Thursday, March 29, 2018

WAUGUZI SABA JELA KWA KUGHUSHI VYETI


Wauguzi saba wanatumikia adhabu ya vifungo jela katika mahakama mbalimbali nchini baada ya kuthibitika kughushi vyeti vya kitaaluma.

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Lena Mfalila amesema hayo leo jjini Dar es Salaam, katika semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya kongamano la kisayansi la wauguzi na wakunga linalotarajiwa kufanyika April 4-7, mwaka huu mkoani Dodoma. 

“Tumekuwa tukipokea malalamiko ya wananchi na tunachukua hatua, 2016 muuguzi mmoja wa Temeke alifungiwa leseni na tukamnyang’anya vyeti vyake baada ya kumkuta na hatia na baada ya adhabu kuisha tulimrejeshea. “Wengine walipatikana na hatia na kufungwa kwa nyakati tofauti, pamoja na hayo baraza tumeendelea kuhakikisha tunasimamia maadili ya wauguzi na wakunga ili kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma bora,” amesema. 

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi na Ukunga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Gustav Moyo amesema kazi ya Uuguzi na Ukunga ni ngumu hata hivyo wahusika wanapaswa kuendelea kutoa huduma kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma.

Dhamana ya mbowe na wenzake imekwama,wataendelea kukaa mahabusu hadi April 3

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru viongozi wa sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kuletwa mahakamani hapo Jumanne Machi 3, ili kutimiza masharti yanayowataka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Sh milioni 20 kwa maandishi.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria ambapo Jamhuri wamewasilisha nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kutoa dhamana kwa washtakiwa hao.
Wakili Mkuu wa Serikali, Fatma Nchimbi andiye amewasilisha nia ya kupinga washtakiwa hao kupewa dhamana hoja iliyopingwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala.
Baada ya mabishano hayo, Hakimu Mashauri alisema: “Hoja ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa kuwapa dhamana washtakiwa hao, imewasilishwa mapema na inatoa amri washtakiwa hao waletwe Jumanne ili kutimiza masharti ya dhamana kwa kuwa leo hawapo mahakamani.”

“Nikitoa dhamana wakati washtakiwa hawapo haina maana zoezi zima lisimame.” -Hakimu 

“Leo washtakiwa hawajafikishwa mahakamani na nimetoa masharti ya dhamana, hivyo kutoa dhamana na washtakiwa wakiwa bado hawajasaini ilo zoezi bado halijakamilika.” -Hakimu 

“Hivyo kwenye hatua ya sasa ni mapema mno kwa upande wa mashtaka kuwasilisha hoja za kukata rufaa wakati bado mchakato haujakamilika.” -Hakimu

“Mahakama inatoa remove order waje mahakamani April 3,2018 na wadhamini wao ili waje kukamilisha masharti ya dhamana.” -Hakimu

WARAMI:CHADEMA WAMEKANYAGA KAA LA MOTO


Na Mwandishi Wetu
WATETEZI wa Rasilimali Wasio na Mipaka(Warami)limesema limesikitishwa na kitendo cha Kamati kuu ya   Chadema kuingilia uhuru wa Mahakama baada ya jana kuitisha mkutano kuzungumzia mambo yalipo mahakamani.

Warami wameongeza kuwa  si tu kuingilia uhuru wa mahakama pia chama hicho kimekwenda mbali zaidi kwa kutoa masharti yanayoashiria uvunjifu wa amani iwapo Mwenyekiti wa Freeman Mbowe na viongozi wengine watanyimwa dhamana leo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugunzi wa Utafiti wa Warami Philipo Mwakibinga amesema jana baadhi ya viongozi wa Chadema kupitia mkutano wao wameonesha dhahiri kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kuanza kushinikisha maamuzi ya Mahakama.

“Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema, Profesa Abdallah Safari na wenzao wakiwa wanajua kuwa Mahakama ni chombo cha haki walitengeneza mazingira ya kuonesha kuwa viongozi hawatetendewi haki kama hawatapa dhamana leo.

“Wanafanya hivyo wakijua wazi jambo hili limelenga kuishawishi , kushinikiza na kuilazimisha mahakama ifanye watakavyo wao kwa kuacha misingi ya haki wajibu na maadili ya kimahakama,”amesema Mwakibinga.

Amefafanua Watanzania ni mashahidi Mbowe na wenzake ambao wapo Mahakamani wamekamatwa kama matokeo ya matendo yao ya kushawishi na kuchochea chuki miongoni watanzania jambo ambalo si la kiutamaduni kwa Taifa.
“Warami tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa sheria ni kama kaa la moto  na unapovunja sharia lazima ujue umeamua kushika kaa la moto kwa hivyo lazima ujiandae kuungua.

