Skip to main content

Posts

Showing posts from March 11, 2018

WANAWAKE WATAKIWA KUCHANGAMANA HILI WAWEZE KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tantrade Tanzania,Jacqueline Maleko akizungumza wakati wa usiku wa Wanawake na tunzo kwa Mwanamke aliyefanikiwa kwa mwaka 2018 iliyoandaliwa na Tasisi ya Shangwe ambapo wanawake kutoka sehemu mbalimbali walikutana na kuzungumza mambo ya ujasilimali na namna ya kuvuka kutoka hatua moja hadi nyingine.
 Mkurugenzi wa Tasisi ya I-learn East Afrika ,Noela Bomani(Kulia) Akikabidhi tunzo kwa Mwanamke aliyefanya vizuri na kuwa kivutio katika mafanikio yake katika kipindi cha mwaka 2017/2018 Joyce Ibengwe ambaye ni mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko  Kutoka kwa Tasisi ya waajiri nchini(ATE).
 Mshindi wa Tunzo ya Mwanamke aliyefanikiw akwa mwaka 2017/2018 Joyce Ibengwe ambaye ni mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko  Kutoka kwa Tasisi ya waajiri nchini(ATE).akizungumza namna alivyopitia mpaka kufikia hatua hiyo kutoka kuitwa mama na watu mpka mke wa mtu.
 Meneja Bima ya magari kutoka shirika la Bima ya Taifa (NIC) Emakulata Mwaitege, akizungumza umuhimu wa Wanawake kuji…

RC MAKONDA AZINDUA WIKI YA MAJI KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda , akizungumza na Wenyeviti wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani pamoja na Wafanyakazi wa Dawasa na Dawasco ambao wameudhuria uzinduzi wa wiki ya maji  kwa mkoa wa Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi , Mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji  kwa mkoa wa Dar es Salaam. ambapo alisema ni vyema Dawasco wakaongeza usambazaji wa maji katika mkoa huo hili kusaidia ukuaji wa maendeleo ya Viwanda .
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza wakati wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji  kwa mkoa wa Dar es Salaam.

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa maji waliofika katika wilaya hiyo ambapo  fursa hiyo kuwaeleza wakazi wa Dar es Salaam mafanikio ya Mkuu wa Mkoa kwa kipindi cha Miaka Miwili.
 Wafanyakazi wa Dawasa na DAWASCO Waliohudhuria kwenye  uzinduzi wa wiki ya maji  kwa mkoa wa Dar es Salaam.
 Wageni wa Waalikwa waliohudhulia …

REPOA YATOA MATOKEO YA UTAFITI WA AFRO BAROMETER YANAYOSEMA WATANZANIA WANARIDHISHWA NA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti ya REPOA, Dr. Donald Mmari akizungumza juu ya matokeo ya utafiti wa Afro Barometer juu ya hali ya uchumi nchini ambapo matokeo yake yameonyesha kuwa wananchi wengi wameridhishwa na hali ya kukua kwa uchumi nchini huku wakipongeza upatikanaji wa elimu bure.
 Mtafiti kutoka Repoa, Thadeus Mboghoma akieleza baadhi ya matokeo ya utafiti huo katika nyanja ya ukuaji wa uchumi na matarajio ya watanzania kwa serikali ya sasa.
 Dr Lucas Katera kutoka Repoa ambaye alikuwa akiongeza mjadala juu ya matokeo ya utafiti huo wa hali ya uchumi nchini akichangia jambo wakati wa mjadala .
 Mtafiti kutoka Repoa, Stephene Mombela akifanya mawasilisho ya Tafiti ya Afro Barometer juu ya hali ya Uchumi nchini ambayo imenesha kuwa Wananchi wamekiri kuwa Uchumi katika serikali hii unapanda
 Msomi na Mtafiti , Profesa Mwesigwa Baregu (Katikati) akichangia mada wakati w amjadala wa matokeo ya utafiti wa Afro Barometer.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti ya REPOA, Dr. Don…

RIDHIWANI KIKWETE AKERWA NA UKOSEFU WA MOCHWARI ZAHANATI CHALINZE

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,ameweka wazi kuwa vituo vya afya katika jimbo hilo vinakabiliwana na ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia maiti .

