Friday, April 20, 2018

JWAZIRI JAFO AFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU NA MADARJA YALIYOBOMOKA MANISPAA YA ILALA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema wizara yake kupitia wakala wa Barabara wa Serikali za Mitaa Tarura itafanya upembezi wa haraka hili kuwez akuhakikisha miundombinu ya barabara iliyoaribika  kutokana na mvua za Masiaka katika barabara za manispaa ya Ilala inarekebishwa haraka sana.

 

Waziri jafo amesema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea madaraja mawili yaliyo katika na maji ya kata ya Gongolamboto Ulongoni A na B  na Pugu Mnadani, ambapo yamesababisha watu kushindwa kuvuka kwa magari kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

“ Hili la ulongoni A litashughulkikiwa kwa haraka kutokana na laenyewe kuonyesha unafuu kidogo lakini Darja la ulongoni B na Pugu wataalamu watabidi wakachini hili waweze kujua ni namna gani yatajengwa hili yasiweze kupata tena madhara pindi mvua kubwa zinaponyesha”amesema Jafo.


 

 Aidha waziri jafoi aliwaomba wale wote waliojenga katika kingo za mto msimbazi kuanz akuondoka haraka kwani madhgara yake ni makubwa kama yalivyoonekana katika mvua hizi ambapo nyumba nyingi zimesombwa na maji na watua wana  pa kukaa.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiwa ameongozana na Viongozi waandamizi wa Manispaa ya Ilala kwenda kuanaglia bafrabra na Madaraja yaliyo athirika wakati wa Mvua.
 W Mkuuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo Sehemu ya Miundombinu iliyoharibika
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Viongozi Waandamizi wa Manispaa ya Ilala waliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema  wakati alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara za Halmashauri. 
Sehemu ya Draraja la Ulongoni A iliyochukuliwa na Maji ambayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo  alikwenda kukagua 

KIWANDA CHA MAFUTA CHA MURZAH CHA TEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM

 Sehemu ya Kiwanda Cha  Mafuta cha MURZAH ikiteketea kwa moto huku baadhi ya ya Magari ya Askari wa kikosi cha Zima Moto wakijitahidi kuzima moto huo ambao mpaka sasa chanzo chake aujajulikana.
  Sehemu ya Kiwanda Cha  Mafuta cha MURZAH ikiteketea kwa moto huku baadhi ya ya Magari ya Askari wa kikosi cha Zima Moto wakijitahidi kuzima moto huo ambao mpaka sasa chanzo chake aujajulikana.
 Askari wa Jeshi la Zima Moto wakijaribu kuudhibiti moto ambao ulikuwa unarukia upande wa pili wa Kkwanda cha Africariers  mara bada sehemu ya Kiwanda cha Mafuta cha Murzah kuteketea kwa moto
Askari wa Zima Moto na baadhi ya wakurugenzi wa Kiwanda Cha Murzah wakiw akatika harakati za kuzima moto huo.

Thursday, April 19, 2018

DIAMOND NA NANDY WAOMBARADHI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI TCRA

 Msanii wa Muziki wa Muziki wa Bong Fleva, Naseeb  Abdul 'Diamond' akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini 'TCRA ' kujifunza kanuni na maudhui ya mitandaoni ikiwa ni siku chache mara baada ya kuweka picha zilizo kinyume na maadili mtandaoni.
 Msanii wa Muziki kizazi kipya anayefanya vizuri kwa Wasichana, Faustina Charles'Nandy' akielezea namna alivyojifunza kwa kupostiwa picha za utupu katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa ameliachia jeshi la Polisi lishughulike na hilo
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, Profesa George Kisaka akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuwaonya wasanii Diamond na Nandy mara walipotembelea ofsi ya TCRA.
  Msanii wa Muziki wa Muziki wa Bong Fleva, Naseeb  Abdul 'Diamond' na  Msanii wa Muziki kizazi kipya anayefanya vizuri kwa Wasichana, Faustina Charles'Nandy' wakisalimiana mara baada ya kufika katika ofisi za TCRA .
  Msanii wa Muziki wa Muziki wa Bong Fleva, Naseeb  Abdul 'Diamond' Akiwasili katika ofisi za TCRA
  Msanii wa Muziki wa Muziki wa Bong Fleva, Naseeb  Abdul 'Diamond Akiwa amekaa na Meneja wake Said Fella.
Msanii wa Muziki kizazi kipya anayefanya vizuri kwa Wasichana, Faustina Charles'Nandy' akiwa na Meneja wake katika ofisi za TCRA.

