ambaye ni Mwanachama wa Jukwaa la Wanawake wa Shirika hilo akiwa katika vipimo vya awali kwa ajili ya uchangiaji damu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani tumbi Kibaha.
 Mmoja ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco akiendelea na zoezi la utojai Damu kwa ajili ya Wagonjwa watakaofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ,Tumbi Kibaha
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi, akichukuliwa vipimo vya mapigo ya moyo kabla ajaingia katika zoezi la utoaji damu
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Tanesco na wanachma wa jukwaa la Wanawake wa Shirika hilo wakiwa katika foleni ya kusubiri kuingia kwenda kuchangia Damu katika Hospitali ya Tumbi Kibaha
  Sehemu ya Wafanyakazi wa Tanesco na wanachma wa jukwaa la Wanawake wa Shirika hilo wakiwa katika foleni ya kusubiri kuingia kwenda kuchangia Damu katika Hospitali ya Tumbi Kibaha

Friday, March 2, 2018

VIONGOZI WANDAMIZI WA ACT WAZALENDO MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA CCM


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Uongozi wa wa Chama Cha Act Wazalendo wa mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na katibu wao Ernest Kalumuna leo wameamua kujitoa katika chama hicho na kujiunga na Chama cha mapinduzi kufuata uzalendo unaonyeshwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli.

akizungumza na Waandishi wa habari leo aliyekuwa katibu wa Chama hicho mkoa wa Dar es Salaam ,Ernest Kalumuna amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya Chama chao kilichokuwa kinajisibu kwa misingi ya uzalendo na kushindw akufuata misingi hiyo hasa kwa kiongozi mku wa Chama.

"tumeshutushwa zaidi na kauli za karibu za kiongozi wa chama chetu ndugu Zitto Kabwe kuhamasisha Viongozi wa Chadema wakae na kufanya maamuzi ambayo anadai sisi tutawaunga mkono huku akimalizia kusema kuwa serikali hii ni rahisi sana kuiangusha  kwa hiyo ni ishara ya juu sana kwa kuona kiongozi wenu wa kisiasa kufirisika"amesema.

amesema wajumbe wa kamati kuu wakilalamika na wengine wakihama chama kwa sababu hakuna tena kamati  kuu siku hizi lakini kuna kakikundi cha wapambe wake ambao badala ya kujenga wanabomoa.

alimaliza kwa kusema kuwa wao kama wanasiasa mahiri hawezi kuendelea kuwa kwenye kikundi cha namna hii kwa pamoja tunatangaza  kujivua  uanachama wa ACT Wazalendo  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ili tufanye Siasa za kweli  za kurudisha nch yetu kwenye misingi ya kuasisiwa kwake.

Thursday, March 1, 2018

KARIA ASEMA SUALA LA BIMA ALIKWEPEKI KWA WACHEZAJI WA TANZANIA


Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Warace Karia amesema atasimamia suala la bima kwa wachezaji wanaoshhiriki katika ligi mbalimbali zinazo simamiwa na shiriki hilo hili kuweza kuwawezesha wachezaji kupata haki zao kwa haraka pindi wanapopata matatizo wakiwa michezo katika maisha yao ya Soka.

Karia amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mafunzo kwa viongozi wa vilabu mbalimbali nchini juu ya umuhimu wa bima yaliyoratibiwa na Tasisi ya ISDL kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Aliance life Insurance ya hapa nchini Tanzania.

"lazima niwaambie ukweli hili suala la Bima mimi kwa sasa nitalifatilia kw aukaribu sana kwa kuhakikisha kuwa kila mchezaji aliyesajiliwa katika kalbu ya ligi kuu na shirikisho anapatiwa Bima ya maisha hili kuweza kupunguza matatizo yanayoweza kujitokeza pindi mchezaji wanapopata matatizo wakiwa uwanjani aua mara baada ya kumaliza mpira wake"amesema Karia.

amesema kuwa kwa sasa lawama nyingi zinatumwa kwa shirikisho la sokoa kuwa aliwahudumii wachezaji wa zamani lakini msingi wa jambo lenyewe kuondokana na lawama hizo ni kuhakikisha kuwa wachezaji hawa kila mmoja anapata Bima ya Maisha yake hili aweze kijikwamua pindi anapopata matatizo.

Karia pia alitumia fursa hiyo kutoa Salamu za rambirambi kwa msiba wa mwanamichezo mkongwe aliyekuwa anakipiga na klabu ya Simba Arthur Mambeta amefariki dunia siku ya jana Jumatano baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.
 Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Semina kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Michuano ya Shirikisho nchini.
 Mwenyekiti wa ISDL , Dr T.M Katunzi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia  kuzindua Semina kwa ajili ya Vilabu mbalimbali hapa nchini.