Amesema changamoto hiyo ni kubwa ambapo husababisha wananchi kupeleka maiti za ndugu zao kwenye Hospitali teule ya rufaa ya Tumbi na wilaya ya Bagamoyo ambako kuna mbali mrefu.

Aliyasema hayo mjini Chalinze,wakati akizungumza na baadhi ya wananchi,na kusema  shida kubwa inatokea hasa pale mgonjwa anapokuwa amefariki.

Ridhiwani alisema jimbo zima la Chalinze hakuna chumba cha kuhifadhia maiti kwenye vituo vyote vya afya hali ambayo imekuwa mtihani mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo .

"Hali ni mbaya kwa wenzetu wa kata ya Kibindu ambao wanapeleka maiti Hospitali ya Bwagala wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ,”

"Wananchi wanaingia gharama kwenda kuhifadhi maiti sehemu nyingine ambako ni mbali na maeneo yao"

“Tunaishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya afya pamoja na zahanati lakini changamoto …

RWANDAMINA ATAJA SABABU MUHIMU ZA USHINDI BOTSWANA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba vijana wake wamejipanga kuhakikisha wanashinda mechi ya marudiano na Township Rollers nchini Botswana na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya kufungwa mabao 2-1 wiki iliyopita katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga inatakiwa kushinda 2-0 mjini Gaborone Jumamosi ili kwenda hatua ya makundi.

Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 10, wakiwemo wanane wa benchi la Ufundi kimeondoka,
Alfajiri ya leo kwa ndege kwenda Gaborone, wachezaji wakiwa na ari kubwa baada ya ushindi wa 3-1 jana dhidi ya Stand United ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Taifa.

Na wakati wa safari Lwandamina amesema kwamba hajakata tamaa kwa matokeo ya kufungwa nyumbani, kwani anaamini hata vijana wake wanaweza kwenda kushinda ugenini pia.

“Kwenye mpira kila kitu kinawezekana, nina matumaini makubwa ya kufanya vizuri ugenini, kutokana na morali  ya vijana wangu ” alisema Lwand…

UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

Mwenyekiti  Umoja wa Vijana Wa CCM (UVCCM)  Mkoa wa Dar es salaam Bw. Mussa Kilakala watatu kutoka kulia, wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa uhamasishaji na chipukizi Wilaya ya Ilala Saady Khimji, na wakwanza upande wa kushoto ni Katibu wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, said Yassin said, wapili  kutoka kushoto ni Joan Kataraiya, wakiwa katika picha baada ya kuwasili ofisi ya CCM Wilaya ya Temeke, (Picha na John Luhende).  MWENYEKITI Umoja wa Vijana Wa CCM (UVCCM)  Mkoa wa Dar es salaam Bw. Mussa Kilakala ameanza ziara kutembelea Wilaya za  Mkoa wa Dar es salaam ambapo leo ameanzia Wilaya ya Temeke  na  amekutana na kuzungumza  na  vijana na watumishi wa Manispaa  hiyo.  Kilakala amesema kuwa  lengo la Ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi  na pia kuangalia Umoja wa Vijana unavyofanyika fanya kazi zake.  Akizungumzia upande wa ujasiriamali ameipongeza  Wilaya ya hiyo  kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi waiopungua Elfu Mo…

DC TEMEKE AELEZA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

DC TEMEKE AFUNGUKA UTEKELEZAJI ILANANI YA CCM 3/12/2018 10:41:00 pm
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva ameeleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama tawala CCM ambapo ametaja miradi inayojengwa kwenye sekta ya elimu, afya pamoja na ulinzi na usalama. Wakati akitoa ripoti ya utekelezaji wa Ilani hiyo kwa  kwa kamati ya utekelezaji  ikiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM- UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, Lyaniva amesema ofisi yake inahakikisha inaimarisha hali ya ulinzi na usalama, ambapo kwa sasa inajenga vituo vikubwa viwili vya Polisi maeneo ya Chamanzi na Toangoma, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Kwa upande wa sekta ya afya,  DC  Lyaniva amesema kuna vituo viwili vya afya vya kisasa vinajengwa katika Kata ya Yombo na Majimatitu ambapo vitakuwa na wodi ya kinamama na vyumba vya operesheni, ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali za Temeke na Zakhiem. Kuhusu sekta ya elimu, Lyaniva amesema wanaongeza madarasa kwenye baadhi ya shule z…

UPANGA EAST YAKABIDHI VITAMBULISHO VYA BIMA KWA WAZEE 48

Na Heri Shaaban
KATA ya Upanga Mashariki wametekeleza agizo la Rais kwa kuwapatia vitamburisho vya Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu wazee 48 .