Wednesday, April 18, 2018

Wadau wa dawa watakiwa kuchangamkia fursa


Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Josephat Kandege amewataka wauzaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wote wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali ya kuwa Mshitiri mteule ‘Prime Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote Tanzania.

Kandege ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa dawa  ‘Vendors Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na wadau wa Afya HPSS’ chenye lengo la kuweka uelewa wa pamoja kuhusu uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.

Amesema “mfumo huu utatumika kupata mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma vitakosa au kupata kiwango pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia utasaidia kupunguza kero za Afya ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya”.

Sasa basi ninyi kama wazabuni muhimu katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo na nia njema na Nchi ya Tanzania mnatakiwa kujitokeza katika mchakato wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila Mkoa ambaye atakidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe. Kandege.

Wakati huo huo Naibu Waziri Kandege aliwafahamisha wadau wa dawa kuwa Serikali imagatua mipango na bajeti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na inapeleka Fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki zilizofunguliwa katika kila kituo hii itasaidia katika kufanya manunuzi ya dawa hizo na kurahisha mchakato wa malipo.

“Hivyo niwahakikishie kuwa utaratibu wa malipo utakua ni rahisi na wa haraka zaidi kwa kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati husika zitahusika kuagiza dawa kwa Mshitiri pale mahitaji ya dawa hizo zitakapokosekana kutoka MSD” alisema Mhe. Kandege.

Alimalizia kwa kuwataka Wadau wote wa Dawa kutumia kikao hiki kuelewa kwa undani kuhusu utaratibu huu na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kumpata Mshitiri Mteule kwani zoezi hili litaendeshwa kwa uwazi na kwa usindani mkubwa.

Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe amesema hivi sasa wako katika uwekezaji Mkubwa katika Sekta ya Afya kwa kuzingatia kuwa Bajeti ya Dawa imeongezwa kutoka Bil 31 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia Bil 269 kwa mwaka 2017/18 hivyo ongezeko hili la bajeti linatakiwa kwenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa dawa na zenye ubora chini ya usimamizi makini wa wataalamu wa Afya.

Dr. Ntuli alisema mpango huu utaleta manufaa kwa wananchi wote ambao watakua chini ya mpango wa Tele kwa Tele na wale wanaopata huduma kupitia mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa; Tunataka kila mmoja apate dawa anayoihitaji kwa wakati.

Naye Mfamasia toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard alisema mfumo wa Mshitiri Mteule umeanzishwa kwa sababu ya changamoto zilizoonekana awali za kutumia mzabuni kama vile taratibu za manunuzi kuchukua muda mrefu na gharama za manunuzi kuwa kubwa na zinazotofautiana kati ya Halmashauri moja na nyingine ndani ya Mkoa mmoja.

Changamoto zingine alizozibainisha ni kubadilika kwa bei mara kwa mara kila manunuzi yanapofanyika, kutokuwa na uhakika wa ubora wa bidhaa kutokana na kuhifadhiwa na kusafirishwa katika mazingira mbayo si salama na zaidi baadhi ya wazabuni na watumishi kutokuwa waaminifu.

Matumizi ya mfumo huu umeelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Sera ya Afya ya Taifa ya mwaka 2007, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya na Sera ya Mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Kikao hiki cha wadau wa dawa ‘Vendor Forum’ kimefanyika kwa mara ya kwanza na kimehusisha wadau kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele) akifungua kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika Ukumbi wa Dodoma Hotel.
  Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya Vendor Forum.
 Mfamasia Mwandamizi  toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard akielezea malengo la kikao cha Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel mapema leo.
  Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.