“Tunawakumbusha Chadema ,hasa wakina Lema na wenzao watii sheria , waache maneno ya kichochezi yasiyo ya kiuongozi na wasiendelee kuropoka ropoka, zama za kuwachekea waropokaji zimepitwa na wakati,”amesema.

Mwakibinga amesema Lema kukamatwa kwa viongozi wa chama chake ni mkakati uliopangwa na Serikali kwa ajili ya kuwakomoa.

Amesema Warami wanawapa changamoto Chadema , wamuulize Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ajitokeze hadharani wakati Augustino Mrema akiwa NCCR-Mageuzi na baadae TLP alivyokuwa anakamatwa na vyombo vya dola je alikuwa analazimisha vyombo vya dola vimkamate wakati Mrema hakuwa na makosa kwa wakati ule.

“Chadema waache kuharibu sifa ya vyombo vyetu vya kiusalama  hasa idara nyeti ya Usalama wa Taifa kwa kuwasingizia mambo ya ajabu ajabu kwa ajili ya kuficha udhaifu wao wa kuimarisha chama,”amesema Mwakibinga.

Ameongeza Warami inawataka Chadema kuacha kukimbia kivuli chao na waswahili wanasema ‘ukilikoroga lazima ulinywe’ .

“Hivyo Chadema walinywe kwa kadiri ya walivyorikoroga.Pia iache Mahakama itafisiri sheria na kwa kuwa wameweka wanasheria wanaowaamini, wawahimize wanasheria wao kuhakikisha wanashinda kesi zinazowakabili,”amesisitiza.

KUHUSU MAASKOFU KUTUMIKA

Mwakibinga amesema mara ya mwisho walihoji iwapo maaskofu wanatumika na vyama vya siasa hasa Chadema.

“Nafikiri wote sasa tumejiridhisha kuwa maaskofu wetu wameamua kutumika kulipa fadhila za waliokuwa wanawapa fedha katika zama za kufanya harambee ya fedha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Matukio ya Chadema kuunga mkono hadharani waraka wa maaskofu ,ACT Wazalendo kunifukuza uanachama kwa mimi kuwakosoa maaskofu na Maalim Seif kutangaza hadharani anaunga mkono madudu yale ya maaskofu,”amesema.

Ameongeza hivyo ni vishiaria na kuthibitisha wazi maaskofu wameamua kutumika na kuyaacha maelekezo na mafunzo ya dini yanayotaka kilicho cha kaisari apewe kaisari na kilicho cha Mungu apewe Mungu.
Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanasiasa, wanaharakati , wanahabari , viongozi wa dini , taasisi binafsi  waanzishe utaratibu wa kuheshimu uhuru wa Mahakama na kutoa kauli za mashinikizo.
 Mkurugenzi wa Utafiti kutoka Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga , akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu mkutano wa  Kamati Kuu ya Chadema uliofanyika jana ukiwa na lengo la kuingia uhuru wa Mahakama.
 Mkurugenzi wa Utafiti kutoka Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga, akiwaeleza jambo waandishi wa habari yaliyojiri katika mkutano mkuu wa Chadema.

Tuesday, March 27, 2018

MBOWE NA WENZIE WASEKWA RUMANDE HADI MARCH 29


 Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa wakiwa katika gari ya Polisi tayari kwa kupelekwa Segerea mara baada ya kukosa Dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kutokana na  Mashtaka yanayo wakabili
  Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa, Kaimu katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba , John Mnyika , Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakiwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu mkazi kisutu mara baada ya kesi yao kuarishwa na kuamuriwa kurudi rumande bila dhamana
 Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa, Kaimu katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba , John Mnyika , Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakiwa wamekaa katika benchi la mahakama ya hakimu mkazi kisutu kusubiri kusomewa mashtaka yao
 Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa, Kaimu katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba , John Mnyika , Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakipandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Baadhi ya viongozi wa Vyma vya Siasa na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya mahakama kusuburi kushuhudia msafara wa viongozi wakuu wa Chadema wakipelekwa Rumande

EFM YAWEKA MILIONI 300 SHINDANO LA SHIKA NDINGA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha Efm Radio, Dennis Busulwa(SEBO) amesema kampuni yake imewekeza kiasi cha zaidi Milioni 300 kwa ajili ya shindano lake la Shika Ndinga  litakalofanyika katika mikoa 6 ya Tanzania bara  na kuanza kutimua vumbi Dar es Salaam katika uwanja wa Mwembe Yanga.