Viongozi wa klabu mbalimbali nchini wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa TFF katika Semina Maalum iliyoandaliwa na ISDL kwa kushirikiana na Aliance Life Insuarance.

DR KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Ashanti Kijaji amesema kuwa mamlaka ya Masoko na Mitaji ni injini katika maendeleo ya uchumi hivyo ni lazima mamlaka hiyo iwafikie wateja.

Kijaji aliyasema hayo wakati akitunuku vyeti kwa wahitimu wa mamlaka hiyo waliopata kwa kushirikiana na chuo cha Uingereza CISI katika fani ya masoko na mitaji, amesema kuwa watu hawana uelewa juu ya masoko na mitaji hivyo wanatakiwa kufikia wateja katika kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano yenye Kauli mbiu ya nchi ya viwanda.
Amesema Mamlaka kwa kutumia watalaam hao lazima wafanye kazi katika kujenga nchi  na kutoa elimu  kuhusiana na masoko na mitaji.

Amesema kuwa kampuni zipo nyingi lakini hazijaweza kuingia katika soko la hisa ni kutokana na kampuni hizo kushindwa kufikiwa ikiwa ni pamoja na kupata elimu.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa katika kufanya kazi mamlaka hiyo lazima iweke mpango mkakati katika kuhamasisha kampuni ziingie katika soko la hisa.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Dk.John Mduma amesema kuwa wanaendelea katika kutoa huduma ikiwa ni pamoja kufanyia kazi maagizo ya Naibu Waziri katika kuwafikia wateja na kuleta matokeo chaya ya maendeleo ya uchumi.
Dk. Mduma amesema kuwa katika kuwa sasa watafungua dirisha la  uhamasishaji katika  kufikia kampuni ziweze kuingia katika soko la hisa.
Afisa Mtendaji Mkuu , Nicodemus Mkama amesema mkataba wa huduma kwa wateja waliouzindua watawafikia wateja wote kuingia dhamana ya masoko na mitaji katika kuendrleza miradi mbalimbali nchini.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizungumza mara baada ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko ya mitaji na uzinduzi wa Mkataba wa huduma kwa Wateja.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi w akitabu cha huduma kwa wateja.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizindua kitabu cha Msaada wa huduma kwa wateja
 Mwenyekiti wa TSEBA,George Fumbuka akitoa neno la Shukrani kwa waziri mara baada ya kumaliza kuzinduliwa kwa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa wateja.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko
 Baadhi ya Wadau walioshiriki katika uzinduzi wa kitabu cha huduma kwa wateja

Monday, February 26, 2018

MANISPAA YA ILALA YATUMIA BILIONI TANO KWA MIRADI YA MAENDELEO

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeweza kutumia jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 5,544,659.471 katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo  katika bajeti ya kuanzia julai 2017 hadi Desemba mwaka huo.

Akizungumza na waaandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu shaibu amesema kuwa fedha hizo zimetumika katika utekelezaji wa miradi inayohusisha  ujenzi wa vyumba  vya madarasa ,vyoo na hosteli.

"kwa upande ya elimu ya msingi  shule mpya  4 zimejengwa kutokana na ongezeko la wanafunzi na ongezeko la wanafunzi ambalo limetokana na mpango wa serikali wa elimu bila malipo pia ametaja kuwa katia mpango huo madarasa 28 yamejengwa katika shule za msingi Bonyokwa, Mongo la ndege, Mbondole, Mji Mpya, Kibaga, Bangulo na Misitu. Madarasa sita yamefanyiwa ukarabati darasa moja kinyerezi na Mchikichini vyumba vitano" amesema Tabu.

amesema kuwa katika fedha hizo jumla ya matundu ya vyoo 96 yamejengwa katika shule hizo huku matundu 40 yakiwa katika shule za zamani na yaliyobakia katika shule mpya.

ametaja kuwa pia fedha hizo zimetumika pia kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali hili kukabiliana na changamoto ya usafiri wa wanafunzi wanaokaa mbali na shule hiyo.

amesema kuwa Halmashauri imefanya ukarabati wa huduma za mama na mtoto katika Zahanati ya Msongola na Mvuti kwa kutumia mapato ya ndani ikiwa pamoja na ukamilishaji na ukarabati wa miradi ya maji katika kata ya Minazi, Tabata, Majohe, Vingunguti, sekondari Pugu, Mkera na Pugu station .

alimaliza kwa kusema katika kipindi hiki Halmashauri imeweza kupeleka kiasi cha Milioni 543,400,000/ kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na walemavu na kukarabati miundombinu ya jiji la Dar es Salaam kupitia mradi wa DMDP.
 Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, akizungumza juu ya taarifa ya utekelezwaji wa bajeti ya Halmashauri hiyo katika kipindi cha julai hadi Desemba 2017.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini Taarifa hiyo ambayo inatolewa na Tabu Shaibu.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...