Wednesday, March 21, 2018             
              JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
9 Barabra ya Ohio
  S. L. P. 5821,
  DAR ES SALAAM.
 

Simu ya maandishi: “ZIMAMOTO KUU”
Simu Nambari:  +255-22-2181093
Telefax:          + 255-22-2184569
Tovuti : www.frr.go.tz

                                                                                                  


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia  uwepo na muendelezo wa matukio ya moto katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo  shule za bweni,   Jeshi la Zimamoto  na  Uokoaji    linatoa tahadhari kwa  Wanafunzi, Wakuu  wa Shule, Wamiliki  na Wananchi kwa ujumla  kuchukua tahadhari  kwa kuwa makini katika matumizi ya vifaa vya umeme.
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkaguzi (INSP) Joseph Mwasabeja amesema, kutokana na matukio haya ya moto kutokea mara kwa mara katika Jamii yetu hususani katika Shule za Bweni hasa Shule za Sekondari na kusababisha uharibifu wa miundombinu kama vile mali, majengo na wakati mwingine majeraha au vifo kwa wanafunzi wetu. Mara nyingi matokeo ya majanga haya huleta hasara na sintofahamu kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Amesema, uchunguzi wa moto ( Fire Investigation) umebaini sababu za matukio hayo ni matumizi mabaya ya umeme yanayofanywa na wanafunzi kwa kujiunganishia nyaya za umeme wenyewe bila ya kuwa na weledi ili wapate sehemu za kuchaji simu na heater za kuchemshia maji kwa kificho kwasababu wanafunzi hawaruhusiwi kuwa na simu wala heater pindi wanapokuwa Shuleni.
Aidha, majanga ya moto yamekuwa yakitokea katika jamii yetu, kwasababu moto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Pia ni wazi kuwa na vyanzo vingi vya moto ni sisi wenyewe (binadamu) kutokana na uzembe au hujuma.
Ili kupunguza matukio haya Jeshi letu limeanzisha ( Fire Klabu) kwa Shule za Msingi na Sekondari, hatua itakayosaidia kuwapa  Elimu Stahiki ya kukabiliana na majanga ya moto na hatimaye kuwa na mabalozi wa Zimamoto na Uokoaji katika Shule na makazi yao.
Wito wangu kwa wamiliki wa Shule walipokee jambo hili kama ukombozi kwao ili kupunguza majanga na madhara ya moto pindi unapotokea katika Shule zao. Pia amewataka Wamiliki wa Shule kuzingatia maelekezo na ushauri unatolewa na Jeshi letu juu ya Kinga na Tahadhari dhidi ya majanga ya Moto.


“Vilevile niwaombe wananchi wote kuwa wepesi katika kutoa taarifa pindi wanapopata majanga ya moto na majanga mengine kwa kupiga namba 114 ili Askari wetu waweze kufika kwa wakati na kuokoa Maisha na Mali. Alisema huku akiwashauri wananchi kuwa na Vifaa vya kuzimia moto (Fire Extinguisher). ’’
Imetolewa na;


Joseph Mwasabeja – Mkaguzi Msaidizi (INSP)
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu
20 Marchi, 2018