MANISPAA YA UBUNGO YATILIANA SAINI MKATABA NA BENKI YA CRDB KUTOA MIKOPO YA VIJANA NA WANAWAKE

--
 Meya wa Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob akizungumza kabla ya kutilina Saini Mkataba na Benki ya CRDB Juu ya Mikopo ya kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Meya wa Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob akitia saini Mkataba wa makubaliano wa kushirikiana na benki ya CRDB Kutoa Mikopo  kwa  kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Mkurugenzi  wa Halamashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akizungumza kablaya kumkaribisha mwakilishi wa benki ya CRDB Kuelezea walivyojipanga kutoa mikopo kwa kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Muwakilishi wa Benki ya CRDB, Philip Stephene akizungumza juu ya benki yake itakavyotoa mikopo kwa kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Wakishuhudia tendo la utiaji saini baina ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na CRDB  kwa kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
Sehemu ya Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakiwaftilia tukio hilo la utiaji saini na benki ya CRDB

Tuesday, April 17, 2018

UHARIBIFU WA MAZINGIRA ULIVYOCHANGIA KUONGEZA MAFURIKO KATIKA BONDE LA MTO MSIMBAZI

 Mmoja wa Wakazi wa Dar es Salaam ambaye alikuwa akivuna chupa za maji taka zilizojaa katika Daraja la Mto wa Msimbazi ambapo imeonesha kuwa uharibifu wa Mazingira na utupaji wa taka hovyo katika bonde la mto Msimbazi kumechangia kuziba kwa mifereji mingi inayopitisha maji kwenda baharini.
 Vijana wa jiji la Dar es Salaam wakiokota machupa katika bonde la mto Msimbazi mara baada ya machupa hayo kuletwa na maji ya mvua yaliyofurika kuja na takatka hizo
 Sehemu ya takataka zilizojaa katikati ya Barabara ya Morogoro amabazo zimeletwa na maji ya mvua yaliyotapishw akutoka mto Msimbazi.
 Mmoja wa wa kazi wa Jiji akiwa amejitika mzigo wake katika bonde la jangwani mara baada ya kuokot katika bonde la mto Msimbazi
Bibi  wa makamo akiwa amejibanza  katika kituo cha mabasi ya yaendayo haraka mala baada ya makazi yake kusombwa na maji katika eneo la Jangwani.

 Muendesha baiskeli ya Magurudumu matatu  akijaribu kiunua baiskeli mara baada ya kuteleza katikati ya barabra ya Morogoro ambapo tope limetanda mara baada ya tope kutapika kwenye mwendokasi


Monday, April 16, 2018

SERIKALI IMESEMA UPO UHABA MKUBWA WA WATAALAM WA USIMAMIZI WA VIATARISHI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

SERIKALI imesema upo  uhaba mkubwa wa wataalam wa masuala ya usimamizi wa vihatarishi,licha ya kwamba nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda ambao unahitaji wabobevu wa masuala ya usimamizi wa  eneo hilo ili kutoa taarifa mapema ya tahadhari za mbeleni.

Kuwepo kwa wataalam wa vihatarishi kutasaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingepotea kwa kutokujua yaliyoko mbele katika masuala ya usimamizi wa mikataba mibovu na hata katika suala la udhibiti wa rushwa.

Mkaguzi  Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga amesema hayo  jijini Dar es Salaam katika mahafali ya pili ya taasisi ya usimamizi wa vihatarishi Tanzania (IRMT) ambapo jumla ya wanafunzi  24 walihitimu katika ngazi mbalimbali.

Amesema tatizo la vihatarishi ni kubwa  nchini hasa katika mabenki katika eneo la mikopo chechefu ambayo imekuwa ikiongezeka na  kama taasisi  hizo  zingekuwa na watu mahiri katika eneo hilo wasingekuwa na kiwango kikubwa cha  mikopo chechefu.

“Ni muhimu eneo la vihatarishi kwenda vizurikatika sekta zote kwa kuwa  ni kichocheo cha uchumi nchini,” alisema Mtonga nakuopngeza kuwa kwa upande wa serikalini vihatarishi  ni pale ambapo malengo  tarajiwa  hayakufikiwa katika nyanja mbalimbali.

Amesema kadri wataalam wa vihatarishi wanavyoongezeka inachangia kuokoa fedha nyingi ambazo zinesababisha hasara kwa nchi na nimuhimu kwa wataalam waliopo kutumia miongozo miwili   ya udhibiti wa vihatarishi iliyotolewa tangu mwaka 2012 ikidhibiti wizi na ubadhirifu .

