Saturday, May 19, 2018

KAMATI YA KUDUMU BUNGE YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI YATEMBELEA MRADI WA KULASIMISHA MAKAZI KIMARA KILUNGURE

 Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akizungumza na Wananchi wa kata ya Kilungule mara alipofanya ziara na Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili kujionea namna mradi wa urasimishaji makazi ulivyofanyika katika eneo hilo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye akizungumza na Wakazi wa Kilungule wakati walipofanya ziara kukagua mradi wa urasimishaji Ardhi unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule A,Emanuel Komba akizungumza jinsi mradi huo ulivyokuwa rafiki kwa wakazi wa eneo hilo .
 Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye katika eneo Kilungule A mahali ambapo watu wa eneo hilo wamerasimishwa makazi yao.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye akiwa na baadhi ya Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu na Ardhi na Maliasili
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye akiwa na Waziri wa Ardhi William Lukuvi  pamoja na Wajumbe wa kamati hiyo

SERIKALI YASAINI MKATABA WA KUWAKOPESHA WATUMISHI WA UMMA MITUNGI YA GESI NA VIFAA VYAKE


 Na Mwandishi wetu
Serikali imesaini mkataba na Kampuni ya Gesi ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa umma.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni juhudi za Serikali za kutaka  kupunguza matumizi ya mkaa pamoja na kuni kwa lengo la kutaka kuhifadhi misitu ambayo imekuwa ikitumika  kama nishati.

Mkataba huo ulisainiwa jana  Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo na   Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan na huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Mej. Gen. Gaudence Milanzi akishuhudia tukio hilo.

Mbali na kusaini mkataba huo, TFS na Kampuni ya Mihan Gas zilizindua kampeni ya kukopesha mitungi ya gesi na  vifaa vya vyake kwa Watumishi wa Umma.


Awali, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi  aliwahimiza watumishi kuchangamkia fursa hiyo ya  kukopa mitungi na vifaa hivyo kwani itasaidia katika kuokoa misitu.

“Hili ni tukio kubwa hasa kwa wale ambao ni watunzaji wa mazingira katika kuwezesha jamii kuanza kutumia  nishati mbadala.’’ Alisema

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu  zaTanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo,alisema upatikanaji wa huduma hiyo ni jitihada za kuhakikisha matumizi ya mkaa yanapungua

Aliongeza kuwa nishati mbadala ndo njia pekee itakayosaidia jamii kuachana na  matumizi ya mkaa na kuni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni hiyo,Hamisi Ramadhani aliishukuru Serikali kwa kuikubalia kampuni hiyo kusambaza gesi kwa watumishi.  
Akizungumzia namna watumishi watakavyonufaika na mpango huo,  Mkurugenzi Mtendaji , Ramadhani alisema kampuni imetenga fungu ambalo litarahisisha ukopeshaji wa vifaa hivyo na kila Mtumishi atapewa nafasi ya kuweza kulipia mwezi mmoja mara baada ya kuanza kuitumia gesi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo (kushoto)  akiwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano kati ya  Serikali na Kampuni ya Mihan Gas wa  kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kushoto) akizungumza na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati)   mara baada ya  mkutano  wa utiaji  saini wa mkataba wa makubaliano na Serikali wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa. Kulia ni Eng. Christopher Bitesigire wa Wizara ya Nishati.    

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS), Profesa  Dos  Santos Silayo (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na   Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia)  mara baada ya kusaini mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma   
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi  akizungumza kabla  ya  utiaji saini mkataba  kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS), Profesa  Dos  Santos Silayo akizungumza kabla ya  utiaji saini mkataba  kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Santos Silayo (kushoto)  na   Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia) wakionesha  hati ya makubaliano mara baada ya utiaji saini mkataba  kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi walioshiriki kwenye mkutano wa utiaji saini kati  ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas  wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi  pamoja na watumishi mara baada  ya zoezi la utiaji saini mkataba  kati ya Serikali  na Kampuni ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa kukamilika katika mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma              

WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE ARDHI NA MALIASILI WATEMBELEA MRADI WA ILMIS NA MAJENGO YA NHC VICTORIA NA MOROCO

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akionyesha Faili lenye viambatanisho vya hati moja katika chumba cha  kubadilisha hati za kawaida kwenda Dijitali kinachosimamiwa na mradi wa ILMIS Ambapo kwa sasa mtu ataweza kupata kuona hati yake kupita mtandao na akihitaji karatasi atapata moja amabyo itakuwa na viambatanisho vyote.
 Msajili wa  Hati kutoka Wizara ya Ardhi, Joanitha Kazinja akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye  wakati walipotembelea chumba cha kubadilishia Nyaraka cha Mradi wa ILMIS
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye  Akizungumza wakati wa kikao cha Majumuisho ya ziara ya kutmebelea Miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mradi wa ILMIS Unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi.
 Mtaalamu wa Maluala ya bacode Katika mradi  wa ILMIS Cristina Selaru akitoa maelezo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili jinsi mfumo huo utakavyokuw aunafanya kazi kumsaidia mtu kujua taharifa zake zote
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili na Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Neema Mgaya akitizama jinsi wafanyakazi wa Mradi wa ELMIS wakijaza baadhi ya nyarak katika mtandao
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye  akizungumza jambo na  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi mara baada ya kutembelea mradi wa Victoria unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauyeakiongoza kikao cha Kamati

Mkurugenzi wa Mfumo wa TEHAMA Wizara ya Ardhi  na Kodineta wa ILMIS , Dk Shabani Pazi Akitoa Maelezo juu mradi huo
Mhandisi Msimamizi wa Mradi wa ILMIS,Carol Roffer akieleza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  walipotembelea kuona mafanikio ya Mradi huo unatoekelzwa na Wizara ya Ardhi
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge wakipanda kwenye gari kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa NHC

Thursday, May 17, 2018

SETHI AIBUKA, APINGA KUNG'OLEWA IPTLNa Mwandishi Wetu

Mkurugenzi na Mmilikiwa kampuni ya PAP/IPTL ,Harbinder Sing Sethi Amekanusha taarifa zinazosambzwa mitandao kuwa amefutwa kuwa Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.
Hayo yameelezwa leo na Mwanasheria   wa mmiliki wa Kampuni ya PAP/IPTL, Harbinder Sing Sethi, Hajra Mungula, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mteja wake na kusema Sethi bado Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.

Wakili Mungula amesema kuwa   watanzania kupuuza kwa taarifa zilizotolewa awali na watu wanaojiita kuwa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa  na Wakili  Hajra Mungula imesema kuwa  yeye kama mwanasheria wa Sethi, amewasiliana na mteja wake, ambaye yuko rumande na kushangazwa na taarifa hizo.

Ilisema hivi karibuni kumeripotiwa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kampuni inayomilikiwa na Harbinder Sing Sethi imebadilisha uongozi katika ngazi za Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Mkurugenzi mtendaji wake.

"Taarifa iliyosambazwa na anayejiita mwenyekiti wa bodi mpya, Ambroce Brixio imemtaja yeye kuwa na cheo hicho na Joseph Makandege kuwa Mkurugenzi wake ambaye kwa miezi kadhaa sasa hajawahi kuonana nae ikiwemo hata kutofika mahakamani siku ambazo kesi imekuwa ikitajwa" imesema sehemeu ya taarifa hiyo.

Wakili Hajra, aliandika katika taarifa hiyo kuwa taarifa hizo zimemfikia kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti halali na mmiliki wa kampuni hii ya kuzalisha umeme ya IPTL ambayo kimsingi inamilikiwa na kampuni anayoimiliki ya Pan Africa Power Solutions(PAP).

Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria huyo, pamoja na kuagiza wanasheria wake kuchukua hatua za haraka za kisheria mwenyekiti Sethi pia hana taarifa zozote juu ya mabadiliko hayo.

"Mwenyekiti Seth anapenda kuutaarifu umma kupitia sisi kwamba wazipuuze taarifa hizo kwa kuwa hazitokani na mamlaka halali za kisheria za kampuni hiyo," ilisema mwanasheria huyo.

Ilisema pamoja na kwamba Mwenyekiti Sethi bado yuko mahabusu akituhumiwa mashtaka kadhaa ya jinai, hiyo haiondoi ukweli kuwa IPTL ni kampuni binafsi yenye wamiliki halali wenye hisa halali na wala sio NGO ambayo mtu yeyote anaweza kutangaza mapinduzi ya kiuongozi wakati wowote.

"Mwenyekiti anapenda kuwahakikishia watanzania wote kuwa licha ya uwepo wa mashtaka yanayomkabili bado kampuni hiyo ipo chini ya usimamizi salama wa PAP na kwamba madeni yote, madai, mali na stahiki zote zizohusiana na kampuni hiyo zipo katika mikono salama mpaka sasa" ilisema sehemu ya taarifa

Aidha, ilisema taarifa hiyo, Mwenyekiti anawahakikishia watanzania kuwa ataendelea kutoa ushirikiano mahsusi kuhakikisha nchi inajiepusha na hasara zinazotokana na matendo ya aina ya kina Makandege na wenzake ya kukurupuka bila kufuata sheria na taratibu


AWAMU YA PILI YA SPORTPESA SUPER CUP KUZINDULIWA

Na Mwandishiwetu, Jiji la Dar es Salaam

Dar es Salaam, Alhamisi 17, 2018. Awamu ya pili na mashindano yanayohusisha timu bora za Afrika Mashariki-SportPesa Super Cup yanatarajiwa kuanza Juni 3-10, 2018 nchini Kenya kwenye uwanja wa Kimataifa wa Moi uliopo Kasarani.

Timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo kutoka Tanzania ni timu zinazodhaminiwa na SportPesa ambazo ni Simba, Yanga, Singida United pamoja na JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi kutoka Zanzibar), wakati kutoka Nairobi timu zitakazoshiriki ni Gor Mahia, AFC Leopards na Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Dar es Salaam ambapo pia walikuwepo wawakilishi na viongozi kutoka TFF pamoja na viongozi wa timu za Simba, Yanga na Singida United Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas alisema “michuano hii kuleta chachu na kumpata bingwa kwa upande wa Africa Mashariki”

“Matayarisho ya mwaka huu yamefanyika mapema na ukiangalia muda wa kupewa na taarifa mpaka kuanza ni zaidi ya mwaka mmoja, hivyo basi hakuna sababu kwa timu zetu za Tanania zisifanye vibaya zaidi ya mwaka jana kwani matayarisho yamefanyoka mapema na kwa hali hiyo timu zikifanya vibaya tutakuwa na sababu za kuwalaumu”

“Kutakuwa na jumla ya timu nane za Afrika Mashariki na mshindi wa michuano hiyo atacheza na 
moja kati ya timu iliyoshiriki ligi kuu uingereza, Everton”
Timu zitakazoingia robo fainali kwenye mashindano haya watapata kiasi cha dola za kimarekani 2,500, nafasi ya nne timu itapata kiasi cha dola 5000, wakati nafasi ya tatu na wa pili dola 7,500 na 10,000 kila mmoja.
Timu itakayoshinda itazawadiwa kiasi cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kuchuana na timu ya Everton katika uwanja wa Goodison Park.