GAVANA WA NIGERIA ATEMBELEA SHULE MAALUM YA SINZA

 Gavana wa mji wa imo nchini Nigeria, Rochas Okorocha, akimpongeza mwanafunzi wa darasa la Sita, Anati Mujib wa Shule ya Msingi Makumbusho, anayefanya vizuri katika masomo yake darasani, wakati Gavana huyo alipoitembelea shule hiyo akiambatana na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson, (kushoto) kwa ajili ya kuzungumza na kuchagua baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu ili kuwasomesha katika shule na Chuo chake kilichopo nchini Nigeri. Gavana huyo akiwa shuleni hapo alitoa zawadi ya Dola 100 kwa kila mwanafunzi aliyeongoza kimasomo katika darasa la tano, Sita na Saba kwa kila mmoja, na Dola 200 kwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu Shule ya Sekondari Makumbusho, Raymond Kalistus, anayefanya vizuri kimasomo darasani, ambapo pia alitangaza kumdhamini mwanafunzi huyo wa Darasa lasaba, Abdul Ausi kwa kumsomesha Sekondari hadi Chuo Kikuu kuanzia sasa kutokana na kufiwa na wazazi wotewawili. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Gavana akimkabidhi zawadi ya Dola 100 mwanafunzi, Anati Mujibu
 Gavana akikumbatiana kwa furaha na mwanafunzi, Abdul Ausi wa daeasa la saba aliyetangaza kumsomesha kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu, kwa kuchagua nchi yeyote aipendayo kwenda kupata elimu.
 Gavana akisalimiana na baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu wanaosoma katika shule hiyo
 Gavana akisalimiana na wanafunzi wa shule hiyo wakati akiaga kuondoka shuleni hapo
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akitafsiri hotuba ya mgeni wake Gavana wa mji wa Imo nchini Nigeria, wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya msingi Makumbusho.
 Gavana huyo akiendelea kuzungumza huku Naibu Spika akiendelea kutafsiri. Kulia ni msaidizi wa Gavana huyo, Tijan Babangida aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa Nigeria.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akitoa hotuba yake na kushukuru ugeni huo.
 Wakielekezana jambo. Kulia ni Tijan Babangida aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Nigeria, ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Gavana huyo....
 Wakisalimiana na viongozi baada ya kuwasili Shule ya Msingi Makumbusho
 Gavana akipozi kwa picha na mwanafunzi Abdul aliyemtangaza kuwa ni mwanawe kuanzia jana
 Picha ya pamoja
Picha ya pamoja....

NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA


Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Nape Nnauye ameishauli Serikali kuboresha mipaka ya nchi kwa wakati ili kuondokana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara kufuatia uvamizi wa wahamiaji kutoka nchi jirani.

Ameyasema hayo katika ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembea mipaka kati ya Tanzania na Uganda Wilaya ya Missenyi upande wa Tanzania Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Isingiro upande wa Uganda.

Nape amesema suala la kulinda mipaka ni muhimu hivyo ni vyema serikali kupitia Wizara ya Ardhi ikatenga fedha za kutengeneza barabara zilizoko mipakani ili kurahisisha ulinzi na usalama wa mipaka yetu na kuwezesha wakazi wa nchi hizi mbili kutambua mipaka ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi.

“Tumebaini kuwa kuingia kwa wananchi wa Uganda hasa kuleta mifugo yao katika lanchi ya Missenyi kunachangiwa na kutokuwepo njia maalumu na alama maalumu zinazotenganisha kati ya nchi na nchi hivyo watu wanaingia kupitia katika vichochoro visivyo rasmi na kuhatarisha amani kwa wakazi wa mipakani alisema Nnauye”
Kamati hiyo pia ilifanikiwa kufika katika vijiji vya Rwengiri, Bwenkoma na Bubale vilivyopo kata ya Kakunyu na kubaini kuwa baadhi ya alama zilizowekwa mpakani zimepotea hivyo wafugaji kutoka maeneo mbalimbali wanaendelea na shughuli za ufugaji bila kujali sheria.

Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa ikikagua mipaka na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kama barabara itatengenezwa katika mipaka yote ya Missenyi kazi ya kuwabaini waarifu itakuwa rahisi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa mpaka sasa Wizara imepokea shilingi bilioni 4 za kuimarisha mipaka ambapo fedha zitakazotumika kuimarisha mpaka wa Tanzania na Uganda ni shilingi Bilioni 1.9 na shilingi Bilioni 2.1 kwa mpaka wa Tanzania na Kenya.

Aidha kupitia ziara hiyo ya kamati Dkt. Mabula ametoa wito kwa wawekezaji ambao ambao wameshindwa kuendeleza maeneo yao kuja kuyaendeleza kabla ya kuchukuliwa hatua za kuyagawa maeneo hayo kwa watu wengine.
“Kuna watu waliomba maeneo wakafuge lakini wameshindwa na baadhi wanayatumia kwa kazi ambazo hazieleweki huku baadhi wakiomba kufugia lakini wanayatumia kwa ajili ya kazi nyingine, nitawachulia hatua kama watashindwa kufanya kazi waliyoomba alisema Mabula.”