Akizindua mpango endelevu wa Serikali Dar es Salaam (leo) Ofisa Mtendaji wa Upanga Mashariki  Nahshon Marwa  alisema awali zoezi hilo lilizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa ajili ya kuwapatia vitamburisho wazee wote wasiojiweza.

"Mpango  huu wa kutoa kadi ya Bima ya  matibabu tumetekeleza kwa ajili ya kuwapa wazee wetu ambao wamestafu kazi awali tulipita katika mitaa yao kuakiki  kwa ajili ya kuwafanyia usaili na kujua Idadi yao" alisema Marwa.


Alisema Upanga Mashariki kuna mitaa Miwili Mtaa wa Kibasila na Mtaa  Kitonga na ina jumla ya wakazi 1,1,167 kaya 2270
na wazee waliopo  250 .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Upanga Mashariki Rukiya Riyami, alipongeza mpango huo wa Serikali katika kuwathamini wazee nchi zima .

Rukiya alisema mpango huo mzuri kwa wazee waliostaafu waweze kupatiwa matibabu katika vituo vya afy…

MBUYU ULIOISHI KARNE MBILI WANGUKA DAR

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mbuyu unaodaiwa kuishi kwa zaidi ya karne 2  katika iliyokuwa ikulu ya Mjerumani na baadae kuwa Hospitali ya wagonjwa wa Saratani ya Ocean Road umeanguka  katika upande wa barabara na kusababisha kukatika  kwa Umeme na foleni katika barabara inayokwenda Sarenda.
Mbuyu  huo ambao  ambao umesababisha kuvunjika kwa ukuta na kukatika kwa nyaya za umeme katika eneo hilo na kupelekea eneo hilo lote kukosa umeme
 Askari wa Usalama Barabarani akiongoza magari wakati Mbuyu   huo ulipoanguka


HABARI PICHA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA WA MAPATO TANZANIA AKUTANA NA MAKAMU KAMISHNA WA IDARA YA FORODHA KOREA

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akisisitiza jambo wakati alipokutana na Makamu Kamishna wa Idara ya Huduma za Forodha Korea, Roh Suk-Hwan (kushoto) pamoja na ujumbe wake jijini Dar es Salaam ili kujadili maendeleo ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Idara hiyo, ikiwemo Mfumo wa Uondoshaji Mizigo Bandarini (TANCIS) na dirisha moja (Single Window System). 


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akisisitiza jambo wakati alipokutana na Makamu Kamishna wa Idara ya Huduma za Forodha Korea, Roh Suk-Hwan (kushoto) pamoja na ujumbe wake jijini Dar es Salaam ili kujadili maendeleo ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Idara hiyo, ikiwemo Mfumo wa Uondoshaji Mizigo Bandarini (TANCIS) na dirisha moja (Single Window System).

TSHISHIMBI MCHEZAJI BORA VPL MWEZI FEBRUARY

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kiungo wa timu ya Yanga, Papy Tshishimbi Kabamba amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa mwezi Februari 2018. Tshishimbi ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili alioingia nao katika kinyang’anyiro kwa mwezi Februari, katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo iliyokutana Dar es Salaam wiki hii.
Kiungo huyo alitoa mchango mkubwa ulioiwezesha Yanga kupata pointi 12 katika michezo minne iliyocheza, ikiwa ndiyo timu pekee kwa mwezi huo kushinda michezo yote.
Katika michezo hiyo, Tshishimbi aliibuka mchezaji bora katika michezo mitatu, ambapo pia kwa mwezi huo alifunga mabao matatu na kutoa pasi ya mwisho moja iliyozaa bao.
Walioshindana na Tshishimbi ni Pius Buswita wa Yanga, ambaye pia alichangia mafanikio hayo ya Yanga kwa mwezi huo, huku pia akifunga mabao mawili.
Mwingine aliyeingia hatua ya fainali ni Emmanuel Okwi wa Simba aliyeisaidia timu yake kupata pointi 10 kwa michezo minne, ikishinda mitatu na kutoka sare m…