“Napenda kuwatakia kila la kheri timu zetu tatu zinazokwenda kutuwakilisha jijini Nairobi, natumaini zitatutoa kimasomaso kwa kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana, wataiwakilisha nchi yetu vilivyo kwa kucheza kwa uweledi na nidhamu” alimaliza Ndugu Tarimba
Kwa upande wa timu ya Simba Ndugu Said Tulliy alisema “Napenda kuchukua nafasii hii kuwataarifu wanasimba kuwa tunakwenda kushiriki mashindano kama timu shindani na si timu shiriki na tunajua mwaka jana tulipata nafasi kama hii lakini tuliipoteza na tusingependa kitu kama hicho kijirudie. Tumeona faida yake kutokana na jinsi wenzetu waliopita ni jinsi gani walivyofaidikakupitia mashindano hayo”

“Kama timu tumejiandaa na tuko tayari kuhakikisha tunalinda heshima ya Simba Sports Club na heshima ya Tanzania, tunakwenda na kikosi kamili ili kuhakikisha tunachukua ubingwa ili tuweze kushindana na timu iliyopangwa”

“Tunathibitisha kuwa tutashiriki mashindano haya kwa sababu ni mashindano muhimu, tuko tayari kwa ajili ya mashindano na timu yetu nzima na tuko tayari ya kushinda” alimaliza Ndugu Said Tulliy

“Changamoto ya mashindano iko pale pale lakini kwa mwaka huu nia yetu kuu ni kuchukua ubingwa ili kuleta heshima kimataifa” Charles Boniface Mkwasa Yanga

“Kwanza napenda kuwashukuru SportPesa kwa sababu wamefanya timu yetu kujulikana kwenye kila kona ya nchi, moja kati ya wadhamini wetu wa nguvu ambao tunajivunia sana kutoka kampuni hii. Jambo kubwa tutakaloenda kulifanya kwenye michuano hii kimsingi kwa mwaka huu tumeweza kushirikishwa mapema ili tuweze kujipanga sisi kama timu lakini kikubwa zaidi ikumbukwe kuwa Singida United ni timu pekee iliyofanikiwa kufika nusu fainali kwa hapa Tanzania na mwaka huu tunaamini tutachukua kombe”

Kwa watanzania na watu wa Africa mashariki tunaombawatuunge mkono timu yetu. Ningependa kuwaomba SportPesa kuhakikisha kanuni na sheria za mpira wa miguu zinafatwa ili michuano hii iweze kumalizika vizuri”–Shabani Mande Singida United
Tunapenda kuwashukuru SportPesa kwa kututambua na kutupa nafasi ya kushiriki katika michuano hii na napenda kuwaahidi hatutawaangusha ingawa hii itakuw mara ya kwanza kushiriki.” Maalim Masoud, Katibu wa klabu, JKU.

KUHUSU SPORTPESA SUPER CUP
SportPesa Super Cup ni mashindano ya mwaka yanayohusisha timu bora kutoka Afrika Mashariki kwa wiki moja mfululizo.
Lengo kuu la mashindano hayo ni kuongeza chachu ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na kati, kuwapa fursa vijana kuonyesha na kufichua zaidi vipaji vyao.
Kama kampuni yenya matawi nchi mbali mbali duniani yenye lengo la kuunganisha wapenda soka duniani na kuonyesha maana ya mpira wa miguu kwa nchi za Afrika na inawakilisha nini.

 Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti  wa SportPesa Tanzania Tarimba Abbas akizungumza na Waandishi wa habari juu ya awamu ya pili ya Mashindano ya Super Cup
 Kiongozi wa Klabu ya Simba, Said Tully akizungumzia umuhimu wa Mashindano hayo ya SportPesa Super Cup
 Katibu wa Mkuu wa Yanga , Charles Boniface Mkwassa akizungumzia timu yake ilivyojipanga katika Mashindano hayo