Akitoa taarifa kwa kamati hiyo, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Dkt. James Mtamakaya amesema kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko ya utawala na kwamba mpaka wa Tanzania na Uganda uliasisiwa na Uingereza na Ujerumani mwaka 1890, ulitafisiriwa mwaka 1902-1904 kwa kutumia marundo 15 ya mawe ambayo baadhi ya malundo hayo yapo mpaka leo.

Kamati ya Bunge ya Kudumu  ya Ardhi, Maliasili na Utalii, ikiwa katika tarafa ya Missenyi ilitembelea kata za Kakunyu, Mutukula na vijiji vya Rwengiri na Lyengoma ambapo ni eneo huria la ranchi ya Missenyi ambalo lilitengwa na serikali kwa ajili ya ufugaji wa Ng’ombe katika ranchi hiyo na baadhi ya maeneo kuwa na wakazi wachache.

Akizungumza na wajumbe wa  kamati ya Bunge mkazi wa kata ya Kakonyo, Wilaya ya Missenyi ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Bwana Faraja Kaijage amesema kuwa kuna changamato kubwa katika mipaka hiyo, ambapo kwa kumbukumbu zake mnamo Disemba 19, 2016  alipigwa na kuumizwa na wafugaji wa Uganda kwa kosa la kukamata mifugo ya waganda iliyokula mazao ya wananchi katika kijiji hicho.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Dennis Mwila amesema kuwa kuna migogoro katika baadhi ya vitalu huria vya Missenyi vilivyogawiwa mwaka 2006 inayosabishwa na ukosaji wa uzalendo kwa viongozi kwa kuwauzia ardhi wahamiaji haramu na baadhi ya vitalu kuleta mifugo aina ya Ng’ombe kutoka Uganda kwa malipo haramu.

Wilaya ya Missenyi ni Wilaya ilianzishwa mwaka 2007 ambapo imepakana na nchi ya Uganda upande wa Kaskazini, Wilaya ya Karagwe upande wa Magharibi na Wilaya ya Bukoba vijijini upande wa Mashariki ambapo pia Wilaya ina tarafa mbili, vijiji 77 na vitongoji 352.

Aidha upande wa mpaka wa Tanzania na Uganda Wilaya inapakana na Rakai na Isingiro zilizopo nchini Uganda ambapo mpaka una kilomita  110.7 na 0.5 ya umbali huo upo katika maji ya ziwa Viktoria.

Kwa upande wa idadi ya vituo vilivyo rasmi vya kupita watu ni vinne ambavyo ni Mutukula, Kilahya, Bugango na Kashenye na njia nyingine zisizo rasmi zipo mipakani takribani 20 vilivyo jirani na mpaka huo.
 Mkazi wa kata ya Kakonyo, Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Bwana Faraja Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii jinsi alivyopigwa na kuumizwa na wafugaji wa nchini Uganda kwa kosa la kukamata mifugo ya waganda iliyokula mazao ya wananchi wa Tanzania katika kijiji hicho mwaka 2016
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua mpaka wa Tanzania na Uganda katika eneo la mto kagera
 Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Dkt. James Mtamakaya akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii mipaka iliyopo kati ya Tanzania na Uganda
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii wakipanda juu ya jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba BP 30 katika kata ya Bugango wilaya ya Missenyi mkoani Kagera(
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii wakipanda juu ya jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba BP 29 katika kata ya Kakunyu wilaya ya Missenyi mkoani Kagera 
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula (mwenye Tshirt ya njano) akiongoza Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii kushuka katika jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba BP 30 katika kata ya Kakunyu wilaya ya Missenyi mkoani Kagera
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii wakiwa mbele ya jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba BP 30 katika kata ya Bugango wilaya ya Missenyi mkoani Kagera (Picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi).

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA
               

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MATOKEO YA OPERESHENI MAALUM ILIYOFANYIKA MJINI MAGHARIBI- ZANZIBAR, KUANZIA TAREHE 14 – 21.03.2018

Ndugu Wanahabari,

1.          UTANGULIZI ;
        Zipo taarifa kuwa baadhi ya wananchi Mkoa wa Mjini Magharibi wanatumia, wanashiriki, wanafadhili au kusaidia biashara ya madawa ya kulevya kama ilivyo kwenye maeneo mengine nchini. 

