Wednesday, April 11, 2018

GABO BALOZI WA SIMU YA TECNO POP 1

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Msanii wa Filamu wa nchini Salim  Ahmed Gabo, ametangazwa kuwa balozi wa simu mpya ya Mkononi kutoka kampuni ya Tecno Tanzania inayokwenda  kwa jina la Tecno Pop 1itakayouzwa katika maduka yote ya Vodashop nchini.

akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa kumtangaza balozi huyo Mkuu wa kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno,Anuj Khosla amesema kuwa wameamua kuileta simu hiyo hili waweze kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kumiliki simu janja .

"tuna furaha kubwa kuwatangazia uwepo wa simu hii ambayo mtu akinunua atapata na GB 10 kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom hili aweze kuperuzi na kujielimisha kupitia simu hii janja ambayo ina uwezo mkubwa"amesema Khosla

kwa upande wake Gabo amesema kuwa anaishukuru Tecno kwa kuweza kumpa nafasi hiyo ya kufungua njia kuwa balozi kwani ubalozi wa kwanza kuupata tangu aanze kujulikana katika tasnia ya filamu.

"ndio mwanzo wa mimi kuanza kufanyakazi na makampuni makubwa kwani kwa kampuni hii ya simu kuniona mimi gabo kuwa naweza kuwa balozi na kutangaza bidhaa zao ni jambo jema ambalo kila msanii anatamani kulifikia ukiacha mafanikio ya sanaa ya kawaida" amesema Gabo.

amesema kwa sasa yeye kama msanii mkubwa anatumia nafasi hiyo kuweza kufikisha ujumbe kwa mashabiki na kuwataka watumie simu hizo ambazo zina uboara na bei nafu mpaka kwa watanzania wa kawaida.
 Mkuu wa kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno,Anuj Khosla akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ujio wa Simu mpya ya Tecno POP 1 itakayotolewa na GB 10 za Vodacom
 Msanii wa Filamu wa nchini Salim  Ahmed Gabo, akionyesha simu aina ya Tecno POP 1inayotolewa na GB 10 Za Vodacom.kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha manunuzi  ya rejareja ya simu tz, Brigita Stephene
Msanii wa Filamu wa nchini Salim  Ahmed Gabo, akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Vodacom na Tecno Tanzania

Sunday, April 8, 2018

WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wakazi wawili wa Dar es salaam, wameibuka washindi katika shindano la shika ndinga lililoendeshwa na kituo cha Radio cha Efm.
Washindi hao ni Ashura Ramadhani  mkazi wa Bunju ambaye alipiga simu na kupata nafasi hiyo kupitia kipindi cha uhondo.

Mwingine ni Abbas Awadhi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala ambaye alipata nafasi ya kushiriki katika shindano hilo kupitia kipindi cha Genge kinachoendeshwa na radio Efm.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi za Washindi hao Meneja Mkuu wa Radio Efm na Tv E, Dennis Busulwa(Sebo) amesema kuwa washindi hao wameshinda pikipiki na kupatiwa tiketi ya kushiriki fainali za   shika ndinga zitakazo fanyika Dar es Salaam mara baada ya kuwapata washindi wa mikoani.

Amesema kuwa siku ya jumatatu washindi hao watafika katika ofisi za Efm na Tv E kwa ajili ya kubadilisha majina ya kadi za pikipiki hizo kutoka jina la kampuni kwenda majina yao.

Washindi hao ambao wamepatikana kupitia mchakato mrefu ulioanza asubuhi kwa mbio za kukimbia na Vikombe vya maji kisha ikaja awamu ya pili ya kukimbia na mayai ambayo iliwapeleka fainali.

Katika hatua ya fainali ya kushika gari ndio iliyotia fora kwa wanawake kuweza kusimama kwa zaidi ya saa moja wakti wanaume ndani ya nusu saa  walikuwa washapata mshindi.
 Meneja Mkuu wa Radio Efm na Tv E, Dennis Busulwa(Sebo), akizungumza kabla ya kukabidhi kadi kwa washindi wa Pikipiki wa shindano la Shika Ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam
 Mshindi wa Shindano la Shika Ndinga kwa Wanawake kwa mkoa wa Dar es Salaam Ashura Ramadhani  mkazi wa Bunju Akiwa jjuu ya pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa na Efm. 
Mshindi wa Shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa Wanaume  Abbas Awadhi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala akiwa juu ya Pikipiki yake mara baada ya kutangazwa mshindi
 wanawake waliongia fainali katika shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam wakichuana wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
 Wanaume waliongia fainali katika shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam wakichuana wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
 washiriki wa  shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam wakichuana wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
 Msanii wa Muziki wa Singeli nchini Man Fongo, akitumbuiza katika shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam   wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
 Wakazi wa Dar es Salaam  waliofika kushuhudia shika ndinga katika Viwanja vya Mwembeyanga


TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...