Sebo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa anazungumza na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa shindano hilo na maadhimisho ya miaka minne ya Efm Radio na kuongezeka kwa masafa kwa kutoka mikoa sita hadi kufika kumi.

"Efm Radio imekuwa na bidhaa mbalimbali za uwezeshaji  kwa wasikilizaji wake ambapo shika ndinga kwa mwaka huu 2018 linaweza kuwafikia watanzania katika mikoa sita zaidi ikiwa ni lengo la uwezeshaji katika jamii "amesema Sebo.

Amesema Shindano la shika ndinga mwaka huu linatarajia kufanyika kwa wiki 7 katika mikoa sita amabayo ni Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mtwara , Mbeya na Pwani  ambapo litaanza tarehe 7 April hadi mei 15 ikihusisha jumala ya Pikipiki 14 na gari aina ya kirikuu mbili.

katika hatua nyingine Sebo alitumia mkutano kuwaeleza waandishi wa habari juu ya mafanikio ya Radio yao katika miaka minne tangu kuanzishwa kwake  kwa kuwa radio namba moja kwa kusikilizwa kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku ikiwa namba mbili katika mikoa ya bara.
 Meneja Mkuu wa EFM Radio,Dennis Busulwa(SEBO), Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo juu ya shamrashamra za Efm Kutimiza miaka minne sanjari na uzinduzi wa Shindano la Shika ndinga linaloendeshwa na kituo hicho cha Radio kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Simu nchini(TTCL), Nicodemus Mushi akizungumza na Waandishi wa habari juu ya udhamini wa shirika lake katika mashindano ya shika ndinga kote nchini.
 Afisa Habari wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Tatu Mzuka ,Petronila Mtatiro akieleza namana watu watakavyoweza kujishindia zawadi mbalimbali wakati wa shindano la shika ndinga.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Chotec Limited inayosambaza vilainishi vya Shell, Tanzania, Choba Mumba akieleza namna wao watakavyoweza kusambaza vilainishi maalum vya pikipiki nchini.
 Meneja Matukio wa Kampuni ya Efm Radio, Jesca Mwanyika akizungumza juu ya matokeo ya washindi wa shindano la Shika ndinga katika msimu uliopita .
 Baadhi ya Wadau na wadhamini wakifatilia mkutano wa Waandishi wa habari juu ya shindano la Shika Ndinga na Miaka Minne ya Efm.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wa waliohiriki Mkutano juu ya shindano la shika ndinga na Miaka minne ya Efm.

Sunday, March 25, 2018

WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

 Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka-WARAMI wameupinga waraka wa Ujumbe wa pasaka kutoka kwa baraza la maaskofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) uliotolewa jana, kwa madai kuwa ulikuwa wa kisiasa wenye lengo la kukososa utendaji wa serikali na kuleta hofu kwa jamii.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Da res Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI, Philipo Mwakibinga amedai kuwa maskofu kama viongozi wa dini wanatakiwa kujikita katika masuala yanayohusu dini na si siasa.

“WARAMI tunaamini kwamba wajibu wetu ni kuhakikisha jamii inapata haki pasipo upendeleo wowote, kufuatia hili tumeona si sahihi kukaa kimya, tukaona tupaze sauti kuona tunaijenga jamii kulingana na tofauti zao. Kwenye nafsi zao wanavyo vyama vyao mbali na uongozi wa kidini. Hisia za kivyama zisilete mtafaruku kwenye Imani. Wajitafakari kuchagua aina ya maneno wanayotoa kwa jamii ili kulinda na kukuza amani,” amesema na kuongeza.

“Tunashangaa kwa nini waraka huu wa salamu za pasaka haukujikita katika kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma biblia na maandiko mengine ya dini na badala yake wanajikita katika maoni yanayong’ata na kupuliza.”

Mwakibinga amedai kuwa, Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka huo ni malalamiko kuhusu mchakato wa katiba mpya na uhuru wa kutoa maoni, ambao ulikwamishwa na wansiasa wa upinzani waliosusia kushiriki mchakato huo.  

“Maaskofu wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini hawajajikita kuelezea kwa kina kisa hasa ni kipi. Sisi tunafahamu kuwa wapo walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa baadhi ya vijana ambayo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya kutokea kwake na si kuyasubiri mpaka leo,” amesema.
 Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini katika ukumbi wa Traventine Magomeni.

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO UCHINA

Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maharufu kama China International Beauty Expo African Hall,Rex Chan akizungumza na Waanddishi w...