Hata hivyo Serikali ipo kwenye vita kali ya kupambana na mtandao wa madawa ya kulevya na Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Polisi Zanzibar waliunda timu kutoka Kitengo cha Operesheni Maalum za Polisi Makao Makuu Dar es salaam kuja kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa kero hii kama ilivyo kwenye maeneo mengine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


2.          MATOKEO YA OPERESHENI ;
S/N
MAFANIKIO
MATOKEO / IDADI
TAARIFA ZA INTELIJENSIA

1.   
Kupatikana kwa taarifa za  watuhumiwa wanaojihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya (kutumia, kuuza, kufadhili au kusaidia)
105
JUMLA KUU
105

WATUHUMIWA  WALIOPATIKA NA HATUA

1.   
Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani

26
2.   
Watuhumiwa waliopo chini ya Upelelezi

16
3.   
Watuhumiwa waliopo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee)
16
JUMLA KUU
58

VIELELEZO
1.   
Heroin  
Kete 1293 na Vifuko 3 sawa na
Gramu 74.385
2.   
Banghi (Vifurushi)
373

3.   
Banghi (Vifuko)
33.          WITO :
        Natoa wito na tahadhari kwa wananchi wote wanaohusika kwenye mtandao huu kuacha mara moja kwa kuwa vita hii imeshaanza na inaendelea kwa lengo la kuhakikisha usalama wa vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo maana madawa haya yanaathiri zaidi vijana ambao ndiyo muhimili na nguvu kazi ya Taifa.


Aidha nawapongeza wananchi wote waliotoa ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu huu bila ya kuona muhali. Niwaombe wananchi wote kuendelea na ushirikiano huu wa kutoa taarifa.

 Mwisho natuma salamu kwa watuhumiwa wote waliotoroka kule walipo wajue kuwa wanatafutwa na watakamatwa ili wahojiwe na hatimae kufikishwa Mahakamani.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza


Liberatus Sabas – DCP
Mkuu Wa Uperesheni Maalum za Polisi Tanzania
21.03.2018

BEI ZA BIDHAA ZA ZA MATUNDA NA MBOGABOGA KATIKA SOKO LA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.

  Mboga aina ya Spinach fungu sh. 500, Tembele sh 500
 Mkungu wa ndizi katika soko la Kinondoni unauzwa kati ya sh 25,000 hadi sh 30,000.

Bei za mchele katika soko la Kinondoni kama inavyonyeshwa katika vibao


 Mfanyabiashara akitembeza biashara zake katika maeneo ya kinondoni
 Embe katika soko la Kinondoni linauzwa kati ya sh 1000 hadi sh 1500, Papai sh 2000 hadi 400 hutegemeana na ukubwa wa Papai, Nanasi  sh 3000 hadi sh 4000, Ndizi Mbivu inauzwa kati ya sh 250 hadi sh 300.(Imeandaliwa na Emmanuel Massaka , Globu ya Jamii)

DC MJEMA AWEKA JIWE LA MSINGI KISIMA CHA MAJI KISUKULU

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi wa kisima cha maji katika kata ya Kisikulu ikiwa shemu ya maadhimisho ya wiki ya maji katika Wilaya hiyo ambapo Kisima hicho kitaweza kusaidia wakazi wote wa kata hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema,akikata utepe na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wa Kata ya Kisukulu wakati wa  kuweka jiwe la smingi wa kisima kirefu cha maji cha kata ya Kisukuru.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema,akizindua jiwe la msingi la ujenzi wa Kisima cha maji cha kata ya Kisukuru leo.
 Diwani wa kata ya Kisukuru, Joseph Kasaenda akitoa neno la Shukrani kwa mkuu wa Wilaya mara baada ya uzinduzi wa jiwe la msingi katika kata hiyo.
 Makada wawili wa Chama Cha Mapinduzi na CHADEMA, wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa jiwe la msingi la Kisima Cha Maji.
 baadahi ya wakazi wa Kisukulu waliofika katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa uzinduzi wa kisima cha maji.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...