“Ni mategemeo yetukuwepo kwa wahitimu wengi katika eneo hilo hasa kwa sasa nchi inaenda uchumi wa viwanda,” alisema na kupongeza taasisi  ya IRMT kwa kuongeza eneo lingine la mafunzo ya vihatarishi katika mafuta na gesii nayotarajiwa kuanza Desemba mwakani 2019.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa IRMT, Buyamba Buyamba alisema lengola taasisi hiyo ni kuhamasisha  taaluma ya vihatarishi nchini pamoja na kuchochea fani hiyokwa watu wote katika menejimenti ya udhibiti wa vihatarishi.

Amesema taasisi hiyo inatoa mafunzo katika  kada tatu ya udhibiti wa vihatarishi, ikiwemo ubobezi wa usimamizi wa vihatarishi.
Vihatarishi ni tukio lolote am,balo likitokea litasababisha taaissi ama mtu binafisi anashindwa kufikia malengo yake iliyokusudiwa

Kuhusu vihatarishi vilivyopo nchini alisema kila taasisi ina vihatarishi  katika  malengo ya kimkakati au ya kiutendaji  na kutolea mfano katika sekta ya fedha  kuwa ndiyo inayokumbana na vihatarishi hususani  fedha katika mikopo haswa pale watu wanaposhindwa kurudisha mikopo.

Amesema kwa serikali, kihatarishi cha watu kutokuwa na maadili katika eneo la  ubadhirifu pia katika utendaji nakwa kuelekea katika uchumi wa viwanda ni muhimu kuwa na mpango madhubuti kuepuka vihatarishi kutokea.

 Mkaguzi  Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga akizungumza katika Mahafali ya pili ya taasisi ya usimamizi wa vihatarishi Tanzania (IRMT) ambapo jumla ya wanafunzi  24 walihitimu katika ngazi mbalimbali.   akizungumza katika mahafali ya pili ya taasisi ya usimamizi wa vihatarishi Tanzania (IRMT) ambapo jumla ya wanafunzi  24 walihitimu katika ngazi mbalimbali.  
 Makamu wa Rais wa IRMT, Buyamba Buyamba akizungumza juu ya lengo la tasisi hiyo kutoa mafunzo hayo kwa watumishi.
  Mkaguzi  Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga akikabidhi cheti kwa Mwanafunzi bora wa kiume katika mahafali hayo.
  Mkaguzi  Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga akikabidhi cheti kwa mwanafunzi bora wa kike katika mahafali hayo
Sehemu ya Wahitimu katika mahafali  ya pili ya taasisi ya usimamizi wa vihatarishi Tanzania (IRMT) ambapo jumla ya wanafunzi  24 walihitimu katika ngazi mbalimbali.  
     Mkaguzi  Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa chuo na Wakurugenzi wa tasisi za fedha waliopata vyeti vya ubora
 Mkaguzi  Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wote wa taasisi ya usimamizi wa vihatarishi Tanzania (IRMT) ambapo jumla ya wanafunzi  24 walihitimu katika ngazi mbalimbali.  

Sunday, April 15, 2018

VERTIV YAJA NA VIFAA VYA KISASA VYA KUKABILIANA NA MAJANGA YA UMEME


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Vertiv imefanya maboresho ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vinavyotumika katika ujenzi, viwandani na maofisini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati yao  wamiliki wa viwanda na kampuni mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.

Akizungumza jana Dar es Salaam, katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Rais  wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk alisema kuwa wamefanya maboresho ya bidhaa zao ili kusaidia wateja wao kujua endapo vifaa vyao vimepata hitilafu au la.

Amesema bidhaa wanazozizalisha ni pamoja na vifaa vya kudhibiti nguvu ya umeme, Ac zinazotumika kwenye viwanda, UPS na ambazo zimewekewa uwezo wa kutoa taarifa kwa mtumiaji  kama kifaa anachotumia kimeshindwa kufanya kazi kwa sababu gani.

‘’Tumefanya maboresho kwa bidhaa zetu ambapo wenye vituo vya data kama vile kampuni za simu, ofisi za serikali na kampuni binafsi watapata taarifa kuonesha kuwa kama UPS au AC za viwandani hazifanyi kazi kwa sababu ya umeme mdogo au kuna tatizo lingine ambalo linapaswa kufanyiwa marekebisho,’’ amefafanua Wyk.