Wednesday, May 16, 2018

HDIF KUANZA WIKI YA UBUNIFU MEI 21 KATIKA KUMBI ZA COSTECH

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Dk Amos Nungu akizungumzia juu ya wiki ya Ubunifu kwa vijana iliyoandaliwa na Tasisi ya HDIF kwa kushirikiana na UKAID
 Mwakilishi wa  Mfuko wa Msaada wa Serikali ya Uingereza UKAID , Berthy Arthy akizungumzia  ufadhili wa UKAID Katika wiki ya ubunifu itakayofanyika COSTECH. Kuanzia May 21.
 Kiongozi Mkuu wa HDIF Tanzania , David McGinty, akieleza namna Vijana ya ushiriki wa Vijana zaidi ya 2000 katika Wiki ya ubunifu  itakayofanyika Costech kuanzia Jumatatu.
 Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano Kutoka Tasisi ya HDIF, Hannah Mwandoloma akitoa maelezo ya ziada kwa Waandishi wa Habari katika Mkutano wa Waandishi wa Habari.
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Waandishi wa Habari wa HDIF Juu ya Wiki ya Ubunifu.

NI MO DEWJI SIMBA AKUBALI KUNUNUA ASILIMIA 49 MABADILIKO YA KATIBA KUMPITISHA JUMAPILNa , Humphrey Shao, Globu ya  Jamii ,Dar es Salaam

Mfanyabiashara Maharufu nchini  Mohammed  Dewji 'Mo' amekubali kununua asilimia 49 za hisa za klabu ya Simba SC kulingana na maelekezo ya Serikali katika mchakato wa mabadiliko ya klabu ya Simba kwenda Kampuni.

Hayo yamethibitishwa  na  Msemaji wa Klabu Bingwa  wa Nchi hii, Haji Manara alipokuwa akizungumza mapema leo za Waandishi wa habari juu ya Mabadiliko ya Katiba  ya klabu ya Simba.

 
Manara  amesema  wanachama wa Simba SC kujitokeza kwa wingi katika Mkutano wa mabadiliko ya Katiba utakaofanyika Mei 20, mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo eneo la Ocean Road mjini Dar es Salaam.

"Mkutano huo ulioitishwa na Kaimu Mwenyekiti, Salim Abdallah ‘Try Again’ utaanza Saa 3:00 asubuhi na tayari wanachama wamekwishasomewa ajenda kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya klabu hiyo, kufungu cha nne" Amesema Manara.amesema Mkutano huo utafuatia ule wa Desemba 3, mwaka jana, ambao uliazimia kumfanya mfanyabiashara Mohammed ‘Mo’ Dewji kuwa mwanahisa mkuu wa klabu katika mfumo mpya wa uendeshwaji wa Simba SC.

Mo pekee aliweka dau la Sh Bilioni 20 kuomba asilimia 50 ya hisa, baada ya klabu kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa Sh. Bilioni 20 miezi miwili iliyopita, ingawa baadaye Serikali ikaagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja.

Wanachama 1320 walihudhuria mkutano huo wa Desemba kutoka Dar es Salaam na mikoa jirani na kwa furaha ya ushindi huo, Mo Dewji alitoa ahadi 10 za kuleta mabadiliko makubwa, ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa mazoezi wa nyasi za asili na nyasi bandia pamoja na hosteli ya kisasa ya wachezaji.

Wakati huo huo: Simba SC inaendelea na maandalizi ya sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku wakisubiri majibu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli aliyeombwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhudhuria mchezo huo ili pia awakabidhi Kombe Simba.

Simba SC wamekwishajikusanyia pointi 68 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kuelekea mechi mbili za mwisho za msimu. Katika mechi 28 walizocheza hadi sasa, Simba wameshinda 20 na kutoa sare nane na baada ya mchezo wa Jumamosi watakwenda kukamilisha msimu kwa mchezo dhidi ya Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Msemaji wa klabu ya Simba , Haji Manara akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya Mkutano wa Mabadiliko ya klabu ya Simba.
 Mwanasheria wa klabu ya Simba SC, Evodius Mtawala akizungumza  katika mkutano na Waandishi wa Habari katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuri aMkutano huo wa Simba 

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO UCHINA

Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maharufu kama China International Beauty Expo African Hall,Rex Chan akizungumza na Waanddishi w...