DC SINYAMULE AAGIZA MTENDAJI KATA YA BOMBO AWEKWE NDANI SAA NANE

Na Mwandishiwetu, Same
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule  ameagiza wa Kata ya Bombo awekwe ndani  chini ya ulinzi mkali kwa   saa 8 kutokana  na kushindwa kusimamia ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari Bombo na kumtaka apewa siku 2 kuleta maelezo kwa nini asichukuliwe hatua.
Dc Sinyamule, amefikia uamuzi huo mara baada ya wataalamu wa kutaka hela za kujenga bweni la Shule ya sekondari ya Bombo zihamishiwe shule nyingine kutokana na wananachi wa kata ya Bombo kutotoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha ujenzi wa bweni hilo unakamilka.
"Fedha za serikali ( P4R) zilipelekwa tangu mapema 2017 na mradi ulitakiwa kuisha Nov. 2017 na  Ikitegemewa kuwa kuanzia hapo ujenzi wa bweni uanze na mpaka leo nimefika hapa March  2018 bado hata msingi haujakamilika kujengwa na kutoa sababu zisizo na tija.
Mtendaji huyu ameshindw akusimamia Vizuri  majukumu yake ya kuhamasisha watu kushiriki katika miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa bweni la shule hii ambayo serikali ilishatoa fedha kilich…

DC SINYAMULE ATAKA WANAWAKE SAME WAANDALIWE KUSHIKA NAFASI ZA JUU ZA UONGOZI

Na Mwandishi wetu ,Same
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule amesema Makundi ya wanaweke kuanzia shule ya msingi, sekondari, vyuo, wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wanasiasa, viongozi katika nyanja zote wanatakiwa kukabiliana kuhakikisha Wilaya ya Same inawaandaa wanawake kushika  nafasi nyingi zaidi za juu katika uongozi na kuwa kati ya wanawake wanaomiliki biashara kubwa nchini.  Sinyamule amewataka Wanawake hao kuwa na kauli moja tu ya kuwa kumiliki viwanda ni haki yao. na kuwataka kuanza kutafuta maeneo ya uwekezaji na kufikiria kukua zaidi, kuchukua hatua bila kusubiri, kushikana mkono.
"Serikali ya Wilaya imejipanga kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali kuu yaanza kuanza kuunda mabaraza ya kata, hili yaweze kutenga maeneo ya uwekezaji vijijini na kuainisha maeneo ya wanawake, yaahidi kutoa % ya wanawake,  vijana na walemavu kwa ukamilifu. pamoja na kuanzisha soko la barabarani kukuza bidhaa za wanawake" Amesema 
Amesema wilaya  yake kwa kushirikisha…

KUMBILAMOTO AFUNGA MASHINDANO YA MPIRA WA PETE YA MKOA WA DAR ES SALAAM

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Vingunguti ambayo imeingia fainali katika michezo ya mpira wa pete ya mkoa wa Dar es Salaam iliyoratibiwa na (CHANEDA) kwa ajili ya kupata timu wawakilishi wa mkoa huu.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Mbagala ambapo timu hiyo nayo ilifika hatua ya fainali kwa ajili ya kupata mshinddi atakaye wakilisha Mkoa wa Dar es Salaam katika Mashindano ya Afrika Mashariki.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na Timu zote mbili kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kw atimu zilizoshiriki ligi ya mkoa wa Dar es Salaam
 Timu za Mchezo wa mpira wa Pete kwa wanaume zikimenyana wakati wa mchezo wa fainali ya mkoa wa Dar es Salaam
Mashabiki wakifatilia michezo fainali ya mpira wa pete wa Wanaume kwa mkoa wa Dar es Salaam.