Amesisitiza kuwa wanaendelea kuboresha bidhaa hizo ambazo zinatumika katika nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki (EAC) na Ulaya kwa kuwa wanaamini ukuaji wa teknolojia unasaidia katika kuleta maendeleo chanya kwa kila nchi.

Naye mshirika wa kibiashara na Mtaalamu wa masula ya mawasiliano, Mihayo Wilmore amesema kuwa uboreshaji wa vifaa hivyo utasaidia maeneo mengi ikiwemo hospitalini na maofisini ambako matumizi makubwa ya teknolojia hufanyika.

Amesema kuwa watu wanaotumia mitambo mbalimbali katika shughuli zao, ni muhimu kujua ni muda gani vifaa vyao vimeweza kuzimika kwa sababu ya kuisha kwa umeme, hutupata ujumbe mfupi wa maandishi kuelezea tatizo lililotokea.

‘’Ni muhimu kwa hospitali kujua UPS wanayotumia inaweza kuzimika kwa muda gani na sababu gani zinazosababisha jenereta kuzimika  hii itasaidia kurahisisha utoaji wa huduma haraka. Pia wameonesha uwezo wa kutengeneza vituo vya data katika simu au kompyuta ili kutoa taarifa kwa haraka kwa wateja wao,’’ ameeleza Wilmore.

 Rais wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk  akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake katika soko la Tanzania Chini ya usambazaji wa kampuni ya Elcom Solution 
  Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano  kutoka  Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, Johan Terblanche akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake juu ya umuhimu wa UPS kutoka Vertiv katika Data Centre. 
 Mkurugenzi wa huduma  wa Vertiv Mashariki  ya Kati , Pascal Bodin akieleza namna kampuni hiyo ilivyoweza kunufaisha Viwanda vya ukanda huo.
 Mshirika wa kibiashara  wa  Elcom Solution  ambao wamewakaribisha Vertiv nchini, Mihayo Wilmore akieleza Waandishi wa Habari umuhimu wa mitambo ya Vertiv katika sekta ya Afya nchini.
 Wakurugenzi  wa EL- COM Solutions , Deen Nathwani, Jimy Apson  na Amin Valji wakizungumza jambo wakati wa Warsha wa kutambuslisha bidhaa za Vertiv nchini.
Wafanyakazi wa Vertiv wakiwa katika picha ya pamoja na Washirika wao El-com Solution na washirika wengine kutoka nchini Kenya mara baada ya kumaliza warsha ya kutambulisha bidhaa zao Tanzania 

AFRIKA ZINDUKA YA BAGAMOYO PLAYERS YATIKISA KIGODA CHA NYERERENa Sophia Mtakasimba(TaSUBa)
Mchezo wa kuigiza wa jukwaani unaofahamika kwa jina la Afrika zinduka, umetikisa tamasha la kumi la kigoda cha Mwalimu Nyerere lililoendelea  katika ukumbi wa Nkuruma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mchezo huo uliobeba ujumbe wa namna  Bara la Afrika linavyoteseka na umasikini mkubwa ile hali  lina utajiri mkubwa wa mali asili , ardhi na madini umetungwa , umeongozwa na kuchezwa na Kikundi cha “Bagamoyo Players” cha Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili kuchagiza ujumbe wa tamasha la mwaka huu uliosema “wimbi la uporaji wa rasilimali Afrika wanyonge wanajikwamuaje”

Akizungumza katika siku ya pili ya Tamasha hilo Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama , amesema kuwa igizo hilo limeakisi namna halisi ya maisha ya sasa ya muafrika hivyo ni wakati wa kuzinduka.

“Wenzetu wa TaSUBa wametuambia Afrika Zinduka ,sasa huu ndio wakati wetu wa kuzinduka na kuona namna Afrika inaweza kunufaika na rasilimali zake.” Alisema bi Mlama

Tamasha la kigoda cha kitaaluma cha Mwl,nyerere  ambalo kwa mwaka huu limetimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake limefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 11-13 Aprili  ambapo mada mbalimbali kuhusu masuala ya kijamii zimejadiliwa .
 Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionyesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
 Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionyesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionyesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
washiriki wa tamasha wakifuatilia igizo la Afrika Zinduka

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...